TANZIA Mustapha Nzogela, Mwanachama wa Yanga na mmoja wa waasisi wa mwanzo kabisa wa Tawi la Yanga Pamoja Mbezi, afariki kwa ajali ya Maji

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
TANZIA

Ndg yetu Mustapha Nzogela, Mwanachama wa Yanga na mmoja wa waasisi wa mwanzo kabisa wa Tawi la Yanga Pamoja Mbezi, alifariki Kwa ajali ya Maji juzi ktk bonde la Mkwajuni akijaribu kupita na Noah yake bila kujua kama maji ni mengi na yanapita juu ya Barabara, mazishi yamefanyika Leo Luguruni, amefariki yeye na Mke wa mdogo wake;

Mke wake na Watoto walitangulia nyumbani kwa daladala mapema kabla ya Maji kuwa mengi

IMG-20231211-WA0113.jpg
 
Jamaa kama namfahamu hivi, kijiwe chake Kikuu ni makondeko pale wanakutana vijana Kwa wazee mida ya jioni kucheza bao na draft
R I P
 
Kifo kinaita. We unaona maji yamejaa tena yanapita juu ya barabara kwa Kasi unaamini gari yako itahimili Kasi ya maji bila kukumbuka kuwa gurudumu za gari zimejaa upepo kitu kinachopunguza balance na uzito wa gari kwenye maji.
Kingine kwa utandawazi huu tushasikia vifo vingi vya namna hii na bado mtu unajipa ujasiri wa kupeleka gari yako kwenye hali kama hiyo. HAKIKA KIFO KINAITA
 
Jambo lingine ni kuwa unapo katiza kwenye maji unakuwa umeyakata/umeyawekea kingo ambayo haina foundatiom chini.

Kinachofanyika yanajaa upande mmoja na kwa kasi yake yanakuhamisha. The rest inabaki historia.

Angeweza kuvunja siti pembeni akapumzika kusubiri yapungue. Angeweza kurudi mjini kwa washkaji kupiga mastori huku akisikilizia.

sema naungana na wewe kifo kinaita
 
Kwanini watu bado hawaelewi jamani
Tyre la gari linaelea kwenye maji mengi,hata gari liwe zito vipi

Rip kwake.
 
Back
Top Bottom