Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Mume mwenza simuelewi ananitafutia jela

Mpangie ratiba aje mara moja kila mwez hawezi no kuja kabisa Mama john mpe onyo kali shenz uchagani huu ushenz hamna
 
Habari wadau
Naanza kuandika kisa hiki kwa maskitiko makubwa
Mwenzenu nina mke nimebahatika kuzaa nae mtoto mmoja lakini mke huyu wakati huo naanza nae mahusiano yetu nilimkuta na mtoto mmoja wa umri wa miaka 5

Kama mjuavyo nilivutiwa na bibie na sikuona uzito wa kumlea mtoto nilifurahi kujua huyu mke ni mlezi na waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake

Mwezi uliokwisha aliibuka bwana mmoja asubuhi kabla ya mimi sijakwenda kwenye shughuli zangu akakaribishwa mimi nikatoka ukumbini nikamkuta huyu bwana amekaa na watoto wote wawili kwenye kochi, nikamuuliza mama watoto akanijibu nilikuwa nasubiri nikufahamishe huyu ni (baba john) si jina rasmi,nikamsalimia tukaletewa chai tukajumuika pamoja kunywa chai na maandazi tukaongea kuhusu maisha kidogo na akanieleza dhumuni la kufika hapa ni kumuangalia mwanawe ,siku zimekuwa nyingi nikawaacha mimi nikaondoka kuelekea kwenye mizunguuko yangu

Swali linalonisumbua kichwa huyu bwana alipajuaje hapa nyumbani na kwanini alikuja asubuhi hana shughuli huyu mtu, na pia hivi sasa nasikia mimi nikitoka na yeye anafika mara mbili kwa siku kuangalia mtoto na akifika anaacha mizigo anaondoka sasa juzi ndio ilikuwa kali nilikuta chupa za bia nikaambiwa nililetewa na mume mwenzangu na yeye ameshakunywa zake nikamuuliza mke akanijibu nisiwe na wasiwasi yule anampitia mwanawe na yeye ni mtu mzima hawezi kutuchanganya,lakini jamani mtu na mtuwe ni kama gari na mteremko

Ok kwa sababu ya likizo ya viroba nikajinoma bia lakini kwa shingo upande na kengele ya tahadhari ikinililia kichwani
Leo hii asubuhi mke ananiaga kuwa kuna shughuli sijui inaitwa kitchen mada kama nimekosea mta sahihisha ya mdogo wake baba john nikamkubalia lakini kwa shingo upande anasema kulingana na ratiba za shughuli atarudi kesho

Jamani mpaka kufikia hapa mimi naona mume mwenzangu ananizunguka mbuyu na sitaki afike hapa kwangu naweza kuua na nikapelekwa jela

Wadau naomba mchango wenu niache mke lakini bado nampenda au amchukue mtoto wake lakini john mwenyewe bado mdogo ili anipe amani ,nitaua mimi

assanteni nasubiri ushauri wenu
We inabidi uchapwe vibao kwanza unaaibisha tasinia ya uanaume
 
Pole sana mkuu! Unapaswa kutambua jambo hili 'majina hata kama ni ya utani hubeba nyota Fulani kulingana na jina lenyewe kwa mfano majina kama Shida,Bahati,Tabu,Riziki,Sikujua n.k.Sasa tazama jina la utani ulilojipa (Kubwa Jinga) linavyo-reflect maisha yako halisi.Jambo jingine unalopaswa kulifaham ktk uhai wako wote ni kwamba ukimwona Mwanadam yeyote mahali popote Duniani tambua kuwa huyo ni matokeo ya muunganiko wa kimwili na kiroho kati Baba na Mama yake, hii ni kusema kwamba kama watu walishawahi kuwa ktk uhusiano wa kimapnz na wakazaa then wakatengana basi watu hawa nyoyo/roho,damu na hisia zao daima zitaendelea kuunganika hata kama watakuwa mbali kimazingira.Tafsir ya jambo hili ni kwamba ww ulimuoa m2 ambaye mwili wake ulikuwa umeungana na mwili wa m2 mwingine kifikra,kihisia na hata kiroho,there4 you are suppose to tolerate the situation kwa sabab falsafa ya mapenz inasema hivi "Kama m2 ameingia kwenye uhusiano na akagundua kwamba amekosea suluhisho pekee ni lazma partner mmoja kati ya hao wawili AFE/AUAWE" kwa sabab ww na huyo mkeo tayar mmeshatengeneza bondage ambayo ina makosa na hakuna namna mnaweza rekebisha makosa hayo.
 
Ebu tueleze ukweli ilianzaje Babaa John kaanza kumtembelea mpaka home?
Maana pengine na wewe umechangia kwa namna moja ama nyingine.
Lakini pamoja na hayo,si mbaya kujuliana hali na mtu kumuona mtoto wake,lakini,hao wamezidi,na hajachelewa kukukaushia;
Mi nafikiri kuna kila sababu pia ya kujua background ya mtu wa kuishi nae,kujua chanzo cha watu kuzaa na kuachana. Kama hawajawa na ugomvi mzito,ni ngumu kumeza.Japo hata ambao hawajazaa wengi wao pia hupata washikaji wakiwa kwenye ndoa,hasa pale wanapokuwa wanaona wananyanyaswa.
Punda wako anabeba na mizigo ya baba John
 
Hivi John huyu ndo yule ndg yake Na yule wa Ngorongoro alieundiwa time


Ndomaaaanaass
 
Hakuna ndoa yoyote duniani iliyodumu kwa kuendeshwa ki demokrasia,, I mean sio umpige mkeo no, I mean fanya maamuzi magumu , mwanaume ni kama simba hakuna kusita sita,,
Nakumbuka kuna mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema ,, Its 'may be' that kill people.
 
Uwezo wetu wa kufikiri kama wanaume unazidi kushuka siku hadi siku,mpaka anafika nyumbani kwako na unaletewa na bia bado unaomba ushauri aiseeeee mke ana bahati ya kupata mteremko sana kama unashindwa kua na suluhisho la jambo dogo kama hili nadhani una haki ya kwenda tu jela maana utakuja kumfanya mwanao nae awe zwazwa.
 
Back
Top Bottom