Jamii Forums inasomwa na watu wengi sana ndani na nje ya Tanzania. Na wasomaji hawa wapo watanzania na wasio watanzania ili mradi wanaelewa kiswahili. Hili jukwaa linatupa nafasi nzuri ya kutoa maoni na michango ambayo kimsingi ni ya kujenga taifa hata kama ni kukosoa basi ni constructive criticism. Na ndio sababu watu wanasema ni jukwaa la 'great thinkers'.
Vyama vya siasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Na vyote vinasajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria husika. CCM, CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP, NLD, DP, Demokrasia Makini vyote hivi vimesajiliwa baada ya kutimiza masharti yaliwekwa.(wasiliana na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kupata nakala). niishie hapo.
IMF - nadhani unaongelea International Monetary Fund ni taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na maswala ya kifedha na uchumi kwa nchi wanachama. Narudia - nchi wanachama. IMF wanachama wake ni NCHI na sio chama au kikundi kimoja kimoja. NCHI.
@GeniusBrain, naomba usome hii "IMF is an organization of 187 countries, working to foster global monetary cooperation, secure financial stability, facilitate international trade, promote high employment and sustainable economic growth, and reduce poverty around the world".
Tanzania ni mwanachama wa IMF na ndio maana tumekuwa tumapata mikopo huko. CHADEMA hata CCM au chama kingine chochote hakiwezi kuwa mwanachama wa IMF hata kama wangetaka iwe hivyo.
Nirudi kwenye point yangu ya msingi, Ndugu yangu GeniusBrain hoja yako si tu ni aibu kwako binafsi bali pia inatuibisha watanzania wote (milioni 42 na ushee), kwamba, hatujui maudhui na kazi za taasisi za kimataifa kama IMF. Na mbaya zaidi hatujui hata vyama vya siasa ndani ya mipaka ya nchi yetu vinanzishwaje.
Sijui ulikuwa unalenga nini hasa kwa kuanzisha hii hoja ila nadhani tuhimizane humu jamvini ili hii kasumba ya porojo, character assissination, mudslinging na cheap political scoring tactic zikome. Ni aibu mno kwetu sisi watanzania.
Mwisho ningekusihi sana ndugu yangu GeniusBrain na wengine wenye maoni kama yako watambue kuwa watanzania wana akili timamu na wana uwezo wa kutenganisha mema na mazuri. Maneno kama...chama fulani kinafadhiliwa na watu wa nje kuivuruga nchi' ni madharau kwa watanzania wenzako (insult to our intelligency).Tabia ya kikoloni hii.
Tutumie hili jukwaa kwa kuongelea mambo ya msingi na yenye tija tuache kuaniaka umbumbu wetu hadharani.