Mume ampiga mkewe nahitaji msaada wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume ampiga mkewe nahitaji msaada wenu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ome, Sep 29, 2010.

 1. O

  Ome Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Kuna familia moja ambayo mama ndiye anayejua watoto wale nini,wasome wapi, wavae nini na waishi wapi kwa maana ya kwamba hadi pango mama ndio anayelipia kodi. Mume hana habari na hivyo vitu, yeye anachojua ni kumpiga tu mkewe usiku kucha na sio mara moja yani akikaa sana ni siku 2 au 3.

  Mama anauza mboga ili kupata mahitaji ya nyumbani, huyo baba sijui kazi yake. Huwa anamwambia mkewe ampe pesa alizopata akigoma anampiga sana, anaweza kaa ndani hata siku 3 bila kutoka kwa maumivu anayopata. Siku akiamua anapiga wote hadi watoto.

  Mimi namuonea huruma huyu mama, ni mtu mzuri sana hafai kuishi na mume mkatili kama huyo. Pia nawaonea huruma hawa watoto kwani ipo siku huyu baba atamuua huyu mama na watoto watabaki wakiteseka.

  Mimi naomba wataokuwa tayari kutoa msaada niwape details ya hii familia inapoishi.

  Natanguliza shukrani zanga!!!!!
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  lakini huyu mama anajitakia, pole zake mana huyo baba ni mzigo mara mbili, yaani mtu tu aseme umpe pesa ambayo hajui umeisoteaje kwa ajili ya kuwatunza watoto wenu ucpompatia kipigo, jamani binadamu wengine hawauthamini utu wao kabisa, namtunzia watoto bado atoke uko anitwange mie na wanangu...haki ya nani kuna watu wamepata wanawake wa kuwachezea......
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  msaada kama upi ?

  kama anaona hawezi kuishi nae si kila mtu achukue good time au ?
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  usiingilie ndoa za watu. Je kama hao watoto mume kadanganywa na anajua si wake? au wewe ni mzazi wao?
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  nenda kamripoti TAMWA watakuja kumsaidia
   
 6. M

  Mswahela Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyamayao hujapata taabu maishani; Kua uyaone
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  kaka/dada yangu, nimepitia ya kunitosha, lakini huwa siendekezi ujinga kwa kweli.
   
 8. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mh kaka utingo mbona ivo?
  ur sound 2selfsh ..ata km si watoto wake kuto a ushauri wa kibinadamu si vibaya wew bwana.kwaiyo wewe kumsaidia mtu ni mpaka akuhusu?apana si ivyo bwana.....whotevev da reasons might b lakin izo swaga za mume afanyi kazi+kumpiga mkewe +mke ndo kubeba mizigo yote dahh mbona ni msalaba mzito?afu wew ndo wasema maneno km ayo......apana usifanye ivo kaka utingo.
  uyo mwambie aende akapange nyumba nyngne......asepe na watoto wake uyo mume hana msaaaada zaidi ya kumsababishia maumivu na mwsho wa sku ataumia sana atashndwa ata kuhangaika tena kupata ela ya chakula kwa watoto na ilo jinamum la kiume!!!!!
  si kiivo bwana
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mambo ya ndoa magumu. Unawea kutaka kusaidia kwa nia nzuri ukashushiwa tuhuma ya uchonganishi.

  Jee huyo mama iwapo kweli anateseka kwa nini asilalamike kupitia mojawapo ya channel nyingi za kawaida kama ndugu, wanadini wenzake, mabest wao, uongozi wa kijiji, ustawi wa jamii, baraza la usuluhishi, nk? Usijekuta mwanandoa moja kumpiga mwingine ndiyo mapenzi yenyewe kwa taratibu zao!
   
 10. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  mnhhhh...jamani mambo ya ndoa magumu haya.."mie nilifundishwa nisiingilie mambo ya ndoa za watu"...soo sina cha kuchangia hapa
   
 11. T

  Teko JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Huyo mama kama kila kitu anajitafutia mwenyewe,yaani hapati msaada wowote kutoka kwa mumewe, kwanini anaendelea kuishi naye? ni bora aishi tu mwenyewe ili ajue moja sina mume basi! Na anaonekana atamudu tu maisha vizuri.
   
 12. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  kale ka nyimbo ka Tshala muana
  "bibi na bwana wakigombana nyumbani, uwache wenye mpaka wataelewana,
  Lakini ukiwaningiliaaa eeeh wakipatana utabaki nalia mieeee mtoto wa mamaaa.!"
  mpe pole zake huyo mama mwambie amuombe mungu atamtoa kwenye hiyo dhiki lakini sio sisi wanadamu nasi tuna yetu chungunzima yametuganda. NDOA si mchezo..!
   
 13. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama yeye ndiye anayelisha familia anasubiri nini hapo?sioni sababu ya msingi ya yeye kuwepo hapo aondoke,kama ni mume mungu atampa wa size yake huyo ni mwanaume suruali!
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Namuonea huruma huyo mdada.
  Ila ushauri kuntu kama kweli anataka msaada. ampeleke polisi huyo jamaa yake.
  Isije ikawa ni mbinu ya kuomba hela maana siku hizi kuna trick nyingi za kujiongezea kipato.
  Peleka polisi uishi na amani na wanao huku ukijitaftia kipato cha daily kwa uhuru. ogopa senti za msaada
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Namuonea huruma huyo mdada.
  Ila ushauri kuntu kama kweli anataka msaada. ampeleke polisi huyo jamaa yake.
  Isije ikawa ni mbinu ya kuomba hela maana siku hizi kuna trick nyingi za kujiongezea kipato.
  Peleka polisi uishi na amani na wanao huku ukijitaftia kipato cha daily kwa uhuru. ogopa senti za msaada
   
 16. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Umemaliza kutatua matatizo yako hata ujihusishe na matatizo ya wenzako?
   
 17. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umenena. Mbaraka Mwishehe katika tungo zake maarufu moja ilikemea mambo ya kuingilia ndoa za watu. Aliimba "Mambo ya mtu na mkewe waingilia kwa nini? "ukipigwa je"?
   
 18. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako Nyamayao unapenda sana watu wote wawe kama wewe.......hilo haliwezekani hata kidogo. Kumshangaa huyo mama hakusaidii sana, hivyo ndivyo alivyo kwahiyo unachotakiwa ni kutoa msaada.
   
 19. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Peleka huyo mwanamme SERO!
   
 20. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  unajua wanaume wengine huwa hawana ustaarabu ila sehemu moja tu ukiwa ustaaarabu wake uko makini basi hata afabye nn mwanamke hamkimbii inawezekana huyu jamaa yuko makini kwa ustaarabu huo

  mwambie avumilie hakuna mkamilifu
   
Loading...