ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,922
- 3,912
Nilifuta kwenye keyboard mkuu. Naona ikaingia ndani.Mkuu yaani hii si ya kufuta kwa njee tu, then ndio ikasiz mazima?
troublemaker 2019. all right received.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nilifuta kwenye keyboard mkuu. Naona ikaingia ndani.Mkuu yaani hii si ya kufuta kwa njee tu, then ndio ikasiz mazima?
troublemaker 2019. all right received.
troublemaker 2019. all right received.Umejaribu kutumia monitor ya nje?Nina mashine yangu laptop ilizingua keyboard nikapeleka kwa fundi,yaani baada ya kuifungua haiwaki mpka leo,inaonesha taa ya kuwaka,feni inazunguka lakini kioo hakipandishi..ni hp 650
Sent using Jamii Forums mobile app
K hata generation ya 4 ni nzuri zaidi kushinda HQ ya gen ya 7.
K ni ya desktop imetengenezwa kwa ajili ya overclock inatumia umeme mwingi zaidi mara nyingi watts 95 ama zaidi na ndio top of overall perfomance.
HQ ni ya laptop yenyewe inatumia watts kama 45 hivi kwa laptop za gen za zamani hii tunaweza kusema ndio top of line.
So inategemea na wewe mwenyewe unataka laptop ama desktop ni cpu ambazo zinakidhi mahitaji tofauti.
Ila kwa laptop kama unanunua sasa hivi tafuta zinazoishiwa na H mfano i5 8400H ama i5 8300H itakuwa na nguvu kushinda i7 zinazoishiwa na HQ za zamani sababu kwenye Gen ya 8 intel ameongeza core hizo i5 zina core 6 compare na HQ zilizokuwa na core 4.
Mkuu Mkwawa,Nina flash tatizo lake kutosoma/kuto-dectect,ilitokea ghafla baada ya umeme kukatika,nahitaji solution ya ku-recover taarifa/data zangu zilizokuwemo maana zina umuhimu kweli,kama Kuna eneo lolote hapa Tz/bongo wanatoa huduma hii itakuwa itakuwa msaada mkubwa kwangu.feedback yako ni muhimu Sana Sana Mkuu.Achana nayo mkuu, ni bora utafute i3 generation za karibu kuliko i7 gen ya 2, hasa kwa laptop.
Unless hio laptop ina dedicated graphics. Kama Nvidia
Tamu sana imenisaidia mnooDaaah....thread tamu na ndo naiona kwa mara ya kwanza....wacha nijitaidi kuipitia yote....heshima kwko CHIEF MKWAWA
Sent using Jamii Forums mobile app
Chief Mkwawa
Naomba utufungulie darasa kwenye mtandao mi binafsi nikotayari kukulipa ilihali nipate besic knowledge kwa tusio na muda wakukaa darasani kumsubiria mwalimu huku majukumu mengi yametubana
Sent using Jamii Forums mobile app
Pentium si ndo zimetajwa processor za kidwanzi au mi ndo sielewi!Naomba ushauri hapa kuna Acer Pentium core 2 kwa 350 je itanifaa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naomba unipe darsa kuhusu graphics nizidi kuiva maana hapo kwenye processor umeua.Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.
Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?
-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.
-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
![]()
Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.
1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.
2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop
3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.
4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.
5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.
6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.
7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.
8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.
Generation ya processor(muhimu)
Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.
- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140
Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.
Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail
Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.
Herufi za mbele ya processor(muhimu)
Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?
1. Herufi kwenye processor za desktop.
Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770
K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.
R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.
![]()
S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.
T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T
2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.
M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M
U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y
HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ
MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ
MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX
Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Hope unamaanisha pentium G3250 hio sio quadcore ni dual core, ina core mbili tu.mkuu Quad core processor(intel pentinium 3250 2.2ghz (4core)
hii ina sifa gani mkuu
Hapana Ni N3250 alafu ni laptopHope unamaanisha pentium G3250 hio sio quadcore ni dual core, ina core mbili tu.
Ni 4th generation na perfomance yake ni ya kawaida tu.
Sema inashare same motherboard na i3/i5/i7 za 4th gen. Unaweza ukanunua hizo cpu na kupachika kuongeza uwezo.
Ni lenovo w520Mkuu w520 ni workstation na my guess hio processor ni i7 2760QM nenda my computer kisha right click kisha properties kuthibitisha.
Hio cpu ina nguvu sana inafanya almost matumizi yote heavy kwa ufanisi. Kuanzia games, video editing, CAD, etc
Sema Gpu yake sio nzuri sana, unles inakuja na dedicated gpu ya Nvidia ama Ati.
Pia sababu ina nguvu sana itakula sana umeme.
Quadro 1000 ni kwa ajili ya proffesional tasks, itafanya video editing, 3d na rendering mbalimbali sema kwa games usitegemee perfomance kubwa.Ni lenovo w520
Intel core i7-2860qm @ 2.5 ghz
RAM 8 GB
INVIDIA QUADRO 1000
Directx 11.2
Ntacheza game gan hapoView attachment 1120536