Muhimbili (MOI): Sakata la Upasuaji Kichwa na Mguu.

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,910
Tanzania 'sorry' for surgery mix-up

Migraine sufferer Emmanuel Mgaya recovering from knee surgery
Tanzania's Health Minister David Mwakyusa has apologised for a recent surgical mix-up where a knee patient underwent a complex head operation.
On 8 November, surgeons at the country's main Muhimbili hospital opened the skull of Emmanuel Didas to remove a non-existent brain tumour.

While Emmanuel Mgaya, who had the tumour, underwent knee surgery.

Speaking to parliament Mr Mwakyusa said: "I would like to say sorry to the victims on behalf of the government."

The minister also said that a preliminary report was being published by the team that was set-up to investigate why the mix-up at Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) happened.

Mr Didas who had been admitted for a knee operation after a motorbike accident is still recovering from the ordeal - he ended up unconscious in intensive care after his head was wrongly operated on.

And chronic migraine sufferer Emmanuel Mgaya is likewise, still recovering from his unplanned knee surgery.

The blunder was blamed on both patients having the same first name.

But a hospital official, Juma Mkwawa said it was the worst scandal that had happened at Muhimbili hospital and that, "sharing a first name cannot be an excuse".

The two surgeons responsible have been suspended.

Baada kusoma kisa kizima nimebakia mdomo wazi. sikuyaamini niliyokuwa nasoma. Hivi kweli kuanzia Nurses, staff nurses, Drs na surgeons hakuna aliyebaini kuwa kichwa hakifananin na Goti. Je Madaktari wa Muhimbili wanapotaka kufanya procedure hawasoni documents? Au ni VIHIYO?? Mbaya zaidi nai majibu ya waziri wa Afya is unacceptable. Hivi mpaka leo hii Tanzania neno accountability halijulikani? Kama hali imefikia hapo je vipi kwa issues sensitive kama Blood transfusion I am sure maelfu wamepewa damu iliyo na virusi. Kama kichwa kinafafa na Goti je vipi damu zinazofanana rangi? kama kuna aliye na data please naomba exactly maana siamini what I read. Ama kweli ukishangaa ya ya Musa utaona ya......
 
Tatizo si la madaktari pekee. Tatizo ni mfumo mzima unahitaji kuangaliwa upya.
 
Dotori kasema kweli. Dhana ya kuwajibika Tanzania ni aina fulani ya mzaha kila mahala na katika kila fani. Hata humu ktk JF, ingekuwa watu wanawajibika kwa makosa yao naamini wengi wangeshajing'atua kama wanaJF!!! NANI ANAWAJIBIKA NCHI HII BWANA?
Msanii, kukubali ukweli na kung'ang'ania nafasi yako kwa kiburi na jeuri haisaidii!! Kubali ukweli UWAJIBIKE!
Swali kuu: nani atakayefufua dhana ya kuwajibika baada ya Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi kuanza kuonesha mfano kule Shinyanga zamani za kale??
 
Thanks for response guys. Ni kweli mfumo mzima hufanyi kazi. Lakini inakuwa jambo la hatari sana pale ambapo hata uhai wa watu unakuwa mshakani. Kama surgeon anaamua kufanya procedure kichwa badala ya Goti jamani inatisha. surgeon ni highly qualified proffessional. Lakini inaonesha dhahiri tulivyobobea kutojali. SERIOUSNESS HAIPO KABISA katika nyanja nyingi tu. Kila pahala. je ni mara ngapi ukiingia maofisini unakuta wapika chai wa bosi 4? Haiyumkini ndivyo ilivyo kila pahala watu hawajui JOB DECRIPTION wanapokuwwa kazini. na kama wamepewa orientation still ka mtindo ka kutojali kako palepale. Kwa hiyo inaashiria Tunahitaji viongozi design ya Charles Taylor na theory X. Sokoine aliheshimika simply because alitumia theory X kuwawajibisha watu. Ungekuwa ni wenzetu huku ughaibuni kuanzia waziri wa Afya na wale wote waliotia mikono yao katika jamaa hao wasingesubiri kuwaambiwa ondokeni. wangeanza na wale physical contacts Drs and Nurses sasa hivi wangekuwa KEKO wakisubiri kuonana na Pilato. Hata vyombo vya habari vya Tanzania sioni vikikemea wala kuonya jamii. vimekalia propaganda na habari za udaku. It is redicolous.
 
mhm labda madaktari wetu according to ufahamu wao kusema kweli kicha kikawa sawa au kimefanana na goti...kuanzia position,size na kila kituuu...there r so many things i hospitali zetu ila angalia kesi itavyomalizwa kichini chinii na kufukiwa kimyaaaaa!!
just immagine ndo ingekua waziri flani kapasuliwa kichwa badala ya mguu...keleeuwiiiiii nadhani madaktari wooote hata manesi wafukuzwa kazii hadi wafagizi!
ila the problem is sio waziri wala member wa family zao watafanyiwa major upasuaji pale waooo wakipata mafua...wanakwea pipa kwenda europe for checkups hata kwa watu wanaojua afya zao hazifai tena for checkups..wala kubadilisha............
 
ulaya wanafuata flujab siku hizi,hiyo ni kinga ya mafua ukipata hiyo wewena mafua kwa mwaka ndio kwaheri
 
Kama Hospitali zinaoza kiasi hicho hata Hospitali ya Rufaa basi kuanzaia Zahanati na vituo vya Afya usiseme. Si unaona ajali ya kapuya aliruka mwenzie mwenyekiti wa wilaya akabaki mwisho chairman akatangulia mbele ya haki.
 
Posted Date::11/22/2007
Tiba MOI:Aliyepasuliwa mguu badala ya kichwa, afariki
Jackson Odoyo na Andrew Msechu
Mwananchi

EMMANUEL Mgaya (19), aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa Jumatatu wiki hii baada awali kufanyiwa wa mguu kimakosa, katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), amefariki dunia jana asubuhi.

Mara baada ya Mgaya kufanyiwa upasuaji wa kichwa, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya kisha kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), hadi mauti yalipomfika jana saa 2:30 asubuhi.

Awali Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa na Emmanuel Didas ya kichwa badala ya mguu, Novemba mosi mwaka huu katika taasisi hiyo.

Akizunguza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu muda mfupi baada ya Mgaya kufariki dunia, mmoja wa wauguzi wa MOI, alisema hali ya mgonjwa huyo, ilianza kuwa mbaya juzi mchana.

Alisema jana asubuhi mapema alipofika kazini, alimkuta akipumua kwa shida, hali iliyoonyesha alikuwa amezidiwa.

Aliongeza kuwa, baadaye madaktari wanaomuhudumia waliwasili katika chumba hicho na kugungua hali yake ilikuwa ni mbaya zaidi.

Hali ya mgonjwa huyo ilianza kuwa mbaya tangu jana (Juzi)mchana na niliporudi kazini leo (jana)alfajiri nilikuta hali yake imebadilika kiasi cha kunipa wasiwasi, lakini madaktari walifika muda mfupi badaye na kumpa huduma za haraka japo hazikuweza kumsaidia, ? alisema muuguzi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini kwa kuwa si msemaji.

Kwa mujibu wa chanzo, jitihada za kuokoa maisha ya Mgaya zilishindika majira ya saa 2:30 mgonjwa huyo alifariki dunia.

Hata baadhi ya madaktari waliozungumza na Mwananchi walithibitisha kwamba Mgaya amefariki dunia.

Kifo cha Mgaya kimetushutua sana kwa sababu tangu alipofanyiwa upasuaji wa mara ya kwanza kila daktari wa taasisi hii alijaaribu kumsaidia kwa karibu, alisema daktari huyo.

Waliongeza kwamba hata Mkurugenzi Mkuu wa MOI, Profesa Laurent Museru, amesikitishwa sana na kifo hicho na kulazimika kuitisha kikao cha dharura kujadili namna ya kufikisha taarifa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kwa ndugu wa marehemu huyo.

Akizungumza na Mwananchi, Profesa Museru amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mgaya.

Ni kweli Mgaya alifariki dunia leo (jana) asubuhi na tumeshawajulisha ndugu zake pamoja kutoa taarifa wizarani, pia mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti,alisema Profesa Museru.

Alisema kwamba utaratibu wa maziko yake, utafahamika baada ya kuwasiliana na ndugu zake. Mgaya ni mwenyeji wa Mkoa wa Iringa.

Habari za kifo cha Mgaya, si tu zimewashtusha wafanyakazi wa MOI, pia Waziri wa Afya, kimesema chanzo chetu cha habari.

Mgaya alifikishwa katika taasisi hiyo, Oktoba 28, mwaka huu akitokea mkoani Iringa na kufanyiwa uchunguzi wa kina kuhusu matatizo yake na madaktari kushauri afanyiwe upasuaji wa kichwa.

Mwanzoni mwa mwezi huu, badala ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa, alifanyiwa upasuaji wa mguu, huku Didas akifanyiwa wa kichwa badala ya mguu.

Kwa sasa Didas amelazwa ICU katika taasisi hiyo huku kukiwa na habari kwamba amepoza upande wa kulia wa mwili.

Tokea Didas amefanyiwa upasuaji huo tata, hajaamka, wala hajaongea na kadri siku zinavyokwenda hali yake, inazidi kuwa mbaya.

Baada ya tukio hilo, Prof Museru aliamriwa na Bodi ya MOI, kuunda tume ya kuchunguza upasuaji huo na kutekeleza hilo, Novemba 2 mwaka huu.

Tume ilikamilisha kazi yake Novemba 13, na kuikabidhi Bod Novemba 15, na Bodi kuipeleka kwa Waziri Novemba 16.

Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyusa ameahidi kutoa taarifa ya Tume hiyo iliyoundwa kuchunguza sakata la upasuaji huo.

Taarifa iliyopatikana jana kutoka katika wizara yake, ilifahamisha kuwa, Profesa Mwakyusa anatarajiwa kutoa taarifa hiyo leo saa 4.00 wizarani hapo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa vya upimaji kwa ajili ya wagonjwa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) jijini Dar es Salaam jana, Mwakyusa aliahidi kutoa taarifa hiyo leo, baada ya kumalizia maandalizi ya mwisho.

Naombeni munivumilie kwa leo, ninamalizia utaratibu wa kuitoa, ila nitaitoa kesho , siewezi kuzungumza lolote leo kwa kuwa ninaweza kuzungumza nusu nusu, nivumilieni kama mlivyonivumilia tangu nilipowaomba kufanya hivyo nilivyokuwa Bungeni Dodoma, Waziri huyo aliwaambia wanahabari waliotaka kujua hatma ya taarifa hiyo.

Alisisitiza kuwa, subira ni suala la msingi, hivyo wanachi hawana budi kusubiri kwa muda ili waweze kupata taarifa iliyokamilika.

Awali Prof Mwakyusa, alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari, akisema taarifa hiyo angeitoa juzi, lakini kwa sababu zisizojulikana, alishindwa kufanya hivyo.
 
Very sad.

Nadiriki kusema kwamba hii haiwezi kuwa kazi ya Mungu. hiki ni kifo kilichotokana na Uzembe wa Madaktari wetu.

Mungu aiweke roho ya Emannuel Mgaya mahali pema peponi Amina
 
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho Yake Pahali Pema Peponi.

Hii habari inatia uchungu kweli. Nawapa pole ndugu, jamaa na marafiki wote.

SteveD.
 
Nawapa pole Familia ya marehemu.
Mwakyusa angejiuzulu ili kuonyesha kuwa anajali na anawajibika na makosa ya watendaji wake.
Mungu ailaze roho ya merhemu mahali pema.
Amina
 
Mwenye enzi mungu amrehemu marehemu huyu!! Pole mingi kwa familia.
 
Kwa Familia...Mko kwenye maombi yangu na marehemu RIP
Nafikiri Waendesha mashitaka wawe tayari! Hii ni murder! Hivi wakati wote huo nilifikiri wangeweza kurakabisha hiyo! Si alikuwa kama kwenye emergency surgery? Kulikoni?
 
inatia uchungu kupita kiasi. Unaweza kujiuliza maswali mengi bila majibu. Mungu airehemu roho ya Emanuel na awatie wanafamilia nguvu.
 
Jamani ndugu zangu watanzania muda mfupi liopita nimesikia tetesi kwamba mgonjwa mmoja kati ya wale waliofanyiwa operation vise versa pale muhimbili MEFARIKI DUNIA.

Je kuna mtu yoyote anazo habari hizi atupashe ni yupi kati ya wale.
 
Ni kweli kuna Taarifa kwamba Mgonjwa Emmanuel Mgaya aliyefanyiwa Operation ya kichwa Jumamtatu AMEFARIKI DUNIA.Ikumbukwe kwamba mgonjwa huyu mara ya kwanza alifanyiwa operation ya Goti,wakati tatizo lilikuwa kichwa.Tafuta muda habari ipo kwenye Gazeti la Tanzania Daima.
 
Mmmmhh!!!! ni habari za kustusha ila bado cjapata taarifa kamili kama jambo hilo limetokea. ila nilicho kisikia ni kwamba yule aliefanyiwa operesheni ya kichwa amepararaizi !! na familia yake italipwa na serikali
 
jamani poleni mgonjwa. uzembe huu mpaka lini. ninawaambieni vifo vingi hasa hasa mikoani vinatokana na uzembe. mgonjwa anaumwa maralia ila mtoto anaandikiwa dozi ya kuhara.......tutaisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom