Mungu Haishi. Maana Si Kiumbe

Mungu Haishi. Maana Si Kiumbe

So kwa akili yako wakati anaumba hivi vyote alikuwa Hai au amekufa?
Jua maana ya Neno Hai kwanza ndugu yangu. Muujiza wake ndio ulioumba haya Yote unayoyaona na Usiyoyaona

Siyo lazima kitu kiwe hai ndio kiumbe kitu. Kwani Ukiota Mzee wako amekuja ndotoni huyo mzee wako yupo Hai?
 
Hata malaika na Majini yanazaliana kama Wewe na Mimi Mkuu ingawa Wewe huyaoni kwa Macho.

Sawa mimi siyaoni kwa macho. Je wewe unayaona. Ikiwa hauyaoni umejuaje yanazaliana?

Hiyo ni imani yako na umeibeba ulimwengu wako wote unauona hivyo.

Mimi siyo imani yangu hiyo na siamini katika hayo yote na hayapo. Kwangu huo sio ukweli.
 
Daah

Kwa hiyo chombo kama chombo unaweza kukila bila msosi ndani yake? Imani na chombo ni sawa. Chombo kidogo msosi kidogo, chombo kikubwa msosi mwingi. Hakuna chombo hakuna msosi.

Imani.
Chombo cha imani ni mtu mwenyewe.
 
Mkuu napenda sana watu wanaofikiri Kwa akili huru, Mimi nishaanza kuamini shetani kwa maana ya kiumbe hayupo, ila mambo yote negative ie wizi, uzinzi, uuaji, matusi etc ndo shetani, yaani shetani ni vitendo na sio kiumbe. Kwasabu nafikiria Yana Lucifer (shetani) kaumbwa na Mungu (kama tunavyofundishwa) alafu baada ya kumuasi, Mungu anapigana vita na yeye. Yani Mungu anapigana vita na kiumbe chake??? Je malaika Michael, au Gabriel naye akiasi itatokea Tena vita huko mbinguni, je wakipigwa wataenda kuungana na Lucifer (shetani tunayehadithiwa) au watantengeneza nao ufalme wao??
Hao wanaopigana Si kwamba Wanapigana na Mungu mwenye Vyote ila Wanapigana Viumbe wao kwa Wao kupigania Mamlaka Fulani kama Sisi Tunavyopigana Huku duniani, Marekani anataka Kupigana na Urusi. Urusi anataka Kupigana na Ukraine. Tanzania na Uganda

Sasa Hawa Viumbe wakaja Huku wakawarubuni Binadamu na Kuandika vitabu na Kuiweka Hiyo Vita Kama Ni kwamba Shetani alikuwa anapigana na Mungu na Akamtupa Duniani halafu Huyo huyo Shetani akaenda Kupiga Stori na Mungu ili akamjaribu tena Ayubu ambaye ni Binadamu. Vitu ambayo kwa Akili timamu haviingii hakilini

Ukiendelea kusoma Vitabu hivyo utagundua kwamba Kuna baadhi ya Mambo Mungu anayezungumziwa kwenye Vitabu alikuwa akitumia MALAIKA wake wakifika eneo hilo wanashindwa. Sasa Unajiuliza hivi Mungu mwenye Vyote anaweza Tuma Jambo likashindikana kweli
 
Kumekuwa na Dhana POTOFU na Dhana Hii imewaharibia sana Akili watu wa madhehebu. Unakutana na Mtu anakuambia, Mungu wangu yu Hai

Kitu kilicho hai ni kiumbe tu. Mwenye Enzi Mungu yupo nje kabisa na Vinavyoishi, yeye aliviumba Viwe vinaishi na akaviweka Katika Sayari mbalimbali vikae huko

Yeye hakai na Viumbe vyake wala Hasaidiani mambo yake na Viumbe vyake alivyoviumba.

Kwahiyo ni makosa makubwa kumfananisha Mwenye Enzi Mungu na Uhai wa Viumbe vyake na kusema Eti Yeye yu Hai, kumpatia Sifa za Viumbe (anakaa, anasema, anatuma malaika, anatamaa, ana wivu n.k n.k ni Makosa na Upotofu mkubwa sana unaoendelea huko Wanakoabudu

Mmeambukizwa Imani za Viumbe waovu na Wenye dhambi (Mashetani, Malaika, Wachawi n.k) Na mnapokuwa mnamwabudu Mungu huyo mnamfananisha na Nyie mlivyo. Mnampa Sifa za Nyie mlivyo(uhai, tamaa, wivu, Utakaji wa vitu). Mungu hana Sifa za Ubinadamu wala sifa za kiumbe chake chochote kile


ASANTENI
Hakika kama Mungu aishivyo, akupe haki yako!
 
Shida inakuja miungu haujawahi sema chochote kile. Zaidi ya wakoloni kutuletea vitabu wakidai miungu inataka nini. Lakini miungu yenyewe haijawahi kusema kitu.
Ndio mjue kwamba Mmepotoshwa sana. Maana Hakuna Sehemu Mungu kaongea zaidi kitabu kinakuwa MUNGU AKASEMA.. MUNGU ALISEMA. Maana yake Hapa Mungu anasimuliwa

Kitabu akisema. MIMI MUNGU NASEMA. MIMI. MUNGU NAKUAMBIA HIVI.. MIMI MUNGU NATAKA UNIABUDU HVI

vyote vinamasimulizi ya kusimulia Mungu kama Hadithi
 
Ukisema nina mwili ni sahihi lakini mimi sio huo mwili.

Ila wewe unakuwa ni Nini?

Huo mwili ni wangu nimepewa na hili silikatai japo unaniwekea maandishi ya kujikana.

Nina mwili ndio.

Kwahiyo Siku ukifa watu wakakuta Mwili wako Upo sehemu watasema Huyo si Bill itabidi waende kumtafuta Bill sehemu alipo
 
Mungu kama hana sifa ya kuishi basi hayupo, ili awepo lazima awe na sifa ya kuishi. Na kuhusu kutokuwa na sifa ya uhai. Embu tuambie uhai ni nini? Na kinyume cha neno uhai ni nini? Kama Mungu hana uhai atakuwa ni mfu
 
Mungu kama hana sifa ya kuishi basi hayupo, ili awepo lazima awe na sifa ya kuishi.
Basi Mngekuwa mnaishi naye Mtaa Mmoja. Kama Atakuwa anaishi basi Ungejua Amepanga au Amejenga Sehemu fulani na Hizo Sadaka na Zaka msingekuwa mnapeleka Kanisani mngekuwa Mnampelekea Sehemu anayoishi.

Viumbe waovu wamewapotosha Sana


Na kuhusu kutokuwa na sifa ya uhai. Embu tuambie uhai ni nini? Na kinyume cha neno uhai ni nini? Kama Mungu hana uhai atakuwa ni mfu

Viumbe ndio walitengeneza Uhai. Na Uhai una Mwisho maana Yake Kufa. Ukimuweka Mungu kwenye Sifa Hizo basi Mungu Kuna Siku Atakufa kitu ambacho najua Hukubaliani macho pia kwamba Mungu atakufa. Kama Hawezi kufa Basi Hana Uhai
 
Mungu hafanani na kitu chochote alafu hapo Mungu kaumba mtu kwa mfano wake. Inafikirisha sana
Watu wamepotoshwa Ndugu yangu. Mungu ameumba Viumbe wengi samaki.. Tembo.. Milima.. Bahari.. Mito.. Malaika.. Majini n.k halafu Eti binadamu tu ndio afanane na Mungu

Halafu kwenye Mahubiri unaambjwa tena Hana Wa Kufanana Naye
 
Mwanadamu kumuwaza Mungu hutaweza kumpatia picha mwisho unaweza ukajikuta unakufuru tu.

MWENYEZI MUNGU YU HAI MILELE DAIMA.

Hivi ulishwahi kujiuliza hizi mbingu zimewezaje kuwa juu yetu pasi na kuwekewa nguzo yoyote ile unayoiona?

Ni nani anaezishikilia hizi mbingu zisitufunike tulio chini yake?

Vp huyo anaezishikilia akisinzia sisi tuliochini yake tutakuwa katika hali gani?

Ukishajiuliza swali hili ndio utajua kuwa MUNGU yupo hai au amekufa!
Acha kuwaza ujinga hakuna kitu kinachiitwa mbingu space ni infinity na ulimwengu unazidi kutanua kwa spidi ya mwanga .unayoiina juu sio mbingu bali ni mwisho wa upeo wa machi yako ,huko juu hakuna mwisho
 
Kabla ya shule ulikuwa unajua kuna herufi A?

Maswali mengine ujijibu mwenyewe.
Unamaanisha Shule hizi za Wakoloni.? Kabla ya Wakoloni ndio A ilikuwa inajulikana na wazee wetu walifundisha

A- A
B-Be
C-Che
D-De

Moja ilikuwa inaitwa Mosi
Mbili ilikuwa inaitwa Kibiri
Tatu ilikuwa inaitwa Bhitatu
Tisa ilikuwa inaitwa Kenda

Wewe umekaririshwa kwamba Wazungu ndio wamekuletea hesabu. Kumbe walikuta watu wanajua ila Wakaita Elimu ya Kishenzi
 
Back
Top Bottom