Mukama: Mbio za Urais CCM, sasa ni zamu ya nyanda za Juu Kusini, Kati na Kaskazini

Ozzie

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
3,217
1,259
Alisema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam...

Mukama alisema: "Kuwa na makundi ni kitu cha kawaida lakini si la mtu fulani, bali ni katika chama ili vitu viende na ni jambo jema katika chama. Kwa mfano, mambo ya urais kikanda Kusini wameshapata,
sasa inaweza ikawa Nyanda za Juu Kusini au Kanda ya Kati na upande wa Kaskazini vilevile, juu kule Mwalimu Nyerere alishatoka."

Alisema hali kama hiyo ndiyo inatengeneza makundi kwa watu wa sehemu fulani kusema: "Mbona kule ameshatoka huku bado hajatoka. Hayo ndiyo mambo yalivyo na si mtu mmoja mmoja kuwa na kundi, hayo yanayosemwa huko siyajui."


 
ina maana ni makinda,nyalandu asha migiro au lowasa!membe hana chake!mwandosya,mwakyembe wagonjwa!MAGHARIBI JEE?
 
Mmmmmmh! Hizi kauli ni za hatari sana! Hivi urais siku hizi unatolewa kikanda? Ni kwa Katiba ipi Rais anachaguliwa Kikanda?
 
Alisema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam...

Mukama alisema: “Kuwa na makundi ni kitu cha kawaida lakini si la mtu fulani, bali ni katika chama ili vitu viende na ni jambo jema katika chama. Kwa mfano, mambo ya urais kikanda Kusini wameshapata,
sasa inaweza ikawa Nyanda za Juu Kusini au Kanda ya Kati na upande wa Kaskazini vilevile, juu kule Mwalimu Nyerere alishatoka

Alisema hali kama hiyo ndiyo inatengeneza makundi kwa watu wa sehemu fulani kusema: “Mbona kule ameshatoka huku bado hajatoka. Hayo ndiyo mambo yalivyo na si mtu mmoja mmoja kuwa na kundi, hayo yanayosemwa huko siyajui.”



Mukama ana maana hii Nyanda za Juu Kusini - Prof Mwandosya; Nyanda ya Kati Mh. Sitta na Kasikazini Mh Lowasa? Utakuwa mpambanio mzuri ndani ya CCM. Kuna wengine wanahoja Wakatoliki na Waislam walishapata sasa ni 2005 ilikuwa iwe zamu ya Walutheri - Prof Mwandosya akahujumiwa. Hata hivyo naona hapa anataka kumwengua Mh. Membe (kusini) kijanja

 
Kwa maneno mengine Mukama anatuambia kuwa utaratibu wa ccm wa kumpata mgombea urais unaangalia sehemu aliyotoka mgombea! CCM hawaangalii matatizo yanayoikabili nchi hii na uwezo wa mgombea katika kutatua matatizo hayo, ila cha muhimu (according to Mukama) ni 'umetoka kanda gani?


Labda Mukama atufafanulie vizuri, ni kwa nini CCM wanaangalia mahala alipotoka mgombea na sio uwezo wake? Nini majukumu ya rais? kutambika?
 
CCM fanyeni kazi ya kutekeleza ahadi zenu "instead of kuwaza urais, haya mambo yatakuja yenyewe muda ukifika. ukanda wa nini sisi tunahitaji kiongozi atakaye tutoa kwenye hili tatizo la umaskini full stop!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Alisema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam...

Mukama alisema: “Kuwa na makundi ni kitu cha kawaida lakini si la mtu fulani, bali ni katika chama ili vitu viende na ni jambo jema katika chama. Kwa mfano, mambo ya urais kikanda Kusini wameshapata,
sasa inaweza ikawa Nyanda za Juu Kusini au Kanda ya Kati na upande wa Kaskazini vilevile, juu kule Mwalimu Nyerere alishatoka

Alisema hali kama hiyo ndiyo inatengeneza makundi kwa watu wa sehemu fulani kusema: “Mbona kule ameshatoka huku bado hajatoka. Hayo ndiyo mambo yalivyo na si mtu mmoja mmoja kuwa na kundi, hayo yanayosemwa huko siyajui.”


Ukiona mtu anaendekeza ukanda basi ujue huyo amefilisika kisiasa. Ukanda ni ukaburu tu. Duh CCM sasa hata kauli za kawaida tu zinakuwa tabu? Chini ya miaka 20 baada ya kifo cha Mwalimu hakuna hata mmoja ambaye alirithi hata robo ya hekima ya mwalimu? Wale tuliokuwa tunaambiwa ni wanafunzi wa mwalimu ndani ya Chama wako wapi?
 
Nimesoma gazeti la mwananchi sijamwelewa Mukama. Katika makundi ndani ya chama sijasikia kama kundi makundi ya ukanda. Sasa anatengeneza tatizo ambalo halipo
 
kuendelea kuwa na
watu kama kina
mkama ni JANGA!!
Wanaanza kutule
taa mambo ya
ukanda?!
 
Jamani mbona wATZ hatuna huruma?
Kichaa cha Lusinde na Mkama kinalipuka tayari,halaf badala ya kuwakamata na kuwawahsha wodini MIREMBE sie tunakazana kuwajadili!
 
mimi napiganga nae, nadhani mtu safi na mwenye uwezo hata kama akitoka pwani tena poa tu
 
Kweli CCM ina matatizo si kidogo kwa kweli.

Mkuu huwezi kuamini kama kweli hayo yameongewa na katibu mkuu wa chama, hizi zilitakiwa kuwa story za kijiweni. What if maeneo yote hayo hayana mwanaCCM ambaye anafaa kuiongoza CCM kukabiliana na changamoto zilizopo sasa? kuna haja ya chama kuwa more serious. Urais 2015 ni muhimu sana kwa Tanzania, kwa hiyo rais anatakiwa kuwa mwelewa na mweye uwezo wa kuongoza nchi.
 
Chadema wakitaka Urais kirahisi wateue mgombea kutoka Kusini. Mbowe, Slaa, Ndesamburo and company zinaua chama
 
Hee kwa hiyo vigezo vitafuata baadae kwanza ukanda???baadae itakuja udini na ukabila ni hatari sana wana magamba twaelekea wapi??vigezo ndio ingekuwa msingi na utaratibu ungebadilishwa iwe chama kinaangalia kada anaefaa kwa wakati huo sio hata kukimbilia kuchukua form
 
Akili hizi ni hatari sana, hebu fikiria huyu ndiye alikuwa Mtendaji mkuu wa Wizara (Katibu Mkuu). Wameleta Udini, Ukabila, Ufalme - yaani kurithisha watoto wao madaraka (Husein Mwinyi, Sioi Sumari, Nape, Amani Karume, Mathayo David, Malima nk.). Wamemaliza sasa Lusinde kaanzisha mradi wa Matusi majukwaani na kabla huo haujamalizika Mukama naye kazindua mradi wake wa Urais kwa Ukanda.

Shame on you Lusinde na Mukama.

Hakika sasa nimeamini CCM kuna akili za KILUSINDE.

Bora CCM ya jana kuliko ya leo - yaani - ni Bora Makamba kuliko Mukama. CCM go to hell!!!!!
 
mimi nilidhani hoja ya ukanda ni ya CDM kumbe hata magamaba wanayo...
Mungu wangu.. tufweee...
 
Back
Top Bottom