Muungano ukivunjika

Muungano ukivunjika

Haaminiki yule , anaweza kuja na ids nyingi na yaelekea yumo kwa jina jengine , ningalikuambia lakini sitaki kupoteza wakati kumcheck ip adress yake
Halafu Avatar yake ameweka jina la Allah nadhani anajitafutia laana.
 
Mwaka jana nilitembelea visiwani Zanzibar nilishuhudia watu walivyo huru wenye furaha wachangamfu,nikawa najisemea rohoni; "wanasiasa bhana, ukiwasikiliza utasema visiwa vinawaka moto."


Suala sio wanasiasa , mbona kwenye ile tume ya Waroba , Wazanzibari wengi waliotoa maoni Yao walitaka muungano wa mkataba ??
 
Zanzibar kisiwa tu mumekivamia sababu ni DINI
Mimi sijakivamia kilivamiwa na John Okello na askari wake 300 je kwanini mlishindwa kujihami wakati jeshi lenu lilikuwa ni kubwa?!
 
Suala sio wanasiasa , mbona kwenye ile tume ya Waroba , Wazanzibari wengi waliotoa maoni Yao walitaka muungano wa mkataba ??
Muungano wa mkataba ndio ukoje?!mimi binafsi nilkuwa niko upande wa Serikali tatu.
 
Mimi sijakivamia kilivamiwa na John Okello na askari wake 300 je kwanini mlishindwa kujihami wakati jeshi lenu lilikuwa ni kubwa?!


Zanzibar ilikuwa ni nchi ya amani na ikiwaona nyinyi watanganyika kuwa ni watu wema . Ni nani alikuambia Zanzibar ilikuwa na jeshi ??

Aliyevamia siye wewe ni Laaanatullahi Nyerere na jeshi lake kwani baada ya kuivamia alimkamata Waziri Mkuu Wake aliyechaguliwa na wananchi pamoja na baraza la Mawaziri na kuwafunga katika magereza ya Tanganyika bila kuwafikisha mahakamani kwa zaidi ya miaka 10 , kabla huo uitwao muungano haujafikiriwa
 
Muungano wa mkataba ndio ukoje?!mimi binafsi nilkuwa niko upande wa Serikali tatu.


Muungano wa Mkataba ni MASHIRIKIANO kati ya nchi mbili au zaidi ambazo kila moja huwa inabaki na mamlaka yake kamili ya KIDOLA kitaifa na kimataifa lakini bado zikawa zina mashirikiano katika maeneo maalum zitakazoamua kushirikiana, mahusiano ambayo huwa yanaongozwa na Mkataba.

Muungano wa Mkataba ni tofauti kabisa na Muungano wa Kikatiba ambao huwa unamaanisha kuwepo kwa Serikali ya Muungano inayosimamia mambo ya Muungano.

Katika Muungano wa Mkataba, kila nchi hubaki na Serikali yake kamili yenye kusimamia mambo yote. Yale maeneo ya USHIRIKIANO husimamiwa kupitia ama KAMISHENI YA PAMOJA au KAMATI YA PAMOJA kwa kadiri makubaliano yatakavyokuwa yamewekwa kwenye Mkataba.

Faida za Muungano wa Mkataba:

1. Hakuna khofu ya nchi moja kuimeza au kuitawalia nchi nyengine.

2. Kila nchi inabaki na uhuru na mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa kuamua mambo yake.

3. Kila nchi mwanachama ina uhuru wa kujitoa katika jambo lolote ililoamua mwanzo kushirikiana pale inapoona hakuna maslahi au faida kuendelea nalo.

4. Huvutia nchi nyingi kuingia katika Muungano wa aina hiyo kwa sababu hakuna khofu ya kupoteza mamlaka au kupunguziwa madaraka au mambo yake kuamuliwa na nchi nyengine.

5. Mahusiano huwa ni ya kirafiki na ya ujirani mwema yanayopelekea kuaminiana na kuondoa kutiliana shaka kusikokwisha.

Zanzibar iwe na mamlaka yepi kitaifa na kimataifa katika Muungano wa Mkataba?

1. Iwe na Serikali kamili yenye Wizara zote ikiwemo Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani na Ulinzi.

2. Iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa na pia uanachama wa Jumuiya zote za Kimataifa zikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC), Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Nchi za Bahari ya Hindi.

3. Iwe na Benki Kuu yake na Sarafu yake.

4. Iwe na mamlaka yote ya kuamua será za fedha na uchumi, kodi na sarafu.

5. Iwe na Uraia wake.

6. Iwe na Paspoti yake na kusimamia Uhamiaji katika nchi yake.

7. Idhibiti Anga yake na Usafiri wa Anga yenyewe.

8. Isimamie Elimu ya Juu yenyewe na kuamua Mitihani gani itumie katika masomo.

9. Isimamie na inufaike na rasilimali zake zote za ardhini na baharini ikiwemo mafuta na gesi asilia.

10. Idhibiti yenyewe eneo la mipaka ya Bahari Kuu (EEZ) katika eneo lote inalopakana nalo.

11. Idhibiti mamlaka mengine yote yanayokuwa yanamilikiwa n anchi kamili.

Ni ipi Mifano ya Muungano wa Mkataba?

– Muungano wa Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 27.
– Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye wanachama 5 mpaka sasa.
– Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS).

PAMOJA TUNAWEZA
 
Ni nani alikuambia Zanzibar ilikuwa na jeshi ??
instead assembled an army of 2,800 men to fight the British. ... Sultan Jamshid bin Abdullah was overthrown a month later during the Zanzibar Revolution.
 
instead assembled an army of 2,800 men to fight the British. ... Sultan Jamshid bin Abdullah was overthrown a month later during the Zanzibar Revolution.


Nani alikuambia Zanzibar kulikuwa na jeshi ??? hujaniambia bado
 
Mbona hati ya muungano ipo na imeongelea hayo yote.
 
Hati ya muungano imeongelea Zanzibar kulikuwa na jeshi ???
Sasa kama sultani jamshid alikuwa hana jeshi mtu yeyote mwenye wanamgambo na Riffles angeweza kuitwaa na kuitawala,sasa nimeanza kuelewa kwa nini Zanzibar imewavutia wavamizi.
 
Hoja za muungano tusizichanganye na mambo ya dini.
 
Ni Zanzibar yenyewe ndio ya kujilaumu, hebu fikiria binti kigoli amevaa khanga moja beach saa za magharibi anawachekea chekea watu ndio ikabidi wanaume wamchangamkie.
 
Zanzibar zaidi kisiwa cha Pemba, wakituhakikishia hawawezi kuwa base ya extremist kama Alshaabab,ISIS,Alqaida nawaunga mkono 100% wajigawe tu.Waachane na haya makucha ya mkoloni mweusi fisiem!
 
Zanzibar kuwa full membership united nation
Zanzibar kuwa na mabalozi wake all over the world

Zanzibar kuwa member wa Fifa
Zanzibar kuwa member wa Caf
Zanzibar kuwa member wa OIC
Zanzibar kuwa na passport yake
Zanzibar kuwa member wa East Africa community(EAC)
Zanzibar kuwa na nyanja nzuri za kiuchumi, kimataifa na kitaifa bila ya vikwazo.
Zanzibar kuwa na sarafu yake.
Zanzibar kuwa na wizara yake ya elimu,
Zanzibar kuwa na wizara ya Anga
Zanzibar kuwa na bank kuu.
Zanzibar kuwa na jeshi lake coast guard
Zanzibar kuwa na jeshi la polisi lake
Zanzibar kuwa na usalama wa taifa
Zanzibar kuwa free port, kama dubai.
Zanzibar kuwa member wa AU


Wizara hizi zote zina ajira zaidi ya 10,000 ni faida kwa wazanzibari.

Kwa upande wa Tanganyika, nahisi kuwa watatumia jina la Tanzania .

Watatumia influence ile ile ya Jamuhuri ya Muungano na Jamuhuri ya Tanzania au tanganyika, ni kubadili kidogo tu.

Siwezi kusubiri case ya Muungano kuja kusikilizwa huku Zanzibar, kwa maana nina kila sababu ya kuunga mkono, faida ni nyingi kwa Wazanzibar kuliko hasara.

InshaAllah
Umesahau kitu kimoja kikubwa sana, "wapemba watapungua kigamboni na dsm, na mikoani, watakuwa either wahamiaji haramu wanaotakiwa kufurushwa au watapata shida sana ya uraia kwasababu zenji wataipenda na bara wataipenda kutokana na kwamba wamewekeza, wamenunua ardhi etc.

Jambo hili nakuhakikishia litakuwa na hasara kubwa zaidi kwa wazanzibari kuliko wabara, kwasababu ukichukua asilimia kubwa ya watu wa bara, waulize kama wanaipenda zenji, utakuja kugundua wengi wao hata haipo vichwani mwao na hawaoni kama kutakuwa na madhara. ukienda mkoa wowote tz kuna wazenji wamenunua ardhi wanaishi kama watz, ila ukienda zenji wabara wenye ardhi ni wa kuuliza, na wengi wanaenda either kufanya kazi na kuondoka tu.

Siku mkivunja muungano (jambo ambalo mimi sitalichukia), mtakuja kujikuta mmepoteza kitu kikibwa sana ambacho mlikuwa hamjui na hamtakuja kukipata tena. huwezi kuujua umuhimu wa Tanganyika hadi pale utakapoipoteza.
 
Back
Top Bottom