Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar!

Mwenyekiti wa maimam Zanzibar amesabisha kuvunjika kwa kikao cha kujadili muswada wa rasimu ya katiba pale alipoamua kuuchana muswada huo mbele ya kamati na kutoka nje.... vurugu a kelele zilitawala na watu kuanza kutoka huku wakiimba "hatutaki muungano".

pia imam aligusia swala za kura za maoni juu ya muungano kwanza kabla ya Zanziba kujadili katiba mpya....!

ni wazi kwamba serikali ili-under estimate response ya watu wa Zanzibar juu ya muungano, pia inawezekana serikali illitambua hili na ndio maana hawakutaka wazanzibari wajadili wenyewe bali waje bara (Dar au Dodoma)

Tafakari....

Source: TVZ
Kweli ccm mwaka huu hawana pa kutokea....huku Bara moto,visiwani moto. BIg up wazanzibari kwa kuuchanachana huo muswada wa ccm.
 
Safi sana kwa kuuchana huo muswada big up zenj watakanyika uchomeni moto mbele za media tena bbc na cnn dunia ifahamu fast moto umewaka bongo.
 
Thanx jabulani, ni ndefu lakini nimeisoma.
Summary yangu ni kuwa zanzibar imefanya marekebisho kwenye katiba yake na kupokonya yale yaliyokuwa chini ya Serikali ya Jamh. ya muungano Tz, ilhali viongozi wa SJMT wanajua na wasiseme.
Kwamba Zanzibar inatambulika kama nchi kamili yenye mipaka na jeshi na mahakama.
So?
Kumbe Muungano ushavunjika siku nyingi tu!
 
haya anna makinda sema!huku bara unasema wanasiasa wanawachochea wanafunzi jee huko zenj sheikh kachochewa na nani?
 
Najua maandishi haya ni mengi na huenda yakawachosha kusoma, lakini mwenye muda asome. Hapo ndipo mtakapojua kwamba CHADEMA ina wabunge makini sana. Tundu Lissu aliwahi kuongea bungeni na kwenye mihadhara mbalimbali ikiwamo pale Nkrumah, lakini alipoongea bungeni nakumbuka wabunge wa CCM walibeza na kusema kwamba "MUUNGANO NI IMARA !" Anne Kilango alikuwa mmojawapo akiijibu hoja ya Lissu kwa mifano ya maridhiano ya CUF na CCM. Huenda wabunge wa CCM hawajui maridhiano ya vyama ni kitu tofauti na Muungano wa nchi. Hii hapa chini ni makala ya mbunge mahiri Tundu Lissu:

Muungano wa Tanzania sasa umekuwa dhaifu zaidi - Tundu Lisu.

Rais Kikwete ameficha wananchi ukweli

MUUNGANO wa Tanzania siyo tena kitu kimoja, hasa baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kufanya mabadiliko katika katiba yake kwa kunyofoa baadhi ya mamlaka ya Serikali ya Muungano.

Tunaweza kusema hatua hiyo imechochea mpasuko mwingine katika Muungano.

Katika hotuba yake ya kwanza mbele ya Bunge, 18 Novemba 2010, Rais Kikwete alisema, "Pamoja na changamoto za hapa na pale zinazoukumba Muungano, bado muungano huo ni imara."

Hata hivyo, rais hakueleza alichoita "changamoto za hapa na pale" ni nini. Badala yake, rais aliishia kutufariji kuwa, "…pande zote mbili za Muungano zina dhamira ya dhati ya kutatua kero zilizopo."

Hapa rais hajaeleza ukweli. Hakusema kwamba Muungano ulioasisiwa na viongozi wetu wawili – Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume – umekuwa dhaifu kuliko ulivyokuwa wakati wa uhai wa waasisi wake.

Wala rais hajasema kwa mfano, Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 na Sheria Na. 9 ya 2010, pamoja na kuleta neema ya kuwapo kwa mwafaka kati ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), yamemong'onyoa misingi karibu yote ya Muungano.

Sheria hiyo iliyoanza kutumika 13 Agosti 2010, haikuishia kwenye kubadili sura ya kisiasa Zanzibar kwa kubadilisha muundo wa serikali, bali imebadili sura ya Muungano wenyewe, mipaka yake na muundo wake.

Pamoja na kwamba hali ya kisiasa visiwani Zanzibar imekuwa tete tangu mwaka 1984 ulipoibuka mjadala wa mabadiliko ya katiba uliosababisha kujiuzulu kwa rais wa wakati huo, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, lakini gharama ya mwafaka, inaweza kuwa chanzo kikuu cha kubomoka kwa Muungano na hata tishio kwa usalama wa mipaka ya taifa.

Hii ni kwa sababu viongozi wakuu wa Zanzibar wametumia kivuli cha maridhiano ya CCM na CUF kufanyia marekebisho katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kwa kuingiza ndani ya katiba hiyo mambo ambayo awali yalikuwa chini ya serikali ya Muungano.

Kwa mfano, wakati makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 yalifuta nchi mbili za Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ili kuunda nchi moja, Ibara ya 3 na 4 ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba zinarudisha kuwepo kwa nchi ya Zanzibar.

Sheria hiyo inasema, "Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar."

Vilevile, Ibara ya 4 ya sheria ya mabadiliko ya katiba inasisitiza, "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Rais anajua kuwa mabadiliko haya ya katiba ya Zanzibar ni makubwa na yana athari za moja kwa moja kwa uhai wa Mungano. Lakini hilo hakulisema.

Wala hakusema pia kuwa hatua ya viongozi wa Visiwani kuingiza vifungu vya katiba vilivyoitangaza Zanzibar kuwa "nchi yenye mipaka kamili," tofauti na mipaka ya nchi nyingine iliyokuwa ikiitwa Tanganyika, ni kinyume cha katiba ya Muungano.

Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa. Katiba ilisema, "Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Lakini mabadiliko hayo ambayo rais ameyanyamazia, yameifanya Zanzibar kuwa nchi yenye uhuru kamili. Kwa mfano, Ibara mpya ya 26(1) inayounda "Afisi" ya rais wa Zanzibar inamtaja rais wa Zanzibar kama "… Mkuu wa nchi ya Zanzibar…"

Wakati Ibara ya 2(2) ya Katiba inatoa mamlaka kwa rais wa Jamhuri – kwa kushauriana kwanza na rais wa Zanzibar – mamlaka ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, Ibara mpya ya 2A ya Katiba ya Zanzibar inampa rais wa visiwa hivyo mamlaka hayohayo kwa kufuata utaratibu wa sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Haya yote rais anayafahamu. Lakini hakuyasema.

Hata muundo wa mahakama za juu za Jamhuri, unaathiriwa na mabadiliko haya. Mathalani, Ibara ya 117(3) ya katiba inaipa mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kusikiliza rufaa kutokana na hukumu au maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Neno "Mahakama Kuu" limetafsiriwa na Ibara ya 151(1) ya katiba kumaanisha "Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar."

Kwa maana hiyo, mfumo wa kimahakama wa Zanzibar umeunganishwa na mfumo wa kimahakama wa Muungano katika ngazi ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sababu rufaa dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu ya Zanzibar zimekuwa zinasikilizwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri.

Lakini sasa, sheria ya Mabadiliko ya Katiba imebadili mfumo huu. Ibara mpya ya 24(3) ya katiba ya Zanzibar inasema, kutokana na maombi yanayopelekwa mahakamani kuhusu masuala ya haki za binadamu, uamuzi wa mahakama Kuu ya Zanzibar "… utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania."

Ibara ya 25A ya katiba ya Zanzibar imebadilishwa kwa kusema, rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika masuala hayo zitasikilizwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 24(3)."

Ni ibara hiyo hiyo iliyofuta haki ya rufaa katika mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Jingine ambalo rais hakulieleza, ni kwamba sheria ya Mabadiliko ya Katiba inajaribu kuficha, suala zima la kuwapo kwa majeshi ya ulinzi.

Ibara ya 54(2) ya katiba ya Zanzibar ilikuwa inatambua uwepo wa kilichokuwa kinaitwa, "Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" –Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo (Magereza) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Kifungu hicho sasa kimebadilishwa na kinaitwa, "Idara Maalum."

Vifungu hivi vipya vya katiba ya Zanzibar vinakiuka moja kwa moja Katiba ya Muungano ya mwaka 1977.

Kwanza, vifungu hivi vinahoji muundo wa Muungano na kutishia usalama wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano kama vilivyoainishwa na katiba.

Hii ni kwa sababu, Ibara ya 1 ya Katiba inatangaza wazi wazi kuwa "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano."

Ibara ya 2(1) inatamka mipaka ya nchi hii kuwa ni "… eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo."

Pili, mabadiliko ya katiba yanapora pia matakwa ya katiba kwa kutwaa mamlaka ya Rais wa Muungano kwa mamlaka hayo kujitwisha rais wa Zanzibar.

Katiba inampa rais wa Jamhuri mamlaka ya kugawa mikoa, wilaya na maeneo mengine katika Jamhuri kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge la Jamhuri.

Utaratibu wa kugawa mikoa na wilaya katika Jamhuri umewekwa na Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997.

Lakini mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yamemnyang'anya rais wa Muungano mamlaka hayo na kumkabidhi rais wa Zanzibar ambaye sasa anaweza kugawa mikoa na wilaya za Zanzibar kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Wakati Katiba inamtaka Rais wa Muungano kushauriana na rais wa Zanzibar katika ugawaji wa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar, chini ya sheria ya sasa, rais wa Zanzibar hapaswi kushauriana na mtu yeyote anapogawa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar.

Tatu, mabadiliko ya katiba yaliyofanywa yamekiuka katiba kwa kuinyang'anya Mahakama ya Rufani ya Tanzania mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Chini ya mfumo mpya wa kimahakama unaopendekezwa na "Sheria ya Mabadiliko ya Katiba" hakuna tena muungano wa kimahakama ambao umewekwa na Ibara ya 117(3) ya Katiba.

Nne, kwa kuhalalisha uwepo wa vikosi vya kijeshi vya SMZ vinavyoitwa "Idara Maalum," sheria ya mabadiliko ya katiba imekiuka moja kwa moja masharti ya Ibara ya 147(2) ya katiba inayoipa serikali ya Muungano mamlaka ya "… kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania."

Katiba inasema wazi, kwamba "ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote."

Tano, sheria ya mabadiliko ya Katiba inaingiza mfumo wa uongozi wa Zanzibar ambao hautambuliwi na katiba. Kwa mfano vyeo vya "Makamo" wa Kwanza na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Vyeo hivi havitambuliwi katika katiba ya Muungano.

Hivyo basi, mabadiliko ya katiba ya Zanzibar, siyo tu yanakiuka katiba, bali pia ni batili na hayana nguvu yoyote ya kisheria.

Kufuatana na Ibara ya 64(3) ya katiba, "endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka…."

Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa Ibara ya 64(5), "… Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika katiba hii, katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka katiba, itakuwa batili."

Kutokana na hali hiyo, hicho rais anachosema mafanikio, ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote. Wala hakuna mashaka kwamba marekebisho haya yakifahamika vema kwa baadhi ya wabunge, yanaweza kugeuza maridhiano yaliyofikiwa kuwa balaa, badala ya neema.

Ilikuwa ni vema mabadiliko hayo ya katiba kufuata njia sahihi za kisheria. Yangefanyika kwanza mabadiliko katika katiba ya Muungano kabla ya mabadiliko hayo kufanyika katika katiba ya Zanzibar.

Hili, kwanza lingeondoa manung'uniko, lisingetikisa Muungano na lisingeleta tafsiri mbaya, kwamba kuna watu wanapinga Muungano au maridhiano yaliyofikiwa.

Lakini hicho hakikufanyika. Hivyo basi, maridhiano yaliyofanyika hayana uhalali kisheria, na hivyo hayawezi kukidhi matakwa ya wananchi. Yanaturudisha katika migogoro mingine na mivutano isiyokuwa na sababu kati ya Bara na Zanzibar.

Haya yasingefikiwa iwapo viongozi wetu wangekuwa wa kweli na wangetenda kazi zao kwa uwazi. Lakini hapa wanaonekana walitenda yote haya kwa njia ya kuviziana.

Mwandishi wa makala hii ni mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wakili wa Mahakama Kuu. 0784 511509.
 
Hivi muungano una faida gani kwa pande hizi mbili? kwa anae elewa faida za muungano naomba anielimishe tafadhali, naomba pia nielimishwe ni nani anataka muungano na nani hataki na kwa maslahi gani, nina imani jibu la swali hili litaelimisha wengi tu. somebody help please :yield:
Mkuu! muungano unafaida kwa CCM tu. Faida yao ya kwanza ni wakati wa uchaguzi mkuu....maana wanapata kura nyingi sana za mgombea wao wa urais (kumbuka wazanzibar wanaruhusiwa kumpigia kura mgombea urais kutoka bara,ila sisi wabara haturuhusiwi kumpigia kura mgombea urais wa visiwani) so kwa mtaji huu CCM huwa wanavuna kura nyingi sana kutika Zanzibar. Faida yao ya pili ni pale wahisani wanapotoa misaada kwa ajiri ya watanzania wote,yaani ikiwemo zanzibar (Kumbuka wahisani wanazisaidia hizi nchi za Africa kulingana na idadi ya wananchi) So chama cha mafisadi(CCM) kimejitengenezea mrija mwingine wa kula fedha za wananchi kwa mgongo wa wazanzibar na wabara kwa kujumlisha wingi wetu pale wanapoomba misaada toka nje ya nchi. Kwa ufupi hakuna mtu mwenye faida ya huu muungano isipokuwa ni miCCM yenyewe tu!.....wanafaidika kwa kupata kura za mgombea wao wa urais na kupatia misaada kutoka nje ya nchi.
 
Nadhani ukweli utagundulika muda si mrefu...ukombozi wa Taifa hili umekaribia,mapambano bado yanaendelea na hakuna wa kuyazuhia hata iweje....si JK,EL,wala RA....hukumu kwa waovu yaja na watakinywea kikombe cha hasira ya watanzania....
 
Jamani Ndugu zangu watanganyika ni wakati sasa wa kuvunja huu muungano, nawakilisha hoja.
 
Muungano hausaidii pande zote ni bora kuuvunja sisi bara tuchukue hizo nyumba zao nzuri maeneo ya Namanga na Mbezi Beach
Bila kusahau Azam Ice Cream na maghorofa yake Kariakoo; watakuwa sio Watanganyika na kama sio Mtanganyika hauruhusiwi kumiliki Ardhi

mtu mwenye akili huwa anajituma wala hategemei cha bure. angalia uganda baada ya kuwatimua wahindi wakidhani wanawakomoa na kuchukua mali zao kiko wapi leo. baada ya kuuvunja muungano na kuwatimua wazanzibar nahisi itabidi ushauri tuwatimue wahaya na wachaga warudi moshi ili ufaidi mali zao. itungwe sheria kama mchaga au mnyamwezi marufuku kumiliki ardhi nje ya mikoa yao. nahisi kama tutatumia akili zako finyu huku ndio tutafikia.
KABLA HUJATOA MAONI YAKO SHIRIKISHA UBONGO WAKO.
 
Najua maandishi haya ni mengi na huenda yakawachosha kusoma, lakini mwenye muda asome. Hapo ndipo mtakapojua kwamba CHADEMA ina wabunge makini sana. Tundu Lissu aliwahi kuongea bungeni na kwenye mihadhara mbalimbali ikiwamo pale Nkrumah, lakini alipoongea bungeni nakumbuka wabunge wa CCM walibeza na kusema kwamba "MUUNGANO NI IMARA !" Anne Kilango alikuwa mmojawapo akiijibu hoja ya Lissu kwa mifano ya maridhiano ya CUF na CCM. Huenda wabunge wa CCM hawajui maridhiano ya vyama ni kitu tofauti na Muungano wa nchi. Hii hapa chini ni makala ya mbunge mahiri Tundu Lissu:

Muungano wa Tanzania sasa umekuwa dhaifu zaidi - Tundu Lisu.

Rais Kikwete ameficha wananchi ukweli

MUUNGANO wa Tanzania siyo tena kitu kimoja, hasa baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kufanya mabadiliko katika katiba yake kwa kunyofoa baadhi ya mamlaka ya Serikali ya Muungano.

Tunaweza kusema hatua hiyo imechochea mpasuko mwingine katika Muungano.

Katika hotuba yake ya kwanza mbele ya Bunge, 18 Novemba 2010, Rais Kikwete alisema, "Pamoja na changamoto za hapa na pale zinazoukumba Muungano, bado muungano huo ni imara."

Hata hivyo, rais hakueleza alichoita "changamoto za hapa na pale" ni nini. Badala yake, rais aliishia kutufariji kuwa, "…pande zote mbili za Muungano zina dhamira ya dhati ya kutatua kero zilizopo."

Hapa rais hajaeleza ukweli. Hakusema kwamba Muungano ulioasisiwa na viongozi wetu wawili – Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume – umekuwa dhaifu kuliko ulivyokuwa wakati wa uhai wa waasisi wake.

Wala rais hajasema kwa mfano, Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 na Sheria Na. 9 ya 2010, pamoja na kuleta neema ya kuwapo kwa mwafaka kati ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), yamemong'onyoa misingi karibu yote ya Muungano.

Sheria hiyo iliyoanza kutumika 13 Agosti 2010, haikuishia kwenye kubadili sura ya kisiasa Zanzibar kwa kubadilisha muundo wa serikali, bali imebadili sura ya Muungano wenyewe, mipaka yake na muundo wake.

Pamoja na kwamba hali ya kisiasa visiwani Zanzibar imekuwa tete tangu mwaka 1984 ulipoibuka mjadala wa mabadiliko ya katiba uliosababisha kujiuzulu kwa rais wa wakati huo, Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, lakini gharama ya mwafaka, inaweza kuwa chanzo kikuu cha kubomoka kwa Muungano na hata tishio kwa usalama wa mipaka ya taifa.

Hii ni kwa sababu viongozi wakuu wa Zanzibar wametumia kivuli cha maridhiano ya CCM na CUF kufanyia marekebisho katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kwa kuingiza ndani ya katiba hiyo mambo ambayo awali yalikuwa chini ya serikali ya Muungano.

Kwa mfano, wakati makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 yalifuta nchi mbili za Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ili kuunda nchi moja, Ibara ya 3 na 4 ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba zinarudisha kuwepo kwa nchi ya Zanzibar.

Sheria hiyo inasema, "Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar."

Vilevile, Ibara ya 4 ya sheria ya mabadiliko ya katiba inasisitiza, "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Rais anajua kuwa mabadiliko haya ya katiba ya Zanzibar ni makubwa na yana athari za moja kwa moja kwa uhai wa Mungano. Lakini hilo hakulisema.

Wala hakusema pia kuwa hatua ya viongozi wa Visiwani kuingiza vifungu vya katiba vilivyoitangaza Zanzibar kuwa "nchi yenye mipaka kamili," tofauti na mipaka ya nchi nyingine iliyokuwa ikiitwa Tanganyika, ni kinyume cha katiba ya Muungano.

Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa. Katiba ilisema, "Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Lakini mabadiliko hayo ambayo rais ameyanyamazia, yameifanya Zanzibar kuwa nchi yenye uhuru kamili. Kwa mfano, Ibara mpya ya 26(1) inayounda "Afisi" ya rais wa Zanzibar inamtaja rais wa Zanzibar kama "… Mkuu wa nchi ya Zanzibar…"

Wakati Ibara ya 2(2) ya Katiba inatoa mamlaka kwa rais wa Jamhuri – kwa kushauriana kwanza na rais wa Zanzibar – mamlaka ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, Ibara mpya ya 2A ya Katiba ya Zanzibar inampa rais wa visiwa hivyo mamlaka hayohayo kwa kufuata utaratibu wa sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Haya yote rais anayafahamu. Lakini hakuyasema.

Hata muundo wa mahakama za juu za Jamhuri, unaathiriwa na mabadiliko haya. Mathalani, Ibara ya 117(3) ya katiba inaipa mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kusikiliza rufaa kutokana na hukumu au maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

Neno "Mahakama Kuu" limetafsiriwa na Ibara ya 151(1) ya katiba kumaanisha "Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano au Mahakama Kuu ya Zanzibar."

Kwa maana hiyo, mfumo wa kimahakama wa Zanzibar umeunganishwa na mfumo wa kimahakama wa Muungano katika ngazi ya Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sababu rufaa dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu ya Zanzibar zimekuwa zinasikilizwa na Mahakama ya Rufani ya Jamhuri.

Lakini sasa, sheria ya Mabadiliko ya Katiba imebadili mfumo huu. Ibara mpya ya 24(3) ya katiba ya Zanzibar inasema, kutokana na maombi yanayopelekwa mahakamani kuhusu masuala ya haki za binadamu, uamuzi wa mahakama Kuu ya Zanzibar "… utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania."

Ibara ya 25A ya katiba ya Zanzibar imebadilishwa kwa kusema, rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika masuala hayo zitasikilizwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 24(3)."

Ni ibara hiyo hiyo iliyofuta haki ya rufaa katika mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Jingine ambalo rais hakulieleza, ni kwamba sheria ya Mabadiliko ya Katiba inajaribu kuficha, suala zima la kuwapo kwa majeshi ya ulinzi.

Ibara ya 54(2) ya katiba ya Zanzibar ilikuwa inatambua uwepo wa kilichokuwa kinaitwa, "Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" –Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo (Magereza) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU).

Kifungu hicho sasa kimebadilishwa na kinaitwa, "Idara Maalum."

Vifungu hivi vipya vya katiba ya Zanzibar vinakiuka moja kwa moja Katiba ya Muungano ya mwaka 1977.

Kwanza, vifungu hivi vinahoji muundo wa Muungano na kutishia usalama wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano kama vilivyoainishwa na katiba.

Hii ni kwa sababu, Ibara ya 1 ya Katiba inatangaza wazi wazi kuwa "Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano."

Ibara ya 2(1) inatamka mipaka ya nchi hii kuwa ni "… eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo."

Pili, mabadiliko ya katiba yanapora pia matakwa ya katiba kwa kutwaa mamlaka ya Rais wa Muungano kwa mamlaka hayo kujitwisha rais wa Zanzibar.

Katiba inampa rais wa Jamhuri mamlaka ya kugawa mikoa, wilaya na maeneo mengine katika Jamhuri kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge la Jamhuri.

Utaratibu wa kugawa mikoa na wilaya katika Jamhuri umewekwa na Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997.

Lakini mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yamemnyang'anya rais wa Muungano mamlaka hayo na kumkabidhi rais wa Zanzibar ambaye sasa anaweza kugawa mikoa na wilaya za Zanzibar kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Wakati Katiba inamtaka Rais wa Muungano kushauriana na rais wa Zanzibar katika ugawaji wa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar, chini ya sheria ya sasa, rais wa Zanzibar hapaswi kushauriana na mtu yeyote anapogawa mikoa na wilaya kwa upande wa Zanzibar.

Tatu, mabadiliko ya katiba yaliyofanywa yamekiuka katiba kwa kuinyang'anya Mahakama ya Rufani ya Tanzania mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Chini ya mfumo mpya wa kimahakama unaopendekezwa na "Sheria ya Mabadiliko ya Katiba" hakuna tena muungano wa kimahakama ambao umewekwa na Ibara ya 117(3) ya Katiba.

Nne, kwa kuhalalisha uwepo wa vikosi vya kijeshi vya SMZ vinavyoitwa "Idara Maalum," sheria ya mabadiliko ya katiba imekiuka moja kwa moja masharti ya Ibara ya 147(2) ya katiba inayoipa serikali ya Muungano mamlaka ya "… kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania."

Katiba inasema wazi, kwamba "ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote."

Tano, sheria ya mabadiliko ya Katiba inaingiza mfumo wa uongozi wa Zanzibar ambao hautambuliwi na katiba. Kwa mfano vyeo vya "Makamo" wa Kwanza na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Vyeo hivi havitambuliwi katika katiba ya Muungano.

Hivyo basi, mabadiliko ya katiba ya Zanzibar, siyo tu yanakiuka katiba, bali pia ni batili na hayana nguvu yoyote ya kisheria.

Kufuatana na Ibara ya 64(3) ya katiba, "endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka…."

Zaidi ya hayo, kwa mujibu wa Ibara ya 64(5), "… Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika katiba hii, katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka katiba, itakuwa batili."

Kutokana na hali hiyo, hicho rais anachosema mafanikio, ni bomu linaloweza kulipuka wakati wowote. Wala hakuna mashaka kwamba marekebisho haya yakifahamika vema kwa baadhi ya wabunge, yanaweza kugeuza maridhiano yaliyofikiwa kuwa balaa, badala ya neema.

Ilikuwa ni vema mabadiliko hayo ya katiba kufuata njia sahihi za kisheria. Yangefanyika kwanza mabadiliko katika katiba ya Muungano kabla ya mabadiliko hayo kufanyika katika katiba ya Zanzibar.

Hili, kwanza lingeondoa manung'uniko, lisingetikisa Muungano na lisingeleta tafsiri mbaya, kwamba kuna watu wanapinga Muungano au maridhiano yaliyofikiwa.

Lakini hicho hakikufanyika. Hivyo basi, maridhiano yaliyofanyika hayana uhalali kisheria, na hivyo hayawezi kukidhi matakwa ya wananchi. Yanaturudisha katika migogoro mingine na mivutano isiyokuwa na sababu kati ya Bara na Zanzibar.

Haya yasingefikiwa iwapo viongozi wetu wangekuwa wa kweli na wangetenda kazi zao kwa uwazi. Lakini hapa wanaonekana walitenda yote haya kwa njia ya kuviziana.

Mwandishi wa makala hii ni mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wakili wa Mahakama Kuu. 0784 511509.
 
kwa kweli hata mimi huu muungano sijawahi kuuelewa vyema. na wamezuia hilo kujadiliwa, sijui wanataka kutuambia kuwa sisi ni sawa na watumwa? mtu huru atazuiwaje kujadili jambo linalomgusa kila siku?

hongera sana imam na wazanzibari wote, tuko pamoja angalau katika hili

Mmmh....kumbe hata kwenye siasa maama humo?.... nilifikiri wewe ni ant kikombe tu basi! Anyway nimefarijika kuona tupo pamoja ktk kuikomboa nchi yetu Tanganyika hadi kieleweke....Big up dada
 
....Kwa kuwa wazanzibari wamesema kuwa tumewanyonya kwa muda mrefu..na kwakuwa wazanzibari hawatusaidii chochote,na kwakuwa Tanganyika yetu imefunikwa na hili li-Muungano...Mh muanzisha thread naunga mkono hoja kwa asilimia 100...Ahsante
 
Muungano ni mzigo usiobebeka, hakuna mtu anayefaidika nao zaidi ya viongozi wanafiki, umefika sasa wakati wa kuuvunja, kila mtu aende kwa amani
 
Jamani Ndugu zangu watanganyika wakati sasa wa kuvunja huu muungano, nawakilisha hoja.

WaTanganyika ndio taifa gani? Mimi nilizaliwa Tanganyika, lakini hiyo nchi ilikufa na hakuna mahali ilipo. Rais wake nani? Bunge lake lipi? Bendera yake ipi? Mbona tunakuwa wanafik, hatutaki kusema kuwa nyerere aliiuwa Tanganyika?

Hakuna wa Tanganyika. Tuanze kwa kudai uhuru toka Tanzania, hususan Zanzibar kwani wao ndi wenye nchi. Sisi tuanze kutafuta jina la kuipa nchi tutakayoidai.
 
Naililia nchi yangu Tanganyika, nani wamekupoteza Tanganyika yetu? Bila Tanganyika hakuna muungano.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom