Muhongo anaivuruga TANESCO, Magufuli yuko wapi?

"baadhi ya maamuzi yake na 'amri' zake kwa
TANESCO yamepelekea deni la TANESCO
liongezeke mara 5 zaidi"

Mkuu The Boss naomba unisaidie ufafanuzi wa hayo maamuzi yaliyopelekea deni la tanesco kuongezeka mara 5
 
kwani hawa tanesco wapo hai bado? mana hapa kwangu kuna waya zimeshuka mpaka watoto wanataka kubembea na wakina mama wanataka kuanikia nguo......jamaa hawaji hata uwafate na masidisi benzi...
hahaaaaa!, ndugu acha kunichekesha, nao naona wamekua kama dawasco, pale kinondoni mkwajuni kuna bomba la maji limepasuka na lina mwaga maji. Nimeliona tangu mwaka jana mwezi wa saba! hadi sasa hivi lina tiririsha maji, alafu si kwamba lipo mafichoni lipo wazi kwenye kituo cha daladala.
 
Wewe inaelekea Ulikuwa na mirija ya Ulaji Tanesco Sasa Muhongo kaziba line zako umeamua kumshambulia sana .
 
Kama management ya tanesco imekaa muda wote huo lakini wameshindwa kushusha umeme,lakin prof ameanza juz tunaona impact yake,ni heri aendelee hivyo hivyo ili mambo yaende
Mleta mada kaamua kusaka huruma JF Kwa njia za ujanja , lakini Muhongo anachapa kazi hata Kama ana mapungufu yake Kama binadamu lakini mazuri ni mengi kuliko mabaya ,
 
Ni kweli,hapo unaweza ukute amemsikia mtu anazungumza basi na yeye ameweka boriti hapo hapo
 
Kwani huyu muheshimiwa ni mkabila gani vile?maana kama ni yale makabila ya pale maeneo flani kujisifia huwa ni kawaida yao wao huwa wanajua kila kitu.
 
Usiwe unatazama mambo kwa roho ya kimasikini

Wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao
ukifanya kazi Daily News gazeti hununui
ukifanya kazi tigo au voda airtime hununui
iko dunia nzima

hata wapiga debe tu daladala hawalipi nauli.....
Wafanyakazi wa tanesco umeme ni jasho lao? U must be kidding...kupewa 700kWh kwa mwezi ni sawa na shs ngapi, while the company makes no profit.

Nimewahi kupanga nyumba ya mfanyakazi wa tanesco, umeme ulikuwa bure...bure kabisa! Kama mpo radhi wafanyakazi wa tanesco wale "jasho lao" while mwingine atanunua 1kWh kwa 290tsh mtakuwa na yenu.

Mleta mada umelalamika tu, toa facts angalau tano ili mada yako iwe tangible.
 
Ili la kushusha bei lilishangaza, mpaka EWURA wanakuwa na wasiwasi kuhusu punguzo linaloombwa! Lakini tunashangaa nini kwa stahili ya sasa tunaiona mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya n.k. wote wanafuatilia 'utendandaji' hadi kwa maofisa wasiowajibika kwao na tena kwa kuruka mamlaka zinazowahusu maofisa hao. Wanawawajibisha bila mamlaka zao kujua au hata kujulishwa - wanazisikia bombani!
 
Naona unaongelea a hear say, na hoja yako inarudi kwa Muhongo wa wakati ule wa awamu iliyopita eti reference yako ni escrow na maandiko ya Zito Kabwe.

Umeombwa utoe japo maamuzi 5 ambayo muhongo amefanya recently na yameingiza hasara TANESCO wewe unataja issue za Escrow.

Acheni jamaa apige kazi, unataja eti Muhongo ni mtaalam wa miamba that hafahamu mambo ya umeme! Hivi Charles Kitwanga ni askari? Mbona anaongoza polisi, Magereza, uhamiaji, etc?

Je Lukuvi ana utalaamu wa Aridhi au mipango miji? Mbona anakwenda vizuri sana na ile wizara?

Inawezekana bado mnahasira ya kujimwa vitalu. Kwa taarifa yako hio Tanesco isipokaliwa kooni tutavuna mabua.
 
Yaani uoni yanayoendelea! Haujashangaa kwa shirika linalofanya hasara kuomba kushusha bei ya huduma zake? Haya ndiyo yalichangia kuua mashirika yetu huko nyuma. Ebu tuache mashirika yanayotoa huduma kibiashara yafanye hivyo ili tusije beba mzigo mkubwa huko siku za usoni.
 
Watu hawajui kuwa unaweza kuwa msomi lakini usiwe umeelimika....! Na Hilo ndio Naona linalomsibu prof.....!
kweli kabisa mkuu,kitendo cha muhongo kuamuru kuondolewa kwa service charge hakikubaliki kabisa
 
Usiwe unatazama mambo kwa roho ya kimasikini

Wafanyakazi wa Tanesco huo umeme ni jasho lao
ukifanya kazi Daily News gazeti hununui
ukifanya kazi tigo au voda airtime hununui
iko dunia nzima

hata wapiga debe tu daladala hawalipi nauli.....
Nadhani unajichanganya sasa.

Unataka tuamini kuwa akina Masamaki wa TRA walikuwa sahihi kukutwa na ndoo za manoti ya fedha kwa sababu wao walikuwa ni wakusanya fedha? Ama habari ya Dr Dau kununua kiwanja kwa shs 1m halafu anaiuzia NSSF 1bn was ok? Kisa ni jasho lao.
 
Tokea prof ateuliwe, UMEME haukatiki ovyo, no service charges, TUNATAKA NINI TENA WATZ????
Nilitaka kuandika hivyo pia, tangu jamaa aingie wizarani umeme umekuwa stable kwa zaidi ya 75%. Tumepunguziwa bei kwa 2%(japo sio kubwa sana), tumeondolewa service charge(5220tsh)....tunataka nini zaidi, especially sisi ambao hatuhusiki huko?

Huko nyuma tuliumizwa, umeme ulikatika ovyo, charges zilikuwa juu. Tuseme management iliyokuwa ilifanya vizuri kipindi hicho? That's lame to say the least. Leo mtu anakuja kusema 700kWh ni jasho la wafanyakazi wa tanesco well, jasho la waalimu, daktari, tra etc litakuwa nini? Kila anayefanya ofisi fulani apewe bure coz ni jasho lake?
I like positive criticism, but this one...nah! Muhongo has been doing well, kama Mramba alishindwa kuongoza then, aliachwa huru na kufanya alivyotaka na tulikuwa tunaumia ni heri waziri akaingilia kati ili tupate unafuu.
 
Prince nakuunga mkono, watz wakisimamiwa wanaleta longolongo, kimsingi hakuna shirika lenye watu wazembe na wapenda rushwa kama tanesco.
Hili shiririka linaingiza pesa nyingi sana shida kuna mchwa wengi na uzembe uliokithiri.
Mtu anaposema kuondoa service charge kunaongeza deni la tanesco haiingii akilini sababu wakati tunalipia hakuna cha huduma ilioboreshwa, mfano nguzo nyingi zimeoza hadi zimeinama, nyaya zimelegea hadi watoto wanaweza kugusa, nyaya zimekatika ovyo ukitoa taarifa watakuja baada ya siku tatu. Unapopeleka maombi ya kuunganishiwa umeme, itachukua zaidi ya mwezi kuja kusavei, vinginevyo wanaomba rushwa sio chini ya ,50 elf wao wanaita nauli.
Tatizo lingine ukimaliza hatua za awali hadi kupata umeme bila nguzo inachukuwa zaidi yawezi, pamoja na nguzo ilikuwa zaidi ya miezi 6.
Maswali kwa mleta uzi;
1) ni nani aliyewezesha wananchi
Kunganishiwa umeme ndani ya
Wiki mbili bila nguzo kama sio
Muhongo?
2) ni nani aliyepunguza miezi toka
Sita hadi mmoja kwa wale wa
Maombi ya nguzo?
3) ni nani aliyesababisha nishati ya
Umeme kupungua bei toka 450,000 hadi 177,000 vijijini na leo ni 150,000?
Acha aingilie kati kwani mlipewa nafasi ya kuomyesha uwezo wenu kuwa mnaweza na mmefeli.
Sina imani na wafanyakazi wa tanesco, wamenitesa.
 
kweli kabisa mkuu,kitendo cha muhongo kuamuru kuondolewa kwa service charge hakikubaliki kabisa
Ni nzuri Kwa upande wa wananchi lakini ingekuwa bora Zaidi gharama Kwa unit zingeshuka......!
 
Tanesco ilikuwa imeoza! Na huu uzi ni ushahidi wa huo uozo! Yaani hatua za kuondoa uchafu zinaonekana kama kuingilia majukumu ya wataalam!?
Yaani waziri akae tu asubirie mtaalam alielikoroga miaka yoote eti ndo ageuke kuwa jiwe kuu la pembeni!!
Kabla hujatumbuliwa yatumbue yote yaliyo ndani ya uwezo wako kaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…