Mungu nisifikie kukata tamaa

Mungu nisifikie kukata tamaa

Jipe moyo mkuu. Mungu atakubaliki na kukunyanyua zaidi ya alivyomnyangua Yesse. Ukiona giza limezidi ujue kunakaribia kucha. Mungu atakufungulia milango ya rehema hadi utashangaa.
Hiki kipindi napitia maisha magumu sana

Nimefukuzwa kazi

Nadaiwa kodi ya miezi mitatu

A 5000 ya umeme

Sina hela

Ndani nina unga tu mboga na hata mchele sina

Nipo mikoa ya mbali na nyumbani

Nimejifungia ndani nashindwa kutoka coz mama mwenye nyumba ni kivuruge na ananidai 5000

Nina mpenzi ambaye anajitahidi kufahamu kipindi ninachopitia ila bado hapati jibu coz i act as if sina matatizo

Nina siku mbili sijala kwa ridhaa yangu yaani nakula kwa kuibia

Natamani kurudi home nauli sina na naona ni udhaifu mkubwa kurudi kukaa na mama na am 24yrs old

Akili inachoka nahisi kuanguka

EEE MUNGU PAMOJA NA MAPITO HAYA NISIFIKIE KUKATA TAMAA

HAYA NI MADOGO KULINGANISHA NA WENZANGU

NISITAMANI KUJIUA

KWA AKILI YA KIBINADAMU UWEZO UNANISHINDA

NAKUOMBA MUNGU UTIMIZE HAJA ZA MOYO WANGUView attachment 1062423

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Okey nimefurahi kusoma comment yako maana ni nzuri na kiupande fulani imenigusa...

Mimi ni mtu ambaye sio social sana na ninajivunia hilo.. Yaani sina hook ya kunikutanisha na watu sana ila huwa nina kitu kimoja "Ninapokuwa na rafiki bhasi anakuwa rafiki kweli ".. Nina cycle ndogo sana ya watu lakini loyal kinyama kiasi kwamba huwa napata hata ramani ya kuanzia business hadi kazi lakini ni mimi tu mwenyewe nimekaa kwenye mstari wangu.. Ila nimekaa na hawa watu kama brothers na tunasaidiana sana

Unajua ni rahisi kumshauri mtu ajichanganye lakini kwa nature aliyonayo kama yangu sio rahisi ila ndio hivyo hana option..

Kwanza kabisa mimi huwa sipati sehemu kupitia watu ila huwa naset targets zangu tu mkuu.. Huwa naangalia ni kitu gani nataka na ninatakiwa kuwa na nini ili nikipate je, ni skills ama uwezo fulani ????...

Baada ya hapo huwa naangalia ni wapi naweza kuzipata yaani hapo huwa siangalii pesa kabsaaa maana najua hiyo pesa nitapata tu pale ntakapofikia lengo.. Tatizon letu vijana wengi wa 20's ni kutokuwa na targets na kuiangalia sana pesa kuliko outcome utakayopata.. its not working kabisaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Brother we share that part.
Am also not a social person and like you i have a small but reliable company.Na hilo kuhus hawa wadogo zetu umenena vyema kabisa.Targets on whatvto achieve hawana
 
Uwe makini na mawazo ya kujinyonga na tambua changamoto zipo kwa kila MTU

kujifungia ndani ni sawa na kujiongezea msongo mkubwa zaidi

Tafuta ushikaji na vijana,hasa wajenzi na watakupa mchongo wa vibarua na vinalipa..

Kuliko kujifungia huko ndani na mwishowe Maza house atakutimua akihofia kujinyonga,jinsi ilivyo jadi yenu
mbeya hom iringa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza pole sana mdogo wangu kwa unayopitia.
Nimepitia mawazo ya watu na shuhuda zao hakika nimefarijika sana. Maana si siku nyingi nimekuwa kwenye kipindi ambacho sikuwahi hata kukiota kama naweza kukipitia.. Kipindi kigumu sanaa. Nikafikia sehemu nikawa namwambia Mungu aniue tuu nipumzike. Ila nikaja kukaa chini na kujitathmini uwezo nilionao (Kiakili na Kielimu) na zawadi ya watu wazuri wanaonipenda na kunitegemea (wazazi, watoto, mke, ndugu, marafiki n.k) zaidi ya yote na afya njema niliyonayo nikajikuta NATUBU kwa Mungu kwa kukufuru! Na kinachoumiza zaidi ni kwamba haya yote yanakuja baada ya kumjua Mungu! Ila nikaja kutiwa moyo na neno lililo katika kitabu cha Ufunuo 12:7-17, kwamba hii ni vita ya kiuchumi na lazima niishinde (tuishinde) ili Mungu ajitwalie utukufu kupitia kushinda kwangu/kwetu. Si kitu rahisi ila kwa msaada wake yeye Mwenyewe tutashinda zaidi ya kushinda.
nakubali kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rudi kwa Mama haidhuru wakati unajipanga kuliko kuishi kwa mashaka kusiko kwako tena

Sent from my iPhone 5s using JamiiForums mobile App
 
Hiki kipindi napitia maisha magumu sana

Nimefukuzwa kazi

Nadaiwa kodi ya miezi mitatu

A 5000 ya umeme

Sina hela

Ndani nina unga tu mboga na hata mchele sina

Nipo mikoa ya mbali na nyumbani

Nimejifungia ndani nashindwa kutoka coz mama mwenye nyumba ni kivuruge na ananidai 5000

Nina mpenzi ambaye anajitahidi kufahamu kipindi ninachopitia ila bado hapati jibu coz i act as if sina matatizo

Nina siku mbili sijala kwa ridhaa yangu yaani nakula kwa kuibia

Natamani kurudi home nauli sina na naona ni udhaifu mkubwa kurudi kukaa na mama na am 24yrs old

Akili inachoka nahisi kuanguka

EEE MUNGU PAMOJA NA MAPITO HAYA NISIFIKIE KUKATA TAMAA

HAYA NI MADOGO KULINGANISHA NA WENZANGU

NISITAMANI KUJIUA

KWA AKILI YA KIBINADAMU UWEZO UNANISHINDA

NAKUOMBA MUNGU UTIMIZE HAJA ZA MOYO WANGUView attachment 1062423
Hongera kwa kupitia hatua hiyo. Kwanza umejifunza mambo mengi sana katika umri mdogo , pili hutaweza kuwa na akili ya ovyo ukubwani, you will always be smart, strong and confident!

Huwezi kufanana uwezo wa fikra, kuongea na kutenda na mtu asiyepitia maisha hayo ! Utajikuta una uwezo wa maamzi sahihi na busara zaidi kuliko walio wengi katika jamii! Hiyo hali inabidi iendelee six months, utakuwa umepikika na kuiva ! Kukata tamaa ni udhaifu wa fikra na akili.
Big up

asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee pole sana hizo changamoto ndio sehemu ya kukufanya upanuke kimawazo na kiakili, cha kukushauri ni hiki usiwe mtu wa kukaa na kujifungia ndani unamkaribisha shetani na hapo ndipo mawazo mbaya huwa yanakuja.
Mimi ni mmoja wa watu niliopitia changamoto ngumu sana hata Maxence Melo anajua nilipata ajali mbaya sana ya gari nikapata skull fracture, nikapoteza kazi huku bado naumwa nikarudi home kwa mama nilikaa kipindi wakati najiuguza Mama nae akanibadirikia alinifukuza kama mbwa lakini ikabidi niingie kitaa nikawa nafanya kazi yoyote ile tena za aibu sana kutokana na jinsi nilivyokuwa na status kipindi cha nyuma lakini nilijipa moyo nikawa aibagui cha kufanya, mpaka leo nipo nazidi kuimarika na nimepata kazi sehemu lakini bado nazidi kupambana.
Muombe sana Mungu akusaidie lakini unapomuomba Mungu uwe na kitu cha kufanya au unatafuta kitu cha kufanya sio umekaa tu ndani kama Mwali.
Mtangulize Mungu kwa kumshukuru yawezekana hiyo sehemu uliyofukuzawa ungeendelea kukaa pale ungebambakiwa hata kesi ya wizi ungeenda hata kufungwa kwa hiyo kila jambo huwa na sababu zake linapotokea. Usilalamike utamkufuru Mungu. Be Positive na usibague kazi fanya kazi yoyote ile ya halali bado una umri mdogo sana.

asante mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother we share that part.
Am also not a social person and like you i have a small but reliable company.Na hilo kuhus hawa wadogo zetu umenena vyema kabisa.Targets on whatvto achieve hawana
Hili ni tatizo mzee.. Watu hawana targets ndio maana wengi hutafuta upenyo wa kutengenezewa ingawa huwezi kupanda bila ya kupewa na fursa na mtu lakini sio kutegemea watu..

Mimi sio social sana na kama tunashea hiki kitu bhasi nimefurahi mkuu maana tunaeza elewana tukikaa meza moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom