Muswada Katiba Mpya, Hoja ya Muungano moto Zanzibar!

Tukivunja muungano wazenji watahangaika sana.Sasa hivi wanaona oa sababu tumewaachia wanavinjari huku bara waache mchezo bana alh!
 
We need one Government or Three Governments.
Nani anatetea maslahi ya watanganyika katika huu muswada?
 
Muungano ulikuwa uamuzi wa viongozi wa nchi mbili kuamua kuungana for the common good...na kwa sababu hiyo common good haiwi experienced na upande mmoja, there is no need to continue with system that hurts and burdens one side....kama ndoa inavunjwa kwa kukosekana kwa common good...sembuse muungano ambao ni suala la makubaliano na maamuzi....kama sisi watanganyika hatuoni faida ya muungano tuendelee tu kuumia kwa sababu kuna wachache wenye mamlaka wana some interest in this monster unity? Watanganyika let us think, and reflect, what have we benefited from Muungano? It is like we have n0o rights of our own while Serikali ya Zanzibar is both autonomous na pia serilaki ya Muungano...sisi ni serikali tu ya Muungano, with no autonomy....
 
Sisi wazanzibari tunathamini msimamo wa CHADEMA kuhusu katiba. Hilo halipingiki na watanganyika wengi hawautaki mswada huu.
 
Since Zanzibar is autonomous hakuna sababu Tanganyika isiwe autonomous pia...sio tu kubaki katika package na Muungano while yule uliyeungana naye ana autonomy yake...sasa Tanganyika imeungana na nani? Or muungano is only at certain aspects or certain levels...if that is the case, then it should not be called muungano bali cooperation. We must wake up and katiba ndio inatakiwa ku-address issues nyeti kama hizo
 
wazenji wamejichokaaaaa. Tukiuvunja wao wataumia zaidi, muda si mrefu mapinduz yatafanyika shein out, kama misri tu
 
Nikiuangalia muungano katika World Politics Persperctives nachelea kuungana na wote wanaotaka muungano huu uvunjwe, huu sio muda wa kuuvunja muungano bali ni muda wa kuuimarisha zaidi muungano kuliko wakati wowote ule uliopita. Nchi zote duniani zenye kuona mbali zinazungumzia kwa namna moja au nyingine kuungana sio kutengana,katika misingi hiyo sioni faida yoyote ya kuvunja muungano bali kuuimarisha uwe bora zaidi.Wazanzibar wanaotaka muungano uvunjike ni wanasiasa wachache wenye uroho wa madaraka tu, naamini wazanzibar wa kawaida wanautaka muungano na ni kweli muungano ni muhimu sana kwa pande zote mbili, japo ni imani yangu binafsi kwamba wazanzibar wanafaidi sana muungano kuliko wabara.Sudan ya kusini imejitenga, sio kwa sababu wanapenda kujitenga la hasha ni kwa sababu ya wenzao wa kaskazini kutowathamini, na ndio maana wanazungumzia kujiunga na Jumuiya ya Afrika mashariki na baadaye East African Federation, kwa kuwa wanaelewa umuhimu wa umoja.Hivi vi nchi vidogovidogo tena maskini katika dunia ya sasa vtaishia kuwa watumwa tu wa nchi za magharibi. Kama kweli waznz katika kujadili muswada wa katiba mpya waliuchana muswada na kuondoka katika mkutano sioni kama huo ni ustaarabu zaidi ya upumbavu, kwa kuwa pale kilichohitajika ni nguvu ya hoja na wala sio hoja ya nguvu.Tuuzungumzie muungano kwa nia ya kuuboresha sio kuubeza wala kuuvunja, na mwingine eti badala ya kutoa hoja yeye anamlaumu nyerere si ujinga huo, nyerere yeye alifanya kazi yake nzuri kwa mujibu wa wakati wake na amekwishajiondokea.Tujenge hoja tuache ubabaishaji.
 
Safi sana...unajua sometimes wazanzibar kichwani zikiwa yes wanafanya mambo ya maana sana....
Sisi wenyewe hatuutaki muungano, na aliyeauandaa muswada bila ya kuwashirikisha ni genious fulani hivi kwani alijua kitakachofuata.
Much thanx to him na wazanzibar kwa ujumla
Yes, I agree 400 percent. Nawashukuru sana Wazanzibar, tena saaaana, kwa kukataa hili li Muungano. I couldn't thank you enough.

Bara ndio tunang'ang'ania Muungano, sijui kwa faida gani, no clue. Tumeshapikwa tukaiva Nyerereism hatuwezi ku question anything he ordained.
 
Nikiuangalia muungano katika World Politics Persperctives nachelea kuungana na wote wanaotaka muungano huu uvunjwe, huu sio muda wa kuuvunja muungano bali ni muda wa kuuimarisha zaidi muungano kuliko wakati wowote ule uliopita. Nchi zote duniani zenye kuona mbali zinazungumzia kwa namna moja au nyingine kuungana sio kutengana,katika misingi hiyo sioni faida yoyote ya kuvunja muungano bali kuuimarisha uwe bora zaidi.Wazanzibar wanaotaka muungano uvunjike ni wanasiasa wachache wenye uroho wa madaraka tu, naamini wazanzibar wa kawaida wanautaka muungano na ni kweli muungano ni muhimu sana kwa pande zote mbili, japo ni imani yangu binafsi kwamba wazanzibar wanafaidi sana muungano kuliko wabara.Sudan ya kusini imejitenga, sio kwa sababu wanapenda kujitenga la hasha ni kwa sababu ya wenzao wa kaskazini kutowathamini, na ndio maana wanazungumzia kujiunga na Jumuiya ya Afrika mashariki na baadaye East African Federation, kwa kuwa wanaelewa umuhimu wa umoja.Hivi vi nchi vidogovidogo tena maskini katika dunia ya sasa vtaishia kuwa watumwa tu wa nchi za magharibi. Kama kweli waznz katika kujadili muswada wa katiba mpya waliuchana muswada na kuondoka katika mkutano sioni kama huo ni ustaarabu zaidi ya upumbavu, kwa kuwa pale kilichohitajika ni nguvu ya hoja na wala sio hoja ya nguvu.Tuuzungumzie muungano kwa nia ya kuuboresha sio kuubeza wala kuuvunja, na mwingine eti badala ya kutoa hoja yeye anamlaumu nyerere si ujinga huo, nyerere yeye alifanya kazi yake nzuri kwa mujibu wa wakati wake na amekwishajiondokea.Tujenge hoja tuache ubabaishaji.
Mike muungano huu haukuwa kwa ridhaa ya wananchi, ni mapatano kati ya Nyerere na karume. Sasa wakati umefika wananchi ndio waamue kama wanauhitaji au la, wasitupelekeshe sisi.Huwezi kulinganisha E.A.C na huu muungano wa kiini macho.
 
Msije kujidanganya kama wazanzibari wanataka muungano.Tokea asubuhi wazanzibari hawakutaka muungano, na wala haitofikia siku wakaingiwa na wazimu wa kutaka muungano.Especially hawaoni faida hata moja kwa nusu karne sasa.

Kinachofanyika ni kulazimisha kimfumo aidha turufu za kisiasa au kijeshi kuiweka Zanzibar chini ya muungano.Huo ndio ukweli wa mambo, mengine ya kuwauliza maoni ya katiba bila ya suala la msingi juu ya muungano ni pumba tupu!
 
WanaJF Kumbe Kikwete anatuonea sisi wabongo-mara Tambwe alete watoto wa shule kufanya fujo kwenye mkutano wa kukusanya maoni, mara mabomu Dodoma kwa wanafunzi wa UDOM ati CDM wanahamasisha fujo nk. Haya sasa amekutana na majabali ya ZBR tangu mlalahoi mpaka vigogo wa serikali ya SMZ na Maimamu na Masheikh wote lao moja!!!!!!!!!!!!!!!! Ile ndiyo ndiyo NGUVU YA UMMA!!!!!! Manasheria wa SMZ amemtahadhaharisha Kikwete kwamba akiipeleka bungeni na kuipitisha amevunja katiba zaidi ya kwamba amekwishaivunja na kudharau SMZ na wananchi wake kwa kutowashirikisha katika maandalizi ya mswada. Sasa amebaki na au kusuka au kunyoa lakini la msingi amekwama mkwamo hasa!!!!!!!!!!
Kitendo cha kuchana nakala za mswada kwenye mkutano mbele ya kamati ya ****** ni UJUMBE TOSHA kwa Kikwete kama ana akili!!!! Jamani Kikwete yaani hata kusoma alama za nyakati ni tabu; ndiyo maana sasa hivi amekabwa na matatizo kibao-CCM vipande vipande, nk
 
Written by mkulima // 09/04/2011 // Habari // No comments

*Wasema imeegemea upande mmoja wa Muungano
*Wahoji kutoshirikishwa SMZ katika maandalizi yake
*Wasema haiwahusu kwa kuzuiwa kujadili Muungano
*Wajipanga kuunda Kamati yao kukusanya maoni hayo
*Walazimisha Mkataba wa Muungano kuwa msingi
Na Mwantanga Ame
WANANCHI wa Zanzibar wameipinga rasimu ya uandaaji wa Tume itayoandaa Katiba mpya ya Muungano, wakidai haiko kihalali na pindipo serikali ya Muungano ikiifisha Bungeni itakuwa imekiuka Katiba ya Muungano.
Maoni hayo waliyatoa jana mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, inayoratibu maoni ya kuweza kupatikana mswaada wa sheria wa kuweza kukusanya maoni ya wananchi juu ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania, mjadala ambao umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Mjadala huo ambao uliwashirikisha viongozi wa serikali ya SMZ, vyama vya siasa na Jumuiya binafsi, wameipinga rasimu hiyo huku wakionekana kuchukizwa nayo kutokana na sehemu kubwa ya mjadala huo ukichangiwa kwa jazba na maoni makali.
Kila kiongozi aliyepata fursa ya kutoa maoni alitamka wazi wazi kuikataa rasimu hiyo na kutaka irudishwe ilipotoka kutokana na kushindwa kuishirikisha Zanzibar kikamilifu katika maandalizi yake kiasi ambacho haina matakwa ya yanayohusu Zanzibar na Rais wa Zanzibar hakuwekwa kama ni mtu muhimu katika uundaji wa Tume hiyo.
Othman Masoud Othman (Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar)
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud, akitoa mchango wake alisema kuwa Bunge liliopo halina uwezo wa kuunda Bunge la katiba, huku akitaka aonyeshwe madaraka hayo yako ibara gani.
Alisema sheria ziliopo zinaelekeza ni namna vilivyotowa uwezo katika kifungu cha 68 ambacho kinatoa mamlaka ya kufanyika kwa marekebisho ya Katiba na sio kazi kuunda sheria.
Alisema jambo ambalo walitakiwa kulifanya kama serikali katika kuunda sheria hiyo walitakiwa kuwepo mapatano kati ya serikali mbili na kinyume cha hivyo watakuwa wanavunja Katiba ya Muungano.
Abukar Khamis Bakary
Alisema sio kweli kama serikali ya Muungano iliihusisha vilivyo serikali ya Zanzibar katika uandaji wa mswada huo kwani hata utaratibu uliotumika ulionekana haukuwa wa kawaida kutokana na mwanasheria wa serikali ya Muungano kumuandikia Mwanasheria wa Zanzibar barua kutaka mapendekezo ya Zanzibar.
Alisema kiutaratibu Waziri Mkuu alitakiwa kumuandikia Makamu wa Pili wa Rais na kumuelezea nia yao lakini hata barua waliyotuma ilikuwa na kasoro huku ikishindwa kuyazingatia mambo ya Zanzibar 14 waliyopendekeza na badala yake kuyaingiza mambo mawili ambayo yanawakandamiza Wazanzibar.
Alisema kilichotakiwa serikali ya Muungao kusema kama iliyapata mapendekezo ya Zanzibar lakini baada ya kuyapata walikaa kimya huku wakiengeza mapya manne ambayo SMZ hiyajui wala Wajumbe wa Baraza la wawakilishi.
Hamza Hassan Juma Mwakilishi (Kwamtipura)
Mwakilishi wa Kwamtipura Hamza Hassan Juma, akitoa mchango wake alisema mswada huo bado haujafikia muda wa kupelekwa Bungeni kwani serikali ya Zanzibar haijashirikishwa kikamilifu na kutaka mjadala wake usiharakishwe.
Alisema mswada huo kwa vile utakuwa na sehemu inayohusu Zanzibar ulitakiwa upelekwe katika Baraza la Mapinduzi kabla ya maandalizi yake ili uweze kujadiliwa na Zanzibar iweze kutoa mapendekezo yake vipi tume hiyo iweze kuundwa.
Kinachotakiwa kuona mswada huo unamshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar huku baadhi ya vipengele vyake vilitakiwa kumpa hadhi Rais wa Zanzibar kutokana na suala litalofanywa litahitaji kuihusisha Zanzibar.
Mansour Yussuf Himid (Kiembesamaki)
Alisema kuletwa kwa mswada huo ni kudanganywa kwa Wazanzibar, akiita siku ya jana kuwa ni siku ya huzuni kwa Wazanzibari.
“Siku hii ya leo (jana), kamati ya Bunge imekuja kutudanganya Wazanzibari na siku ya leo (jana) ni huzuni kubwa sana, kama Mtanzania kama Mzanzibari naona tunafanyiwa kiini macho, kama Baraza la Wawakilishi hatujashirikishwa, basi hakuna haja ya kukubali hilo”, alisema Mansoor.
“Lazima tushirikishwe ipasavyo na Muungano huu tumeungana kwa hiari sisi tumekwenda katika Jamhuri wenyewe hii ni Jamhuri ya pande mbili tumekwenda kwa hiayari tutarudi kwa hiyari tutabaki kwa hiyari”, alisema Mansoor.
Alisema hiyo ni nafasi pekee ya kuhakikisha Muungano unafanyiwa marekebisho kwani kukaa bila ya kukataa hilo hiyo ni fursa ya mwisho ambayo wananchi wa Zanzibar hawataipata tena iwapo mswada huo ukenda Bungeni na kupitishwa.
“Hii ndio fursa yetu ya mwisho Wazanzibari na kwamba tukicheza hapa ndio basi hatutakiona kitu chochote ndio basi tena” ,alisisitiza.
Mohmoud Abdulla Musaa (Kikwajuni)
Alisema haiwezekani kubakia na mfumo unaotaka kutumiwa na Bunge kutokana na kuwa haujazingatia matakwa ya Zanzibar.
Omar Dadi Shajak
Akitoa maoni yake alisema ndani ya mswada huo kinachoonekana umeandaliwa kama sheria nyenginezo zilizopelekwa Bungeni na kusahau kuwa Zanzibar ina mamlaka yake na kinachoonekana ni kuzingatia maoni ya upande mmoja pekee.
Alisema kuwa aina iliyotumiwa katika maandalizi ya rasimu hiyo Zanzibar haiwezi kukubaliana nayo kwani imefanywa kama ni mshiriki na ni vyema ikarejeshwa katika kiti cha Bunge.
“Wameiweka mashariki kwenye jua kali ili kipa asiweze kuona wapate kutufunga hili halikubaliki kwani kutompa mamlaka Rais wa Zanzibar kushauriana na Rais wa Muungano hili ni hatari na Rais wa Muungano atakuwa anamuamulia Rais wa Zanzibar” , alisema Dk. Shajak.
Katibu Mkuu huyo, alikosoa kipengele kinachoipa mamlaka Tume itayoundwa baada ya kukamilisha kazi yake ripoti itayoiandaa kukabidhiwa Rais wa Muungano pekee na badala kutaka ripoti hiyo wakabidhiwe marais wote kwani Muungano ni wa nchi mbili.
Alisema hatua hiyo itaweza kuwasaidia viongozi hao kuweza kukaa na kuiangalia kwa pamoja na badae kutoa mapendekezo yao kama viongozi wa nchi mbili balada ya Rais wa Muungano pekee.
Ali Saleh (Alberto)
Mwandishi huyo wa habari Muandamizi wa Shirika la BBC, alisema muswada huo haukugusa katiba ya Zanzibar hivyo ni kuzarau makubaliano ya Muungano ambayo yapo mambo yangepaswa yawemo haki za binadamu lakini jambo la kusikitisha halijaumuishwa.
“Kura ya maoni ni kitu gani je! Wazanzibari wakisema hawataki athari yake itakuwa nini? tusifikiri Wazanzibari watapinga katiba je! athari zake zitakuwa ni nini? Na kuhojia kwanini Tume hiyo isipelekwe mahkamani, akisema huko ni kuizuiya Demokrasia”.
Alisema mabadiliko hayo yamekuwa ni mazowea kutoka upande mmoja wa Muungano ndio maana watu hawashirikishwi ambapo alisema ni lazima katiba ibadilishwe na huo ni wajibu wa baraza la Wawakilishi.
Hassan Nassor Moyo
Akitoa mchango wake alisema wakati umefika hivi sasa wa serikali ya Muungano kukubali kuwapo kwa mabadiliko katika mambo ya Muungano na kuacha kung’anag’ania mambo waliyozoweya.
Alisema mambo waliyofanya miaka iliopita wakati wa kina Lusinde, Hassan Moyo na Sitta, hivi sasa hayapo tena na wasizuie kuwapo kwa mabadiliko kwani kazi yao imekwisha na watafanya makosa kuzuia mambo ya Muungano Wazanzibari waasiyajadili katika katika mpya.
“Haiwezekani hata kidogo wapewe nafasi waseme kwani hili nalisema ndani ya moyo wangu Nyerere alikuja Zanzibar na karatasi ina mambo 11, mimi nilikuwa Waziri wa Sheria alinipa faili na hakuna hata sentesi moja iliotolewa leo tunaambiwa kuna mambo 22 na Jumbe alipotaka kuengeza alifukuzwa kazi, sasa mnaposema tusizungumze mambo ya Muungano maana yake nini mnawaambia nini Wazanzibari”,alisema Mzee Moyo.
Alisema amesikitishwa kuona Mwanasheria wa Zanzibar kueleza kuwa hana taarifa ya mswada huo jambo ambalo ni la maajabu kwa serikali kwani kinachotengenezwa ni katiba mpya na sio kutia viraka na ni vyema kamati hiyo ikapeleka ujumbe wa Wazanzibari nini wanachotaka.
“Mnasema tusiseme mnataka tuzungumze utumbo, lazima mabadiliko yafanywe kwani hivi sasa vijana wamesoma na hawakubali kuamuliwa, Nyerere alikuwa anakubaliana na mzee Karume hakua anatoa maamuzi, Wewe sita umefanya kazi na Nyerere, Jumbe na Karume msifanye mambo ya wakati ule ‘is over’ ”, alisema Mzee Moyo.
Ali Mwinyi Msuko
Kada huyo wa CCM, alisema wanasheria wa Zanzibar wakae na wanasheria wa Tanzania bara kuupitia upya mswada huo na hakuna sababu ya kuharakisha kupelekwa Bungeni, rais Nyerere na Karume walikubaliana katika Muungao huo na kwa sasa nchi mbili hizi zikubaliane.
Alishauri kwamba mswada huo urudi tena Bungeni na ufuate taratibu kwa kisheria na kwa sasa hakuna sababu yeyote ya kujadiliwa huku akitoa mfano kwamba kujadili mswada huo ni sawa na kutwanga maji kinuni.
Salum Bimani
Mkereketwa huyo wa CUF, alisema anashangazwa na Waziri Sitta kutokana na kujipa maadaraka ya kuandaa taratibu za kuingiza Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki jukumu ambalo halikupata ridhaa ya wazanzibari,
Ali Omar NCCR Mageuzi
Alisema kinachoonekana ni muendelezo wa serikali ya Muungano kuiburuza Zanzibar kwa kuona kuwa haiwashikishi katika mamaunzi makubwa.
Hamad Mussa Yussuf (CHADEMA)
Alisema madaraka ya wananchi yapo mikononi mwao na inashangaza kuona bado serikali ya Muungano imekuwa ikiamua bila ya kuishirikisha Zanzibari.
Awadh Ali Said
Alisema baada ya miaka 50, Wazanzibari wanataka kujua Muungano umewaletea tija gani na una kasoro gani.
Alisema licha ya kuwa hakuna uwiano lakini yeye hakubaliani na hilo kwa kuwa lazima maslahi ya pande mbili yazingatiwe huku akilaumu kwamba mswada huo unaonekana ni wa upande mmoja wa Muungano wakati kuna nchi mbili zilizoungana.
Sheikh Azan Khalid Hamdan
Alisema ipo haja Tume hiyo ikarudi na mswada huo kwani Wazanzibari hawautaki na wanaweza wakasababisha kutokea kwa mgogoro na atahakikisha wanawaeleza waumini wao kuukataa.
Sheikh Muhidini Zubeir Muhidini
Alisema watawaeleza Maimamu wa misikiti yote waukatae mswada huo na watahakikisha wanapinga hadi kwenye madrasa na kuwashawishi Wabunge wa Zanzibar watoke katika Bunge kama rasimu hiyo itajadiliwa na kama watabakia wasirudi Zanzibar.
Salama Aboud
Alisema serikali inahitaji kuyaangalia mahitaji ya Wazanzibari kwani kinachoonekana hakuna uwiano uliotumika katika kutayarisha rasimu hiyo.
Mohammed Ahmed Mugheiry
Alimtatahadharisha Waziri Sita kutokana na kumuona kuwa anacho kifanya kitamharibia sifa yake kwani wanapaswa kutambua kuwa serikali iliopo imechaguliwa na wananchi na hivi sasa Zanzibar kuna serikali ya umoja ya kitaifa ambayo tayari imekaa vizuri.
Samuel Sitta
Akiwasilisha madhumuni na sababu za mswaada huo Samwel Sitta alisema mswada huo umependekeza kutungwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya nchi ya mwaka 2011 ambapo mswada unakusudia kuanzishwa kuweka masharti uanzishaji wa tume pamoja na sekretari kwa madhumuni ya kuendesha na kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mchakato wa mabadiliko ya katiba pamoja na muswada pamoja na masuala mengine utaangalia chimbuko na mahusiano ya katiba iliyopo kwa kuzingatia uhuru wa wananchi mfumo wa siasa ambao unatarajiwa kukamilika Aprili 1014.
Alisema pindi mswada huo utakapopitishwa na kuwa sheria utakuwa na utaratibu wa kisheria utakaomwezesha rais kuunda tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba na kuunda bunge la katiba kwa madhumuni ya kutunga katiba mpya.
Sitta aliwataka Wajumbe hao kushirikiana na Kamati hiyo kuwashawishi wananchi kukubaliana nayo na itapofikia wakati watoe maoni yao kwani wamelazimika kufanya hivyo kutokana na hivi sasa wanataratajia kuwasilisha kupata bajeti inayokadiriwa kufikia bilioni 30 na mwezi huu wa nne itakuwa ni wa matayarisho ya Bajeti hiyo.
Hata hivyo Sitta aliahidi kuyafikisha maoni ya Wazanzibari kama yalivyotolewa katika mkutano huo.
Wakati watu wakichangia hamasa na jazba zilitanda huku wakipiga makofi ya kukataliwa mswada huo na kuimba nyimbo ya ‘sisi sote tumegomboka kwa ndugu’

Muungano hatuutaki tena umejaa udanganyifu mwingi.

Tanganyika nyuma ya Pazia la Tanzania matapeli na Serekali yenu."]
 
Mtoto akiwa mkorofi usimwazibu wakati hajatenda kosa. Msubilie pale atakapotenda kosa hapo hapo muanzishie adhabu ya nguvu. Zanzibar naona wanakaribia kutenda kosa na kwa sababu tunajua ni wakorofi basi hapo ndo watajua kwamba sisi ni watawala wao. Tunasubiri siku wakitangaza wamejitenga, ndo watajua kwamba sisi ni nchi na wao ni mkoa. Sijui watakimbila wapi tena na hiyo bahari. Hamtaki muungano au hamutakaki muungano na Tanganyika ila na Waarabu. Akili zote za wazazibari zipo Uarabuni. Jaribu muone
Mkuu.

CCM ndio wamekuwa na kauli kama hizi zako. lakini kama umezisoma sababu zao za kuukana au kuukataa mswada unaotajwa basi wametoa sababu nzuri tu, tena ni sababu ambazo kwa miaka mingi wamekuwa wakizitoa, lakini CHAMA kushika hatamu ilitumika kuwaburuza.

wakati unasema tutawashughulikia wao, na hawa waliopo Tanganyika, CDM, na wananchi wanaoupinga mswada huu mtawafanya nini?

Lakini kauli yako inajibu hoja ya watu humu wanaosema wazenj wana kila kitu ,kwa nini hawatangazi kujitenga?
Wale wanaotaka kujua ugumu basi wasome mchango wako, wataelewa. Kuwa muungano unalazimishwa kwa wazanzibar, si kitu wanachokitaka katika muundo huu uliopo na kwa namna unavyoendeshwa.

Wamepiga kelele, mayowe kuwa wanaburuzwa, wanabanwa....sasa wanasema enough is enough.
Uzuri ni kuwa mswada huu sio kuwa unakataliwa Zanzibar tu lakini pia na majority ya wananchi wa Tanganyika aka Tanzania bara.

sasa tutaliamrisha jeshi liwatende vibaya wazenj? ....NATO na US wanaanza ku-draft No-fly zone!!!! Umeshalifikiria hili?
Mkuu. Usijidanganye , na watanzania wa leo sio wale mwaka 2000 au 2005.
 
Wazanzibari hawataki kujadili katiba wanataka kujadili muungano tu,kwa sababu zanzbar tunayo katiba yetu ambayo inaongoza nchi ya zanzibar,ndio huu mswaada tukaupinga,kutokana hauruhusu kujadili muungano.
 
kama muswaha haukutaja KAdhi na OIC. ni ovias utakataliwa na wala-urojo

Mkuu.
CHADEMA pia wanaukataa kwa sababu kama ulizozitaja hapa? Au CHADEMA ni wala urojo?
Last time I checked muswada huu unapingwa na wengi, Tanganyika na Zanzibar.

Kama wewe si mmoja ya wanaoupinga mswada huu basi ni wazi wewe ni kada wa CCM, tena katika wale wachache wanaovuna shamba la bibi. Huku mkijificha nyuma ya pazia la Muungano.

Sasa watanzania, watanzania bara, wazanzibari, watanganyika wametambua mbaya wao ni nani. Mnaweza kukawilisha mwenendo wa mageuzi lakini kwa ujanja wenu mtasombwa na tsunami ya mageuzi.

Someni alama za wakati na mpate hekima kuiepusha kuiingiza nchi katika machafuko kwa kufuata matakwa ya umma.
Usanii na ubabaishaji hautawasaidia katika kipindi hiki.
 
218173_10150146350811176_721596175_6946051_3575373_n.jpg na mie nasema vunjaaa vunjaa,tujipange upya
 
WANANCHI wa Zanzibar wameipinga rasimu ya uandaaji wa Tume itayoandaa Katiba mpya ya Muungano, wakidai haiko kihalali na pindipo serikali ya Muungano ikiifisha Bungeni itakuwa imekiuka Katiba ya Muungano.
Maoni hayo waliyatoa jana mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, inayoratibu maoni ya kuweza kupatikana mswaada wa sheria wa kuweza kukusanya maoni ya wananchi juu ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania, mjadala ambao umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Mjadala huo ambao uliwashirikisha viongozi wa serikali ya SMZ, vyama vya siasa na Jumuiya binafsi, wameipinga rasimu hiyo huku wakionekana kuchukizwa nayo kutokana na sehemu kubwa ya mjadala huo ukichangiwa kwa jazba na maoni makali.
Kila kiongozi aliyepata fursa ya kutoa maoni alitamka wazi wazi kuikataa rasimu hiyo na kutaka irudishwe ilipotoka kutokana na kushindwa kuishirikisha Zanzibar kikamilifu katika maandalizi yake kiasi ambacho haina matakwa ya yanayohusu Zanzibar na Rais wa Zanzibar hakuwekwa kama ni mtu muhimu katika uundaji wa Tume hiyo.
Othman Masoud Othman (Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar)
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud, akitoa mchango wake alisema kuwa Bunge liliopo halina uwezo wa kuunda Bunge la katiba, huku akitaka aonyeshwe madaraka hayo yako ibara gani.
Alisema sheria ziliopo zinaelekeza ni namna vilivyotowa uwezo katika kifungu cha 68 ambacho kinatoa mamlaka ya kufanyika kwa marekebisho ya Katiba na sio kazi kuunda sheria.
Alisema jambo ambalo walitakiwa kulifanya kama serikali katika kuunda sheria hiyo walitakiwa kuwepo mapatano kati ya serikali mbili na kinyume cha hivyo watakuwa wanavunja Katiba ya Muungano.
Abukar Khamis Bakary
Alisema sio kweli kama serikali ya Muungano iliihusisha vilivyo serikali ya Zanzibar katika uandaji wa mswada huo kwani hata utaratibu uliotumika ulionekana haukuwa wa kawaida kutokana na mwanasheria wa serikali ya Muungano kumuandikia Mwanasheria wa Zanzibar barua kutaka mapendekezo ya Zanzibar.
Alisema kiutaratibu Waziri Mkuu alitakiwa kumuandikia Makamu wa Pili wa Rais na kumuelezea nia yao lakini hata barua waliyotuma ilikuwa na kasoro huku ikishindwa kuyazingatia mambo ya Zanzibar 14 waliyopendekeza na badala yake kuyaingiza mambo mawili ambayo yanawakandamiza Wazanzibar.
Alisema kilichotakiwa serikali ya Muungao kusema kama iliyapata mapendekezo ya Zanzibar lakini baada ya kuyapata walikaa kimya huku wakiengeza mapya manne ambayo SMZ hiyajui wala Wajumbe wa Baraza la wawakilishi.
Hamza Hassan Juma Mwakilishi (Kwamtipura)
Mwakilishi wa Kwamtipura Hamza Hassan Juma, akitoa mchango wake alisema mswada huo bado haujafikia muda wa kupelekwa Bungeni kwani serikali ya Zanzibar haijashirikishwa kikamilifu na kutaka mjadala wake usiharakishwe.
Alisema mswada huo kwa vile utakuwa na sehemu inayohusu Zanzibar ulitakiwa upelekwe katika Baraza la Mapinduzi kabla ya maandalizi yake ili uweze kujadiliwa na Zanzibar iweze kutoa mapendekezo yake vipi tume hiyo iweze kuundwa.
Kinachotakiwa kuona mswada huo unamshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar huku baadhi ya vipengele vyake vilitakiwa kumpa hadhi Rais wa Zanzibar kutokana na suala litalofanywa litahitaji kuihusisha Zanzibar.
Mansour Yussuf Himid (Kiembesamaki)
Alisema kuletwa kwa mswada huo ni kudanganywa kwa Wazanzibar, akiita siku ya jana kuwa ni siku ya huzuni kwa Wazanzibari.
“Siku hii ya leo (jana), kamati ya Bunge imekuja kutudanganya Wazanzibari na siku ya leo (jana) ni huzuni kubwa sana, kama Mtanzania kama Mzanzibari naona tunafanyiwa kiini macho, kama Baraza la Wawakilishi hatujashirikishwa, basi hakuna haja ya kukubali hilo”, alisema Mansoor.
“Lazima tushirikishwe ipasavyo na Muungano huu tumeungana kwa hiari sisi tumekwenda katika Jamhuri wenyewe hii ni Jamhuri ya pande mbili tumekwenda kwa hiayari tutarudi kwa hiyari tutabaki kwa hiyari”, alisema Mansoor.
Alisema hiyo ni nafasi pekee ya kuhakikisha Muungano unafanyiwa marekebisho kwani kukaa bila ya kukataa hilo hiyo ni fursa ya mwisho ambayo wananchi wa Zanzibar hawataipata tena iwapo mswada huo ukenda Bungeni na kupitishwa.
“Hii ndio fursa yetu ya mwisho Wazanzibari na kwamba tukicheza hapa ndio basi hatutakiona kitu chochote ndio basi tena” ,alisisitiza.
Mohmoud Abdulla Musaa (Kikwajuni)
Alisema haiwezekani kubakia na mfumo unaotaka kutumiwa na Bunge kutokana na kuwa haujazingatia matakwa ya Zanzibar.
Omar Dadi Shajak
Akitoa maoni yake alisema ndani ya mswada huo kinachoonekana umeandaliwa kama sheria nyenginezo zilizopelekwa Bungeni na kusahau kuwa Zanzibar ina mamlaka yake na kinachoonekana ni kuzingatia maoni ya upande mmoja pekee.
Alisema kuwa aina iliyotumiwa katika maandalizi ya rasimu hiyo Zanzibar haiwezi kukubaliana nayo kwani imefanywa kama ni mshiriki na ni vyema ikarejeshwa katika kiti cha Bunge.
“Wameiweka mashariki kwenye jua kali ili kipa asiweze kuona wapate kutufunga hili halikubaliki kwani kutompa mamlaka Rais wa Zanzibar kushauriana na Rais wa Muungano hili ni hatari na Rais wa Muungano atakuwa anamuamulia Rais wa Zanzibar” , alisema Dk. Shajak.
Katibu Mkuu huyo, alikosoa kipengele kinachoipa mamlaka Tume itayoundwa baada ya kukamilisha kazi yake ripoti itayoiandaa kukabidhiwa Rais wa Muungano pekee na badala kutaka ripoti hiyo wakabidhiwe marais wote kwani Muungano ni wa nchi mbili.
Alisema hatua hiyo itaweza kuwasaidia viongozi hao kuweza kukaa na kuiangalia kwa pamoja na badae kutoa mapendekezo yao kama viongozi wa nchi mbili balada ya Rais wa Muungano pekee.
Ali Saleh (Alberto)
Mwandishi huyo wa habari Muandamizi wa Shirika la BBC, alisema muswada huo haukugusa katiba ya Zanzibar hivyo ni kuzarau makubaliano ya Muungano ambayo yapo mambo yangepaswa yawemo haki za binadamu lakini jambo la kusikitisha halijaumuishwa.
“Kura ya maoni ni kitu gani je! Wazanzibari wakisema hawataki athari yake itakuwa nini? tusifikiri Wazanzibari watapinga katiba je! athari zake zitakuwa ni nini? Na kuhojia kwanini Tume hiyo isipelekwe mahkamani, akisema huko ni kuizuiya Demokrasia”.
Alisema mabadiliko hayo yamekuwa ni mazowea kutoka upande mmoja wa Muungano ndio maana watu hawashirikishwi ambapo alisema ni lazima katiba ibadilishwe na huo ni wajibu wa baraza la Wawakilishi.
Hassan Nassor Moyo
Akitoa mchango wake alisema wakati umefika hivi sasa wa serikali ya Muungano kukubali kuwapo kwa mabadiliko katika mambo ya Muungano na kuacha kung’anag’ania mambo waliyozoweya.
Alisema mambo waliyofanya miaka iliopita wakati wa kina Lusinde, Hassan Moyo na Sitta, hivi sasa hayapo tena na wasizuie kuwapo kwa mabadiliko kwani kazi yao imekwisha na watafanya makosa kuzuia mambo ya Muungano Wazanzibari waasiyajadili katika katika mpya.
“Haiwezekani hata kidogo wapewe nafasi waseme kwani hili nalisema ndani ya moyo wangu Nyerere alikuja Zanzibar na karatasi ina mambo 11, mimi nilikuwa Waziri wa Sheria alinipa faili na hakuna hata sentesi moja iliotolewa leo tunaambiwa kuna mambo 22 na Jumbe alipotaka kuengeza alifukuzwa kazi, sasa mnaposema tusizungumze mambo ya Muungano maana yake nini mnawaambia nini Wazanzibari”,alisema Mzee Moyo.
Alisema amesikitishwa kuona Mwanasheria wa Zanzibar kueleza kuwa hana taarifa ya mswada huo jambo ambalo ni la maajabu kwa serikali kwani kinachotengenezwa ni katiba mpya na sio kutia viraka na ni vyema kamati hiyo ikapeleka ujumbe wa Wazanzibari nini wanachotaka.
“Mnasema tusiseme mnataka tuzungumze utumbo, lazima mabadiliko yafanywe kwani hivi sasa vijana wamesoma na hawakubali kuamuliwa, Nyerere alikuwa anakubaliana na mzee Karume hakua anatoa maamuzi, Wewe sita umefanya kazi na Nyerere, Jumbe na Karume msifanye mambo ya wakati ule ‘is over’ ”, alisema Mzee Moyo.
Ali Mwinyi Msuko
Kada huyo wa CCM, alisema wanasheria wa Zanzibar wakae na wanasheria wa Tanzania bara kuupitia upya mswada huo na hakuna sababu ya kuharakisha kupelekwa Bungeni, rais Nyerere na Karume walikubaliana katika Muungao huo na kwa sasa nchi mbili hizi zikubaliane.
Alishauri kwamba mswada huo urudi tena Bungeni na ufuate taratibu kwa kisheria na kwa sasa hakuna sababu yeyote ya kujadiliwa huku akitoa mfano kwamba kujadili mswada huo ni sawa na kutwanga maji kinuni.
Salum Bimani
Mkereketwa huyo wa CUF, alisema anashangazwa na Waziri Sitta kutokana na kujipa maadaraka ya kuandaa taratibu za kuingiza Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki jukumu ambalo halikupata ridhaa ya wazanzibari,
Ali Omar NCCR Mageuzi
Alisema kinachoonekana ni muendelezo wa serikali ya Muungano kuiburuza Zanzibar kwa kuona kuwa haiwashikishi katika mamaunzi makubwa.
Hamad Mussa Yussuf (CHADEMA)
Alisema madaraka ya wananchi yapo mikononi mwao na inashangaza kuona bado serikali ya Muungano imekuwa ikiamua bila ya kuishirikisha Zanzibari.
Awadh Ali Said
Alisema baada ya miaka 50, Wazanzibari wanataka kujua Muungano umewaletea tija gani na una kasoro gani.
Alisema licha ya kuwa hakuna uwiano lakini yeye hakubaliani na hilo kwa kuwa lazima maslahi ya pande mbili yazingatiwe huku akilaumu kwamba mswada huo unaonekana ni wa upande mmoja wa Muungano wakati kuna nchi mbili zilizoungana.
Sheikh Azan Khalid Hamdan
Alisema ipo haja Tume hiyo ikarudi na mswada huo kwani Wazanzibari hawautaki na wanaweza wakasababisha kutokea kwa mgogoro na atahakikisha wanawaeleza waumini wao kuukataa.
Sheikh Muhidini Zubeir Muhidini
Alisema watawaeleza Maimamu wa misikiti yote waukatae mswada huo na watahakikisha wanapinga hadi kwenye madrasa na kuwashawishi Wabunge wa Zanzibar watoke katika Bunge kama rasimu hiyo itajadiliwa na kama watabakia wasirudi Zanzibar.
Salama Aboud
Alisema serikali inahitaji kuyaangalia mahitaji ya Wazanzibari kwani kinachoonekana hakuna uwiano uliotumika katika kutayarisha rasimu hiyo.
Mohammed Ahmed Mugheiry
Alimtatahadharisha Waziri Sita kutokana na kumuona kuwa anacho kifanya kitamharibia sifa yake kwani wanapaswa kutambua kuwa serikali iliopo imechaguliwa na wananchi na hivi sasa Zanzibar kuna serikali ya umoja ya kitaifa ambayo tayari imekaa vizuri.
Samuel Sitta
Akiwasilisha madhumuni na sababu za mswaada huo Samwel Sitta alisema mswada huo umependekeza kutungwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya nchi ya mwaka 2011 ambapo mswada unakusudia kuanzishwa kuweka masharti uanzishaji wa tume pamoja na sekretari kwa madhumuni ya kuendesha na kusimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mchakato wa mabadiliko ya katiba pamoja na muswada pamoja na masuala mengine utaangalia chimbuko na mahusiano ya katiba iliyopo kwa kuzingatia uhuru wa wananchi mfumo wa siasa ambao unatarajiwa kukamilika Aprili 1014.
Alisema pindi mswada huo utakapopitishwa na kuwa sheria utakuwa na utaratibu wa kisheria utakaomwezesha rais kuunda tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba na kuunda bunge la katiba kwa madhumuni ya kutunga katiba mpya.
Sitta aliwataka Wajumbe hao kushirikiana na Kamati hiyo kuwashawishi wananchi kukubaliana nayo na itapofikia wakati watoe maoni yao kwani wamelazimika kufanya hivyo kutokana na hivi sasa wanataratajia kuwasilisha kupata bajeti inayokadiriwa kufikia bilioni 30 na mwezi huu wa nne itakuwa ni wa matayarisho ya Bajeti hiyo.
Hata hivyo Sitta aliahidi kuyafikisha maoni ya Wazanzibari kama yalivyotolewa katika mkutano huo.
Wakati watu wakichangia hamasa na jazba zilitanda huku wakipiga makofi ya kukataliwa mswada huo na kuimba nyimbo ya ‘sisi sote tumegomboka kwa ndugu’

Muungano hatuutaki tena umejaa udanganyifu mwingi.

[caption id="attachment_29787" align="alignnone" width="300" caption="Tanganyika nyuma ya Pazia la Tanzania matapeli na Serekali yenu."]
 
Wadau Leo, mjumbe mmoja baada ya kuchangia na kuwauliza wananchi wa Zanzibar iwapo wanaikubali rasimu ile, wakakataa, aliichana mbele ya Sitta na vyombo vya habari. Wananchi wengine nao wakafuata na ukawa mwisho wa kongamano. Kwa nilivyomuona Sitta kapigwa na butwaa, I think message delivered correctly
 
Back
Top Bottom