Kwanini siwezi kuomba lift kwenye difenda la polisi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
Kuna afande mkubwa juzi aliwatangazia wananchi kuwa wasiogope kuomba lift kwenye difenda la polisi.. Maoni yalikuwa mengi

Mimi katu sithubutu (tena) kuomba lift kwenye difenda la polisi...
Siku moja Ijumaa jioni mwaka 2005 mwezi wa tisa hivi kipindi hicho kampeni za vyama zikiwa zimepamba moto nilikuwa bar maarufu ya Kongo bar karibu na club ya Yanga namwagilia moyo
Kidogo likaja difenda la polisi likapaki pale bar alishuka mmoja aliyekuwa amekaa pale mbele siti ya dereva na kuingia huko ndani ya bar mimi nilikuwa nimekaa viti vya nje

Nyuma kwenye difenda kulikuwa na askari wawili waliovaa kiraia mmoja akiwa na radio call yake! Akawa anafanya mawasiliano na upande wa pili anasema Roja...roja... Huu ni uelekeo wa mabibo mwisho.. Kopi..kopi over..!

Dah si nikaona zali ndio ndio hili! Maana nilikuwa napiga hesabu za kufika round about ya kigogo nichukue basi la mabibo maana miaka ile bodaboda hazikuwa kivile kama siku hizi
Basi nikamaliza kinywaji changu fasta nikalipa na kuomba lift kabla mkubwa hajatoka kule ndani. Kwenye difenda la polisi anayekaa mbele ndio boss
Yule boss akatoka kule ndani akapanda tukaondoka.. Ile tunakaribia Kigogo radio call ikaita tena.. Na yule jamaa akapokea na kupewa taarifa kwamba pale Bar ya Chawote mtaa wa nyuma kuna vibaka wamekamatwa hivyo wanahitaji msaada
Difenda hilo mpaka Chawote kwa nyuma tukakuta vibaka wamefungwa kamba mikokoni, wakatiwa pingu tukaondoka.. Kufika polisi post ya kigogo njiapanda ya kuelekea Tabata dampo yule mwenye radio call akashuka na kumpa aliyebaki kwenye gari tukaondoka
Mimi nilikuwa nashuka mwembeni kituo kimoja kabla ya kufika mabibo mwisho hivyo tulipokaribia nikaomba kushuka.. Dah yule pot akaniwakia nbaya na kuniuliza kwanza nimepandia wapi. Duh yani hata hajui nimepandia wapi? Nikajieleza lakini akasema kwanza hana kumbukumbu hiyo kumbukumbu na difenda halisimami njiani kushusha raia aliyeomba lift kwa ubahili wake likiwa na vibaka! Alinisimanga sana!

Nikavumilia nikasema Mabibo mwisho sio mbali nitashuka nirudi mdogomdogo kwa miguu.. Tunafika polisi post ya mabibo mwisho kuna vijana wa CUF wamekamatwa pale uwanja wa soko la ndizi eti kwa madai ya kufanya fujo kwenye mkutano wa CCM!

Msiba juu ya msiba hali pale ilikuwa tete kuna askari wa FFU na difenda lao walio kikazi zaidi.. Tulishushwa kwenye difenda mimi na wale vibaka kikatili mno! Mpaka tunaingizwa ndani konyagi yote ilishakata!

Najiuliza nimefikaje pale wala sielewi nimejaribu kujitetea sieleweki naamrishwa kuvua mkanda viatu na kukabidhi vitu vyangu kaunta.. Hakuna kusikilizwa ni amri na maguvu..

Kufupisha story nilikuja kutoka pale kituoni saa mbili usiku tangu saa 12 jioni tulipofika pale tena kwa msaada wa askari mmoja hivi na kuacha chochote kitu
Nimeingia msafi nimetoka mchafu
Nimeingia nanukia nimetoka nanuka..na mengine mengi
Mimi tena niombe lift kwenye difenda la polisi...! Nimekoma
 
Pia mmeambiwa msiogop3 kuwatania..
Wanatafuta namna ya kuongeza mahabusu hawa
Screenshots_2023-02-18-09-21-27.jpg
 
Back
Top Bottom