Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Habari wadau
Naanza kuandika kisa hiki kwa maskitiko makubwa
Mwenzenu nina mke nimebahatika kuzaa nae mtoto mmoja lakini mke huyu wakati huo naanza nae mahusiano yetu nilimkuta na mtoto mmoja wa umri wa miaka 5

Kama mjuavyo nilivutiwa na bibie na sikuona uzito wa kumlea mtoto nilifurahi kujua huyu mke ni mlezi na waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake

Mwezi uliokwisha aliibuka bwana mmoja asubuhi kabla ya mimi sijakwenda kwenye shughuli zangu akakaribishwa mimi nikatoka ukumbini nikamkuta huyu bwana amekaa na watoto wote wawili kwenye kochi, nikamuuliza mama watoto akanijibu nilikuwa nasubiri nikufahamishe huyu ni (baba john) si jina rasmi,nikamsalimia tukaletewa chai tukajumuika pamoja kunywa chai na maandazi tukaongea kuhusu maisha kidogo na akanieleza dhumuni la kufika hapa ni kumuangalia mwanawe ,siku zimekuwa nyingi nikawaacha mimi nikaondoka kuelekea kwenye mizunguuko yangu

Swali linalonisumbua kichwa huyu bwana alipajuaje hapa nyumbani na kwanini alikuja asubuhi hana shughuli huyu mtu, na pia hivi sasa nasikia mimi nikitoka na yeye anafika mara mbili kwa siku kuangalia mtoto na akifika anaacha mizigo anaondoka sasa juzi ndio ilikuwa kali nilikuta chupa za bia nikaambiwa nililetewa na mume mwenzangu na yeye ameshakunywa zake nikamuuliza mke akanijibu nisiwe na wasiwasi yule anampitia mwanawe na yeye ni mtu mzima hawezi kutuchanganya,lakini jamani mtu na mtuwe ni kama gari na mteremko

Ok kwa sababu ya likizo ya viroba nikajinoma bia lakini kwa shingo upande na kengele ya tahadhari ikinililia kichwani
Leo hii asubuhi mke ananiaga kuwa kuna shughuli sijui inaitwa kitchen mada kama nimekosea mta sahihisha ya mdogo wake baba john nikamkubalia lakini kwa shingo upande anasema kulingana na ratiba za shughuli atarudi kesho

Jamani mpaka kufikia hapa mimi naona mume mwenzangu ananizunguka mbuyu na sitaki afike hapa kwangu naweza kuua na nikapelekwa jela

Wadau naomba mchango wenu niache mke lakini bado nampenda au amchukue mtoto wake lakini john mwenyewe bado mdogo ili anipe amani ,nitaua mimi

assanteni nasubiri ushauri wenu
Stuka ww ushaliwa umebeti vibaya arifu.
 
Mambo ya single mother HAYO 😱😱😱
 
Alaf kuna wanaume wengine wajinga wajinga sana sasa hapa unaleta story gani 🙁 unakera we jamaa siumsire huyo wife ashakusoma akili zako amejuwa wewe tutusa ungekuwa timamu usingeletewa maigizo hayo

oi.jpg
 
Mkumbushe tu Mama John asiwe anasahau zana za kazi, huyo ni mke wenu nyote , haaa kuoa mwanamke mwenye mtoto labda niwe na miaka 40 na kuendelea
 
Da we kweli kondoo...mi siwezi angalai ujinga huo unafanyika...day one angenieleza huyo kaja vipi kwangu...ikibidi amfuate huko huko
 
Mwanaume mwenzio eti anakuja kwako kumuona mtoto wake...kama anamjali si amchukue...we ni boya sana... Au mke naye kakuteka naona anamuita tu na kumuonesha jamaa yake wa zamani anapoishi na wewe tena bila uoga
 
Pole sana...

Kutokana na jina la ID yako ni sawa kabisa kufanyiwa hayo... Na bado kuambiwa tu, embu tupishe tunamazungumzo ya faragha...

Wanajifungia chumbani, mkuyati unatembezwa baada ya hapo unaambiwa, peleke maji ya kuoga bafuni...

Cc: mahondaw
🙂
 
100% watu wameshakula.. Sasa hio kitchen party kwa mume mwenza afu analala huko huko tangu lini kitchen pati ikawa kama msima watu wanalala huko huko?
Inawezekana mke anakbuka sana mapigo na msuguo wa jamaa yake. Hapo kwisha kazi
 
Wahenga walituasa TUSIOE WANAWAKE WALIOKWISHAZAA AU KUACHIKA... Haya ndo matokeo yake... Pole bana THE LESS YOU KNOW THE SAFER YOU ARE...
 
Wanawake km hawa ndo wanatufanya single mothers tuogopwe na waoaji, muache aende kwa baba John wake asikusumbue akili, jela sio bar mkuu usije kujaribu kuwadhuru waache na maisha yao kwa amani kabisa
 
mhhhh apo kwenye atarud kesho hahhaa mkuu stuka baba john anaenda kumfumua
 
kama ujalishwa limbwata basi ni marioo unatuzwa na mam john maana hizi akili ni za kitoto sana. anapataje ujasiri wa kuja kwako tena mapemaaa

mama john alisha mweleza kuwa ww n boya na huna ujanja wa kupindua apangacho. hapo mpige chini mama john wala usihangaike na jamaa.
 
Dah pole mkuu Kjj labda washukuru waliokupa ushauri wa kujenga na kubomoa,labda niwaulize hawa wachangiaji hakuna kwao waliokutana kwa mama na baba zao wapo na wanafika majumbani kwenu kuwasalimia mbele ya baba zenu wa kufikia acheni hizo mshaurini vizuri huyu mtu atapata kesi kavurugwa,nimepita tu msije mkanishambulia mshambulieni jombaaa kjj baba johniiiii!
 
funga CCTV camera/ Hidden camera kwako kwa siri utajioea mwenyewe wanachokifanya ukiwa umenda kazini..but tahadhari ujiandae kisaikolojia kabla hujaziangalia hizo video
 
Back
Top Bottom