JS nitakupa hadithi yangu
Kulikuwa na mtoto (I call him mtoto kwa sababu he sounded like one) alikoseaga namba siku moja akapiga kwangu. Sikuwa namfahamu so nikamsalimia na kumwuliza nimsaidie nini. Akanambia anamhitaji mwenye simu nikamwambia ni mie, akajibu mbona si kama sauti ya Aunt Leila, nikamwambia basi umekosea namba. Akanijibu kistaarabu tu samahani dada yangu aksante. Akakata. Baada ya siku moja akanipigia tena- safari hii usiku wa saa tano-- akaanza na samahani dada najua nimekosea namba (eti anajua amekosea but bado akapiga!!) naomba kujua unaitwa nani na unakaa wapi? Nikamwambia samahani sasa hivi ni usiku na ningependa kupumzika. (sikuona sababu ya kumjibu naitwa nani wakati keshajua amekosea!!). Huweziamini akawa anabeep (kila dakika) kila siku usiku kuanzia saa tano sita. Mr akawa anakuja juu sana na hata nikimweleza story ilivyokuwa hakuwa anaamini nikawa naulizwa swali la Barnaba .....haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi"... huyo ni mtu wako na mnajuana.
Ilikuwa inaniumiza kichwa sana na bahati mbaya kimeo changu hakikuwa na technologia ya kubloc so niliteseka kwa muda hadi nikafikiria sijui nimtegee nimwombe tukutane kisha nimwendee na police maana ndoa yangu ilikuwa inashake haswa kwa ajili yake (whoever he was). Maana sikuwa naweza kuzima simu usiku au kuimute -nitaambiwa nina mambo yangu ati. So nikaanza kumchunia, akibeep nakaa kinywa na Mr akirauka nakaa kimya nikaambiwa nina dharau, kiburi, jeuri na kila kisifa kilichonifaa. But alikujachoka mwenyewe akaacha yaani hadi niliicremugi ile namba!!
So what I want to write here ni kuwa usimlemaze huyo if he daa want to understand you kiutuuzima, mwaga mboga kabla hajamwaga ugali. And the more you delay ndo unarise maswali kwa Mr right wako
kuna majibu mengine yanatoka hapa naishia kucheka tu ..
ati umpe ili haki itendeke! haahaha jamani weeee
Hahahaha! Hommie hapo hata mwalimu wetu Gaijin atachemka!! Au ni do the needful?
Jamani wadau naombeni msaada kuna mume wa mtu kaniganda kweli kweli. Tulikutana mtaani kwenye starehe hizi tukawa tunapiga stori na mambo kama hayo mwishowe tukabadilishana namba za simu.
Sasa kila kukicha ni simu ni text messages. ananitaka kimapenzi. nishamuambia sina hisia kwake na kwamba nina mpenzi wangu tayari na there cant be anything between us. haelewi kabisa kagoma kuelewa.
Nimfanyeje mtu wa aina hii na tamaa zake za mwili??
Jamani mbona mnamwonea sweetie hapa? Hakuna ubaya hata kidogo kubadilishana namba za simu si ndio connections, madili na urafiki unapoanzia? Tatizo hapa ni huyo fisi kuitumia vibaya namba aliyopewa. Ingekuwa hakuna kubadilishana simu si ingekuwa hakuna maana ya kuwa na simu basi maana kama ni kuwasiliana na nduguzo mngekutana majumbani na za kikazi mngekutana ofcn au kutulia land lines??
JS mamii huyo ni wa kumpiga stop kungali mapemaa tena asiposikia dada hebu deka kidog kwa mpenzio... mweleze taratibu kuanzia A to Z tangu mlipokutana hadi kuexchange number tena mwombe na msamaha wa kutomwambia mapema juu ya hilo (Ikibidi finya macho mpendwa ili umconvince kujutia kwako-Si ndio mapenzi yenyewe ati?)
Kisha mwombe akusaidie kuondokana na jinamizi hilo. The way I know my shem is a man enough he will know what to do lovie so dont worry
Kila la kheri
Jamani wadau naombeni msaada kuna mume wa mtu kaniganda kweli kweli. Tulikutana mtaani kwenye starehe hizi tukawa tunapiga stori na mambo kama hayo mwishowe tukabadilishana namba za simu.
Sasa kila kukicha ni simu ni text messages. ananitaka kimapenzi. nishamuambia sina hisia kwake na kwamba nina mpenzi wangu tayari na there cant be anything between us. haelewi kabisa kagoma kuelewa.
Nimfanyeje mtu wa aina hii na tamaa zake za mwili??
Jamani wadau naombeni msaada kuna mume wa mtu kaniganda kweli kweli. Tulikutana mtaani kwenye starehe hizi tukawa tunapiga stori na mambo kama hayo mwishowe tukabadilishana namba za simu.
Sasa kila kukicha ni simu ni text messages. ananitaka kimapenzi. nishamuambia sina hisia kwake na kwamba nina mpenzi wangu tayari na there cant be anything between us. haelewi kabisa kagoma kuelewa.
Nimfanyeje mtu wa aina hii na tamaa zake za mwili??
Hahahah Kaizer ni kweli huwa si vema kusema kuwa umetongozwa kwanza wajua inakera na wala si sifa kwako wala kwa mpenzio lakini ukiona umemkatalia mtu kistaarabu na hasikii inapaswa kumlipua mapema kabla hajakuharibia maana hapa ni suala la kulinda interest zako ati.
Mzima lakini best? long time eeh?
Mume wa mtu kakutaka..... mwambie "mie mke wa mtu sikutaki"! Simple
Tatizo hajaolewa WoS,,
Hilo wala sio tatizo.
Give me a break Ngoshwe ina maana wewe hujawahi kukutana na msichana any place iwe hata kwenye starehe you had a chat mwishowe mkabadilishana namba za simu?? ina maana unakuw aunamtaka huyo msichana?? hakuna cha maswali ambayo hana majibu
Sijasema nawasiiliana naye kama umesoma between the lines
Nina simu ya kawaida haina hiyo huduma ya kublock number
Sasa tukueleweje wewe umeshasema humtaki alafu unauliza ushari? Uko tayari kufuta ushauri wa kimapenzi ambao sio chaguo lako? Je wewe una miaka mingapi?
Kwanza jiulize hisia zako zinamkataa sababu ni mume wa mtu au sababu hujavutiwa naye kwa lolote lile?
- Kama humtaki na anakusumbua na umekeraka kachukue mchukulie RB ya polisi . otherwise mripoti ustawi wa jamii. wamsaidie.
- Namna gani vipi kama una "mshikaji wa karibu" wa kukusaidia mpe number ya huyo jamaa. mpe na latest script ya sms alizokutumia. Then jamaa aanze kwa kumbwatukia. Ukiona inafaaa nipe hiyo kazi mimi kama huna mshikaji wa karibu.