Kwani ni nini maana ya Hammaz?Akhi unabishana na mtu anayejiita hammaz? Huyo jamaa anawasingizia wanazuoni tu wala haweki marejeo yao humu.Wapo watu wengi sana watakutajia majina lukuki na rejea nyingi za uongo za wanazuoni wengi waliotangulia . Aqidah ya ahlul sunna wal jamaa ipo wazi kabisa kuwa ALLAH yupo juu ya arshi..ipo hivyo na itaendelea kuwa hivyo.
Hao wanaosema kuwa ALLAH hayupo juu ya arshi yake wanaficha tu aqidah zao , mwisho wa siku atajifunua na kusema ALLAH yupo kila sehemu.
Hata mwanangu mdogo wa mwaka mmoja nikimuuliza suali kuwa ALLAH yupo wapi ,atanijibu kuwa ALLAH yupo juu!!
Zitakuja wala hakuna shaka!Umesahau kutupa marejeo ya hizi hadithi.
Tuko pamoja.Zitakuja wala hakuna shaka!
Hiyo mbingu ya saba ipo wapi?A'rsh ya ALLAH ipo juu ya mbingu ya saba!!
Kabala A'rsh haijaumbwa Allah alikuwa wapi?A'rsh ndio kiumbe kikubwa zaidi kuumbwa na ALLAH .
Hizi Mbingu saba zipo wapi?Wanaadamu tupo chini kabisa ,juu yetu kuna mpangilio wa mbingu saba, then kuna kursiy, then kuna maji na juu yake kuna A'rsh ya ALLAH...then juu kabisa yupo ALLAH.
Haya maswali ni yana mantiki kubwa sana.Hiyo mbingu ya saba ipo wapi?
Kabala A'rsh haijaumbwa Allah alikuwa wapi?
Hizi Mbingu saba zipo wapi?
Hayo majibu yako yanawezekana kama tu unaongelea Mungu kama alivyoelezwa na Biblia. Check majibu yangu mwanzoni mwa mada yatakuongezea kituHaya maswali ni yana mantiki kubwa sana.
Ukitafakari mbingu zimeumbwa lakini zimeumbiwa kwenye nini? Hapa hauna jawabu!
Hivyo palipoumbiwa mbingu huwezi sema ni juu ama chini au kulia ama kushoto na si mbele wala nyuma. Pengine panaweza kusemwa pako juu kwa sababu dunia ipo chini.
Lakini hivi vyote dunia na mbingu na vilivyomo ndani yake vipo wapi? Itasemwa kwenye space. Space itasemwa lakini utakosa jawabu! Hivi vyote vimeumbwa pasipo na mahali yaani ombwe! Yaani hakuna kitu. Na kabla ya chochote Mungu alikuwepo yaani hakuna mbele, nyuma, juu, chini, kulia wala kushoto. Kwa tafsiri nyengine hakuna kilichomfunga wala kilichomkusanya (ametapakaa pasipo na kitu wala pasipo na mipaka).
Ikiwa mbingu na ardhi zimeumbwa pasipo na kitu na kuletwa kwenye hali ya ukitu, aliyekuwepo pasipo na chochote kuwepo ambaye hakukuwa na mipaka wala kilichomkusanya na akaileta hiyo mbingu na ardhi kwenye uwepo pa ambapo hakuna kitu yaani ime hang wapi, huwezi kusema yupo juu! Kwa sababu alikuwepo pasipo na chochote hata hiyo mipaka haikuwepo! Hivyo Mungu hahimiliwi na mipaka! Hayupo juu wala chini, wala kulia wala kushoto, wala mbele wala nyuma.
Hivyo nikiulizwa Mungu yuko wapi sitokuwa na jibu kwa sababu hakukuwa na mipaka iliyomfunga alikuwa ametapakaa. Yaani mahali popote tulipo Bwana Mkubwa yupo! Hata huko pasipo na mipaka ambapo alikuwepo kabla ya kuumba chochote alikuwa ametapakaa kwa kuwa hakuna mipaka hakuna kilichomfunga.
Hivyo nikiulizwa Mungu yupo wapi nitajibu; alikuwepo Mungu kabla ya sehemu au mahali, na alipokuwepo huko huko kabla ya sehemu ndipo alipoku huko huko!
UFO sio viumbe mkuu bali ni kama ndege za aliens.kwenye summarian tablet ushahidisha kwamba alieans ndo walimuumba binadam na step zote na erros zilizo tokea zimerekodiwSi binadamu pekee ndo walioumbwa na Mungu zipo sayari zingine pia zipo na watu na viumbe vingine. Mfano UFO ni viumbe halisi na Wana akili zaidi kuliko binadamu. Yote mapya Yaliyomo kwenye ulimwengu huu yamekuwepo kwenye sayari zingine miaka 3000 kabla. Sayari zingine wao wapo mbele yetu kitechnolojia miaka 3000 mbele
[emoji28][emoji848][emoji848]Wakiwa wanakujibu, wanajibu pia je hadithi ya mnara wa baberi ni kweli au si kweli. Maana ndio hadithi inayozungumzia chimbuko la lugha.
Je huo mnara ulikua na urefu gani hadi Mungu aone binadamu watamfikia?.. maana vyombo vya usafiri vinatoka hadi nje ya dunia
PERFECT [emoji106],Swali zuri japo ukishaelewa msingi linakuwa la kijinga sana. Kwa hiyo nitakusaidia kuuona msingi na kuona kwa nini ni swali lisilo na maana.
Kitu cha msingi hapa ni kuwa yote nitakayoongelea ni kwa mujibu wa Biblia na kwa sababu naamini, kwa sababu nzito tu, kuwa Biblia ni Neno la Mungu na kuwa Mungu aliyejifunua ndiye Mungu muumba mbingu na nchi. Kwa hiyo jibu ni very specific. Kama unataka majibu juu ya jumla sina na wala sitawajibika kujibia miungu.
Biblia inafungua na mstari huu:
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi" - Mwanzo 1:1
Hapo maneno ya msingi ni Mwanzo, Mbingu na Nchi. Mstari huu unatuonesha kuwa kuna kipindi kulikuwa na mwanzo yaani muda haukuwepo ziku zote ulianza katika "kipindi" fulani. Kabla ya mwanzo hakukuwa na muda.
Pili tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi. Mbingu na nchi au ulimwengu (universe) kama unavyofahamika kisayansi ni nafasi. Tunajua kuwa Ulimwengu upo katika muda na nafasi. Muda unatuambia wakati kitu kimefanyika au kimekuwepo na nafasi inatuambia mahali tukio lilifanyika. Huwezi kuwa na muda bila nafasi, kwa sababi ili kitu kifanyike au kiwepo kwenye ulimwengu huu lazima kiwe katika nafasi fulani na huwezi kusema nafasi ni nafasi mpaka iwepo ndani ya muda.
Kwa sababu wakati-nafasi sio mada niishie hapa. Ila ili ulimwengu wetu uwepo ni lazima wakati na nafasi viwepo kwa wakati mmoja. Na hapa Biblia inatuambia Mungu aliumba wakati na nafasi.
Tunajuaje? Kwa sababu Biblia si tu inatuambia Mungu aliumba mbingu na nchi "hapo mwanzo", bali pia inatuambia kuwa huyu Mungu alikuwako tayari kabla ya huo mwanzo. Kwa lugha rahisi kabla ya huo mwanzo (muda) kuwepo, Mungu alikuwepo!
"Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika" Yohana 1:1-3
Na ndio maana jina lake anaitwa NIKO. Yaani baada ya muda Yeye yuko, "hapo mwanzo" Yeye yuko na kabla ya muda Yeye yuko!
"Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake nβnani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu" - Kutoka 3:13-14
Kwa hiyo msingi hapa ni kuwa
1. Ulimwengu na vyote vilivyomo, vinavyoonekana na visivyoonekana viliumbwa hapo mwanzo
2. Muda na Nafasi havikuwepo milele, kuna wakati hakukuwa na wakati wala nafasi.
3. Mungu Yehova Yeye Yuko, kabla ya wakati na wakati utakapokoma.
Tukirudi swali la msingi, ambalo lina sehemu mbili:
Kuuliza Mungu yupo wapi maana yake unadhania Mungu anafungwa na muda na nafasi. Maana ukisema yuko wapi unaongelea muda na nafasi. Mfano tukisema Mwanyuma yuko wapi, jibu litakuwa linaambatana na nafasi na muda. Kwa hiyo jibu la swali hili lina dhahania ndani yake kuwa "wapi" hiyo itakuwa ndani ya huu ulimwengu uliofungwa kwa muda na nafasi.
Basi Jibu lake ni kuwa Mungu yupo kila mahali, katika ulimwengu wetu huu. Lakini kwa sababu Mungu hafungwi na muda na nafasi, basi kuna jibu ambalo linapaswa kufafanuliwa hapa kwamba nje ya ulimwengu huu wa muda-nafasi Mungu Yuko! Kwa sababu nje ya huu ulimwengu hakuna kitu kinaitwa wapi, kwa sababu ili kuwe na wapi unahitaji uwe na muda na nafasi.
Kujibu swali lako kwa ukamilifu ni kuwa Mungu YUKO! iwe ni mahali popote, muda wowote au iwe nje ya muda, Yeye Yuko!
Kabla ya kuumba vyote, hakukuwa na muda wala nafasi. Kwa hiyo kusema alikuwa wapi ni swali la kijinga kwa sababu hakukuwa na wapi bado. Au ukisema Mungu alianza lini ni swali la kipuuzi pia kwa sababu ukirudi nyuma kabla ya mwanzo hakuna muda na hivyo kuanza (muda) hakupo!
Kwa hiyo jibu rahisi ni kuwa kabla ya vyote kuumbwa Yeye alikuwepo. Siku zote Yehova Yuko na ndio maana jina lake ni MIMI NIKO!
Hauna kashata hapo mkuu uniongeze!!?Sayari ya dunia pamoja na na galaxy yetu yenye sayari 9 (solar system) ni changa sana kiumri ukilinganisha na galaxy zingine. Kwenye uumbaji basi solar system ni ya Karibuni.
Swali ni yupo wapi????Majibu ya mungu ni nan yuko wap yapopande mbili kisayansi na kiroho,kisayansi mpaka leo Wana UNANSWERED QUESTION y juu ya mungu na uwepo wake ila mungu yupo na ndie anaesababisha ucku na mchana,kiangazi masika,kucontro moyo oxygen in na carbon out,hvyo ukitafakari saaaaaaaana juu ya mungu utaishia kukufuru ila jua MUNGU YUPO
Kustawi??? Ukiwa na maana gani?? Hicho kiti cha enzi kina kazi gani??1. Mola muumba yuko juu ya mbingu ya saba juu ya Arshi(hiki ndiyo kiumbe kikubwa zaidi kati ya viumbe alivyo viumba Mola wetu mlezi) yake chini ya Arshi kuna maji na juu ya Arshi kuna kiti cha enzi amestawi huko.
2. Dunia na ulimwengu ni katika viumbe vya mwishoni mwishoni kuumbwa na Mola ila kiumbe cha mwisho kabisa kuumbwa ni sisi wanadamu.
3. Kwa jinsi alivyo jielezea na alivyoelezewa na mitume wake ni kuwa amestawi huko ila hajajielezea kama ameketi kwa namna gani
4. Kuhusu sayari nyingine hakuna mahali katika vitabu vyake vinaonyesha hilo ila tunafahamu ya kuwa kuna viumbe ameumba ambavyo hatuvijui na vyenyewe viko katila uwili. Kwahiyo kama imethibitika kweli sayari zipo basi nazo zimeumbwa na Mola muumba.
5. Yeye ndiyo amejaalia uhai katika dunia, na si pengine. Kwa upande wangu mimi binafsi siamini kama kuna uhai katika sayari nyingine kama zipo lakini, na kama kungekuwa na uhai basi mitume wangetuambia.
Shukrani.
Kwa hiyo kusema alikuwa wapi ni swali la kijinga
Mungu yupo wapi??