Mungu Haishi. Maana Si Kiumbe

Mungu Haishi. Maana Si Kiumbe

Pole sana ndugu, maadam umeamua kuanza safari ya kumjua Mungu atakusaidia uendelee kumwelewa zaidi. Safari ndio umeianza lakini weka akili yako wazi kupokea michango ya wadau upate uelewa zaidi.

1. Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake. (Udongo jumlisha pumzi ya Mungu).
2. Mungu aliumba mbingu na nchi na vyote viijazavyo.

Inawezekana vipi kisicho na uhai kiumbe vilivyo na uhai.

Mungu akasema......na ikawa. Kabla ya kusema nini kinatangulia. Ni kuwaza au mawazo. Kwahiyo mawazo (niite consciuosness kwa kizungu cha Uingereza) ndiyo kiini cha uhai. Leo wewe ukipoteza consciousness umekwisha.

Endelea kujifunza ndugu. Mungu yu hai na anaishi milele.
 
Kitu kisicho na uhai kinaweza kuumba viumbe vyenye uhai
Wewe ni Binadamu una uhai ila Unatengeneza magari na Vitu visivyo na Uhai kama Wewe. Muujiza wa Mungu umetenda hayo Yote umeumba

MALAIKA, MAJINI, MASHETANI, n.k nao wameumbwa kama Wewe na Hawaonekani na Hata Mchawi anakuja Kwako anachukua Vitu na Kukuwangia Ila Humuoni jiulize kwanza Hayo kabla Hujauliza muujiza wa Mungu umetendaje Haya Yote

Labda kama Huamini kama Huyo huyo aliyemuumba Malaika ndio kamuumba Jini na Wewe binadamu

Na pia Ujiulize kiliumbaje Mawe na Miamba Ambayo haina Uhai pia
 
Pole sana ndugu, maadam umeamua kuanza safari ya kumjua Mungu atakusaidia uendelee kumwelewa zaidi. Safari ndio umeianza lakini weka akili yako wazi kupokea michango ya wadau upate uelewa zaidi.

1. Mungu alimwumba mtu kwa mfano wake. (Udongo jumlisha pumzi ya Mungu).
2. Mungu aliumba mbingu na nchi na vyote viijazavyo.

Sijakataa Unaposema Hayo kwamba Mungu ameumba ila Unaposema Amekuumba kwa Mfano wake. Je malaika na Majjini wameumbwa kwa Mfano wa nani!

Maana Unaposema Una Mfano wa Mungu basi Mungu wako ana Upendeleo

Inawezekana vipi kisicho na uhai kiumbe vilivyo na uhai.

Mawe, Kokoto, dhahabu almasi zina Uhai ndugu yangu??. Au vyenyewe havijaumbwa

Mungu akasema......na ikawa. Kabla ya kusema nini kinatangulia. Ni kuwaza au mawazo. Kwahiyo mawazo (niite consciuosness kwa kizungu cha Uingereza) ndiyo kiini cha uhai. Leo wewe ukipoteza consciousness umekwisha.

Mungu hana Sifa hizo ulizoziweka Hapo. Mungu hasemi na yeyote yule. Kuwaza na Kuchanganua ni Viumbe ndio wana Sifa hizo

Endelea kujifunza ndugu. Mungu yu hai na anaishi milele.

Kitu kilicho na uhai lazima Kife. Kuishi ni sifa za Viumbe ndugu yangu. Mungu hana Uhai na Wala haishi
 
Wewe ni Binadamu una uhai ila Unatengeneza magari na Vitu visivyo na Uhai kama Wewe. Muujiza wa Mungu umetenda hayo Yote umeumba

MALAIKA, MAJINI, MASHETANI, n.k nao wameumbwa kama Wewe na Hawaonekani na Hata Mchawi anakuja Kwako anachukua Vitu na Kukuwangia Ila Humuoni jiulize kwanza Hayo kabla Hujauliza muujiza wa Mungu umetendaje Haya Yote

Labda kama Huamini kama Huyo huyo aliyemuumba Malaika ndio kamuumba Jini na Wewe binadamu

Na pia Ujiulize kiliumbaje Mawe na Miamba Ambayo haina Uhai pia
Mkuu umeniquote ila sijaelewa point yako ni nini hasa?
 
Quran 2:255

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.

Mkuu umeniquote ila sijaelewa point yako ni nini hasa?
Umeniuliza inakuwaje Mungu si hai akaumba Kitu kisicho hai. Nimekujibu kwa kukuambia Ameumba Vitu vingi Visivyo na Uhai pia na Vilivyo na Uhai

Mawe/Michanga/Dhahabu hayana uhai ila kayaumba. Kwa Mantiki yako ili jiwe liumbwe Mungu angetakiwa asiwe hai ili aliumbe hilo jiwe.

Unaposema Mungu yu Hai Maana Yake Umemuweka Kama Kiumbe ulivyo wewe wakati Hayupo hivyo. Vilivyo na Uhai na Kuumbwa Hufa
 
Endelea kuamini unachokiamini.
 
Mwanadamu kumuwaza Mungu hutaweza kumpatia picha mwisho unaweza ukajikuta unakufuru tu.

MWENYEZI MUNGU YU HAI MILELE DAIMA.

Hivi ulishwahi kujiuliza hizi mbingu zimewezaje kuwa juu yetu pasi na kuwekewa nguzo yoyote ile unayoiona?

Ni nani anaezishikilia hizi mbingu zisitufunike tulio chini yake?

Vp huyo anaezishikilia akisinzia sisi tuliochini yake tutakuwa katika hali gani?

Ukishajiuliza swali hili ndio utajua kuwa MUNGU yupo hai au amekufa!
 
Fikiria hivi! Kilichasababisha wewe ukawepo ni wazazi wako. Na wao wazazi wao, ukienda hufiki mwisho ila utagundua kuna kisababishi cha mwanzo. (First cause) Hicho hakina ihai? Huenda ni uhai usiokuwa na mwanzo au mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom