Mungu Haishi. Maana Si Kiumbe

Kitabu kuandikwa " Mungu akasema" au kikaandikwa "mimi Mungu nasema" ni maamuzi ya muandishi. Maamuzi ya muandishi si maamuzi ya miungu. Haitbibitishi kama vimetoka kwa miungu, hiyo ni style tu ya uandishi.
 
Babu zetu walio ishi na kufa kabla ya hivi vitabu havijaja,walimjua Mungu ?
Quran 16: 36

Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.


Babu zako walishapata muonyaji ila kama kawaida walimdhihaki au hata kumuua mwonyaji kama mnavyofanya sasa vitukuu vyao.
 
Kwahiyo sasa Mungu yupo na sifa gani....yaani Hayupo hai na wala hafi?

Upo sawa kichwani kweli au umeamka na hangover?
 
Majibu ninayo ila muda wa kukwambia sina maana ushaufanya moyo wako kuwa mgumu
Moyo wangu si mgumu kama Kuna Ukweli. Mfano Wewe umezaa mtoto huyo Mtoto Asipokupa Hela Utamlaani!? Kama Ungekuwa na Uwezo wa Kumlaani

Sasa Mungu amekuumna Halafu bado anataka Vitu kutoka Kwako je Yeye kakosa Nini Mpka aombe sadaka ili Aridhike
 
Sasa haya ni maneno ya kitabu walichoandika wakoloni. Nani kawambia miungu lazima igombanie vitu pale ilivyoandikwa,"ingekua hivyo basi kila Mungu angelichukua alivyoumba".
Wewe unajuaje kama miungu iligawana kuumba viumbe tofauti kwenye sayari tofauti utajuaje? Hata waarabu walioandika kuran hawawezi thibitisha chochote.
 
Sayari zipo nyingi. Sio lazima miungu igombanie ardhi ya dunia hii. Inaweza kugawana. Hakuna anaejua chochote
 
Kitabu kuandikwa " Mungu akasema" au kikaandikwa "mimi Mungu nasema" ni maamuzi ya muandishi.

Basi Vitabu ni vya Waandishi si vya Mungu wala mtu asiseme mwandishi aliongizwa na Roho Mtakatifu kuandika kama Maamuzi anayo yeye mwandishi aandike ajuacho

Maamuzi ya muandishi si maamuzi ya miungu. Haitbibitishi kama vimetoka kwa miungu, hiyo ni style tu ya uandishi.

Haya Ndio ukweli kwamba Vitabu vingi ni maamuzi ya Waandishi ndio maana Vitabu hivyo vinaupotoshaji mwingi. Unaambiwa Injili ni ya YOHANA ila Si Yohana aliyeandika. Kama Angekuwa ni Yohana basi Tungetakiwa kusikia kwamba Mm Yohana nilipanda Mlimani na Yesu nikamuoma Yesu akiongea na Musa na Elia
 
Watu wamepotoshwa Ndugu yangu. Mungu ameumba Viumbe wengi samaki.. Tembo.. Milima.. Bahari.. Mito.. Malaika.. Majini n.k halafu Eti binadamu tu ndio afanane na Mungu

Halafu kwenye Mahubiri unaambjwa tena Hana Wa Kufanana Naye
Shida ni watu hawataki kujifunza historia za chimbulo la hzi dini ktk mlengo wapili
 
Hao tunajua Wanaishi kama Yalivyo majini n.k Maana Wapo katika Sayari yao na Si Hii Tunayoishi sisi wangekuwa wanaishi hapa Kwetu tungejua Wapo Mtaa fulani
Wewe Umejuaje kama yanaishi kama yalivyo majini? Na hiyo sayari yao inaitwaje? Na kama umeweza kujua ya kwamba uthibitisho wa hao malaika kuishi hakujahusisha wewe kuona wakipanga mtaani kwako au kujua walikopanga asa ni vipi kuishi kwa Mungu unataka mpaka aonekane mitaani au kujulikana nyumba aliyopanga?
 
Ukileta vitabu kumtetea Mungu Unakuwa Unaendelea Kujipotosha zaidi
 
Ndo apo sasa??
 
Kuna Elimu kubwa Hapa ndugu yangu

Malaika wanaonekana kwa Macho Na Majini pia yanaonekana kwa Macho. Wametoka sayari Yao kuja Duniani kimagendo

Refer Biblia yako kama Ww ni Muumini wa Huko Maria Aliyemzaa Yesu alisema Alimuona Malaika Gabrieli.. Wale walioenda kwenye Kaburi Pia Waliwaona Malaika Waliwaambia kuhusu Yesu

Refer pia Biblia yako kuhusu mji wa Sodoma na Gomora Wale Malaika wanajivika Miili Ya Binadamu tu
 
Ni kweli.
Miungu haijawahi kusema chochote.
Ni wakoloni waliotuletea hizi dini ndio wanaoendesha mawazo yetu na wala si miungu bali ni wakoloni.
 
Mtoa maada Mungu ambaye jina lake halisi ni Yehova sio kiumbe kwaSABABU HAJAUMBWA
 

Kwahiyo wewe reference yako ni biblia je unaamini vilivyomo kwenye biblia? Tunajadiliana kimaandiko au kwa uelewa wako? Kama kimaandiko basi biblia hiyo ambayo uliotumia kuniaminisha mimi kuwa malaika wanaonekana kwa macho si ndio hiyo hiyo iliyosema kuwa Mungu anaishi milele na ukakataa na kudai kuwa Mungu hana uhai? Sasa ninapokuuliza maswali na ukatumia reference ya kitabu cha dini kuniaminisha mimi, maanake hapo hatupo kwenye facts bali tupo ndani ya imani humo humo za kidini.
 
Kwahiyo hata Yale Mapepo aliyokuwa anatoa Yesu si ya kweli. Vitabu vyote ni Uongo
Nilipokuwa mdogo nilikuwa najua mawingu ndo Mungu, unadhani ningekuwa na uelewa huo Hadi Sasa ,nikaandika kitabu kumuelezea Mungu, unadhani ungeunga mkono mawazo ya kitabu changu?
 
Kwahiyo wewe reference yako ni biblia je unaamini vilivyomo kwenye biblia?
Nimekupa Reference hiyo ili uamini kwanza Kama Upo huko. Ningekupa Stori zingine tofauti usingeniamini na Ndivyo Vitabu vilivyoandikwa na Hao Malaika na Viumbe vingine

Tunajadiliana kimaandiko au kwa uelewa wako? Kama kimaandiko basi biblia hiyo ambayo uliotumia kuniaminisha mimi kuwa malaika wanaonekana kwa macho si ndio hiyo hiyo iliyosema kuwa Mungu anaishi milele na ukakataa na kudai kuwa Mungu hana uhai?

Nimekujibu hapo juu kwamba Nimetumia Hiyo kama Reference itakayo amini kwamba viumbe wengine pia wanaishi na Wana uhai.

Na Tunajadili kwa Kutumia Akili Timamu hatujadili kwa kutumia Maandiko. Viumbe hao Walikuwepo na Walikuwa wanaonekana kabla ya Kitabu chako hicho ndugu


Sasa ninapokuuliza maswali na ukatumia reference ya kitabu cha dini kuniaminisha mimi, maanake hapo hatupo kwenye facts bali tupo ndani ya imani humo humo za kidini.

Nikikuambia Mengine yanayotokea hapa Ulimwenguni utayaamini!? Maana Nataka kwanza Nikuambie Yale unayoyamini uliyoambiwa ukapotoshwa Halafu Baadae ndio uambiwe Yaliyo nje ya Vitabu.

Maana Malaika na Majini yanaonekana kwa Macho kitu ambacho kwenye Vitabu pia Ipo ingawa si kwamba Walianza Kuonekana pale kitabu chako kilipoandikwa walikuwa wanaonekana kabla ya Vitabu hivyo ndugu yangu
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa najua mawingu ndo Mungu, unadhani ningekuwa na uelewa huo Hadi Sasa ,nikaandika kitabu kumuelezea Mungu, unadhani ungeunga mkono mawazo ya kitabu changu?
Sijaelwa vizuri haya Maelezo yako ndugu yangu
 
Mtoa maada Mungu ambaye jina lake halisi ni Yehova sio kiumbe kwaSABABU HAJAUMBWA
UPO SAHIHI

Ingawa Mungu hana hayo majina Mnayompa. Yehova.. Yire.. Yahe.. Allah.. Ukifuatilia kwa Makini hayo ni Majina ya Viumbe Wanaojipa Ukuu wa Mungu asili ya Majina Hayo mengi ni Miungu siyo Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…