Mume wa mtu huyu mbona haniachi jamani?

Mume wa mtu huyu mbona haniachi jamani?

cathy14

Member
Joined
Apr 11, 2014
Posts
37
Reaction score
23
Habari ndugu zangu,

Nashindwa kuelewa mpaka sasa nimetokea kupendwa na mume wa mtu tangu niingie kwenye mahusiano sijawahi kuwa na mahusiano na mwanaume ambaye yupo single,

Amekuwa akinisaidia sana katika maendeleo yangu mume wa mtu huyu ndie mshauri wangu hata iweje yupo mbele yangu kunijali ananipenda sana mara nyingne nawaza siwezi kufika naye mbali tayari yeye ameshakuwa na familia yake na Mimi nilazima nitakuwa na familia Yangu tutaishi maisha haya mpaka lini na tangu tujuane huu ni mwaka wa 6 najitahidi kumuacha lakini jamaa na yeye anapigana kutokuniacha mke wake mpaka leo hajui kama mume wake ana mchepuko nje, nishaurini nahitaji na Mimi kuwa na maisha yangu nimpata mume wangu nitamtumikia huyu jamaa mpaka lini? Nipeni hata njia mbadala matata ili niachane naye.
 
Wewe kwanza unajua unachofanya ni unyama kwa mwanamke mwenzio, put yourself in her shoes, ungependa mumeo achepuke. Achana na mume wa mtu kuanzia leo, tafuta wa kwako, mbona single tuko wengi hutuoni?
 
Najua siyo vyema kula tonge la mtu nimelijua hilo ndio maana nilijitahid kumuacha siyo vyema kabisa Lakin mwanaume ndio mgumu kuniacha nafanya vituko Vingi ili nimuuzi anichoke aondoke kwangu ndio nimeshindwa nikaja kwenu mnishauri
 
Ile principle ya Karma what goes around comes around so bora tu uendelee naye manake ukiolewa tu na mumeo ataanza hayo unayomfanyia mwenzio
 
mama jitoe tu mapema if u want your own family... tell him kwamba for now u need to focus on your life na uwe na mpenzi ambae utaingia nae kwenye ndoa kama kweli anakupendi he will give u a space na we upunguze ukaribu nae that all
 
Najua siyo vyema kula tonge la mtu nimelijua hilo ndio maana nilijitahid kumuacha siyo vyema kabisa Lakin mwanaume ndio mgumu kuniacha nafanya vituko Vingi ili nimuuzi anichoke aondoke kwangu ndio nimeshindwa nikaja kwenu mnishauri


Wewe ni mchepuko wake! Furahia kuitwa mchepuko maana huenda ndo karma yako hapa ulimwenguni! Ulivoanza mahusiano naye ulimuuliza nani?
 
Endelea naye tu uwe bi Mdogo

Ukitafuta mwingine utajuta awo unaowaona wako single watakuumiza adi utamkumbuka uyo mme wa mtu

Sisi vijana tuna michepuko mingi is better stay with him
 
Back
Top Bottom