Sijui kama na nyie wengine mmelifikiria hili...
Pindi Mh. Lissu atapopona na kurejea katika hali yake ya kawaida [ni matumaini yangu atapona kabisa], hali ya usalama wa maisha yake na familia yake itakuwaje?
Ni nani atamlinda? Chama chake kitampatia walinzi binafsi wasio na uhusiano wowote ule na serikali ya CCM au?
Manake kwa jinsi ambavyo wingu la ushukiwa wa uhusika dhidi ya serikali ya Magufuli lilivyotanda juu yake, kweli kabisa mnadhani serikali ikitoa ulinzi huo ulinzi utaaminika?
Ingekuwa ni mimi nisingeweza kabisa kuamini walinzi nitakaopewa na watu ambao wananchi wengi wanawahisi kuwa ndo wahusika wakuu wa jaribio la ushambulizi dhidi ya uhai wangu!
Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba, kwa vile hao watu hawakumaliza hiyo kazi yao ovu [kumuua], huenda huko waliko sasa hivi wanapanga mkakati wa jinsi ya kuimaliza hiyo kazi endapo akirudi tena nchini.
Na je, Lissu atarejea tena nchini pindi apatapo afueni au ataamua kuishi ukimbizini kwa kuhofia maisha yake?
Mimi nadhani atarejea nchini hata kama hali ya usalama wake haitokuwa ya kueleweka wala kuaminika.
Kwa jinsi alivyo sitoshangaa kabisa kama atawathubutisha [dare them] wammalize kabisa kuliko kuacha kupigania kile anachokiamini.
Hili jambo naamini linaweza kuitia doa kubwa sana serikali ya Magufuli na CCM. Ni muda tu ndo utaotuambia kama huu ndo mwanzo wa mwisho wa CCM kushika dola na hatimaye kumeguka vipande vipande .
Jumapili njema.