Mungai amlipua Lowassa kwa propaganda anazofanya

Mungai amlipua Lowassa kwa propaganda anazofanya

Status
Not open for further replies.
Mungai kuna kitu amesahau, yeye ndiye aliyefuta michezo mashulen, yeye ndiye aliye tuchanganyia masomo, physics na chemistry kuwa somo moja
 
Mungai kuna kitu amesahau, yeye ndiye aliyefuta michezo mashulen, yeye ndiye aliye tuchanganyia masomo, physics na chemistry kuwa somo moja

ni kweli kabisa lakini pale anapoona mapungufu upande wa mwenzake lazima ayaseme na nina mpongeza kwa hili
 
Mi nadhani Lowasa ndie mtu anaetusumbua kwa sasa hatuli wala hatulali jamani' haipiti siku huyu mtu hajatajwa humu jukwaani' yani ni kama vile mtu ameachana na men wake au manzi wake then bado anaonyesha kumfatilia anayoyafanya=interst
 
Wazo na msukumo ulitoka kwa nani kama si yeye.Mungai akili yake hakuwa nayo wakati akiwa waziri wa elimu labda kama aliyemuazima kamrudishia.

Aliondoa elimu ya michezo shuleni akavuruga masomo ya sayansi labda kwa makusudi kwa vile anaaminika ni Mkenya.Ndipo alipokabidhiwa dhamana Mama Sita akasema pale bungeni aliyefuta michezo mashuleni hana akili.Sasa leo anakuja na hekaya za abunuwasi akafie mbali kama Nepi alivyosema..... wanasubiri kufa.

Pamoja na mapungufu ya Mungai,wahenga wanasema, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kasema ukweli leo, LE hakujenga chochote kati ya hivyo anavyojinadi kuvifanya, hilo halibadiliki, asirubuni wananchi kwa kuusaka uongozi wa juu.
 
Naamini tutakapopata uelewa halisi wa democrasia na soko huria na kujenga mazingira sahihi kwa haya kukua basi tutakuwa tumepata jibu. Swali lina baki ni vipi?

Mimi naweza jibu simply time will tell. Je hili litatosha kuwa jibu?Kwangu mimi naona ndilo jibu linaloweza kuwa sahihi.Sababu ya kupendelea jibu hili ni hii:

Democrasia inavyopanuka ndivyo opportunities zinavyozidi kuwa sawa kwa wote.Na free market inakuwa vizuri ktk democrasia.Free economy inamfanya kila anyejituma na kuwa na uwezo kufanikiwa.

Kufanikisha hili tunahitaji kuweka mazingiza safi na huru kwa ukuaji wa democrasia na soko huria.Nikimaanisha usawa na free enviroment.Hapa bado serikali haijaweza kuaichia huo uhuru ingawaje si kwa ni mbaya kwani watanzania bado hawapo tayari kuhimili hilo.

Mojawapo ya vitu vinavyoleta maana ktk democrasia na soko huria ni pamoja na elimu sahihi.Sasa hapa elimu sahihi ya washikadau ktk mazingira ya Kitanzania ni balaa jingine.Na hili si tu kwa tabaka la wasiofika shule,bali tabaka zima la wasomi wa Kitanzania.Wasomi wetu wetu wa kitanzania wana perspective tofauti kuhusu utandawazi democrasia, maendeleo ya sayansi na teknologia pamoja na mahusiano yetu na mataifa yaliyoendelea kwa ujumla.Sasa kupotoka kunaanzia ktk tabaka la wasomi na wanachuoni na kuendelea kupotoka kunajizidisha hadi kwa raia.

Raia wamekuwa wakijengewa hofu na mtazamo potofu kuhusu democrasia kabla hata mfumo wa vyama vingi kuingia na baadaye hali hiyohiyo ikajikuta ikiingia ktk utandawazi.Leo hii wasomi wetu hawajaonesha nia madhubuti na na kuandaa mipango ambayo si tuu itatuwezesha kulitua soko la marekani kupitia AGOA bali kufanya hata kaujanja tuweze litumia vizuri zaidi ya wenzetu.Soko la Marekani ni soko Tamu na lenye utajiri mkubwa kiasi cha kufanya kila taifa Duniani kupigana kikumbo kulifuata.

Usalama wa raia na mali ndio kitu cha kwanza kuangaliwa,kutoka usalam wa raia na mali zao,bima ndio inatakiwa ifuatie ili kutoa uslama kwa makampuni, baada ya bima mabenki yatakuwa huu kuchukua risk ktk kulegeza masharti, unafuu wa masharti nio utaleta uhuru wa kiuchumi kwa mtanzania ktk kuanzisha chanzo cha mapato.Ushindani ktk soko huria utamlazimisha kila mtu kutafuta usahihi kwa kila muda unaojishuhulisha ktk biashara. Kupanga kodi kwa usahihi kutaleta mvuto ktk biashara halali zaidi na hivyo kuachia uchumi kwa wote.

Kufikia maendeleo kunahitaji ufanisi ktk kila sector na pengine kuanguka kwa wale wasio imara.Hapa namaanisha kuweza kuwa mshindani na kama huwezi ushindani basi uweze jibadili na kuanzisha njia nyingine ila legho ni kujikomboa.Sasa hali hii haijaweza hata fanywa na wasomi wenye kila kitu elimu na njia za kupata mitaji ila wanakosa kitu kimoja ubunifu.Tunavyozidi kubuni vitu ndio tunavyofungua mzunguko wa hela na mifumo ya kiuchumi.

Kutokana na mapungufu haya na mengine ni wazi kuwa tutajifunza kupitia makosa, kutakuwepo na wale watakaoenguliwa na kujiengua hadi pale watakapopatikana waelewa na pale mazingira yatakapokuja kuwa mazuri na huru.Hapa hapatakuwepo watu dhaifu kiakili kwa wakiwepo basi watakuwa wakitumika na kama hawatabadilika basi watajikuta wakibaki wakitumika.

Kwa hiyo kwa jamii yetu nadhani muda ndio utasema na kutupa jibu. Tutashuhudia wengine wakifanikiwa tutashudia tukishindwa na hapo ndipo tutakuwa tumejenga jamii yetu kitaaluma na zaidi tutakuwa na uelewa sahihi wa mazingira. Huku kuelewa mazingira ndipo kutakapotusaidia tafuta njia ya kuyatawala au kuishi ndani yake.

Hapa elimu sahihi ndio itaongoza majadiliano sahihi na hivyo kutupa majibu sahihi na utendaji sahihi popote na muda wote.
Ahsante.
Khaaaas we nae hata aibu huna!???
 
MUNGAI KASEMA KWELI KABISA.
LOWASSA HAJAJENGA SHULE ZA KATA WALA CHUO KIKUU DODOMA.
MAMBO HAYA YAMEANZA KWA MKAPA.

WAFUASI WA LOWASSA TUAMBIENI KITU GANI KAFANYIA NCHI YETU? Hili tumchague... Mimi sioni kabisa zaidi ya ufisadi komavu....
Mimi ccm hikimpitisha naondoka ccm na familia yangu yote...
 
Lakini in fact Lowassa ni mdandiaji wa hoja na projects za watu,ukitaka kushtukia lowassa kua ni problem muulize swali lolote la ubadhilifu na ufisadi utagunda hana kitu na magnitude za kupambana nayo kwa sababu na yeye ni mmoja wapo
 
Mungai ni mshenzi wa tabia,vitendo na kauli........huyu jamaa alinifanya nisome fizikia na kemia kama somo moja!!!!Kaharibu elimu na ndoto za watoto wa Tanzania afu leo anajifanya ana hekima saaaana,,,,,Akafie mbali huyu jamaa sina hamu nae
 
Eti nimesoma history ilihal niko Technical school.....kafuta masomo ya ufundi,kilimo!!!!!!!duh yawezekana ni Mkenya kweli ase
 
Naona Mungai anamuumbua mheshimiwa rais kabisa badala ya Lowassa.
Sasa Kikwete ameanzisha nini?
 
Mungai tutamkumbuka kwa kuchanganya Physics na Chemistry pamoja na kufuta masomo ya Kilimo na Biashara.
 
Lakini in fact Lowassa ni mdandiaji wa hoja na projects za watu,ukitaka kushtukia lowassa kua ni problem muulize swali lolote la ubadhilifu na ufisadi utagunda hana kitu na magnitude za kupambana nayo kwa sababu na yeye ni mmoja wapo


mwekundu..

Inakuwaje mkuu.. Long time no see you mkuu.

Back to the point

Lowasa raisi 2015 either kwa mvua au kwa Jua..
 
Last edited by a moderator:
Eti Mungai boga, ni sahihi.Alivuruga elimu,akafuta michezo mashulen.TRUE.Ni Mungai huyuhuyu alisimamia uanzishwaji wa shule za kata.Eti mungai ana asili ya Kenya,true kabsa.Na ccm ni hamnazo coz walmteua wazr ilihari wakijua ni mkenya,true indeed.kama kuna mtu anabsha ana walakin.
 
Mungai unatuchelewesha.wewe ndio umeharibu elimu ya tz ili uuze vitabu vyako.kaa kimya speed ya saizi huiwezi.
 
Kama kuna mtu ameua elimu Tanzania, basi ni Joseph Mungai...

SIjui anapata wapi courage hata ya kusimama na kubwabwaja

ANyway, hata Lowassa needs to relook at his strategies na kujipanga upya, inaonekana ana timu yenye armateurs wengi sana kwenye campaign trail yake na ameamini watu wasiomtakia mema kwenye safu yake, kuna strategies anatumia kwakweli zinatia shaka...

Mipango ya timu yake inaonyesha ni jinsi gani hatufai, haina miguu wala kichwa.
 
Mungai ana credibility ipi ya 'kumlipua' Lowasa? Waandishi maganga njaa bhana! Ndio maana polisi wanatandika virungu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom