nadry
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 606
- 596
Kama kichwa cha habari kilivyoanza hapo juu wengi watafikiri labda ni utani lakini sio utani ni kweli.
Mimi nimezaliwa Mtwara, mara baada ya kumaliza darasa la saba nikawa sina dili, nikawa niponipo tu kijijini lakini akili zangu zikinituma nitimkie Dar kutafuta maisha.
Nikatafuta vibarua vya kupalilia mikorosho ili nipate nauli ya kwenda Dar maana akili yangu haipo sawa nafikiria Dar tu. Ilikuwa nikiona vijana wenzangu wakija kijijini kutoka Dar mambo yao safi, nguo nzuri wana fedha za kutosha nikapiga mzigo nikapata 170,000/=
Mwaka 2010 nikanda gari pruuu mpaka Dar, breki ya kwanza Tandika Sudani nimeshuka pale sina ramani nashangaa shangaaa sina pa kwenda. Usiku ukaingia nikapata menu nikalala stand.
Siku ya pili nikakutana na jamaa mmoja katika kupiga story nikamwambia mimi natoka Mtwara kumbe na yeye anatoka Mtwara lakini mshikaji alikuwa anafanya biashara ya kuuza mayai, basi nikamwambia mimi ndio nimeingia jana yake kutoka Mtwara, akaniambia mjini kugumu nikwambia nataka nijumuike na yeye tufanye biashara ya mayai akaniambia hakuna tatizo, mshikaji alikuwa anaishi Mbagala mgeni nani.
Siku zikaenda vijihela vyangu vikaisha mtaji ukafa kwasababu ya mahitaji ya kujikimu kila siku. Kutabalisha biashara tukauza nguo za mali kauli, tembezeza sana nguo kila sehemu Dar lkn nikao nikazi ngumu wakati mwingine unaporwa nguo unaporwa hela.
2011 kuna jirani mmoja alikuwa ni fundi ujenzi akanishawishi niwe msaidizi wake ktk ujenzi nimwambia hamna shida.
Site ipo mbweni, basi wasaidizi walikuwa kama watano nyumba ilikuwa ya ghorofa moja. Nyota ilianza kuwaka baada bosi mwenyumba kuniambia niwe mlinzi wa malighafi za ujenzi, mshahara 100,000/= kwangu nilimshuru Mungu sana, huku nalipwa kama kibarua na mwisho wa mwezi nadaka.
Yote kwa yote site ikaisha kila kitu boss akajenga kikota kidogo akaniambia nikae pale kama mlinzi na mshahara ukawa 150,000/=nikashukuru sana mchana naenda kufanya dai waka nyingine usiku pakulala papo.
Mwisho wa mwezi ukifika boss anakuja na funguo za nyumba yote nafanya usafi na ananiletea mshahara wangu.
Mwezi wa kwanza alikuja kama kawaida, mwezi alikuja kama kawaida, mwezi watatu alikuja akaniachia funguo za vyumba vyote akaniambia nyumba anaipangisha kwahiyo nyumba iwe safi muda wote na nisitoke kwenda kokote ili akileta mteja apate kuikagua.
Basi nilikaa na funguo nisubiri boss alete wateja miezi minne ikapita kimya na mshahara wangu nilikuwa sijapata nikaamua kwenda hewani kumtafuta boss simu yake haipatikani. Miaka 10 imepita sijamuona boss na namba yake baada ya miaka ikawa amepewa mteja mwingine.
Mwaka jana niliamua kujilipua nikaamua kuipangisha ile nyumba 700,000/= kwa mwezi mpangaji aliponiona nikamwambia mimi ndio mwenyumba alikataa maana nipo kisela na nimechoka kimaisha na hajui kinachoendelea kuhusu nyumba.
Swali ninalojiuliza yule boss yupo hai kweli maana miaka 10 imepita. Wananzengo au nimekosea kuipangisha.
Mwenye ushauri wowote anishauri