Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,790
Habari za jioni wapendwa,
Shost alinipitia kazini, tulikwenda Kariakoo kutafuta vifaa vidogo vidogo ikiwa ni pamoja na nguo mbili tatu kwa ajili ya dada wa kazi, niligundua shost anabadilisha dada wa kazi karibu kila baada ya miezi miwili/mitatu.
Baada ya kununua vifaa tulielekea wote kwake kwasababu alikuwa na mzigo wangu wa magimbi, alirudi nao wakati anarudi na dada mpya wa kazi. Basi nimefika nyumbani, bwana shemeji mume wa shost alikuwepo, kama kawaida shemeji ni mchangamfu kupita maelezo. Niliuliza jamani dada P ilitokea nini tena mbona aliondoka ghafla, shemeji amedakia, tuligundua ni mvuta bangi yule, analeta bangi mpaka ndani ya nyumba.
Wakati wote huo shost alikuwa kimya akimwangalia mumewe usoni. Wakati ananisindikiza ndiyo ananieleza kuwa kila housegirl anaekuja kwa bwana shemeji ni kosa, lazima apitie kidogo. Mimi kwa mawazo yangu nimeona ugonjwa anaufuga mwenyewe, sasa atabadilisha madada mpaka lini? Nilimshauri atatafute kijana, lakini anasema watoto ni wadogo na haamini vijana wa kiume.
Amemwambia mume wake, hii iwe mwisho, akimgusa huyu na yeye anaondoka. Haya mlioko kwenye ndoa shost huyu mtampa ushauri gani?