Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hmaster, Apr 8, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu watanzania wenzangu sikutegemea kama zenji wana uchukia muundo wa muungano au muungano wenyewe hadi ninapofuatilia mjadala juu ya muswada huo kupitia TVZ. Sitta anapata wakati mgumu sana kuamini kama kweli zenji ipo hivyo. Sasa hivi Sitta anazungumza nakuomba umtazame!
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  duuu mkuu wengine hatupati we leta habari tuu!
   
 3. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  CCM wanaweza kuwa wameparaganyika kiasi ambacho bado watanzania wengi hawajakifikiria.
  Leo katika Public Hearing ktk hoteli ya Bwawani Zanzibar (ambako Mh. Sitta amejifuta jasho mpaka lesso ikashindwa kuhimili) yameibuka mambo!
  Wazanzibari wanalalamika kuchoshwa na kunapelekeshwa sana katika maswala ya Muungano na wenzao wa Bara. Imedaiwa na kuthibitishwa na Waziri wao wa Sheria kwamba kabla ya kuandaa Muswada unaojadiliwa sana sasa kuhusiana na mchakato wa kupata katiba mpya, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijashirikishwa kiasi cha kutosha na jamaa wameongea kwa hasira ile mbaya.
  Inavyoonekana Mwanasheria Mkuu alipeleka nakala moja tu kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na kutaka maoni ya SMZ wakati ambapo huku Bara Baraza la Mawaziri lilikaa kikao kujadili. Iweje huko Baraza la Mapinduzi lisipelekewe rasmi kuujadili? Ndugu zetu wameuliza.
  Bahati mbaya Sitta naye akataka umaarufu kutoka kwa wazenji kwa kuanza kujisifu oooh!... Rais kanituma huku kwa kuwa mimi ni waziri mzito.. mara ooh...! mimi ni mkweli..! Wapi!...Haikusaidia kitu. Wazanzibar kwa kushirikiana na viongozi wao wanaonekana wamechoka. Sijui wanawaza nini wenzetu wale lakini, kama mawazo hayo yanawakilisha mawazo ya wengi basi ni bora rais JK akakubali mabadiliko makubwa katika muundo wa muungano hata ikiwezekana tuwaache washikaji waende zao na watakachochagua kama wataamua kuungana na Oman au Quatar basi tusiwalazimishe kubaki na wadanganyika sie.
  Tatizo CCM wamekuwa waoga kushughulikia kero wakidhania wanaulinda muungano lakini ukweli ni kwamba Muungano hautatulia hadi watu wamepewa nafasi ya kuujadili na kuchagua wanaungana katika yapi na kuacha yapi. Mambo yanatarajiwa kuendelea tena kesho katika shule ya Haille Selasie.
   
 4. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  ni kama baba anapokuwa hana uwezo wa ku provide kwa familia yake na familia yake ikawa inalishwa na jirani....ndivyo serikali ya ccm ilivyo.
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hali inatisha, nimemsikia waziri Yusuf Mansour pamoja na Ally Saleh...aah kiukweli naanza kuhisi harufu ya dhoruba siku si nyingi na mparanganyiko mkubwa ktj suala hili zima la Katiba. Kuna UHUNI upo ktk hii iitwayo 'public hearing' ya Katiba.
   
 6. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Kwani baraza la mawaziri la Tanzania haliwahusu Wazanzibari? Haya ndiyo matatizo yanayotakiwa kuwekwa sawa katika katiba mpya.Huwezi kuwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano yenye mawaziri kutoka pande zote, baraza la mawaziri lipitishe jambo halafu useme upande mmoja haujashirikishwa.
  Hao mwaziri na wabunge wa JMT kutoka zanzibar wanafanya nini kama siyo kuwawakilisha?
   
 7. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kwa nini jamaa wamekuwa wazito kuruhusu muundo wa Serikali tatu?
  Mpaka leo sijui jamaa kama wanatumia akili wanapoahirisha matatizo ya Muungano kila siku. Wanauenzi Muungano kwa kuogapa kutatua matatizo na kuchukua uamuzi sahihi na mwisho yamejiri yaliyojiri. Na hapa kazi ipo wanajamvi wenzangu wazanzibari wengine hata kuuelewa muswada bado lakini ukisikia wanavyoponda uchakachuaji wa mambo ya muungano utashtuka.
  Sijui watu mwishowe wataamua nini lakini jambo muhimu ninaloliona hapa ni kwamba watu waachwe kujadili Muungano kwa uhuru mpaka watakapofikia muafaka sahihi. Hakuna kisichowezekana Zanzibar as long as CUF na CCM-Zanzibar wameweza kuungana. Hawa jamaa wasiposikilizwa wakaridhika kuna uwezekano mkubwa Muungano ukavunjika kwa gharama kubwa zaidi hapo baadaye.
  Je tunataka Muungano? Kama Ndiyo basi, tuujadili kwa kina pasipo kuacha kitu. Kama hatuutaki basi tukubali kujadili ni namna gani tutatengana pasipo kugombana na kuwadhuru ndugu zetu waliosambaa katika maeneo ya pande tofauti za Muungano.
  Naipenda Tanzania kama ilivyo lakini nachukia zaidi makelele na malalamiko yanayoishia kuvurugana na hatimaye kuchukiana.
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Nadhani hili ndio walikuwa wanaliogopa na kusema mkutano utafanyika Dar tu na waalikwa wataletwa kutoka znz!
  Heko kwa walio komaa na kufanikisha mkutano kupelekwa znz!
   
 9. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi hii serikali inaendeshwa na maharamia wa somalia? mbona hakuna hata moja jema serikali inaweza kufanya kwa usahihi na uhakika?
   
 10. BWANYEENYE

  BWANYEENYE Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na bado CCM watakiona cha mtema kuni kama wamezoea bora liende watachoka maana wakija bara Chadema wamekaba koo wakenda Zenji watu wameshika tumbo!!!!!!!!!!na matatizo mtaani kibao wananchi hasira tupu.....wanasubiri kianzishwe tu wamalizie...........OOOHHH GOD Tupe mwisho mwema na Tz yetuuuu
   
 11. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Mimi sijawahi kupata jibu kamili je Zanzibar wanataka nini hasa? ni kitu gani kikubwa ambacho wanataka na sasa hakipo?
   
 12. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,062
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  ooooohhh! toba,ndio maana wakasema eti muungano hakuna kujadiliwa!! bora wazee wa kubonyeza nao waone jinsi chama chao kilivyo ...serikali imechimba kaburi isubiri kuingia yenyewe ...kule kwetu tuna msemo unasema 'ekalya ako'muzana basheka,keyalile aka'mukama wayo...
   
 13. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huo msemo una maana gani?
   
 14. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Shangaa! Unajua mtu akichoka anaweza kulalamika kupitia njia yoyote hata kama njia hiyo haileti sura halisi ya malalamiko yake. Unajua muundo wa serikali mbili (iwe ni mzuri au mbaya) haueleweki kabisa kwa wananchi. Unawezaje kuwa katika Muungano ukawa na serikali mbili wakati nchi zilizoungana ni mbili?
  Inawezekana Mwalimu alicheza karata hiyo kuepuka nchi kugawanyika haraka kutokana na hali iliyokuwapo wakati huo kama mapinduzi ya tawala kama ilivyokuwa Ghana, Nigeria nk. Ukiwa na serikali tatu jamaa wanaweza kuamua mara moja kutangaza kuchoshwa na Muungano na kuamua kutengana na hivyo kukuacha kiongozi wa Muungano huo ukielea kama ilivyoanguka Urusi. Kwa muundo wa mwalimu unaweza kupunguza hilo ndiyo maana tuko pamoja hadi leo.
  Swala la Baraza la Mawaziri la Muungano kuonekana ni la Watanganyika linatokana na ukweli kwamba ndiyo hilo hilo linashughulikia mambo ya Bara pasipo kubadili sura yake. Hata mimi ningekuwa Mzanzibari ningewaza hivyo hivyo. Kama tunapendana na kuaminiana kiasi cha kutosha basi ni vizuri tuwe na serikali moja na kama hilo haliwezekani basi na tuwe nazo tatu.

   
 15. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Siungi mkono zanzibar kuondoka kwenye muungano ila nasema kuwa kama hawa jamaa wana kero zinazowasumbua kitu ambacho naju kipo basi ni vizuri sana zijadiliwe mapema sana. Zanzibar ni sehemu muhimu sana kwetu..
   
 16. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Viongozi wetu hawaamini kama wananchi wamechoka kuvumilia utumbo wao kwa kisingizio cha kulinda amani. Angalia RA, EL, Karamagi, YM wanavyotajirika kwa fedha zetu wakati wakala wao kama JK, Makinda, Makamba nk wanashangilia. Nani haoni tofauti ya uendeshaji wa Bunge leo na wakati wa Sitta?. Fedha wanazowasaidia mafisadi papa kupora wananchi na baadaye kupewa chao kidogo ili kupata nafasi za uongozi wakidhani ni ujanja watashtuka na kushangaa wakati muda umeshapita. Angalia kauli za Spika kwa mfano, yaani unaona kabisa kawekwa pale na watu fulani na yupo pale kuwatumikia kwa nguvu zote. Sijui naye atasemwa ni mfano wa wanawake walioweza baada ya kuwezeshwa na RA kupata uspika!
  Nchi yetu ina matatizo makubwa na kwa kuwa hatuna patriotism ya kutosha ni wazi katiba nzuri itakuwa njia pekee nzuri ya kuanzia kuisafisha nchi iliyotiwa najisi na wajinga wanaojiona wajanja kwa kujaza matumbo ya mafisadi.

   
 17. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Nafikiri si kweli kwamba ilivyo sasa muungano ni vigumu kuanguka, hapana tungekuwa na serikali moja hapo sawa lakini mbiliii. Kwa muundo ulivyo leo Zanzibar wanaweza tangaza kujiondoa na kusema tangu leo muungano kwishaaa.

  Mie kweli nawashangaa wazanzibar wanalalamika wakati uwezo uko ndani yao, Kwa waTanganyika ndo kugumu ku declare kuvunja muungano maana serikali yao ni virtual.
  Angalia, makamu wa Rais wa serikali ya Muungano akiwa mzanzibari , waziri wa ulinzi mzanzibari, waziri wa mambo ya ndani mzanzibari nk, unafikiri hawa watadeclare kuvunja muungano wakale wapi?? Hata maalim self akiwa rais wa muungano hatokubali kuvunja muungano akale wapi?

  Serikali ya mapinduzi iliyo na wazanzibari kwa asilimia 100% ndo yakuvunja muungano, utawashangaa nao wanajumuika kulalamika wakati guts zimo kitandani mwao zakufanya watakalo.
   
 18. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Hata mimi nisingependa Washikaji waondoke lakini if that is what it takes to have a strong muungano hapo baadaye ni bora. Maana kuna uwezekano kuvunja muungano kwa kuchelewa kushughulikia kero lakini baadaye wakapatikana viongozi wanaojua majukumu yao kwa taifa (na si wauza sura wanaodhania kupanda kwao magari ya kifahari kutawasaidi watu kupata maendeleo) na kujenga Muungano mpya kwa makini na taratibu.
  Umewahi kujiuliza kwa nini sikukuu kama ya Muungano inasherehekewa kwa kukagua gwaride na kupunga mikono badala ya hotuba itakayozungumzia mafanikio halisi na kujibu hoja za kero? Mwananchi anafaidika nini kuona makomandoo wa jeshi lake la ulinzi wanapita mbele ya jukwaa kuu kwa mchakamchaka wakati hana uhakika wa kusafirisha bidhaa zake kutoka Zanzibar na rais wa jamhuri hajatoa maelezo yoyote kuhusiana na kero za aina hiyo?
  Kwa nini hatutaki kuwaelewesha wananchi sababu za Muungano kuwa katika sura hii iliyopo ambayo kwao ni ngumu kuelewa mpaka sasa? Kwa nini serikali moja haiwezekani na kwa nini tatu haziwezekani pia? Kuna mawaziri wanalipwa mishahara ya kufuru kwa madai wanashughulikia Muungano tu lakini hadi leo watu bado wanakaguliwa Bandarini na kutozwa kodi inayodaiwa ilipunguzwa wakati bidhaa zinaingia Zanzibar kutoka nje. Je ni lazima sana kuwa na aina hiyo ya taratibu wakati mtu anaenda sehemu moja ya muungano kutotoka upande wa pili?
  Serikali zetu hasa ya Muungano imekuwa inaendesha mambo mengi kama genge fulani tu la wahuni wanaotaka kutajirika saana kuliko wengine kwa kupitia uvumilivu wa watu hao kama mwanya. Watu wengi tumechoka and so are the Zanzibaris.

   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huwezi kujuwa wanataka nini kwasababu wakati wewe mwenyewe hujuwi kitu gani kilichopo!
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duuhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!111
   
Loading...