Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

kubwa jinga jr unataka ushauri wa kuvumilia mkeo kuwa na wanaume wawili au?
 
Daaaah una uvumilivu sana mkuu. Unalea tatizo kama halijakua basi tegemea siku moja litakua......

Mimi kwanza tokea siku ya kwanza reaction yangu hivyo vimaandazi na chai wangekunywa pekeyao. Na hizo bia chupa zingemuishia mwilini huyo mama Jonii. Halaf baada ya hapo ungeona kama ana nguvu za kwenda kitchen pati na kulala huko. Eti nini?? Mkeo anaenda kulala kwenye sherehe ya ex wake?

Shabaaaash...
mkuu nilitumia busara tu kuondoka lakini kwa kweli njia mzima nilikua ninamfikilia yeye
 
Acha ufala huyo sio mwanamke wako unakaribisha mwanaume mwenzio kwako na bia anakununulia akili yako ndogo wacha amtafune kwa uboya wako na usilala mike mpuuzi wewe
 
Pole sana...

Kutokana na jina la ID yako ni sawa kabisa kufanyiwa hayo... Na bado kuambiwa tu, embu tupishe tunamazungumzo ya faragha...

Wanajifungia chumbani, mkuyati unatembezwa baada ya hapo unaambiwa, peleke maji ya kuoga bafuni...


Cc: mahondaw
 
Mkalishe mkeo kitako mwambie hutaki hayo mazoea yake na baba John iwe mwanzo na mwisho mbona analeta balaa huyu mwanamama hajafundwa kwao??

Ashavuka mipaka tayari, aachwe abaki na Baba John.

Yeye ajipange upya, hapo familia yake ishabuma.
 
Nisiongee sana kumbuka kama wewe ni B tambua A japo ni wa mwanzo ila anahitajika pia kwenye herufi zinazomfuatia ili kuleta utam wa sentence
 
Habari wadau
Naanza kuandika kisa hiki kwa maskitiko makubwa
Mwenzenu nina mke nimebahatika kuzaa nae mtoto mmoja lakini mke huyu wakati huo naanza nae mahusiano yetu nilimkuta na mtoto mmoja wa umri wa miaka 5

Kama mjuavyo nilivutiwa na bibie na sikuona uzito wa kumlea mtoto nilifurahi kujua huyu mke ni mlezi na waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake

Mwezi uliokwisha aliibuka bwana mmoja asubuhi kabla ya mimi sijakwenda kwenye shughuli zangu akakaribishwa mimi nikatoka ukumbini nikamkuta huyu bwana amekaa na watoto wote wawili kwenye kochi, nikamuuliza mama watoto akanijibu nilikuwa nasubiri nikufahamishe huyu ni (baba john) si jina rasmi,nikamsalimia tukaletewa chai tukajumuika pamoja kunywa chai na maandazi tukaongea kuhusu maisha kidogo na akanieleza dhumuni la kufika hapa ni kumuangalia mwanawe ,siku zimekuwa nyingi nikawaacha mimi nikaondoka kuelekea kwenye mizunguuko yangu

Swali linalonisumbua kichwa huyu bwana alipajuaje hapa nyumbani na kwanini alikuja asubuhi hana shughuli huyu mtu, na pia hivi sasa nasikia mimi nikitoka na yeye anafika mara mbili kwa siku kuangalia mtoto na akifika anaacha mizigo anaondoka sasa juzi ndio ilikuwa kali nilikuta chupa za bia nikaambiwa nililetewa na mume mwenzangu na yeye ameshakunywa zake nikamuuliza mke akanijibu nisiwe na wasiwasi yule anampitia mwanawe na yeye ni mtu mzima hawezi kutuchanganya,lakini jamani mtu na mtuwe ni kama gari na mteremko

Ok kwa sababu ya likizo ya viroba nikajinoma bia lakini kwa shingo upande na kengele ya tahadhari ikinililia kichwani
Leo hii asubuhi mke ananiaga kuwa kuna shughuli sijui inaitwa kitchen mada kama nimekosea mta sahihisha ya mdogo wake baba john nikamkubalia lakini kwa shingo upande anasema kulingana na ratiba za shughuli atarudi kesho

Jamani mpaka kufikia hapa mimi naona mume mwenzangu ananizunguka mbuyu na sitaki afike hapa kwangu naweza kuua na nikapelekwa jela

Wadau naomba mchango wenu niache mke lakini bado nampenda au amchukue mtoto wake lakini john mwenyewe bado mdogo ili anipe amani ,nitaua mimi

assanteni nasubiri ushauri wenu
Mke wako wampenda lakini ni mshenzi. .
Pole sana kiongozi.
 
Wewe kweli kubwa jinga!sasa mpaka sasa haujui nin kinaendelea apo?unamegewa!kinachokufanya ukashindwa kumface na kumpiga marufuku kuja home kwako ni nini?embu tumia busara na hekima...suala hili ni dogo sana.
Sasa hata kama atampiga marufuku ndio hata megewa ?
Huyo mke mshenzi tu. Amrudishe mwanae kwa Baba yake na mke awe na msimamo basi.
 
Back
Top Bottom