Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,723
2,000
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.


Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.


Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
 

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,723
2,000
Vipi HP ProBook 4330s?
hii ina

Intel Core i3 2310M / 2.1 GHz

-kwanza ni intel i3 ambayo siombaya

-pili namba yake imeanziwa na elfu mbili yaani 2310 inamaana ipo second generation pia sio mbaya

-herufi ya mbele ni M ina maana ni mobile hivyo utapata perfomance kubwa kushinda za U na Y
-clock speed ni 2.1ghz ambayo nayo kwa laptop ni nzuri tu.

hata single core perfomance ya hio processor ni nzuri

overall ni laptop nzuri kwa matumizi ya kawaida huwezi kuwa slow
 

TZ boy

JF-Expert Member
Jan 11, 2012
628
225
hii ina

Intel Core i3 2310M / 2.1 GHz

-kwanza ni intel i3 ambayo siombaya

-pili namba yake imeanziwa na elfu mbili yaani 2310 inamaana ipo second generation pia sio mbaya

-herufi ya mbele ni M ina maana ni mobile hivyo utapata perfomance kubwa kushinda za U na Y
-clock speed ni 2.1ghz ambayo nayo kwa laptop ni nzuri tu.

hata single core perfomance ya hio processor ni nzuri

overall ni laptop nzuri kwa matumizi ya kawaida huwezi kuwa slow
Thanks Bro
 

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
985
1,000
Ndugu Chief-Mkwawa naomba nikuulize swali, processor za Intel i3 2nd generation zinaweza kuwa na bei gani madukani hapa kwetu Tanzania?
Kwa dukani processor ya i3 1st, 2nd gen si chini ya 280k ila mtaani hata i3, i5, i7 generation yoyote unapata kwa bei yoyote hata 50k kwasababu hazina demand sana, asilimia kubwa ya watu wanamiliki(desktop) pentium 4, na core2duo, na wachache core2quad, xeon na pia wachache sana i3, i5, i7,
 
Last edited by a moderator:

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,723
2,000
Ndugu Chief-Mkwawa naomba nikuulize swali, processor za Intel i3 2nd generation zinaweza kuwa na bei gani madukani hapa kwetu Tanzania?
kaka mimi si mzungukaji sana kwa maduka ya tanzania na kusema kweli sifahamu ila siku nikiamua kuzitafuta nitaupdate thread, ila kwa experience yangu maduka ya bongo huwa hawashushi bei kwenye stock za zamani, huwenda bei ikawa ni sawa na 4th gen au tofauti ikawa ndogo. na kwa kukadiria bongo zitakuwa kwenye 200k mpaka 300k

why usitumie amazon? siku hizi wanafilter kabisa bidhaa zinazoship tanzania na i3 ni dola 99 tu pamoja na gharama za kuship huwenda isifike hata 200,000 maana processor si nzito sana.
 
Last edited by a moderator:

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
22,723
2,000
Chief-Mkwawa
Shukrani sana kwa hili somo limetufungua macho wengi, Vipi kuhusu Mother Board Compatibility na hizo procesor, in case nikataka nibane bajeti kwa kununua cheap mother board ili ni upgrade procesor.
kwa haswell? kama unataka motherborad za hizi 4th generation anandtech wana article nzuri wanaelezea ila bei sio cheap kivile ila zipo za dola 110 na 135.

kama upo on budget kuna processor moja ya pentium unaweza kui-overclock ni dual core lakini single core perfomance ni kubwa hakuna i3 inayoipita power hii pentium na i5 na i7 zisizoweza kuoverclock pia zinapitwa na hii pentium.

tatizo lake itabidi ununue gpu na pia ni dual core kuna tetesi game za 2015 kuanza kudrop dualcore na tayari kuna game limetoka minimum requirement ni quadcore processor.

kwa motherboard tembelea hapa
AnandTech | Holiday Guides 2014: Z97 Motherboards for Haswell
hio processor icheki hapa
Amazon.com: g3258 pentium
benchmark ya single core
PassMark - Intel Pentium G3258 @ 3.20GHz - Price performance comparison
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom