Muhimu: Zijue athari za kuondoa thermostat kwenye gari yako

duh afadhali kuna bwege mmoja nusu aniingize mkenge kisenge yan kuhusu iyo ishu ya kutoa thermostat..nikamwambia hii imekaa hapa kwa sababu walioweka sio wajinga

Ni vizuri ulifanya hivyo mkuu. Na hata ikitokea siku ikaleta shida basi funga tu nyingine ila usiitoe jumla.
 
Shukrani sana Mkuu yaani umeeleza vizuri sana....
dah mkuu ulichokisema ndicho kimenikuta, mwaka 2017 nilinunua noah sr40 showroom ikiwa vizuri sana but baada ya miezi minne ikawa inachemsha sana, nikampelekea fundi akasema kuchemsha kunasababishwa na thermostat so tuitoe, akaitoa gari ikawa vizuri kwa wiki tu ikaanza kuchemsha tena nikampelekea akaunga radiator fan ikawa inazunguka na engine wakati wote, ikapelekea gari kubadili behaviour ikawa inakula wese sana japokuwa tatizo limekwisha.

sasa mkuu naomba ushauri nini nifanye ili gari irudi kama zamani, kumbuka thermostat haipo na fan inazunguka muda wote
 
dah mkuu ulichokisema ndicho kimenikuta, mwaka 2017 nilinunua noah sr40 showroom ikiwa vizuri sana but baada ya miezi minne ikawa inachemsha sana,nikampelekea fundi akasema kuchemsha kunasababishwa na thermostat so tuitoe, akaitoa gari ikawa vizuri kwa wiki tu ikaanza kuchemsha tena nikampelekea akaunga radiator fan ikawa inazunguka na engine wakati wote, ikapelekea gari kubadili behaviour ikawa inakula wese sana japokuwa tatizo limekwisha.
sasa mkuu naomba ushauri nini nifanye ili gari irudi kama zamani, kumbuka thermostat haipo na fan inazunguka muda wote

1. Rudisha thermostat kwa maana thermostat ikiharibika inatakiwa kuwekwa nyingine na siyo kuondolewa.

2. Radiator fan pia irudishwe kama zamani ilipokuwa inawaka na kuzima.

Kama kutakuwa na tatizo basi hilo tatizo liangaliwe wakati hayo mawili yakiwa tayari yamesharekebishwa.
 
Asante mkuu nitafanya hayo ubarikiwe sana
 
Dah....umeniokoa mleta mada......gari yangu coolant kila baada ya wiki inaisha kuna fundi nikaongea nae akaniambia niende atoe hiyo thermostat....ndo nlikua najipanga niende....

Kazi ya thermostat ni kuhakikisha engine inafanya kazi katika joto linalotakiwa.

Sasa kwa akili ya kawaida kabisa thermostat haiwezi kuwa inapelekea maji kupungua kwenye rejeta. Na hivyo kuiondoa hakutaondoa hilo tatizo bali ni kuongeza matatizo mengine ambayo ni makubwa.

Angalia kama radiator fan zinazunguka na pia jaribuni kutafuta kama kuna sehemu kuna leak ambayo inapelekea maji kuvuja.
 
Mkuu kwema mimi nina kirikuu jamaa alitoa thermostat sasa toka niitoe gari inashake/ vibrate sana hasa wakati nataka kuiwasha wakati mwingine unawasha gari inawaka ila ina vibrate mpaka inazima tena
 
Thermostat Ni muhimu sana , inashauriwa hata Kama imefail , ibadilishwe sio kutolewa , kuna sababu pia kwa nini maji yapo pale Kama coolant na sio liquid nyingine

Tuchukulie mfano huu, chemsha maji kiasi Lita 2 yafike boiling point kabisa 100c mathalan maji ya kupika ugali kabla hujaweka unga, then chukua maji baridi , kikombe cha chai uweke kwenye hayo maji yaliyochemka , kitakachotokea yataacha kuchemka na kuanza upya kuitafuta boiling point ....
Mkuu kama wameshaitoa sasa naweza kupata nyingine mpya nikairudishia aina ya gari ni Suzuki Carry cabreta
 
Asante,
Naendelea kufuatilia,ngoja tusubiri na utetezi wa wale wanaomini kwanini thermostat inapaswa kutolewa
Gari ya mzee ilitolewa thermostat miaka 10 iliyopita ila mpaka leo ipo vizuri na haina tabia ya kuchemsha wala haijawahi kubadilishwa na huwa inaenda safari ndefu
 
Mkuu kwema mimi nina kirikuu jamaa alitoa thermostat sasa toka niitoe gari inashake/ vibrate sana hasa wakati nataka kuiwasha wakati mwingine unawasha gari inawaka ila ina vibrate mpaka inazima tena

Sometimes gari ikiwa inamiss huwa inavibrate...
 
Asante,
Naendelea kufuatilia,ngoja tusubiri na utetezi wa wale wanaomini kwanini thermostat inapaswa kutolewa
Gari ya mzee ilitolewa thermostat miaka 10 iliyopita ila mpaka leo ipo vizuri na haina tabia ya kuchemsha wala haijawahi kubadilishwa na huwa inaenda safari ndefu

Atakuwa ashaingiliwa sana kwenye mafuta bila kujua.
 
Kuna msururu wa mafundi wengi ambao wamekuwa wakiwashauri wamiliki wa magari au wao wenyewe kuondoa thermostat katika gari bila kujua umuhimu wa hicho kifaa hasa pale gari inapoanza kuoverhit. Kwanza kabisa Thermostat ina kazi mbili kubwa katika engine. Ambazo ni:-

1. Kuifanya engine iwarm up haraka hadi kufikia operating temperature ya engine kwa kublock flow ya maji kutoka kwenye radiator kwenda kwenye engine...
Tuna shida kubwa ya mafundi wa magari kiasi mm sio fundi but i wish to start my own Garage
 
Back
Top Bottom