Mulugo: Division Five haipo na sifuri ipo palepale

Mulugo: Division Five haipo na sifuri ipo palepale

Hiki ndicho chama chetu cha mapinduzi, kila mtu na msimamo wake halafu bado tunadai tuna serikali makini!!!!!
 
Itabdi tubadilishe mfumo JK aje kujb maswali bungen mana hawa mawazr wake hawana tofauti na hzo Div-V
 
Kuna mdau mmoja wakati anatetea huu mgawanyo mpya wa madaraja alisema wadau wote wameshirikishwa!!
Moja ya alama kuu ya ushirikishwaji wa wadau ni kuwa na kauli moja kama hitimisho, sasa hapa tueleweje?
Huyu ni kiongozi ambaye chama chake ndicho kilichotoa sera inayotumika anatofautiana na anaowaongoza!


Twende hivi hivi, watafika sehemu tu wenyewe watasema wameshindwa!
 
Kwa mtazamo wangu huyu naibu waziri anayeitwa Mulugo ni sawa na picha iliyobandikwa hapo Wizarani. Hajui Muungano uliozaa Tanzania umetokana na nchi gani, atajuaje Div za matokeo? Majanga Makubwa Sasa...
 
553188_548982921852373_1415430007_n.jpg
Philipo Mulugo; Bungeni akijibu maswali;
Anadai hakuna daraja la Tano;
ni daraja la kwanza; pili, tatu, nne, na ziro; daraja la tano hakunaagaaaa;Unadai ni mkanganyiko wa taarifa;;
Swali nani mkweli; waziri au Katibu wa Elimu; Siasa kwenye elimu ni Ugonjwa;
Serekali inatufanya hatuoni au hatusikii;Tunafahamu kila kitu;

Division "O" ilikuwepo muda wote baada ya I, II, III na IV. Makosa yaliyofanyika ni kutoipa neno division ziro, na ibabaki kuwepo. Labda tuko wazito kuelewa. Kwa maana hiyo tunazo siku zote division 5, nne za ufaulu na moja ya kushindwa.
 
hivi hilo tamko halikupishwa na balaza la mawaziri? katibu mkuu wa wizara anaweza kupisha maamuzi mazito bila waziri wake kujua? kweli hii ndio tz
 
sijajua kama wakubwa nao ni watumiaji wazuri wa ule unga wa sembe.... ila leo huyu kaongea point kidogo,,,,...
 
sasa ndio nimegundua kwanini tumetengwa kwenye EAC
cha ajbu kuna mahayawani yanayojiita simiyu yetu, lizabon na wehu wenzao watakuja hapa kutetea uozo huu unaofanywa na hawa wanyang'anyi wanaojiita serikali
 
Sasa hapa ndipo tunaona udhaifu wa serekali yetu, Anatofautiana na Prof. Mchome! Hapa mawasiliano; yapo

 
ni dhahiri kuwa wamekurukupuka kutangaza mambo kabla ya kuyajadili hata wao kwa wao. Sasa hao wadau ni nani
 
ni nani anawashauri hawa mawaziri wa elimu?ni makatibu wao?ni wake zao au ni wale wa nyumba ndogo?hakika haiwezekan waziri huyu anakuja na hili mwingne anaibuka na kupinga lile alosema mwenzake hawa watu wanafanya kazi kama team au kila mtu anafanya kivyake?nani amewaroga hawa watu?nani kawavuruga hawa watu wamechanganyikiwa wanatuchanganya na sisi.nini kifanyike?
 
Kwenye uzi kama huu huwezi kuwaona buku saba.
Hapo ndio utajua nani mwenye kutaka maslahi binafsi na nani mwenye kutaka maslahi ya nchi.

cc: chama, Ritz, Simiyu Yetu, Taswira.......tatizo huwezi kujua nani anatumia hizi ID leo. anaweza akawa Wasira na Mzindakaya au hata Makamba na yule ---- wa UVCCM.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna wa kumwamini, tusubiri tu leo vijana wa Form IV wameanza pepa. Wakitoa majibu tutajua nani mwongo na nani mkweli kama Div 5 au 0, yangu macho time will tell
 
kila mtu anakuja na lake, tumwelewe nani? elimu inachezewa sasa.
 
Ni aibu mkubwa kufanya mambo ya kitoto mbele ya watoto wanaojifunza na kuiga kesho
 
Back
Top Bottom