Muhimbili (MOI): Sakata la Upasuaji Kichwa na Mguu.

jamani ni kweli yule mgonjwa amefariki nimesoma muda huu gazeti la habari leo kwenye mtandao
 
baada ya kuboronga kwa mara ya kwanza, busara ya kawaida tu ingetumika wangonjwa wale wangepelekwa kutibiwa kule wanakokwenda kutibiwa wakubwa na maswahiba wao. uchunguzi wa nani alikosea wapi ungeendelea hata kama wangonjwa wangekuwa wanatibiwa CHINA, kwani rekodi na mashahidi wapo bongo.

Sasa mgonjwa wa kichwa aliyepasuliwa goti amefariki baada ya kupasuliwa kichwa! Nasubiri yule wa mguu aliyepasuliwa kichwa (na sasa amekuwa boga) mara atakatwa kabisa mguu uliokua unamuuma. hakuna cha ajabu bongo.
 
Kuna Thread ilishatoka Jana kuhusu Kifo hiki na watu wameendelea kuchangia kule, kama inawezekana ziunganishwe
 
Niliiona hii post jana usiku, few hours before going to bed na huwezi amini NIMEIOTA! Ndo maana baada ya kuamka tu leo nimelazimika kukaa mbele ya PC yangu.
Nahisi uzembe uliosababisha mix up ya kwanza kutokea ni ubovu wa taratibu zilizopo MOI au kutofuatwa kwa taratibu hizo zilizopo. Mwanzoni mkasa huu ulipotokea nilishauri hapa kwamba victims watafute solicitor mzuri ili waweze kuclaim compensation kwa maumivu waliyoyapata na loss of earning kwa muda wote ambao wameshindwa kufanya kazi na kujiingizia kipato cha kutosha kujikimu wao pamoja na familia zao. But the poor lad(RIP) is dead now, what is next?
Marehemu ndo hivyo ameshafariki,nothing can be done to get him back- whether watu wanaresign au kufukuzwa,whether MOI inafungwa.Ningeshauri next of kin au beneficiaries wote watafute 1st class solicitor achukukuee hii kesi, hata kama hawana hela za kutosha najua wataalam wengi wa sheria wanajua kwamba its gonna be easy to win this one and its gonna be loads of money-they will be prepared to take it on NO WIN NO FEE BASIS.
I would really like to see MOI being hit really hard in their pockets kiasi ambacho watakaa chini na kuhakikisha kwamba kitu kama hiki hakitokei tena.
 
Jamani lini tutaamka watanzania, kumuombea huyu ndugu yetu "alale pema peponi milele amina" peke yake, kutasaidia kubadilisha hali hii muhimbili? Kwanini japo tusijadili nini kichukuliwe kuwaadhibu waliofanya huu ujinga? Members wenye know how ya udaktari wamesema wazi kuwa it is unthinkable for this kind of mistake to happen, japokuwa mistakes zinatokea. This is purely techinical/professional matter kwa nini tunabase kwenye upande wa Mungu milele amina?
Ni vema aanze Mwakyusa mwenyewe kuwajibika na aingie waziri mwingine ambaye kwanza afanye usafi, and then ndio tuanze kumuombea huyu ndugu yetu. Otherwise tutaendelea kuomba mungu tu until jesus comes back, na hiyo labda ni 5 bilion years to come
 
Inasikitisha sana maisha ya binadamu yanavyopukutika kwa uzembe. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi...ingekua nchi za wenzetu waziri husika na baadhi ya watu wangekiuzulu....ila kwa li nchi letuuuuuuuu...
swali langu ni moja tuuu na nilishawahi uliza tena..je ingekua hao wagonjwa ni waziri flani na waziri flani ndo wamefanyiwa hivyooo na waziri mmojawapo ndo kakata roho ingekuaje???maana naona kwa vile ni watz wa kawaida wenzetu na sie things r not taken seriously kabsaaa au kwa sababu muhi2 na other tanzanian hospitals sio za wakubwaaa?
 
Kitendo cha madaktari hawa kinaonyesha udhaifu uliopo katika fani za wataalam wetu ambao wanafanya kazi bora liende bila kuweka mbele taratibu na kanuni za fani zao. Tunaiombea roho ya marehemu amina.
 
Nasikitika kwanza kwa kumpoteza kijana mdogo na mwanafunzi wa secondary ambaye no one knew where his life would lead him to!! Nasema hivi kwa kuamini kabisa kwamba He who giveth life is the only one Who taketh!
Kujiuzulu kwa waziri or anyone wont make these things change maana madaktari wa MOI wanaonekana kabisa kwamba kuna Laxity that has grown in their mind kiasi kwamba hawawezi kuact professionally! Kwa kawaida taratibu za operation yoyote zinajulikana na zinatakiwa kufuatwa no matter how small the operation may seem!!! lakini this is not tha case for MOI just because we have a lot of specialist in Orthopediatrics there who think they can bypass the procedures!!!
Mimi naona specifically kwanza wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu na hata ikiwezekana wafungiwe kupractice for a period ili wajirekebishe. Alafu ndo turudi MOI tuwape adhabu kwa uzembe wa kufuatilia taratibu zao!!!
May the soul of our late young brother rest in peace!!!
GOD BLESS TANZANIA AND GOD BLESS JF MEMBERS!!
 
Mmmmhh!!!! ni habari za kustusha ila bado cjapata taarifa kamili kama jambo hilo limetokea. ila nilicho kisikia ni kwamba yule aliefanyiwa operesheni ya kichwa amepararaizi !! na familia yake italipwa na serikali

Naomba ufafanuzi hapa, kama huyu mgonjwa ameparalyze na hajafariki na kukiwa na suala la fidia, anaetakiwa kulipwa fidia ni mgonjwa mwenyewe au ni familia yake?

Zaidi natoa pole kwa familia ya marehemu.. hii habari inasikitisha na kupoteza imani tuliyokuwa nayo kwa madaktari wetu.
 
Yule aliyekosewa kwa kufanyiwa operesheni ya goti badala ya kichwa amefariki jana. Hii imetokea baada ya kufanyiwa ile operesheni yake ya kichwa iliyompeleka Muhimbili. Nasikitika sana. Nilihisi toka mwanzo kwamba hali hiyo ingetokea kwani yule aliyefanyiwa operesheni ya kichwa kilichokuwa hakina tatizo lolote aliishia ICU kwa siku kibao na hadi sasa hajiwezi japo keshatoka ICU. Sasa kama huyo aliyekuwa mzima kaharibiwa na operesheni, unategemea nini kwa yule mwenye ugonjwa kichwani? Mtu ambaye akipewa mtu mzima anamfanya mgonjwa, akipewa aliye mgonjwa atamuua, hakuna maelezo mengine. Akumulikaye mchana (ilhali hakuna giza), usiku atakuchoma (kwa moto). Ndicho kilichompata mtanzania mwenzetu. Kwa nini madaktari hao wasikubali tu kuwa kazi hiyo hawaiwezi kuliko kutuulia watu wetu hovyohovyo? Inasikitisha sana. Mungu amweke mahala pema peponi, amina.
 
Kwanza niwape pole wafiwa,E.Mgaya R.I.P
Binafsi nafikiri tukio hili tusilijadii tu kama uzembe wa madaktari,bali twende mbele zaidi na kujadii uzembe unashughulikiwa vipi hapa TANZANIA!Ajali ya MV.Bukoba,kuanguka kwa treni Dodoma,ajali za mabsi yaendayo mikoani ,Kuzama kwa kivuko cha ferry nk ni matukio yaliyosababishwa na uzembe.Lakini tujiulize hatua gani zilichukuliwa?ziliundwa tume,hela zikatumika ,matokeo yakawekwa kabatini,waliofanya uzembe wanadunda.....mimi ni daktari(siko muhimbili,lakini nilisoma pale nayaelewa mazingira ya MOI na idara za upasuaji kwa ujumla).kusimamisha madaktari wanne ni usanii mtupu,hadi mgonja kufika kwenye kitanda cha upasuaji watu zaidi ya watu sita wanakuwa wamehusika.kwa wastani sio chini ya watu sita walishiriki kwa kila operesheni,wako wapi manesi,bw/bi usingizi?vipi swala la rushwa mbona halitajwi?nilidokezwa kuwa mgonjwa wa mguu(E.Didas)alitoa rushwa ili apangwe kwenye listi ya Op....ndugu zake wankesi ya kujibu?

Kwangu mimi naona kuna mambo mengi ya kujadiliwa hapa
 
Dr Kizimkazimkuu,

Hebu tusaidie hapa. Hivi Muhimbili wanao uwezo wa kufanya hizo operesheni za kichwa na mgonjwa kubaki salama? Mbona wote ninaowafahamu waliofanyiwa operesheni hapo za kichwa walikufa ama kupata vilema vya maisha? Na mbona wanaofanyiwa operesheni hizo nje (ninaowafahamu, akiwemo mmoja niliyefanya naye kazi Chuo cha Ushirika, alifanyiwa nchini India) wanarudi salama na kuendelea na majukumu yao kama kawaida? Je unazo data zinazoonesha success rate za operesheni za kichwa hapo MOI? Maana musinganganie tu mambo ambayo hamuyawezi jamani mtatumaliza? Bora nife kwa ugonjwa wangu kuliko kuuawa jamani, inauma sana. Tafadhali nasubiri jibu.
 
Dr Kizimkazimkuu,

Hebu tusaidie hapa. Hivi Muhimbili wanao uwezo wa kufanya hizo operesheni za kichwa na mgonjwa kubaki salama? Mbona wote ninaowafahamu waliofanyiwa operesheni hapo za kichwa walikufa ama kupata vilema vya maisha? Na mbona wanaofanyiwa operesheni hizo nje (ninaowafahamu, akiwemo mmoja niliyefanya naye kazi Chuo cha Ushirika, alifanyiwa nchini India) wanarudi salama na kuendelea na majukumu yao kama kawaida? Je unazo data zinazoonesha success rate za operesheni za kichwa hapo MOI? Maana musinganganie tu mambo ambayo hamuyawezi jamani mtatumaliza? Bora nife kwa ugonjwa wangu kuliko kuuawa jamani, inauma sana. Tafadhali nasubiri jibu.

if wat ur sayin is true..basi kazi ipo Tz yetu
 
Mimi ni Daktari,lakini hili la Mgaya (apumzike kwa amani)limenisikitisha sana.Ni kweli hakuna daktari ambaye afanyi makosa,lakini kwa hili la Mgaya,hatua za kisheria lazima zichukuliwe, kwangu mimi huu ni uzembe na inaelekea MOI kuna kitu
 
Uwezo wa kufanya operation za kichwa wanao tatizo ni uangalifu wa wakati na baada ya operation,hapa ndio kuna tatizo (post operative care) ndio tatizo. Mimi pia ni mfano moja wa mama aliyefanyiwa operation ya kichwa Belgium, and she is doing fine. At MOI, there is something going on, there.
 
Mimi ni Daktari,lakini hili la Mgaya (apumzike kwa amani)limenisikitisha sana.Ni kweli hakuna daktari ambaye afanyi makosa,lakini kwa hili la Mgaya,hatua za kisheria lazima zichukuliwe, kwangu mimi huu ni uzembe na inaelekea MOI kuna kitu

MOI kuna fundamental problem ya Systems. Kudos kwa Prof Mwakyusa kwa ku-handle suala hili professionally. Lets not be judgmental basing on what you read in papers.
 
mgonjwa wako au wewe mwenyewe au mimi mwenyewe nikipona pale muhimbili uwa naesabu siku zako zilikuwa bado na mungu wako kakupigania kweli kweli,ukipeleka mgonjwa pale 99% ni mgonjwa kufa na si kupona pale ni jahanam ndogo hapafai hata kwa mafua
 
Ndugu zangu kweli mwenye macho haambiwi tazama,,ni kweli jamaa wamearibu labda ukweli wanaujua wenyewe kwanini walifanya ville,,nduguzanguni kuhusu kifo labda mimi sitki kuwa msemaji wa familia ila naweza kusema yalikuwa ni mapenzi ya mungu,,hali halisi nii hii
kaka yetu bahati mbaya amekufa namaumivu yasioitajika,,ndugu yetu kweli madaktari walijichanganya kwa hili,,baadaye wakamfanyia operesheni ya kichwa,,ndugu yetu alikutwa na kansa ya ubongo ambayo kwa kweli kupona ilikuwa majaliwa yamungu,,
kabla ya kufanyiwa operesheni madaktari walikataa kabisa
mpaka wawepo watu toka wizara ya afya na ruhusa toka kwa maseru na waziri wa afya,,pamoja na hayo waliitaji kuakikishiwa usalama wao baada ya kazi,,kabla ya kufanya w2alituita ndugu wakaeleza wazi wanamfanyia operesheni lakini uwezekano wa kupona mdogo ndipo walipokubali,,,,tuwahukumu kwa makosa yao lakini si kifo,,hayo yalikuwa mapenzi ya mungu,,mungu amweke mahali pema peponi

amen
pdidy
 
Tatizo lliopo pale moi profea mwakyusa analijua,,na hata hili linaonekana kama ni hali ya kumfanya huyu bwana maseru achukue zake mapema,,si siri ukiwa unauliza pale kisa hasa nini,,,watakwambia kuna watu wanapewa vyeo na bwana maseru pasipo kuangalia muda wa kufanya kazi pamoja na elimu ya mhusika,,
mwakyusa embu lifanyie kazi hili mkuu
 
Back
Top Bottom