Muliro: Msiogope kuomba lifti kwenye Difenda

Halafu wakazifanyie nini
Mwizi na mchawi wote hawana akili. Furaha yao wakutese au kukutia hasara. Mwizi yupo tayari akuibie kitu aischokitumia..ilimradi aisirudi mikono mitupu.

So polisi watafuata vimiamia walivyobakiza watotokwenye ubuyu wakikosa watapitia hata vichongeo ilimradi tu. Washenzi sana hawa watu, sijui roho za utu hua wanaziacha wapi
 

"Kuna mtu alishawahi kuomba lift kwenye Difenda hakupewa? Kwanini wanapanda watuhumiwa tu?

Kwa mfano Difenda linakwenda Bunju, Tegeta, Kunduchu, Kitunda au Mwanagati, Kivule analiona kabisa limeandikwa Polisi na wewe unakwenda maeneo hayo kwanini usilisimamishe ukaomba lift?
Hahahaha, wakienda nishusha sentro atakuja kunitoa?
 
Siku moja jamaa moja alikuwa na begi la nguo alipofika line polisi akakuta maaskari wengi akatimua mbio mara maaskali wakamwona na kuamua kumfukuzia kwa kasi ya ajabu, walipofanikiwa kumkamata wakapekuwa begi lake na kukuta ni nguo tu. Wakamwuliza ulikuwa unakimbia nini? Huku akitetemeka alijibu kwa unyonge kuwa nilipoona umati wa maaskari niliamua nijisalimishe mapema kwa kukimbia maana maaskari huwa wanakamata watu na kuwapiga vibaya,hiyo ndiyo sababu iliyonifanya nikimbie.
 

"Kuna mtu alishawahi kuomba lift kwenye Difenda hakupewa? Kwanini wanapanda watuhumiwa tu?

Kwa mfano Difenda linakwenda Bunju, Tegeta, Kunduchu, Kitunda au Mwanagati, Kivule analiona kabisa limeandikwa Polisi na wewe unakwenda maeneo hayo kwanini usilisimamishe ukaomba lift?


Mwaka 2004 niliwahi omba lift gari ya police toka kijiji fulani ambapo usafiri ulikua gari moja tuu Mara 2 kwa siku

Nilifika salama na kwa haraka

Asante jeshi letu la police
 
Kwa ushauri tuu, msije mkadhubutu
Mtaunganishwa na watuhumiwa..

Askari sio watu wa kawaida.. Kuna mmoja aliniambia kesi zipo nyingi za uchunguzi na hazina watu wa kuwapa.. Na hawashindwi kumtengenezea mtu yoyote.. Na kumbambika..

Shida ni moja.. Maslai madogo kwa askari... Hivyo wanatafuta hela kwa nguvu kwa raia...
 
Wanajeshi huwa naona wanasimamisha basi zao wanapakia wanafunzi wanaosubiri daladala ila hao washenzi hawawezi fanya hivyo. Kwanza wanaweza kuwaibia wanafunzi penseli zao na vichongeo.
Niliwahi kupanda karandinga la jeshi miaka fulani natoka job. Mvua ilikiwa inanyesha Sana alafu Usafiri mgumu. Wanajeshi wakatupa lift.

Picha linaanza,tuliwakuta wanajeshi Kama Saba hivi kule nyuma wametulia tuli hawana stori na mtu. Kuna jamaa wawili tulipanda nao si wakaanza kupiga stori ndani ya gari!! Mwanajeshi mmoja akawauliza nyie mnapiga stori kwa ruhusa ya nani,wakakaa kimya.

Adhabu waliyopewa waliambiwa wainuke walipokaa wasimame na wasijishikie popote wakati gari linatembea(waliambiwa wasimame kikakamavu Kama wanaimba Mungu ibariki).

Jinsi walivyokuwa wanaangukia watu na kuyumba yumba kila mmoja mule ndani aliangua kicheko.

Wanajeshi nao walikuwa uso wa mbuzi lakini iliwabidi nao wacheke tu kwa vituko vya wale jamaa wawili. Mwishowe wakawasamehe wakaambiwa wakae chini.
 
Huu siyo mtego kweli ...

Mzee wa Msoga aliwahi kusema "akili za kuambiwa changanya na zako".

Mwenye masikio na asikie .

Uzi tayari.
0ad6fec08e6b4cf2af6edfdf5d7f72ff_1676361660097.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom