ukichukulia mfano wa nchi nyingi za Afrika na za Asia (Far East) mf Singapore, Korea Kusini na Kaskazini, Japan zimeendelea sana kwa kuwa dini zao Budhissm au Shinto hazikupewa nafasi ya kuongoza sera za nchi wakati kwa Afrika dini zinaingia kwenye siasa
Nchi za Asia zilisisitiza elimu za sayansi na hesabu wakati Afrika hawakutoka kwenye dini na wawakuwa na elimu ya ufundi
North Africa ina nchi saba, nchi nne tu ndio zina unafuu, Nchi zenye maendeleo kiasi na unafuu West Africa ni za Wagalatia wengi na Nigeria ambayo iko nusu kwa nusu.
Kumjibu mtoa hoja ni kwamba maendeleo hayajatokona na dini bali utawala bora, elimu, miundombinu , technology na sera za kijamii
Dini inachangia moja kwa moja tu kwa maadili ya kijamii mf, nidhamu ya kazi, uaminifu na mshikamano wa kijamii (social cohesion)
Una nchi zenye maendeleo kwa nchi kama za Asia zenye dini tofauti mf Shinto -Japan, Budhism,-S Korea, Hindu-India: Atheists na wakiristo kwa nchi nyingi za Ulaya na waislam kwa nchi za Bara Arab mf Saudi Arabia, Oman, UAE, Qatar na Afrika kama Morocco, Algeria nk
Kuna umaskini kwa nchi zenye dini hizo kama Budhist kwa Vietnam, Cambodia Nepal, Greece, baadhi ya Eastern Europe kwenye wakiristo kama Bulgaria na Hungary na nchi pia kwa za kiarabu au zenye waislam wengi kama Yemen, Bangladesh na Afrika kwa nchi kama Mauritania, Comoro na Djibout
Ukienda South America pia trend ni hiyo kuna nchi zinafuata dini sana kama Brazil na Argentina lakini kuna tofauti ya maendeleo baina ya nchi na nchi kama Colombia, Peru na Nicaragua kwa dini hiyo hiyo na ufuasi wenye kiwangi hicho hicho