Mukama ameikejeli Katiba!

Laiti Mukama angejuea kuwa Osama angekufa jana yake ange-cancel hafla aliyowaandalia wahariri pale Krmpiski jana Jumatatu na kutoa pumba zake. Leo hii magazeti yoote, ni habari za Osama tu katika lead story zao, isipokuwa HABARI LEO tu ndiyo imetoa kipaumbele pumba za Mukama pale Kempiski kwa kuzifanya lead story.
Na hivyo hivyo kwa habari za Ris-One katika kuukana ubilionea wake.
Hii safi sana Wahariri wa magazeti – Big Up! Tuko pamoja!

Mkuu umesoma magazeti au na ww pia unaleta pumba zako? Soma magazeti acha kujiaibisha humu JF mkuu.
  • Mtanzania - front page ' CCM YATOA MSIMAMO, Mukama asema maazimio ya NEC yasipotoshwe, Aataka chama kiheshimu taratibu, aisulubu chadema
  • Tanzania Daima - Front page , Mukama , Nape wagawanyika
Sasa unayo sema ww una ushahidi nayo ? jivue gamba mkuu !
 
Ukweli unauma , sishangai juu ya hilo

yea...naumia kweli kuona wajinga ndani ya ccm wanajaribu kuondoa discussion kwenye ishu za msingi na badala yake wanaenda kuongelea vitu vingine. Kasome ripoti ya judge Nyalali ndio utaelewa vyama vyingi vilianzaje.
 
Matatizo ya CCM si CHADEMA, ni malfunction ndani ya CCM yenyewe. Badala ya Mukama kuongelea CHADEMA angeangalia zaidi mvugano na ukiukwaji wa maadali ndani ya ccm.

Haya matangazo ya CHADEMA ni zao la IMF hayawezi kujenga ccm.
 
CCM ni chama kinachokufa, juzi Mtikila alituambia kuwa CCM inakuwa kwa ugunjwa ambao kwa Kipangwa unaitwa Nambulila.. ugonjwa utokanao na tego kwa mtu aliyechukua mke wa mtu. Ukiugua Nambulila unakufa machoni kwa watu wanaokuzunguka ingawa wewe unajiona uko hai wa afya ila tatizo ni kwamba unakuwa huna nguvu wala huwezi kutoa sauti kuwazuia wasikuzike.. ukiwasikiliza CCM wanaongea wanadhani Chama chao kina nguvu na afya tele ingawa watu wengine wote wanaona ni chama kilichopoteza mwelekeo na kinakufa ...mfano suala la mafisadi kila mtu anasema lake (Nnauye, Chiligati na Kikwete wanasema kuna mafisadi wanatakiwa kuondoka kwenye chama wakati Mukama anasema hakuna kitu kama hicho!)
 
Lilombe: Inaonekana wachangiaji wengi mnabeba huyu mtoto CDM kama glasi kwa tahadhari kubwa na hamtaki kusikia tofauti na "peoples' power" kwa kweli maji ya bendera ya CDM yamelogesha, itawabidi muanze safari ya Samunge mkapate kikombe cha BABU. Ukweli Ndio Huo CDM kina mkono wa IMF hivyo MTEI alipewa kazi maalum na Viranja kusajili chama ili wao waweze kupenyeza mawazo yao na kukidhi mahitaji yao!
GeniusBrain:Mauaji ya arusha yaliisha ongelewa sana humu na chanzo ni CDM. Kuhusu bungeni Spika , Katibu wa bunge wameisha sema hawajawahi kuona bunge bovu kama hili kwa wabunge wa CDM kuuza sura badala kujadili hoja

GeniusBrain:Soma magazeti ya leo : Mtanzania etc
GeniusBrain Sio mwaka jana tu, hata maandamano wanayo fanya hivi sasa ni maagizo ya IMF. Jamaa hawa ni vibaraka si wenzetu mkuu

GeniusBrain: Jibu jepesi kwa hoja nzito, ndio tatizo la wana CDM humu JF

Ugonjwa wa "nambulila" ndio huu hapa. Ule wa mtu kufa na kuzikwa huku anajiona. Na hii ndiyo "hazina" kubwa ambayo chama tawala kimejisazia baada ya kuwaweka kando wale wengine akina makamba sr na Tambwe hiza. Yaani ndio ile top layer ya "thinkers" wao. :caked:Ndio maana wakatumwa JF Patamu kweli hapa!
Na hizo ndizo wanazoziita "hoja". Safi sanaa!:music:
Faraja yangu kubwa ni kwamba kelele za mwendawazimu hazijawahi kuziba vinywa vya werevu. Punde tuu mwendawazimu hujipambanua, watu humweka mahala pake stahili na kikao huendelea. JF ,kazi iendelee!

Faraja yangu pia,kwamba, watu wengi hupita humu kuchota hekima. Yamkini hata wanasiasa. Ninafahamu kuwa watachukua hekima na busara na kwenda nazo. Upupu wote watauacha. Yeyote aliye makini na anayejipenda kamwe hawezi kuchukua michicha ya akina nani brain sjui,au babu yao MS akaenda nayo hadharani. Kwani hajipendi?

Na mwisho faraja yangu. Huu ni mkakati mwingine mbovu wa CCM kutoka katika uchovu wa fikra na mawazo mgando miongoni mwa washauri wao. Wanafahamu fika kwamba JF ina members maelfu kadhaa tu. Na wanafahamu asilimia nyingi (zaidi ya 90%) za members wake ni watu waerevu ambao kamwe hawawezi kutilia maanani mawazo finyu kama hayo ya watumishi wao. Na wanafahamu fika kwamba machinga wa kariakoo na mkulima wa kyabakari na mvuvi wa kemondo (zaidi ya 80%) ya population hawapiti JF. Lakini bado wanapoteza muda na nguvu kazi hapa JF. Nawahurumia!
Ushauri kwa CCM:

  1. GeniousBrain na wenzako,kwanini msimpe Nape hizi "hoja" nzito namna hii,akazipeleka huko mikoani katika harakati zake za UENEZI ili chama kistawi?:tonguez:
  2. Kumbe mna hoja nzito namna hii,hakikisheni mnazitunza na tafadhari 2015 msikimbie midahalo! Watanzania watahitaji sana kuzisikia hizi.
 
Hata mimi jana nilipata shida kidogo baada ya kuisikia hiyo kauli yake. Nikajiuliza kuwa mbona CCM siku zote wamekuwa wakisema wao ndio waasisi wa mageuzi (vyama vingi) kwa maana kwamba bila wao kuridhia na kusingekuwa na vyama vingi leo. Leo ghafla wamegeuka na wameanza kusema vyama vilianzishwa kwa matakwa ya IMF. Kipi ni kipi sasa?
 
CCM WAMEFILISIKA SERA;
MWANZO WALISEMA CDM NI CHAMA CHA WACHAGA
MAJUZI WAKASEMA NI CHAMA CHA WAPENDA FUJO,
JANA WAKASEMA NI CHAMA CHA KANISA KATOLIKI,
LEO MNASEMA NI CHAMA CHA IMF,
HPE KESHO MTASEMA NI CHAMA CHA WANANCHI WENYE MACHUNGU NA TAIFA LAO, hahahahaha natabiri nape nnauye akiwa chin ya usaidiz mzuri wa mkama ndie atayekipiia msumari wa mwisho
 
Hivi humo CCM kuna mwenye akili kweli? Kama Mukama ndio "gamba jipya" na anaanza na "CDM ni ya IMF" tunategemea nini kutoka kwa this bunch of loosers?

Jana Nape kaja na mpya "Mtu akitaka kuoga huanzia kichwani"! Alikuwa anamaanisha Kamati Kuu ya CCM kujiuzulu kishkaji na kuundwa "upya" CCM imeanza kuoga kichwani. Hoja ndogo tu - wataunda misemo ya taarabu mingi lakini sisi tunasubiri majina ya mafisadi wanaotakiwa kuondoka CCM, maana bado. Tumesikia magamba yamevuka lkn hatujaona mtu ameondoka, na sasa kuoga unaanzia kichwani. We need names.
 
Asante kwa analysis yako, lakini kuna mambo mawili kwenye tafakuri yako ambayo inabidi tuyaweke sawa. Kwanza chanzo cha ugomvi wa Nyerere na mzee Mtei sio kuwa Nyerere alitaka shilingi ishuke thamani na Mtei kukataa. Bali Mtei alitaka Nyerere aridhie masharti ya IMF na Nyerere hakukubaliana naye.

Pili, China haikuambiwa ishushe thamani ya sarafu yake, ila Marekani wanataka china ipandishe thamani ya sarafu yake kwa sababu sarafu ya china inathamani ndogo kitu ambacho kinafanya bidhaa za kutoka china kuwa na bei nafuu nchi za nje
 
Mkuu nadhani umefanya makosa mengi ktk kupinga hoja ya Mukama kiasi kwamba yaonyesha unakubaliana naye hali kuna uzushi mtupu ktk taarifa yake.

Kwanza kabisa mimi nijuavyo ni Mtei aliyemtaka mwalimu ashe thamani ya fedha yetu na sii Nyerere..Aliyekataa ni Nyerere.
Pili, shinikizo la kuanzisha vyama vingi lilifanywa na IMF kwa nchi yetu chini ya utawala wa Mwinyi ili tupate mikopo, IMF haikulenga kuanzishwa kwa Chadema bali kujenga demokrasia nchini, na hii ni moja ya sifa ambazo Mwinyi atakumbukwa ingawa ilitokea kwa shinikizo la IMF.

Kwa hiyo mimi sijamsoma Mukama vizuri ila yaonyesha hata yeye hajui vizuri historia ya nchi yetu na hasa mchango wa viongozi wake ktk taifa hili. Na kibaya zaidi ni kwamba Katibu mkuu wa chama anapoombea chama cha Upinzani kife hii ni dalili ya kuonyesha jinsi alivyop mtupu ktk maswala ya siasa kwani kuombea Chadema ife demokrasia itakuwa wapi au haamini ktk demokrasia?. Kama anataka CDM ife kuna njia rahisi zaidi ya kuua vyama vingi na hatutakuwa na CDM wala CUF..
 
Huyo Mukama inaonekana bado ana hangover ya Nyerereism....... to hell with Nyerere pumbaf!
 
jamaa anaongea kama walimu wa biologia hasa wafundishapo classification, utasikia nyoka kawaida yake ni kujivua gamba ifikapo muda fulani, mara anasema maswala ya baridi na damu kuganda na mifano mingine ambayo hailandani.
Kweli jamaa ni mwalimu sio mwanasiasa kabisa.

hahaha umenichekesha sana sema huku mukama anachojua kizungu tu!mimi mwanzoni nilidhani ni mhaya
 
Nivyema umetoa yaliyo moyoni mwako. Yaelekea ww magazeti huwa huyasomi ila unasimuliwa. Kasome ya magazeti yote ya leo utajigundua ulivyo. Pole!!!!!!
Laiti Mukama angejuea kuwa Osama angekufa jana yake ange-cancel hafla aliyowaandalia wahariri pale Krmpiski jana Jumatatu na kutoa pumba zake. Leo hii magazeti yoote, ni habari za Osama tu katika lead story zao, isipokuwa HABARI LEO tu ndiyo imetoa kipaumbele pumba za Mukama pale Kempiski kwa kuzifanya lead story.
Na hivyo hivyo kwa habari za Ris-One katika kuukana ubilionea wake.
Hii safi sana Wahariri wa magazeti – Big Up! Tuko pamoja!
 
Hilo lijamaa linajidai kuongea kwa kuchanganya na kiingereza kama kawaida ya Nshomile ni famba tu, aongee masuala ya msingi si mambo uchwara uchwara, miaka 50 baada ya uhuru nchi mmeimaliza kabisa, wananchi wanamatatizo kibao, wafanyakazi hata mshahara ni aibu, mashule hoi, hospitali hoi yaani 80% ya watz wana stress ya ugumu wa maisha wewe unaleta propaganda hapa! katubu umrudie bwana mungu wako. kazi yako kubwa kulinda matumbo yenu tu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Jamaa anaongea kama walimu wa Biologia hasa wafundishapo classification, utasikia nyoka kawaida yake ni kujivua gamba ifikapo muda fulani, mara anasema maswala ya baridi na damu kuganda na mifano mingine ambayo hailandani.
Kweli jamaa ni mwalimu sio mwanasiasa kabisa.

Vyema umetambua uwezo wa Mukama. Ukiona mti wa matunda haupopolewi na mawe ujue matunda hayo c mazuri na hayaliwe na wanadamu.
 
Vyema umetambua uwezo wa Mukama. Ukiona mti wa matunda haupopolewi na mawe ujue matunda hayo c mazuri na hayaliwe na wanadamu.

Kwanza karibu JF -- Mr Mukama kwa kuingia JF leo tu baada ya kuona dongo hilo. nadhani jamaa wamekuudhi sana -- lakini ndiyo magazeti ya Bongo -- muulize Ma-rope aliyekutangulia. angalau baadaye aliweza kuyavumilia.

Nitajie magazeti ambayo yametoa habari za Mukama kama lead story katika front page zao leo. Simple question - usilete gamba lako hapa!
 
Mukama ametoka kijiweni juzi tu. Anatafuta atoke vipi ili kumridhisha aliyempa hilo chaka. Njaa mbaya jamani!!! Acha kabisa.
 
Back
Top Bottom