Muhimu: Zijue athari za kuondoa thermostat kwenye gari yako

Kwa kuongezea tu athari za kuondoa thermostat , kutaifanya Air condition kutofanya kazi vizuri as radiator inakuwa na joto Muda wote , kwa magari makubwa inaweza kuchangia kuchemsha pia hasa kwenye milima mirefu , maana maji yanakuwa yanachemshwa yote kwa pamoja .

Sent
Mmmmmmmhmn bro, thermostat inafanya kazi ya kupush temperature up sio kuishusha. Yaani ipo kudetect kiwango cha juu cha joto kinachotakiwa. Sasa ukisema thermostat ikifa radiator inapata joto, then nambie inapataje joto?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuelewa hili somo inahitaji umakinu kidogo Ila nitajaribu
Chukulia thermostat Kama geti lililofungwa na hufunguka tu baada ya joto kupanda . Ukiichunguza thermostat huwa Zina maandishi ya ufanisi wake , mathalan nyingi huandikwa 85c.maana yake ni kuwa hii itazuia Maji yasipite Hadi itakapofikia 85 c .
Unapowasha gari asubuhi engine huwa ni ya baridi , inachofanya thermostat ni kuyazuia Maji hayo ya baridi yasiende kwenye radiator kupoozwa , bali yazunguke humo humo kwenye engine Ili kupata optimum combustions ,joto likipanda thermostat hufunguka Ili kuruhusu Maji ya baridi kutoka kwenye radiator yaingie kwenye engine kupooza . Kiufupi thermostat huwa Inachelewesha Maji kuchemka.
 
nimewasikiliza (kuwasoma) watetezi wengi wa THEMOSTAT......

Kuna kiyu kimoja muhimu kwetu sisi TUNAOTOA THEMOSTAT.........

Mliyoyaeleza KITAALAMU hayapo hivyo KIHALISIA.........

Yote mliyoeleza nikinyume chake kihalisia....... BINAFSI NAPENDEKEZA KUTOA THEMOSTAT KWA GARI ZA SHURUBA NA MASAFA

Ila kwa hawa wa MAGARI YA KULA BATA, na yale ya KUSHINDA OFISINI....MSITOE ASILANI........

Ila kwa wale ambao GARI IKIWASHWA ASUBUHI ITAZIMWA USIKU ........nashauri ONDOA tena Ondoa tena
 
Bado kazi ya thermostat huijui.

Na mjerumani kwa kujua uwepo wa watu kama nyinyi akaweka thermostat ya umeme. Ambayo inasoma position kama iko open au close hata ikifa fasta sana ukifanya diagnosis unajua kama iko stuck open au close.

Na zaidi huwezi chomoa hiyo thermostat na ukaendesha hiyo gari kama mnavyofanya kwa mjapani.
 
kwa sisi watumia magari ya kijapani....... Tunajua umuhimu wa kuondoa hiyo SEMOSITATI,

1. Ulaji wa mafuta
2. uchokaji wa injini
3. kuchemsha (gari itachemsha mara moja , mbili ama tatu baada ya kutoa huo upuuzi, baada ya hapo ni mwendo mdundo)
 
Thermostat Ni muhimu sana , inashauriwa hata Kama imefail , ibadilishwe sio kutolewa , kuna sababu pia kwa nini maji yapo pale Kama coolant na sio liquid nyingine

Tuchukulie mfano huu, chemsha maji kiasi Lita 2 yafike boiling point kabisa 100c mathalan maji ya kupika ugali kabla hujaweka unga, then chukua maji baridi , kikombe cha chai uweke kwenye hayo maji yaliyochemka , kitakachotokea yataacha kuchemka na kuanza upya kuitafuta boiling point .

Mifumo wa thermostat ni kama nilivyoelezea hapo,inafungia maji kwenye engine na kuacha mengine ya baridi nje , joto likiongezeka kwenye engine inaruhusu kiasi kidogo Cha maji ya baridi yaingie kwenye engine na kuruhusu mengine yaende kwenye radiator ambapo Kuna maji mengi ya baridi, yakifika kule yanapozwa haraka , na haya maji ya baridi yaliyoingia kwenye engine yanafanya kama nilivoelezea hapo juu , cycle ni hiyo hiyo , japo inaweza kuongezeka frequency kutokana na kazi engine inafanya,

Faida zake ni kuwa
1 fan haitakuwa on muda mwingi Mana radiator inakuwa na kiasi kikubwa cha maji ya temp ndogo,

2.water pump itadumu sana Mana muda mwingi inakuwa imepumzika,

3.fuel consumption itakuwa nzuri maana , kuendesha fan na water pump Ni mzigo mwingine mkubwa tu hasa kwa magari makubwa,

4.Radiators zitadumu pia sababu kwa kupokea maji ya moto kwa muda mfupi tu, hasa radiator hzi za plastic,

5. Engine isiyo na thermostat huwa haina maisha marefu hii husababishwa liquid hammering ,maana muda mwingi cylinder zinakuwa na rich mixture ya mafuta , na hii huondoa ufanisi wa oil Kama kilainishi.

Sent
Samahani utaijuaje kuwa themorstat ya gari yako sssa ni mbovu?
 
kwa sisi watumia magari ya kijapani....... Tunajua umuhimu wa kuondoa hiyo SEMOSITATI,

1. Ulaji wa mafuta
2. uchokaji wa injini
3. kuchemsha (gari itachemsha mara moja , mbili ama tatu baada ya kutoa huo upuuzi, baada ya hapo ni mwendo mdundo)
Si sahihi unachoongea ukitoa thermosta ulaji wa mafuta unaongezeka
 
Samahani utaijuaje kuwa themorstat ya gari yako sssa ni mbovu?
Kwa gari za kijapani

Ikiwa mbovu kwa kustuck open ni ngumu kidogo kujua japo kama ni mtumiaji wa function ya defrost kwa ajili ya kuondoa ukungu kwenye kioo mara kwa mara utanote kwamba ukungu hautoki haraka kama siku zote.

Ikistuck close gari itachemsha.

Kwa gari ya Kijerumani au gari yoyote yenye thermostat ya umeme, ikistack either kwa kuclose au kuopen basi gari itawaka check engine lakini pia inaweza kuchemsha kama imestuck close au isichemshe kama imestuck open.
 
tupate mfano hai kwa watu wa aina tatu.....

1. Mtu aliyemiliki gari (mawili itakuwa vizuri) kwa muda mrefu , say zaidi ya miaka 5 moja ametoa SEMOSITATI na lingine hajatoa

2. Mtu mwenye magari mengi (mfano 10) na kati ya hayo mengine ametoa na mengine hajatoa (ni vizuri magari haya yawe ya shughuli pevu mfano DALADALA

3. MTU mwenye gari moja na hasa haya ya kisasa ikiwezekana yenye SEMOSITATI ya umeme

Hakika nakuambia kwa wote hawa watakuwa na majibu tofauti juu ya umuhimu wa kifaa hicho.

Pasipo kusahau pia kuwe na MAFUNDI wa aina mbili, WALE WA KITABU na wale wa CHINI YA MWEMBE (experience is a good teacher) wote hawa watakuwa na majibu tofauti

NI SAWA NA MJADALA WA JE AC ya kwenye gari inachangia ulaji mkubwa wa mafuta au haichangii........ JIBU LA SWALI HILI litakuwa tofauti kwa MAFUNDI WETU WASOMI NA WATU WENYE MAGARI YA KISASA ukilinganisha na mafundi wetu wa chini ya mwembe na wenye magari ya siku nyingi........

La kuongezea tu kuhusu ULAJI WA MAFUTA unapotoa SEMOSitati REJEA unapoendesha gari wakati wa usiku na mchana ......... JE MAFUTA YANALIKA SANA JOTO LIKIWA JUU ama JOTO LIKIWA CHINI?????
 
Gari zote zikiwaka zinawakia kwenye Open loop, baada ya joto zinaingia kwenye closed loop.

Gari yako isipoingia kwenye closed loop lazima uje ufungue uzi humu ndani kwamba gari yako imekuwa jini.
 
GARI Hizo labda zisiwe gari za kazi........ ziwe (hizo za kwenu) za PUSH TO START.......!
 
Back
Top Bottom