Nimeishi na kushuhudia Chaguzi mbili za Kenya isitoshe nina relatives kule wenye "interest" na siasa za Kenya.Honestly mimi sio shabiki wa siasa zao au mtu lakini ni mfuatiliaji mzuri wa siasa zao.
Ni vigumu kutabiri nini kitatokea kwenye uchaguzi ujao kwa kumbukumbu tu: kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1992 Ford kiikuwa chama kinachounganisha makabila yote kulikuwa na
Keneth Matiba (kikuyu)
Oginga odinga (luo)
Kijana Wamalwa (Lhuya)
Lakini kabla ya uchaguzi mkuu Matiba na Oginga wakagawanyika Moi akapenya kirahisi kwa sababu Wakikuyu wakawa na Kibaki na Matiba,waluo na Oginga, Wakamba na Charity ngilu.....Kwa Moi ukiongeza na madaraka yake akawa na wakalenjin (Rift valley)...Wagiriama na Miji kenda (Cost) na watu wa north eastern.
1997 the same story...lakini utaona pia pamoja na Wamalwa na Raila kutengana lakini bado Raila akashika nafasi ya tatu nyuma ya Kibaki ambaye kimsingi alikuwa mkongwe na mgombea mwenye nguvu kwa wakikuyu.
ya 2002 na 2007 yanajulikana.Lakini hebu tuangalie mwaka huu, kama nilivyosema awali siasa zao hazitabiriki usije kushangaa Musyoka (mwanasiasa asiyetabirika) anaungana na Raila...ama muungano wa G7 unaparaganyika.Muhimu kukumbuka ni kuwa Raila ni Mr. vurugu lakini ni very strategies..anaonekana kama mwanasiasa mstaarabu na anajua namna ya kucheza na siasa za Kenya kuliko mwanasiasa yeyote aliyeko kilingeni.
Uhuru hana nguvu kubwa kwa wakikuyu nje ndio kabisaa..kumbuka Uhuru anatoka kwa wakikuyu wa high class ambako kuna Charles Njonjo mwanasiasa mkimya/Msomi lakini mwenye nguvu (ana-support ODM)..
Ruto bado nguvu yake ndogo hata Rift valley kwake ingawa yuko na Uhuru (hatuna hakika watakuwa mpaka mwisho).Hata Mudavadi naye ana nguvu sehemu tu ya walhuya..kumbuka kuna Eugine Wamalwa (mluya) ambaye yuko G7.