Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar!

...Nadhani ni wakati wa Sitta kurudi nyumbani,wananchi wamechoka na blabla za CCM,asije akaendelea kujishushia heshima yake kwa kusimamia mambo yasiyo na manufaa kwa Taifa hili...
:rip: CCM na mswada wa mabadiliko ya Katiba
 
duh kwa hili zanzibar nimewakubali. Huwezi kutania watu kwenye vitu vya msingi
 
Wzanzibar wanasema kukurupuka tu Mh Karume kuunganyisha nchi bila ya Ridhaa ya wenye nchi ilikuwa ni kosa kubwa na asari zake ndio tunazo zivuna sasa.
Wanasema katu haingii akilini watu millin 1.2 tuungane na watu million43 haingii akilini kabisa.
Hatutaki Muungano Fake basi tumechoka.
Kuendelea Muungano huu bila ridhaa ni kutawaliwa kinguvu na Tanganyika (Tanzania)"] [/caption]

Kumbe mnajua kuwa mumeolewa talaka tutawapa tu, hilo wala msihofu....
 
mwisho wa wananchi kudanganyika umefika,kilichofanyika zanz ni ujumbe mzuri sana uwafikie mafisadi wa ccm
 
Mimi ni Mtanganyika lakini ninaamini kuwa ni uonevu wa hali ya juu kwa Wazanzibari, kama serikali ya Mwungano inaweza kuuandaa mswada wa Katiba ya Mwungano wa Tanzania ambamo na Zanzibar imo, bila ya kuwashirikisha Wazanzibari, bila ya kujali kama Mswada huo ni wa ovyo (kama ulivyo) au ni mzuri. Mawaziri waliopo ndani ya serikali ya mwungano siyo mawaziri wanaowakilisha serikali ya Zanzibar, na hiyo ni kati ya complexities za Mwungano wetu.

Mimi ninaamini kuwa katika katiba mpya muundo wa Mwungano ni jambo muhimu sana la kujadiliwa kwa kina ili kila upande uridhike. Tumeungana kwa kuamini kuwa mwungano utaleta faida kwa pande zote mbili na siyo mwungano uwe ni kongwa la utumwa na mateso ya kisaokolojia kwa upande wowote wa mwungano au kwa pande zote. Tuujadili mpaka tufikie mahali wote tuamini kuwa mwungano huu unatusaidia. Kama kila upande unaamini kuwa muundo na items za mwungano huu havina faidi, sasa kwa nini tunaendelea kung'ang'ania muundo huo huo na items zile zile?

Kwa kuwa Wazanzibari kwa namna fulani wana turufu katika masuala ya mwungano, na pia Wazanzibari wana hulka ya kutokuvumilia mambo ya kijinga kama walivyo Watanganyika, ni vema tukaungana nao kuukataa upuuzi huu na mambo ya kijinga ambayo yamekuwa yakendelezwa na CCM na serikali yake. Hongereni sana Wazanzibari.
 
kama muswaha haukutaja KAdhi na OIC. ni ovias utakataliwa na wala-urojo
huu mswada pia umekataliwa wala panya,,na buku,,
Nawahamasishwa watanganyika mubebe mabango siku ya sherehe za muungano ya kutamka muungano vunjaa vunjaa
 
Safi sana Zanzibar hakuna kukubali kupelekwa kama Punda lazima maslahi ya wazanzibari yaangaliwe kwa upana wake na mridhike, vinginevyo hakuna kulala mpaka kieleweke. Walishazoea kuwaamulia mambo kutoka bara. Ilikuwa ni dharau kubwa kwenu. SIMAMENI KIDETE KAMA NI KUUVUNJA MUUNGANO UVUNJIKE KUWE NA MKATABA MPYA.
 
He, "Wazanzibari wachana muswada wa katiba" hayo yamo kwenye mwananchi ya 10Th April 2011, hayo ndo yalojiri live bila chenga, hawa watu hawataki muungano kabisaaaa
 
Wavunjilie mbali shensi type, wazanzibari wamekuwa kula kulala tangu 1964, na wamepora ardhi zetu. Pia wameharibu harakati zetu za kujikomboa kwa kafu kufunga ndowa na sisemu.

Ukivunjika tu wafunge virago warudi makwao wanatutia joto na karaa. Wakishuhulikiwa na serikali huko kwao wasikimbilie kwetu.

Nenda mwana kwenda!
 
Waambie wakubwa wakoCHADEMA wawewke hilo katika harakati zao za maandamano kama mko serious na hilo!
 
Tukivunja muungano wazenji watahangaika sana.Sasa hivi wanaona oa sababu tumewaachia wanavinjari huku bara waache mchezo bana alh!

Ivyo kuna tofauti gani ya huko na Zanzibar? Umasikini, mlo mmoja, umeme wa mgao na mambo kibao. Pengine tukiondoka si mtapunguziwa mzigo???
 
Muungano ulikuwa uamuzi wa viongozi wa nchi mbili kuamua kuungana for the common good...na kwa sababu hiyo common good haiwi experienced na upande mmoja, there is no need to continue with system that hurts and burdens one side....kama ndoa inavunjwa kwa kukosekana kwa common good...sembuse muungano ambao ni suala la makubaliano na maamuzi....kama sisi watanganyika hatuoni faida ya muungano tuendelee tu kuumia kwa sababu kuna wachache wenye mamlaka wana some interest in this monster unity? Watanganyika let us think, and reflect, what have we benefited from Muungano? It is like we have n0o rights of our own while Serikali ya Zanzibar is both autonomous na pia serilaki ya Muungano...sisi ni serikali tu ya Muungano, with no autonomy....

Theoretical yes but practical you are everything. You are Tanganyika and you are Tanzania contrary to what you try to suggest that zanzibar holds two identities.
I would like to ask you when and how do your interests are hindered by Union? Whatever you do you do in the cover of Tanzania and never happened that you are not able to fulfil your wishes only because Tanzania (union) forbides you.
On the other side of coin there is Zanzibar which can not do anything without Tanganyika interference. You should take a case of OIC where Tanganyika ministers and legislaters questioned what you claim autonomous of Zanzibar to issues thatn are only concerned Zanzibar.
 
Sitta anusurika kipigo
• Aondolewa na FFU ukumbini

na Mwandishi wetu, Dodoma

amka2.gif
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais (Muungano) Samia Suluhu Hassan, wamenusurika kipigo baada ya kutokea vurugu kwenye kikao cha kujadili muswada wa mabadiliko ya Katiba mpya visiwani Zanzibar.
Sitta, alikuwa akiwasilisha rasimu ya marejeo ya katiba kwa niaba ya Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, ambapo wakati akitoa mada hiyo hali ndani ya ukumbi ilikuwa shwari.
Vurugu hizo zilitokea katika ukumbi wa Shule ya Haile Selassie mjini Zanzibar jana, baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, kuchangia kwa maneno makali na baadaye kuuchana hadharani muswada huo na kutoka nje ya ukumbi.
Tukio hilo lilisababisha baadhi ya wajumbe kuzichana nakala za muswada huo huku wengine wakinyanyua viti juu wakiashiria kwamba mkutano huo umekwisha na baadhi yao wakimfuata Sheikh Farid nje ya ukumbi wa mkutano.
Kitendo hicho kilisababisha hali ya wasi wasi na kusababisha mtoa mada, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kuondolewa kwenye ukumbi chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Akichangia muswada huo, Sheikh Farid, alisema kabla ya kupelekwa muswada huo visiwani Zanzibar upelekwe wa Katiba ya Tanganyika, ili kuuangalia Muungano ambao hivi sasa haupo kwenye hali nzuri.
Alisema haoni sababu ya kujadiliwa mabadiliko hayo ya katiba kabla ya wananchi wa Zanzibar hawajaulizwa kwa njia ya kura ya maoni iwapo Muungano huo wanautaka au hawautaki.
“Napenda kutoa usia wangu kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya umoja wa kitaifa kuitisha kura ya maoni wananchi waulizwe wanaotaka Muungano na wale wasioutaka”, alisema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu, huku baadhi ya wajumbe wakinyanyua mabango yaliyoandikwa ‘Hatuutaki Muungano Jamani’.
Sheikh Farid, alisema zama za udikteta wa Nyerere zimekwisha, wananchi wa Zanzibar wapo huru kutoa maoni yao na kama serikali inaogopa wananchi wapo tayari.
Naye aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Afro Shirazy Party, Baraka Shamte, alisema muswada huo usijadiliwe hadi hapo marekebisho yatakapofanywa na kuundwa jopo la wanasheria kutoka pande zote mbili za Muungano.
Alisema muswada huo uandaliwe upya na yale yanayokosolewa yaondolewe kwa lengo la kufanikisha mpango wa kupata katiba itakayosaidia kuimarisha Muungano wenyewe.
Akichangia muswada huo, Diwani Arafa Mohammed Said, alisema kuna haja ziundwe tume mbili za kukusanya maoni juu ya Katiba mpya, ikiwemo tume ya Tanzania Bara na tume ya Zanzibar .
Alisema kwakuwa Zanzibar wananchi wake ni wachache si vizuri wakaingizwa katika mjadala wa jumla na hatua hiyo ya kuundwa tume mbili itawapa nafasi ya kupata ukweli juu ya kile wananchi wa Zanzibar wanachokitaka.
Mwanasheria, Abdulkadir Mohammed Amour, alisema bila ya marekebisho yanayopigiwa kelele kufanyika, muswada huo iwapo utapitishwa na Bunge mwisho wake utakuwa Kisiwa cha Chumbe na hautahusu Zanzibar.
Askari mstaafu, Miraji Kiongwe, alisema inashangaza tangu kufikiwa Muungano wa mwaka 1964, vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vikiongozwa na wakuu wake kutoka upande mmoja wa Muungano.
Alisema hakuna mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) au Jeshi la Polisi hata mmoja aliyetoka Zanzibar, wakati vyombo hivyo ni vya Muungano.
Akitaja majina ya wakuu waliowahi kuongoza vyombo hivyo, alisema vyombo hivyo havina tofauti na Bunge, kwa vile hakuna spika hata mmoja aliyewahi kuongoza Bunge hilo kutoka Zanzibar.
Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Ibrahim Mzee, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi, (BLW) alisema inashangaza tume zote zilizowahi kuundwa Zanzibar imekuwa ikipewa nafasi ya umakamu na mwenyekiti hutoka upande wa Tanzania Bara.
Alitoa mfano wa tume hizo kuwa ni ile ya Jaji Kisanga, Jaji Nyalali na kutaka utaratibu huo kuangaliwa upya, ili Zanzibar nayo iweze kutoka watu wa kuongoza tume hizo za kitaifa.
Akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo, alisema Bunge la Muungano halina mamlaka ya kutunga katiba na kazi hiyo inatakiwa kufanywa na Bunge la Katiba.
Alisema kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano kazi yake ni kutunga sheria, hivyo kuwepo na Bunge la Katiba na lazima liwe na wajumbe sawa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.
Alieleza kwamba muswada huo una upungufu mwingi na kushauri kuwa unahitaji kuangaliwa upya, ikiwamo mamlaka makubwa aliyopewa Rais wa Jmahuri ya Muungano.
Mzee alisema haikuwa muafaka kusema wajumbe wa tume hiyo uteuzi wao ufanyike kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar, kwa vile suala la ushauri ni jambo la hiari na badala yake kuwepo makubaliano kati ya viongozi hao.
Akizungumzia vurugu hizo, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, alisema waliofanya vurugu hizo ni wahuni.
Alisema kikundi hicho cha wahuni kilikwenda katika mkutano huo kwa malengo maalumu, ili ionekane watu hawataki Muungano.
Aidha, alisema amesikitishwa na kitendo cha watu kuchana nakala za muswada huo na kutoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya jazba, lakini alisema maoni yote yaliyotolewa kamati imeyachukua na itayafanyia kazi.
Wakati huo huo, Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara (TLS), wameukosoa Muswada wa Marejeo ya Katiba unaotarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma kutokana na kuwa na kasoro nyingi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Rais wa TLS Francis Tola, alisema wanatarajia kukutana na Rais Kikwete ili kumshauri juu ya mapitio ya muswada huo.
“Muswada ni mzuri (kwa wazo), lakini una kasoro nyingi, haustahili kupelekwa bungeni na kupitishwa bali wananchi wapewe muda wa kutosha ili kutoa maoni yao kwanza,” alisema.
Alisema muswada huo umepelekwa bungeni kwa mfumo wa hati ya dharula, hivyo ni kama kitendo cha zima moto kinafanywa na serikali ili kupata maoni ya wananchi na wadau mbalimbali kwa muda mfupi.
Rais wa TLS alisema hati ya dharura pia inawanyima uhuru na haki kwa wananchi na wadau mbalimbali wa sheria kushiriki katika kutoa maoni yao kwa muda mrefu.
Alisema kitendo cha kuandaa mijadala ya wazi ya Muswada wa Marejeo ya Katiba kwa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar kwa niaba ya wananchi wa mikoa mingine si haki na usawa.
“Naona serikali inafanya haraka katika jambo hili, na wanachukulia mzaha, haiwezekani ukafanya mijadala katika mikoa hiyo na kuafiki kwamba hayo yaliyotolewa ndiyo mapendekezo ya wananchi wote wa Tanzania.
Tunamtaka Rais Kikwete na Mwanasheria Mkuu kuondoa hati ya dharula, endapo hawatatekeleza pendekezo hilo ni wazi kwamba hakutakuwa na maana nzima ya kupata maoni kutoka kwa wananchi na wadau wengine,” alisema.
Aliongeza kuwa muswada huo una kasoro ya lugha, kutokana na kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza, hali itakayowafanya wananchi wasiofahamu lugha hiyo kutoshiriki kikamilifu katika kutoa maoni.
Alitaja kasoro nyingine ni kupewa jina la Muswada wa Mapitio ya Katiba, lakini unajipinga wenyewe kutokana na kuwa na kifungu kinachoeleza kwamba muswada huo ni wa Kutunga Katiba Mpya.
Alisema kuundwe Bunge la Katiba litakalowajumuisha wadau mbalimbali ambalo litakuwa na jukumu la kuratibu masuala ya Katiba.
 
na Mwandishi wetu, Dodoma

amka2.gif

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais (Muungano) Samia Suluhu Hassan, wamenusurika kipigo baada ya kutokea vurugu kwenye kikao cha kujadili muswada wa mabadiliko ya Katiba mpya visiwani Zanzibar.
Sitta, alikuwa akiwasilisha rasimu ya marejeo ya katiba kwa niaba ya Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, ambapo wakati akitoa mada hiyo hali ndani ya ukumbi ilikuwa shwari.
Vurugu hizo zilitokea katika ukumbi wa Shule ya Haile Selassie mjini Zanzibar jana, baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, kuchangia kwa maneno makali na baadaye kuuchana hadharani muswada huo na kutoka nje ya ukumbi.
Tukio hilo lilisababisha baadhi ya wajumbe kuzichana nakala za muswada huo huku wengine wakinyanyua viti juu wakiashiria kwamba mkutano huo umekwisha na baadhi yao wakimfuata Sheikh Farid nje ya ukumbi wa mkutano.
Kitendo hicho kilisababisha hali ya wasi wasi na kusababisha mtoa mada, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kuondolewa kwenye ukumbi chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Akichangia muswada huo, Sheikh Farid, alisema kabla ya kupelekwa muswada huo visiwani Zanzibar upelekwe wa Katiba ya Tanganyika, ili kuuangalia Muungano ambao hivi sasa haupo kwenye hali nzuri.
Alisema haoni sababu ya kujadiliwa mabadiliko hayo ya katiba kabla ya wananchi wa Zanzibar hawajaulizwa kwa njia ya kura ya maoni iwapo Muungano huo wanautaka au hawautaki.
“Napenda kutoa usia wangu kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya umoja wa kitaifa kuitisha kura ya maoni wananchi waulizwe wanaotaka Muungano na wale wasioutaka”, alisema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu, huku baadhi ya wajumbe wakinyanyua mabango yaliyoandikwa ‘Hatuutaki Muungano Jamani’.
Sheikh Farid, alisema zama za udikteta wa Nyerere zimekwisha, wananchi wa Zanzibar wapo huru kutoa maoni yao na kama serikali inaogopa wananchi wapo tayari.
Naye aliyekuwa Katibu wa Umoja wa Vijana wa Afro Shirazy Party, Baraka Shamte, alisema muswada huo usijadiliwe hadi hapo marekebisho yatakapofanywa na kuundwa jopo la wanasheria kutoka pande zote mbili za Muungano.
Alisema muswada huo uandaliwe upya na yale yanayokosolewa yaondolewe kwa lengo la kufanikisha mpango wa kupata katiba itakayosaidia kuimarisha Muungano wenyewe.
Akichangia muswada huo, Diwani Arafa Mohammed Said, alisema kuna haja ziundwe tume mbili za kukusanya maoni juu ya Katiba mpya, ikiwemo tume ya Tanzania Bara na tume ya Zanzibar .
Alisema kwakuwa Zanzibar wananchi wake ni wachache si vizuri wakaingizwa katika mjadala wa jumla na hatua hiyo ya kuundwa tume mbili itawapa nafasi ya kupata ukweli juu ya kile wananchi wa Zanzibar wanachokitaka.
Mwanasheria, Abdulkadir Mohammed Amour, alisema bila ya marekebisho yanayopigiwa kelele kufanyika, muswada huo iwapo utapitishwa na Bunge mwisho wake utakuwa Kisiwa cha Chumbe na hautahusu Zanzibar.
Askari mstaafu, Miraji Kiongwe, alisema inashangaza tangu kufikiwa Muungano wa mwaka 1964, vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vikiongozwa na wakuu wake kutoka upande mmoja wa Muungano.
Alisema hakuna mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) au Jeshi la Polisi hata mmoja aliyetoka Zanzibar, wakati vyombo hivyo ni vya Muungano.
Akitaja majina ya wakuu waliowahi kuongoza vyombo hivyo, alisema vyombo hivyo havina tofauti na Bunge, kwa vile hakuna spika hata mmoja aliyewahi kuongoza Bunge hilo kutoka Zanzibar.
Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Ibrahim Mzee, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi, (BLW) alisema inashangaza tume zote zilizowahi kuundwa Zanzibar imekuwa ikipewa nafasi ya umakamu na mwenyekiti hutoka upande wa Tanzania Bara.
Alitoa mfano wa tume hizo kuwa ni ile ya Jaji Kisanga, Jaji Nyalali na kutaka utaratibu huo kuangaliwa upya, ili Zanzibar nayo iweze kutoka watu wa kuongoza tume hizo za kitaifa.
Akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo, alisema Bunge la Muungano halina mamlaka ya kutunga katiba na kazi hiyo inatakiwa kufanywa na Bunge la Katiba.
Alisema kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano kazi yake ni kutunga sheria, hivyo kuwepo na Bunge la Katiba na lazima liwe na wajumbe sawa kutoka Zanzibar na Tanzania Bara.
Alieleza kwamba muswada huo una upungufu mwingi na kushauri kuwa unahitaji kuangaliwa upya, ikiwamo mamlaka makubwa aliyopewa Rais wa Jmahuri ya Muungano.
Mzee alisema haikuwa muafaka kusema wajumbe wa tume hiyo uteuzi wao ufanyike kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar, kwa vile suala la ushauri ni jambo la hiari na badala yake kuwepo makubaliano kati ya viongozi hao.
Akizungumzia vurugu hizo, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan, alisema waliofanya vurugu hizo ni wahuni.
Alisema kikundi hicho cha wahuni kilikwenda katika mkutano huo kwa malengo maalumu, ili ionekane watu hawataki Muungano.
Aidha, alisema amesikitishwa na kitendo cha watu kuchana nakala za muswada huo na kutoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya jazba, lakini alisema maoni yote yaliyotolewa kamati imeyachukua na itayafanyia kazi.
Wakati huo huo, Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara (TLS), wameukosoa Muswada wa Marejeo ya Katiba unaotarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma kutokana na kuwa na kasoro nyingi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Rais wa TLS Francis Tola, alisema wanatarajia kukutana na Rais Kikwete ili kumshauri juu ya mapitio ya muswada huo.
“Muswada ni mzuri (kwa wazo), lakini una kasoro nyingi, haustahili kupelekwa bungeni na kupitishwa bali wananchi wapewe muda wa kutosha ili kutoa maoni yao kwanza,” alisema.
Alisema muswada huo umepelekwa bungeni kwa mfumo wa hati ya dharula, hivyo ni kama kitendo cha zima moto kinafanywa na serikali ili kupata maoni ya wananchi na wadau mbalimbali kwa muda mfupi.
Rais wa TLS alisema hati ya dharura pia inawanyima uhuru na haki kwa wananchi na wadau mbalimbali wa sheria kushiriki katika kutoa maoni yao kwa muda mrefu. Alisema kitendo cha kuandaa mijadala ya wazi ya Muswada wa Marejeo ya Katiba kwa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar kwa niaba ya wananchi wa mikoa mingine si haki na usawa.

“Naona serikali inafanya haraka katika jambo hili, na wanachukulia mzaha, haiwezekani ukafanya mijadala katika mikoa hiyo na kuafiki kwamba hayo yaliyotolewa ndiyo mapendekezo ya wananchi wote wa Tanzania.
Tunamtaka Rais Kikwete na Mwanasheria Mkuu kuondoa hati ya dharula, endapo hawatatekeleza pendekezo hilo ni wazi kwamba hakutakuwa na maana nzima ya kupata maoni kutoka kwa wananchi na wadau wengine,” alisema. Aliongeza kuwa muswada huo una kasoro ya lugha, kutokana na kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza, hali itakayowafanya wananchi wasiofahamu lugha hiyo kutoshiriki kikamilifu katika kutoa maoni.
Alitaja kasoro nyingine ni kupewa jina la Muswada wa Mapitio ya Katiba, lakini unajipinga wenyewe kutokana na kuwa na kifungu kinachoeleza kwamba muswada huo ni wa Kutunga Katiba Mpya. Alisema kuundwe Bunge la Katiba litakalowajumuisha wadau mbalimbali ambalo litakuwa na jukumu la kuratibu masuala ya Katiba.
 
Sijawahi kuona Spika ambaye ni stinking pro-CCM kama huyu mama. Nambashiria hatafika mwisho wa Bunge hili.
 
Back
Top Bottom