Mume na mke wamepata watoto mapacha baada ya miaka 43 ya ndoa

Hawa watoto wa uzeeni wanakua watundu hawa, huyu baba ataweza kukimbizana na mipira au ndiyo kulea wakina Junior!
 

Niliwahi kuwa clinic ya mama wa miaka 53, mume wake akiwa 55. Walibarikiwa mtoto wa kiume
 
Mlikaa muda gani Boss?
 
Mungu apewe heshima, sifa, utukufu na shukrani nyingi
 
Mungu ni muweza wa kila kitu, kila kinachokuja duniani yeye ndio anajua kitalelewa vipi. Umeanza vizuri umemaliza kwa maelezo mabaya na ya kuvunja moyo kwa ambao hawana watoto!
Pitia uzi wa Bujibuji ili uweke akili yako sawa!!
Katoto kenyewe kabaya, kaache kafe
 
pre
Vipi ndugu, jamaa na marafiki hawakuanza kukupa pressure uchepuke au uoe mke mwingine?
pressure ya kwanza nilipata kwa ndugu, nilidharauliwa mno na ndugu walitaka kumbeba wife waende naye kwa mganga nikagoma. tukaishi tu kwa imani hadi tulipopata wa kwanza, hapo ndio ikawa kama tumefungulia bomba. huyu Mungu huyu, we acha tu.
 
Reactions: BAK
Hongera sana. Utukufu wa Mungu ni mkubwa.
hili huwa siachi kumsimulia kila ninayekutana naye, kwasababu usiombe upitie jaribu la kukosa watoto, linauma kuliko hata kusalitiwa kuliko chochote kwasababu kama ni mwanaume utajihisi wewe sio mwanaume kamili (kumbe Mungu kakuumba kamili na hata kama haupo kamili anaweza kurekebisha),the same kwa mwanamke. ukitembea ukaona watoto wa watu wanavyovalishwa, siku za sikukuuu etc yaani unatamani ardhi ipasuke ujifiche. kizuri ni kwamba watoto ni zawadi toka kwa Mungu na Mungu ndiye anatoa watoto. watoto hawatoki kwa mganga wala kwa daktari.
 
Hongera sana Mkuu ME wengi wasio na msimamo wangewaruhusu ndugu ilk mke abebwe na kuhangaika naye kwa Waganga, bila ya shaka mkeo alikupongeza sana kwa msimamo wako.
pressure ya kwanza nilipata kwa ndugu, nilidharauliwa mno na ndugu walitaka kumbeba wife waende naye kwa mganga nikagoma. tukaishi tu kwa imani hadi tulipopata wa kwanza, hapo ndio ikawa kama tumefungulia bomba. huyu Mungu huyu, we acha tu.
 
Hongera sana Mkuu ME wengi wasio na msimamo wangewaruhusu ndugu ilk mke abebwe na kuhangaika naye kwa Waganga, bila ya shaka mkeo alikupongeza sana kwa msimamo wako.
kuna mawili, wangempeleka kwa mganga, na chengine, wangempa mdogo wangu au ndugu yangu anibambike mimba. lakini yote katika yote, nilikuwa sitaki mtoto toka kwa mganga, nilikuwa nataka mtoto toka kwa Mungu, na Mungu akatupatia watoto hadi sasahivi tunapambana na vijiti, aliweka mara vinamdhuri anatoa, mara mavidonge etc kuzuia mimba. wanaposema Mungu huwa anaweza kukupatia chakula kingi ukala hadi ukasaza mbele ya maadui zako, ni kweli, imenitokea, nimesaza watoto hadi tunapambana asipate mimba ingine kwasababu watoto ni wengi wa kutosha, sebule limezungukwa na watoto furaha tupu. its a real thing that happened in my life na nitamtukuza Mungu na kuwaambia watu jambo hili maisha yangu yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…