Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.

Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.

Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.

Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
 
Zugak17

Zugak17

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2014
Messages
1,042
Points
1,500
Zugak17

Zugak17

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2014
1,042 1,500
Ndio mkuu na siku zote kwa same generation i3/i5/i7 zinakuwa na GPU moja. Hivyo GPU ya i3 5005u ni sawa na i5 5200u au i7 5500u, ndio maana unaona japo i3 inapitwa performance ila GPU ipo vizuri.
Nimekupata Mzee
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Chief naomba niangalzie hii Dell
Processor akeView attachment 1182874
Processor yake inaitwa core M mkuu, na Hapo ameandika generation ya Saba.

Ila M3 6Y30 Kama alivyoandika yeye Ni generation ya 6 na sio Saba. Ingekuwa gen ya 7 ingekuwa m3 7y30

Ila nimeicheki online hio model Ina 7th generation, hivyo kimoja wapo Hapo juu amekosea, Ni vyema kabla hujanunua ukahakiki mwenyewe specification Hawa Jamaa hawaaminiki.

Kuhusu laptop yenyewe sababu Ina core m Ina maana itakula umeme kidogo Sana, core m inakula umeme kidogo Kushinda hata taa ya kawaida ya nyumbani just 4W tu.

Hivyo Kama unataka laptop yenye umbo Dogo na inayokaa na chaji, hio Ni laptop sahihi.

Kama unataka laptop yenye nguvu na ya kucheza games na kufanya kazi nzito achana nayo, tafuta laptop ya 8th gen, gape la performance baina ya 8th na 7th gen Ni kubwa Sana.
 
Joe Unruly

Joe Unruly

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Messages
215
Points
250
Joe Unruly

Joe Unruly

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2016
215 250
Processor yake inaitwa core M mkuu, na Hapo ameandika generation ya Saba.

Ila M3 6Y30 Kama alivyoandika yeye Ni generation ya 6 na sio Saba. Ingekuwa gen ya 7 ingekuwa m3 7y30

Ila nimeicheki online hio model Ina 7th generation, hivyo kimoja wapo Hapo juu amekosea, Ni vyema kabla hujanunua ukahakiki mwenyewe specification Hawa Jamaa hawaaminiki.

Kuhusu laptop yenyewe sababu Ina core m Ina maana itakula umeme kidogo Sana, core m inakula umeme kidogo Kushinda hata taa ya kawaida ya nyumbani just 4W tu.

Hivyo Kama unataka laptop yenye umbo Dogo na inayokaa na chaji, hio Ni laptop sahihi.

Kama unataka laptop yenye nguvu na ya kucheza games na kufanya kazi nzito achana nayo, tafuta laptop ya 8th gen, gape la performance baina ya 8th na 7th gen Ni kubwa Sana.
Nmeona insta jamaa wanaziuza....ila bei za kule siziamini mana pc ina specs kubwa afu bei chee
 
utakuja

utakuja

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Messages
894
Points
1,000
utakuja

utakuja

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2010
894 1,000
makaveli10

makaveli10

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Messages
14,087
Points
2,000
makaveli10

makaveli10

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2013
14,087 2,000
Bei ni 460,000 Tshs
Product name (BRAND NEW)
HP Pavilion x360 - 14-ba078tx
Microprocessor
Intel Core i7-7500U (2.7 GHz base frequency, up to 3.5 GHz with Intel Turbo Boost Technology, 4 MB cache, 2 cores)
Flash cache
8 GB
Memory, standard
8 GB DDR4-2133 SDRAM (1 x 8 GB)
Video graphics
NVIDIA GeForce 940MX (4 GB DDR3 dedicated)
Hard drive
2TB 5400 rpm SATA SSHD
Display
35.56 cm(14) diagonal FHD IPS WLED-backlit multitouch-enabled edge-to-edge glass (1920 x 1080)
Keyboard
Full-size island-style backlit keyboard
Pointing device
HP Imagepad with multi-touch gesture support
Wireless connectivity
802.11a/b/g/n/ac (2x2) Wi-Fi and Bluetooth 4.2 combo
Expansion slots
1 multi-format SD media card reader
External ports
1 HDMI; 1 headphone/microphone combo; 1 USB 3.1 Type-C Gen 1 (Data up to 5 Gb/s); 2 USB 3.1 Gen 1 (Data transfer only)
Dimensions (W x D x H)
33.48 x 22.69 x 1.99 cm
Weight
Starting at 1.63 kg
Power supply type
65 W EM AC power adapter
Battery type
3-cell, 41 Wh Li-ion
Webcam
HP Wide Vision HD Camera with integrated dual array digital microphone
Audio features
Dual speakers; B&O PLAY; HP Audio Boost
#warrant 1year

Mkuu kuna mtu kaniuliza kama hiyo itamfaa au lah!!
Nb: anapenda kucheza games.
 
Mkuu hata kwa dawa hupati hio machine kwa 460,000 Hapo Kuna harufu ya utapeli nje nje, muulize kaona tangazo online? Awe makini na hao matapeli.

Ila Ni machine nzuri na games nyingi kwa 720p inacheza.
 
Zeus1

Zeus1

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Messages
3,554
Points
2,000
Zeus1

Zeus1

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2017
3,554 2,000
Yani 460??alafu mpya??sidhani mzee

Ila kama kweli fanya mpango na mimi nataka hii machine.

Mie nilimwambia, nahisi kuna utapeli fulani, lakini nilihitaji kusikia zaidi kutoka kwa walionizidi.
 
makaveli10

makaveli10

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Messages
14,087
Points
2,000
makaveli10

makaveli10

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2013
14,087 2,000
Yani 460??alafu mpya??sidhani mzee

Ila kama kweli fanya mpango na mimi nataka hii machine.
Nahisi itakuwa used, ila naona kama kuna usanii,
Ngoja nihakikishe ikiwa fresh, nitakupanga.
 
Product

Product

Member
Joined
Sep 7, 2019
Messages
70
Points
125
Product

Product

Member
Joined Sep 7, 2019
70 125
intel (r) core (TM)2 duo CPU e7500 @2.93 ghz

Hii ipoje chief...samahani kwa usumbufu mkuu Chief-Mkwawa
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
intel (r) core (TM)2 duo CPU e7500 @2.93 ghz

Hii ipoje chief...samahani kwa usumbufu mkuu Chief-Mkwawa
Mkuu core 2 duo Ni kabla ya hizi i3/5/7 Ni za zamani kidogo Kama miaka 10 iliopita Ila matumizi ya kawaida zinafanya vizuri tu.
 
Product

Product

Member
Joined
Sep 7, 2019
Messages
70
Points
125
Product

Product

Member
Joined Sep 7, 2019
70 125
Mkuu core 2 duo Ni kabla ya hizi i3/5/7 Ni za zamani kidogo Kama miaka 10 iliopita Ila matumizi ya kawaida zinafanya vizuri tu.
sina uwezo wa kuondoa hii cpu na kuweka cpu kubwa na latest ya sasa hivi chief?
na kama uwezekano upo chief gharama zake zinaweza kufikia kiasi gani? maana hii mashine pamoja na kuijaza RAM 12GB ila sioni umuhimu wake maana inashindwa speed na mashine hapa pembeni ina ram 4gb tu ila speed ni nzuri kabisa.

unanishaurije hapa chief
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
na kama uwezekano upo chief gharama zake zinaweza kufikia kiasi gani? maana hii mashine pamoja na kuijaza RAM 12GB ila sioni umuhimu wake maana inashindwa speed na mashine hapa pembeni ina ram 4gb tu ila speed ni nzuri kabisa.

unanishaurije hapa chief
Mkuu huwezi badili kwenda cpu ya kisasa maana cpu unabadili kwenda same generation. Mfano i3 gen ya 7 unaweza ukaitoa na kuweka i7 gen ya 7.

Kwa core 2 duo unaweza ukaiongeza perfomance kwa kuweka sad. Itaifanya iwe fast lakini still hutaweza kufungua apps na games nzito.

Kama hizo ram Ni za ddr3 unaweza tafuta machine ya kisasa na ukahamisha vitu vyako Kama ram, HDD na Mambo mengine kwenda hio machine mpya.
 
Krait

Krait

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Messages
2,720
Points
2,000
Krait

Krait

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2012
2,720 2,000
Mkuu huwezi badili kwenda cpu ya kisasa maana cpu unabadili kwenda same generation. Mfano i3 gen ya 7 unaweza ukaitoa na kuweka i7 gen ya 7.

Kwa core 2 duo unaweza ukaiongeza perfomance kwa kuweka sad. Itaifanya iwe fast lakini still hutaweza kufungua apps na games nzito.

Kama hizo ram Ni za ddr3 unaweza tafuta machine ya kisasa na ukahamisha vitu vyako Kama ram, HDD na Mambo mengine kwenda hio machine mpya.
Kuna jamaa tupo nae kwenye Group letu la mafundi simu upande wa software ye kafanikiwa kubadili processor kutoka AMD (kama sikosei) kwenda core i3 3rd generation
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Kuna jamaa tupo nae kwenye Group letu la mafundi simu upande wa software ye kafanikiwa kubadili processor kutoka AMD (kama sikosei) kwenda core i3 3rd generation
Haiwezekani mkuu unless kabadili motherboard nzima na kuweka ya Amd,
 
Forum statistics

Threads 1,336,673
Members 512,696
Posts 32,547,374
Top