Muongozo: Mapokezi ya Lissu

Muongozo: Mapokezi ya Lissu

Amani iwe nanyi wadau wote!

Najua Tanzania tuko na msiba mzito wa mzee wetu Benjamin William Mkapa na pia siku ya Jumatatu tutakuwa na tukio kubwa na la kipekee la kumpokea shujaa yetu, mtu wetu na nuru iliyoletwa kwetu na Mungu. Si mwingine bali ni Tundu Antipas Lissu.

Hivyo basi katika siku Hii ni mapendekezo yangu kuwa watu wengi tujitokeze kwa wingi kumpokea huyu shujaa wetu pale uwanja wa ndege kuanzia Majira ya asubuhi kwa ajili ya kumpokea.

Pia kutokana na siku hii kuwa pia na huu msiba mzito napendekeza watanzania wote siku hiyo tuvae nguo nyeupe na nyeusi kwa sababu kuu mbili.

Nguo nyeupe zitaashiria alama ya Nuru kutokana na kuja kwa Tundu Lissu anayewakilisha Nuru kwa watanzania.

Nguo nyeusi zitaashiria kuomboleza kwetu kutokana na Kofi cha mzee wetu Benjamin William Mkapa.

Kama watanzania tukifanya hivi tutakuwa tumeheshimu msiba wa mzee wetu na mapokezi makubwa ya Nuru iliyotumwa kwetu na Mungu Tundu Antipas Lissu.

Tumpokee wa wingi shujaa wetu Tundu antipas Lissu huku tukimuomboleza mzee wetu Mkapa.

Maandamano ya kumpokea Lissu yatakuwa ya amani na hakutakuwa na fujo yeyote.

No Hate No Fear
Alikuwa wapi kwa kipindi chote hicho... Nani kamtuma kuja kugombea uraisi,,, kwa nn hajagombea ubunge.
 
Mapokezi ni ya amani kama tu ilivyokuwa kwenye mapokezi ya Hussein Mwinyi kule UNGUJA na Pemba bwashee. Hakuna haja ya kubeba maji na vitambaa . Tuaenda kufanya kama wana CCM walivyomfanyia Hussein Mwinyi kule Zanzibar

Sawa ila Mimi nitabeba kabisa Maji yangu ya Kuoshea Uso wangu, nitavaa Raba Nyepesi na kuhakikisha Vichochoro vyote Muhimu viko Kichwani.
 
Acha kudandia treni kwa mbele! Wakristo wamezoea kuvaa nyeusi na nyeupe msibani hivyo usije ukajifanya baadaye kuwa nilisema.

Pili mlikuwa na Tahirts zenu jitahidini kuzifua mvae, pia hizo mlizochapisha zivaeni maisha yaendelee.

Mwisho kama kawaida wazee wa kuandamana mitandaoni tunawatakia kila lakheri. Vidole na macho vitaendelea kudumu kwenye keybords zenu.

Pumzika kwa Amani Mzee wetu Benjamin William Mkapa. Tunaheshimu msiba wako na atakaeleta fyoko imekula kwake.

Queen Esther
Queen Esther
Naomba ushuhudie iyo jumatatu kama ni maandamano ya mtandaoni au la!!!

Tunampokea kishujaa mtu wa Mungu Tundu Antipas Lissu huku tukimuomboleza mzee wetu mkapa.

Na mwisho hapo October 2020 yaliyotokea Malawi yanaenda kutokea Tanzania. Usiyempenda Tundu Antipas Lissu anaenda kuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania
 
Sawa ila Mimi nitabeba kabisa Maji yangu ya Kuoshea Uso wangu, nitavaa Raba Nyepesi na kuhakikisha Vichochoro vyote Muhimu viko Kichwani.
Sawasawa ila watanzania na wanachadema tunampokea kwa amani bila vurugu zozote.
 
USIMUHUSISHE MUNGU NA UHUNI WENU NA HUYO TUNDU LISU WENU MNAMCHOSHA SASA HUYO ANA NURU GANI BEBERU MKUBWA HUYO

Naona unasaka mabasha kinguvu hapa jukwaani, sio kila mtu anataka hiyo huduma dogo.
 
Sawasawa ila watanzania na wanachadema tunampokea kwa amani bila vurugu zozote.

Nimesikia mahala japo ni Tetesi kuwa kuna uwezekano mkubwa Anga la Tanzania Siku hiyo likafungwa kwakuwa tunapulizia Dawa ya COVID-19.
 
Tungeomba a cancell flight tumuomboleze na kumhifadhi mpendwa wetu kwanza maana msiba ni Jambo la ghafla tukishamaliza kulia then ndo tusherekee ujio wa mshinda mauti mbeba maono.
Mwaka huu mwenge haujakimbizwa ishukurikiwe corona zindiko limekiukwa chochote chaweza tokea,kupigwa spana kwa wahamiaji, kuondoka kwa mwamba wa siasa za ccm dhahiri Mungu amesikia kilio cha wengi.( Unabii ).
 
Hahaha Genta Kama Genta. Ndege anayokuja nayo inakuja na watalii 100

Nasikia Tetesi kuwa Ndege zote ziwe za Watalii au za Mizigo hazitaruhusiwa Kutua nchini kwani Ndege za ' Wajeda ' zitatawala Anga tu Siku hiyo.
 
USIMUHUSISHE MUNGU NA UHUNI WENU NA HUYO TUNDU LISU WENU MNAMCHOSHA SASA HUYO ANA NURU GANI BEBERU MKUBWA HUYO
Mbona juzi mliwasomba watu kutoka unguja na Tanganyika,kwenda Pemba kumpokea mgombea wenu ili wapemba wamfahamu.
 
Wafuasi wa Lisu na akili imejaa matope!
Hahaaa..... Mkuu km ulikua hujui basi jua leo kua haya mashetani maccm hayashindwi.......
Lkn km ww ni wale wasiofikiri nje ya box basi endelea kubeza......
 
Mbona juzi mliwasomba watu kutoka unguja na Tanganyika,kwenda Pemba kumpokea mgombea wenu ili wapemba wamfahamu.
Wamefeli sn ng'ombe hawa....... Mshenzi Mwingine eti anamtumbua mkandarasi kwa kutokukusanya wananchi....... PATHETIC
 
Back
Top Bottom