Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Umeshakua wewe. Kwanzia sasa haita itwa kubwa jinga jr utaitwa kubwa jinga sr.
 
Unakubalije mazoea ya hivyo mkuu?

Yani huyo akitaka kuja kwako inabidi awasiliane na ww,sio na mkeo.
 
sasa sipati tena shida nikimuona..
JF imekua ya kila aina ya kiumbe..
Just tread carefully.
Exactly.. ni kuficha hasira tu maana utabaki kuwatukana kila siku
 
Fanya maamuz ya kiume,maamuz ya kiume yanaumiza lkn kwakuwa ww ni mwanaume unayavumilia tu, piga chini na ushaur wa bure kabla hujaoa jaribu kupeleleza sababu za mwenza wako kuachana na mwenza aliyepita na ukigundua sababu ya kutengana kwao c nzto bas jiandae kumegewa
 
Aaahhh mambo mengine bana afadhali unyamaze mwenyewe tu huko, sasa ushauri wa nini hapo na umeyataka mwenyewe, mume mwenzako anakuja kwako tena unatambulishwa halafu Unaondoka unamuacha ndani ya nyumba yako na mke wako? Dah una roho ngumu wewe lakini nyepesi
 
Habari wadau
Naanza kuandika kisa hiki kwa maskitiko makubwa
Mwenzenu nina mke nimebahatika kuzaa nae mtoto mmoja lakini mke huyu wakati huo naanza nae mahusiano yetu nilimkuta na mtoto mmoja wa umri wa miaka 5

Kama mjuavyo nilivutiwa na bibie na sikuona uzito wa kumlea mtoto nilifurahi kujua huyu mke ni mlezi na waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake

Mwezi uliokwisha aliibuka bwana mmoja asubuhi kabla ya mimi sijakwenda kwenye shughuli zangu akakaribishwa mimi nikatoka ukumbini nikamkuta huyu bwana amekaa na watoto wote wawili kwenye kochi, nikamuuliza mama watoto akanijibu nilikuwa nasubiri nikufahamishe huyu ni (baba john) si jina rasmi,nikamsalimia tukaletewa chai tukajumuika pamoja kunywa chai na maandazi tukaongea kuhusu maisha kidogo na akanieleza dhumuni la kufika hapa ni kumuangalia mwanawe ,siku zimekuwa nyingi nikawaacha mimi nikaondoka kuelekea kwenye mizunguuko yangu

Swali linalonisumbua kichwa huyu bwana alipajuaje hapa nyumbani na kwanini alikuja asubuhi hana shughuli huyu mtu, na pia hivi sasa nasikia mimi nikitoka na yeye anafika mara mbili kwa siku kuangalia mtoto na akifika anaacha mizigo anaondoka sasa juzi ndio ilikuwa kali nilikuta chupa za bia nikaambiwa nililetewa na mume mwenzangu na yeye ameshakunywa zake nikamuuliza mke akanijibu nisiwe na wasiwasi yule anampitia mwanawe na yeye ni mtu mzima hawezi kutuchanganya,lakini jamani mtu na mtuwe ni kama gari na mteremko

Ok kwa sababu ya likizo ya viroba nikajinoma bia lakini kwa shingo upande na kengele ya tahadhari ikinililia kichwani
Leo hii asubuhi mke ananiaga kuwa kuna shughuli sijui inaitwa kitchen mada kama nimekosea mta sahihisha ya mdogo wake baba john nikamkubalia lakini kwa shingo upande anasema kulingana na ratiba za shughuli atarudi kesho

Jamani mpaka kufikia hapa mimi naona mume mwenzangu ananizunguka mbuyu na sitaki afike hapa kwangu naweza kuua na nikapelekwa jela

Wadau naomba mchango wenu niache mke lakini bado nampenda au amchukue mtoto wake lakini john mwenyewe bado mdogo ili anipe amani ,nitaua mimi

assanteni nasubiri ushauri wenu
Alichokuwa anakitaka ni mtu wa kumuoa na ameshakupata,hayo mengine kuwa mpole tu kaka,hawa watu ni pasua kichwa sana,ukiwaona wanavyojifanya wapole yakishawakuta tofauti na walionayo kwenye mioyo yao...
 
Mkeo inabidi aachane na baba John, hakuna sababu ya yete kuhudhuria sherehe ya mdogo wa baba John. Mtoto akiwa mkubwa atakwenda mwenyewe kwa ndugu zake lama kina shughuli. Mkeo hana sababu ya kujishughulisha kiasi hicho kama vile anakwenda kwa familia ya mume wa ndoa.
 
Back
Top Bottom