Mukama ameikejeli Katiba!

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema, "CCM siyo mama yangu." Je, nani zaidi ya Mwalimu? Mukama anayesisitiza kuwa CCM ndiyo ya kudumu?
Mukama karibu Chadema ukajenge nchi
.
 
Inaonekana wachangiaji wengi mnabeba huyu mtoto CDM kama glasi kwa tahadhari kubwa na hamtaki kusikia tofauti na "peoples' power" kwa kweli maji ya bendera ya CDM yamelogesha, itawabidi muanze safari ya Samunge mkapate kikombe cha BABU. Ukweli Ndio Huo CDM kina mkono wa IMF hivyo MTEI alipewa kazi maalum na Viranja kusajili chama ili wao waweze kupenyeza mawazo yao na kukidhi mahitaji yao!

Kuna mizezeta mingi humu ndani mpaka inabore hata kuchangia!!
 
Kwa mantiki hiyo vita ya ufisadi ndani ya CCM haitafika popote ndugu zangu. Nadhani wameonywa na wazee (Kingunge, Malecela na Msekwa). Wawaache mafisadi (Lowasa, Rostam na Chenge) maana hiyo move kwa mujibu wa wazee hawa itaua chama. Wameshauri wapambane tu na hoja za wapinzani wasipigane wao kwa wao. Na JK akaona hiyo hoja nzuri akapata ahueni. Mkakati sasa hivi ni kumzuia Nnauye kusema sema badala aseme Mukama ambaye ndiyo mkuu wa genge hili.

Kwa hiyo sasa vita inaelekezwa kwa wapinzani na hasa Chadema, watatumia Dola (siyo USD), Fedha, na siasa za maji taka kuhakisha wanaua upinzani.

Subirini muone.
 
Sasa kama vilianzishwa kwa shinikizo mbona vinakubalika? Na wao mbona wanajivua gamba kwa shinikizo la Chadema?. Rais Kikwete alisema hivi ni vyama vya msimu na havimnyimi usingizi mbona sasa halali? vikao vyao mpaka saa 7 usiku. Jaribu kila mbinu mzee labda utafanikiwa.
 
Hivi humo CCM kuna mwenye akili kweli? Kama Mukama ndio "gamba jipya" na anaanza na "CDM ni ya IMF" tunategemea nini kutoka kwa this bunch of loosers?

Jana Nape kaja na mpya "Mtu akitaka kuoga huanzia kichwani"! Alikuwa anamaanisha Kamati Kuu ya CCM kujiuzulu kishkaji na kuundwa "upya" CCM imeanza kuoga kichwani. Hoja ndogo tu - wataunda misemo ya taarabu mingi lakini sisi tunasubiri majina ya mafisadi wanaotakiwa kuondoka CCM, maana bado. Tumesikia magamba yamevuka lkn hatujaona mtu ameondoka, na sasa kuoga unaanzia kichwani. We need names.

Unashangaa bendi ya taarab pwani? CCM ni chama cha Taarab na music so kuwa na misamiati ni hasa sehemu yake kwasababu bila hizo beti hazi nogi. Alianza Mkapa ooh siasa za wazi na kweli mara baada ya muda akajipinga mwenyewe 'ILANI ya CCM haitekelezeki' kwamba ukiwa fisadi huwezi kuwa mwazi na kweli; akaja JK maisha bora kwakila mtanzania mara naye akajipinga kwamba akili za mbayu wayu changanya na zako..akatangaza mwenyewe hadharani wafanyakazi kama mbayuwayu walichukulia ILANI yao hiyo kuwa ni kweli na kushindwa kuchanganya na zakwao kuwa maisha bora ni kwa mafisadi na watanzania wengine mlie tu ndiyo maana amegoma kuwawajibisha walioiba pesa zetu na kusaini mikataba faki...Sasa leo wakija na msamiati murua wa CHADEMA ni chama cha IMF si ni heri kwetu sisi wanachadema maana kati ya CHADEMA na CCM nani ni mbeba bakuli la matonya huko IMF? Aise ikolezeni hiyo statement ili hizo za kimatonya zidondokee kwenye chama chetu. Kesho IMF wakija juu utasikia tulikuwa tunatania tu hatukumaanisha duuh! inahitaji moyo kuwa member wa hiki chama.

Wengine tumeshachanganya za mbayuwayu na za kwetu and soon you will know kuwa kweli zinachanganyika vizuri na kuleta concotion kama ya babu wa Loliondo yenye uwezo wa kudhibiti virus, bacteria hadi biochemstry ya mwili.
 
Mukama=Makamba=Tambwe=Nape hamna tofauti, bora hata yule aliekuwa anaimba mashairi yao kidogo anaonekana kuwa na akili...
 
Yaani Mukama kamkosoa mpaka M/kiti wake. Wakati M/kiti alisha sema anayosema Nape ndiyo kauli ya chama.
Haya sasa tusubiri matamko kama kawaida yao UVCCM, UWT, BARAZA LA WAZEE nk.
:israel:
 
‘………………………chama kimeanzishwa kwa shinikizo la shirika la fedha ulimwenguni (IMF). You can quote me on this (nikariri katika hili) . Yule aliyetofautiana na Nyerere ndiye aliyekwenda kukianzisha’.

Kauli ya Mukama

My take : Kama hali ni hii basi haya pia yapo :
  1. CDM ni chama cha kutoka nje na kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi. Ili wakifanikiwa kuchukua dola, wale walio watuma na kuwafadhili wawalipe fadhila
  2. Kama aliye kianzisha alikorofisha na Mwasisi wa Taifa hili , basi alikuwa hana akili na adabu. Kutokana na msingi wa laana hiyo basi ndio maana CDM inazidi kuwatafuna kwa kutotii sheria za nchi. Mifano ipo wazi kabisa mauaji ya Arusha , utovu wa nidhamu bungeni nk

Ndugu yangu kutokana na jina lako nilifikiri utakuwa mwerevu ktk hoja zako nafkiri unazi au ushabiki umekujaa kiasi kwamba hutaki kutumia uerevu wako ktk kuchanganua mambo.
Kuhusu suala la vyama vingi lilikuwa agizo la IMF likiwa na lengo la kupanua demokrasia na kuongeza uwajibikaji wa serikali hili lilikuwa agizo kama la ubinafsishaji au cost sharing ambalo serikali ya CCM iliridhia na mwl nyerere mwenyewe aliliunga mkono.
Kuhusu suala la muasisi wa CDM na Nyerere kutofautiana mawazo ni jambo la kawaida na kile ambacho alikikataa kwa Mtei walikuja kukubali baadae tena likaleta hasara kubwa refer urasimu wakati wa ubinafsishaji so mwalimu angelikubali wakati ule haya yote yasingetokea, pia azimio la arusha ambalo pia lilileta kutokubaliana halikufanyiwa kazi ipasavyo na watenda kazi wa mwalimu coz lilikuwa more individual ideology. Kwa taarifa yako mwalimu alikuwa anamuheshimu sana Mtei na ushauri wake ndo mana hadi wakati anaaga dunia still alikuwa anamuita governor akisema once a governor always a governor na kuhusu kutofautiana kwao idea hebu fuatilia kilichojiri ktk mkutano wa nec 1977 pale arusha wakati mtei alipotakiwa kutoa ushauri wa kitaalamu kama gavana na kusema hali ya uchumi na kuhusu azimio la Arusha. Kwa msaada zaidi kuhusu hili naomba usome kitabu cha autobiography ya Edwin Mtei kinaitwa from ''Goatherd boy to Governor'' kuna kila kitu kuanzia tofauti yake na Nyerere hadi uanzishwaji wa CDM.
Ktk hili la kutofautiana mawazo na Nyerere si jambo la ajabu kwani mwalimu hakuwa malaika alikuwa na mapungufu yake pia kutofautiana idea ktk masuala fulani ni jambo la kawaida kwa intellectuals mfano mzuri ni mimi na wewe jinsi ambavyo hatujakubaliana ktk hili na sio kosa. Mbona mwalimu alitofautiana na Kwame Nkrumah ktk suala muungano wa africa sasa hapo nani alikosea? Any normal being kutofautiana idea ni kawaida since human beings are unique beings.
Mwalimu hakuwa Mungu alikuwa na mapungufu mengi, kuhusu kuwa CDM ni chama cha IMF ckubaliani na wewe wala Mukama kama ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Tanzania utakumbuka kuwa baada ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa wanasiasa wa zamani ambao walikuwa hawkubaliani na siasa za mwalimu ktk mustakabali wa tanzania walianzisha vyama vya siasa vikiwa na malengo mazuri tu ya kuichallenge ccm na idea zake sema ccm ilivihujumu kwa kujaza mamluki wake huko na kuviua na cdm ilibaki na ikaendelea kustawi taratibu kwa stability ya mzee mtei mfano wa vyama hivo ni CUF chini ya James Mapalala yeye aliishia kufukuzwa, UMD chini ya Chief Abdalah Fundikira, TADEA ya Oscar Kambona na wengine kina kasela Bantu na Kasanga Tumbo wakiwa UDP so msianze kuleta uzushi kuhusu CDM cjui nini oohh nini timizeni wajibu wenu ebo! Ni chama kama vyama vingine vya siasa sema kimesurvive tsunami ya umamluki iliyoandaliwa na CCM thats why now mnaanza kuleta majungu na ninajua cdm kina malengo mazuri kwa tanzania kama yalivyokuwa mawazo ya nyerere ila katika persepective tofauti na ya mwalimu na ccm yake.
Anothertime geniousbrain use your ''high iq brain'' kusoma historia ya kitu before judging into conclusion, i know ur genious use ur ability
 
Edompo ndie Mukama!!

Pole Mukama yaelekea Mafisadi washakutisha unaanza kutoa Povu Washakutumia Jini la Tabora Lile Linakufanya uwe na Hasira Lilishawahi mpata Ditopile akawa mtu wa hasira hadi Akaua... hohohohoho Umejiponza mwenyewe RA kakumaliza

Weweseko lako sasa Unabishana na wenzako hadi mwenyekiti opsssss!

Kweli Siasa ni Mchezo Mchafu!
 
Mukama mimi naona yeye ni mwana propaganda kuliko hata Makamba! Kama huyu ndio mtendaji mkuu wa Chama Cha Magamba (CCM) basi chama hakina Katibu kabisaaaa!!! Kwa kauli zile za mukama nafikiri CCM tatizo bado liko pale pale. "Aliponiacha hoi ni pale aliposema kjuwa CCM ni chama cha matajiri kuliko vyama vingine kwahiyo hakiwezi kufa" Lkn kilichonishangaza ni kwamba mawazo ya Katibu huyu wa Magamba bado anaamini kuwa wataendelea kununua wanachama kwa utajiri wao! Sidhani kama Mtanzania wa sasa bado unaweza kumdanganya kirahisi kwa kanga, T-shirt na kofia!!
 
Pamoja na kwamba Ndiamukama ni kiongozi wa chama kisichokubali mabadiliko kwa ujumla wke, huyu baba binafsi ni msomi na anajua maana halisi ya KATIBA hivyo nitasita saaaaaaaaana kuamini madai yoyote kwamba eti kakejeli alama ya muongozo mzito kama huo.
 
Back
Top Bottom