Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.

Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.

Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.

Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
 
Krait

Krait

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Messages
2,720
Points
2,000
Krait

Krait

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2012
2,720 2,000
Haiwezekani mkuu unless kabadili motherboard nzima na kuweka ya Amd,
Sina uhakika kama ni AMD ila alisema ni hizi zinazotoka bila shida watu tukamwambia haitawezekana mwisho wa siku akatutumia picha za processor aliyoagiza ebay na baada ya kuipachika akatutumia picha

Kwa maelezo yake alisema alianza kufuatilia mtandaoni ni processor ipi inayoweza kuingiliana na pc yake

Bahati mbaya niliflash simu na nilisahau kufanya backup ya whatsapp chart ningetupia screenshot humu
 
Mkuu kinachofanywa ubadili processor Fulani Ni motherboard, kwenye motherboard kunakuwa chipset husika ambayo inakuwa na support ya hizo processor.

Mfano hizi Ni chipset za karibuni za Intel na picha zake

Lga 1151

Hii inakubali cpu za Skylake na kabylake (gen ya 6 na 7)

Lga 1150

Hii inakubali haswell na broadwell (gen ya 4 na 5)

Lga 1155

Hii ilikuwa Ni Sandy bridge na ivy bridge (gen ya 2 na 3)

Ukiangalia kwa makini hizo picha hizo socket na pini hazifanani hivyo hata processor haziingiliani, huwezi ukatoa amd ama Intel nyengine ukachomeka tu socket yoyote inabidi ujue kwanza motherboard Ina support processor zipi na kununua processor inayokubali.
 
Ukisoma tena hapo juu utaona kwamba jamaa alianza kufuatilia mtandaoni ndo akakuta aina ya Processor inayoingiliana na iliyopo

Sisi wenyewe kwenye Group tulimwambia haitowezekana ila jamaa alifanikiwa ku update
Nakuinbox namba yake umuulize vizuri
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Ukisoma tena hapo juu utaona kwamba jamaa alianza kufuatilia mtandaoni ndo akakuta aina ya Processor inayoingiliana na iliyopo

Sisi wenyewe kwenye Group tulimwambia haitowezekana ila jamaa alifanikiwa ku update
Nakuinbox namba yake umuulize vizuri
Mkuu nilipinga Intel kwenda Amd process, Ila Kama Ni processor za same generation inawezekana kabisa.
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Intel(R) Core(TM) i5-3470 CPU @3.20GHz 3.20GHz hii imekaaje chief
Gen ya 3 mkuu, kuanzia gen ya 2 mpaka ya Saba hizi CPU hazina utofauti Sana Hapo unatafuta tu gpu low end unakuwa na machine nzuri.
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
9,762
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
9,762 2,000
Bei ni 460,000 Tshs
Product name (BRAND NEW)
HP Pavilion x360 - 14-ba078tx
Microprocessor
Intel Core i7-7500U (2.7 GHz base frequency, up to 3.5 GHz with Intel Turbo Boost Technology, 4 MB cache, 2 cores)
Flash cache
8 GB
Memory, standard
8 GB DDR4-2133 SDRAM (1 x 8 GB)
Video graphics
NVIDIA GeForce 940MX (4 GB DDR3 dedicated)
Hard drive
2TB 5400 rpm SATA SSHD
Display
35.56 cm(14) diagonal FHD IPS WLED-backlit multitouch-enabled edge-to-edge glass (1920 x 1080)
Keyboard
Full-size island-style backlit keyboard
Pointing device
HP Imagepad with multi-touch gesture support
Wireless connectivity
802.11a/b/g/n/ac (2x2) Wi-Fi and Bluetooth 4.2 combo
Expansion slots
1 multi-format SD media card reader
External ports
1 HDMI; 1 headphone/microphone combo; 1 USB 3.1 Type-C Gen 1 (Data up to 5 Gb/s); 2 USB 3.1 Gen 1 (Data transfer only)
Dimensions (W x D x H)
33.48 x 22.69 x 1.99 cm
Weight
Starting at 1.63 kg
Power supply type
65 W EM AC power adapter
Battery type
3-cell, 41 Wh Li-ion
Webcam
HP Wide Vision HD Camera with integrated dual array digital microphone
Audio features
Dual speakers; B&O PLAY; HP Audio Boost
#warrant 1year

Mkuu kuna mtu kaniuliza kama hiyo itamfaa au lah!!
Nb: anapenda kucheza games.
nimeiona instagram hata location tu imenitisha. kuna utapeli hapo. labda uipandie boti kwenda kuthibisha mwenyewe.

eti yuko chake chakezanzibar. maana mwisho wa siku atataka umtumie ela ili akutumie.
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
9,762
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
9,762 2,000
bei mil 1.3

1568219875641-png.1205244

HP Notebook - 15-db1003dx

Microprocessor

AMD Ryzen™ 5 3500U with Radeon™ Vega 8 Graphics (2.1 GHz base clock, up to 3.7 GHz max boost clock, 6 MB cache, 4 cores)

Chipset

AMD Integrated SoC

Memory, standard

8 GB DDR4-2400 SDRAM (1 x 8 GB)

Video graphics

AMD Radeon™ Vega 8 Graphics

Integrated

Hard drive

1TB

Optical drive

DVD-Writer

Display

15.6" diagonal HD SVA BrightView micro-edge WLED-backlit touch screen (1366 x 768)

Wireless connectivity

Realtek RTL8723DE 802.11b/g/n (1x1) and Bluetooth® 4.2 combo

Network interface

Integrated 10/100/1000 GbE LAN

Expansion slots

1 multi-format SD media card reader

External ports

2 USB 3.1 Gen 1 Type-A (Data Transfer Only); 1 USB 2.0 Type-A (Data Transfer Only); 1 RJ-45; 1 AC smart pin; 1 HDMI; 1 headphone/microphone combo

Minimum dimensions (W x D x H)

37.6 x 24.6 x 2.25 cm

Power supply type

45 W AC power adapter

Battery type

3-cell, 41 Wh Li-ion

Webcam

HP TrueVision HD Camera with integrated digital microphone

Audio features

Dual speakers
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
bei mil 1.3

View attachment 1205244

Ryzen 5 Ni machine nzuri Sana kubalance baina perfomance na Bei. Zinafaa Sana Huku kwetu.
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Hiyo vega 8 ina gb ngapi hivi video ram
Nafkiri 1GB sema GB kwenye gpu hazina maana yoyote bila kujua speed kwanza, Iris pro Zina Hadi 128MB vram Ila zinakimbiza balaa, sababu zinatumia storage zenye bandwidth kubwa Sana zinaitwa edram ambayo inakwenda Hadi 100GB per second.

Unakuta GPU Ina vram 8GB lakini Ni ddr3 ram zake usitegemee perfomance yoyote ya maana.

Sema inacheza games zote bila wasiwasi uki sacrifice quality.
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Hiyo vega 8 ina gb ngapi hivi video ram
Nimeicheki Tena Ni shared, inatumia system ram, hivyo ukiwa na ram zenye speed zaidi nayo inakuwa na nguvu zaidi, pia ikiwa dual Chanell nayo nguvu inaongezeka.
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
9,762
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
9,762 2,000
Nafkiri 1GB sema GB kwenye gpu hazina maana yoyote bila kujua speed kwanza, Iris pro Zina Hadi 128MB vram Ila zinakimbiza balaa, sababu zinatumia storage zenye bandwidth kubwa Sana zinaitwa edram ambayo inakwenda Hadi 100GB per second.

Unakuta GPU Ina vram 8GB lakini Ni ddr3 ram zake usitegemee perfomance yoyote ya maana.

Sema inacheza games zote bila wasiwasi uki sacrifice quality.
Inasaport kweli 4kGB DDR4-2400 SDRAM (1 x 8 GB)

So kama unachukua hiyo inabidi ram uongeze ifikia angalau gb 16?
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Inasaport kweli 4kGB DDR4-2400 SDRAM (1 x 8 GB)

So kama unachukua hiyo inabidi ram uongeze ifikia angalau gb 16?
Ndio mkuu kununua 8GB nyengine kunaongeza perfomance, ama unauza hiyo na kununua 4GB mbili.

Na 4K inaplay vizuri hizi compressed file Kama za YouTube, Netflix etc
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
9,762
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
9,762 2,000
Ndio mkuu kununua 8GB nyengine kunaongeza perfomance, ama unauza hiyo na kununua 4GB mbili.

Na 4K inaplay vizuri hizi compressed file Kama za YouTube, Netflix etc
Hiyo ina 8gb so ni kuongeza iwe na 16 gb maana slot imetumika moja.

Hii ryzen 5 inakimbizana na i series gen ya ngapi kwenye intel?
Na hii vega 8 inakimbizana na gtx ipi kwenye invidia?
 
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Messages
21,021
Points
2,000
Chief-Mkwawa

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined May 25, 2011
21,021 2,000
Hiyo ina 8gb so ni kuongeza iwe na 16 gb maana slot imetumika moja.

Hii ryzen 5 inakimbizana na i series gen ya ngapi kwenye intel?
Na hii vega 8 inakimbizana na gtx ipi kwenye invidia?
Assume hio Ni version ya 25W, na una ram nzuri na dual Chanell Basi Ni equivalent ya nvidia 150mx.

Kwenye cpu Ni equivalent ya i5 latest gen 8 ama 9 zenye core 4 na thread 8.

I5 yoyote ya zamani ya gen ya 7 kushuka inapitwa na hio ryzen.
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
9,762
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
9,762 2,000
Assume hio Ni version ya 25W, na una ram nzuri na dual Chanell Basi Ni equivalent ya nvidia 150mx.

Kwenye cpu Ni equivalent ya i5 latest gen 8 ama 9 zenye core 4 na thread 8.

I5 yoyote ya zamani ya gen ya 7 kushuka inapitwa na hio ryzen.
Kwani 150mx na 940mx 4gb ipi ina uwezo zaidi?

Tuseme nina pc core i5 6th gen with gtx 1650(desktop)
Na na hiyo vipi ukizicompare na hiyo ryzen 5 with radion vega 8(laptop)
Maana zote gharama inaingia humo humo mil 1 hadi mil1.3
 
Joe Unruly

Joe Unruly

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Messages
215
Points
250
Joe Unruly

Joe Unruly

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2016
215 250
nimeiona instagram hata location tu imenitisha. kuna utapeli hapo. labda uipandie boti kwenda kuthibisha mwenyewe.

eti yuko chake chakezanzibar. maana mwisho wa siku atataka umtumie ela ili akutumie.
Uyoo co anaejiita big sale znz insta??
 
Forum statistics

Threads 1,336,689
Members 512,697
Posts 32,547,763
Top