Mume Wangu Hataki Kunipiga, Nataka Talaka

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Mume Wangu Hataki Kunipiga, Nataka Talaka'
4515378.jpg

Friday, May 21, 2010 10:59 PM
Mwanamke mmoja nchini Iran amemfikisha mumewe mahakamani akidai talaka kwakuwa mume wake hajawahi kumpiga hata siku moja. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 24 [jina kapuni] alifungua kesi katika mahakama ya masuala ya familia mjini Tehran akilalamika kuwa mumewe hampigi hivyo anataka apewe talaka.

Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku la nchini Iran, mwanamke huyo aliiambia mahakama "Mume wangu ananitumikia na kunitunza vizuri sana lakini mimi nataka awe ananipiga, kama hawezi basi naomba anipe talaka yangu".

Mume wake ambaye ana umri wa miaka 28 alijitetea mahakamani "Mke wangu nampenda sana, sioni sababu ya kumpiga au kutumia maguvu dhidi yake".

Kwakuwa mwanamke huyo alisisitiza kuwa anataka awe anapigwa na mumewe au la apewe talaka, mahakama ilimruhusu mumewe awe anamshushia kipigo mkewe siku moja moja ili kuilinda ndoa yake.

Mumewe kwa shingo upande alikubali na aliahidi kuwa atakuwa akimshushia kipigo mkewe ili kumridhisha.
 
Huyo mama inabidi atafutiwe mme kutoka "ire pande ya kure" kama anataka kuifaidi ndoa yake!.:brick:
 
Mtu mwenyewe ninja sishangai, si ndio hawa huwa wanajilipuaga.:target:
 
wakipigwa wanadai talaka, wasipopigwa wanadai talaka...oh myg..viumbe wa ajabu sana
 
hahahahahha duh mie nilijua wakurya peke yao ndio wanatakaga kipondo...hii kali
 
Inawezekana Kupigwa kunakozungumziwa hapo ni kupigwa kwa aina nyingine na sio magumi na mateke. huyo mwanamama anamaana nyingine.
 
some women are retarded .... and this's the dumbest shit I've ever heard! aah :yuck:
 
JAMANI KUMBE WATANI ZANGU WAKURYA MMEENDELEA SANA .....ONA SASA MLIVYOTEMBEA NA WAARABU MMEACHA MBEGU ZENU HUKO MNASABABISHA MATATIZO KATIKA NCHI ZA WATU ........huyo bint atakuwa anaitwa ROBI au GHATI.......!
 
hahahahahha duh mie nilijua wakurya peke yao ndio wanatakaga kipondo...hii kali
Mpendwa,
1. KIPONDO ni "universal language" kama music!...... haijui mzungu, muhindi, mchina, mwafrika, tajiri, maskini, ....... hulka ikishakuwepo ipo.
Hakuna jamii iliyo violence free.Its all about power expression....kuna watu hawajui negotiations in relationships.... hawajui ku deal na conflict situations... wanachojua ni ugomvi/kupiga.

2.Huyu mume aliyeshtakiwa huenda hana mabavu..anapenda kunegotiate...na huyu mwanamke inaelekea kakulia mazingira ambapo aliona mwanaume akipiga mke... na huenda baada ya kupigana mwanaume huishia kuangukia na kuomba msamaha wa bei mbaya na ndipo watu hutafsiri kuwa ili ujue unapendwa shurti ubondwe!

NB: Vipondo vingine huhatarisha maisha..wakati vingine huishia watu kupeana mapenzi na zawadi kemkem!All in all kupigana ni kitu kibaya.
 
Inawezekana Kupigwa kunakozungumziwa hapo ni kupigwa kwa aina nyingine na sio magumi na mateke. huyo mwanamama anamaana nyingine.

hata mimi nimeelewa hivyo...kipigo anachotaka huyu si cha mangumi, inaelekea jamaa hajui kupiga mapigo double double
 
Inawezekana huyu dada ana tafsiri nyingine ya kupigwa lakini mahakama haikumwelewa. Ngoja tusubiri tuone
 
Inawezekana Kupigwa kunakozungumziwa hapo ni kupigwa kwa aina nyingine na sio magumi na mateke. huyo mwanamama anamaana nyingine.

Hapoo Basi, umelenga mshale bahali yakhe. Yataka wakati mwengine tu-read btween the Lines jamani
 
Kupiga ni neno pana kuliko upana wenyewe jamani wanajamii usibaki katika maana moja tu ya kina MURA, labda jamaa hayajui mapigo ya ktk porno ukizingatia vitu hivyo Uajemi havipo.
 
Back
Top Bottom