Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,174
- 143,959
Nakuelewa, ila ukiangalia kwa makini mijadala ya namna hiyo huwa ni ile ya kutafuta ushindi, yaani kati ya upande huu na upande ule ni upi umeshinda. Kwenye jamvi hapa hatujagawanyika makundi mawili kwa hiyo upambanaji wa personality siyo wa muhimu kabisa.
Halafu kumbe huwa unawaangalia jamaa hao? FOXNews na mimi mbalimbali kabisa, hasa huyu Bill O'Reilly.
Ha ha ha! Hatred. Hatred. Hatred. Brother, take it easy. This is just a forum. I am sorry you are frustrated by my way of discussing mpaka umejipa u-Dr. Phil. Ha ha ha!
Mkubwa, one thing you can be sure: nitaendelea na mawe tu - hata kama unaniombea kifo.
Kakalende,
Wala usiwe na taabu kabisa kwani hapa nyumba ya ubishi kama ilivyosema!.....sina taabu lakini moja tu usije na story za kuwahukumu watu ambao hawana hatia kwa makusudio ya kuficha ukweli.
Haikuwa lengo langu kujadili mtu yeyote humu na hata siku moja siwezi kuanza kukujadili wewe hali sikufahamu. Ukitazama kwa makini mashambulizi ya personal yametoka upande mmoja!.. mimi husubiri tu with my Ace card!
Kitu kikubwa nachopinga mimi ni hii mikwara ya kutaka watu wasizungumze kitu kuhusu hawa mafisadi wakubwa wanao endesha nchi yetu kwa mitulinga. Kazi zao kutwa ni kutumia watu na kutuma PM kwa watu kutishia tuuuu!... Nina hakika Mwanakijiji kisha fuatwa sana mbali na hoja za humu kupinga kila analojaribu kufanya. Na sasa kujipumzisha kwake nina mashaka nako vile vile!
Nia na madhumuni yao ni kuzuia watu to speak up their mind! na bahati mbaya wapo watu wanaokubali kununuliwa.
Mjomba hakuna price tag kwa Mkandara!...na ndio maana kamili ya neno Babu Ubishi! sikubali kuona watu wakidhulumiwa haki zao hata siku moja na nafuata mtazamo wangu mwenyewe ktk swala na sio CCM, Kiongozi fulani wala babu yake - Hii ni forum huru!
Huyu mwandishi Rweyemamu kaniboa na kanitibua sana kuweka tungo zake hapa kwa sababu wakati data zake zote tunazijua vizuri. Na kama nasema uongo ajitokeze humu kama walivyofanya waandishi wengine!
Mkandara,
Longolongo na maneno marefu pembeni. Leta source yako, inayothibitisha kwamba Rais alienda kumuona Amina mchana wa siku aliyokufa, kama ulivyoahidi. Kama huwezi, basi leta facts za ku-dispute "timeline" niliyoitoa ya Rais kuanzia 25 June hadi 27 June.
It is important to sort this out kwasababu ulisema with certainty kwamba Rais more or less alienda kumuaga Amina mchana wa siku aliyokufa kwasababu he knew what would happen jioni yake.
My beef ni kwamba ni lazime ifike mahala tukaheshimiana hapa JF kwa kuleteana taarifa za ukweli, hasa pale tunapo-accuse watu. Mwenzako Mzee Mwanakijiji kawa muungwana na ka-withdraw statement yake ya kwamba Mwandosya alikataza ujenzi Serengeti. Na vilevile ameng'amua kwamba katudanganya aliposema Nchimbi na Kayombo wanagombea nafasi moja ya NEC kule Ruvuma. Na wewe mkubwa ng'amua kwamba umeleta JF habari isiyo ya kweli kwasababu Rais hakuwa Dar siku Amina aliyokufa. Period.
MugongoMugongo,
Amini usiamini haiwezi kubadilisha kitu wala maelezo yako wewe hayawezi kubadilisha ukweli kuwa alikwenda na pia kwenda kwake hakuna uhusiano wowote na issue ya Rweyemamu.
Nimekuomba source umesema ulikuwepo wewe hali najua hukuwepo hata kidogo ktk msafara huo. Na kama huyo mpoiga picha wa rais ndio umezungumza nane kwa simu tufanye 3 way sasa hivi! source yako ikiwa kwa salamu sina haja...
Wewe huna ushahidi zaidi ya kusoma magazeti ambao hawafahamu kabisa misafara ya rais zaidi ya kuwa wamealikwa.
Sinatatizo na beef lako. Wee tuendelee tu ndio starehe ya JF, kwa sababu beef lako naliweza, bring it on brother!
Masatu,
Unafikiri mimi siwafahamu wewe na huyo Mugongo Mugongo?... mnatunga mengi tu hata mmefikia kusema JK alikwenda kuhani baada ya tafrija za BBC! huu ni uongo kwa sababu JK alikuwepo hapo jioni ya tarehe 27 lakini sii hoja kwani mnatafuta ufa wa kupenyea ktk sakata hili la marehemu. I have my sources na nitaziweka nitakapo ona kuna kila haja lakini mnazunguka tuuu na habari za magazetini ambazo pia zimewashinda kudhihilisha!
Haya hakwenda kumwona mnachotaka nini hasa!....does it change kuwa mnahusika na kutetea watu wahalifu walio muua AC.
Na bado mtatafuta njia zaidi lakini hamtaweza kunifumba mdomo!...Nchimbi na wauza Unga wote mnahusika na kifo cha marehemu!.
mugongoX2,mkandara,
kama Raisi alikwenda kumuona Marehemu AC, au hakwenda itasaidia nini haswa? Je, ndiyo itamrudisha AC? What are you guyz trying to achieve?
Sawa mimi MUONGO! iache kama ilivyo!....twambie wewe mkweli.
Jokakuu,
Lini nyie mtaacha woga kuwachimbua hawa waovu?... CCM ni jina kubwa zaidi ya hawa watu wachenzi wachafu ambao mnajaribu kuwabeba na kulipaka tope jina la chama. Kazi ya hawa jamaa ni kubadilisha maneno!...naona na wewe umeingia mkenge wao kuwa nazungumzia chama kizima cha CCM.
Nchimbi is behind all this kwa sababu wauza unga wote wana mitego yao hadi serikalini. Kama unakumbuka marehemu alipewa warning kwa message akiwa Bungeni baada ya kulianzisha sakata hili kabla hata halijatoka nje. marehemeu kweli alinyang'anywa simu yake asiweze kuwasiliana na mtu yeyote... naleo hii tunawaona hawa jamaa wakija hapa kuchangia Kila mada inayohusu marehemu kupinga dhana zozote zinazowahusu hawa washenzi!
Written by Maxence M. Melo Tuesday, 26 June 2007Rais Jakaya Mrisho kikwete akiweka saini Kitabu cha maombolezo Nyumbani Kwa Wazazi wa Marehemu Amina Chifupa jana jioni. Rais alikwenda nyumbani hapo kifariji familia ya marehemu.