Muhimbili (MOI): Sakata la Upasuaji Kichwa na Mguu.

Kafara, point nzuri sana hiyo. Inaonekana ni kuwa kilichotokea ni kama kuporomoka kwa dominoes... kuna ndiye aliyesababisha kwa uzembe, kutokuwa mwangalifu au pure idiocy majina kuchanganywa... na hata alipogundua labda alitumaini "mtu mwingine" atasahihisha; which reminds me of that 200,000 check that JK received...
 
Tusiwalaumu sana madaktari na manesi wakati wao hawakuwekewa mfumo mzima wa kubadilishana wagonjwa. Tangu wanafanya practical/word rounds wamezoea kuona nesi anauliza eeeeh musa ni nani, ukisema ni mimi basi unapewa vidonge vyako vya flagyl unameza. Sasa wakati wote huu waliounda huu mfumo na supervisor pamoja na management team hawakuweza kubaini risks zinazoweza tokea kutokana na mfumo uliopo. Since everything went well na kila mtu alijua anafanya kazi yake hapa hatyuwezi kumblame nurse au daktari.
Niliwahi kufanyiwa upasuaji Muhumbili na tulikuwa wagonjwa kama watano tunasubiri kuingia theater na yule nurse wa theater alikuwa amekaa kwenye dawati kwenye kona na sisi tupo kwenye tuvitanda vyetu huku mikononi tuna drips tukisubiri upasuaji. Yule nurse alikuwa na mafaili yetu na alikuwa akiita kama darasani eeeeh kinyau(***********) ni nani kati yenu halafu unanyoosha kidole au kuitika ni mimi then unakuwa wheeled till theater
(niliingiwa ana hofu maana kuna wagonjwa wawili walifanana first name) na aliyewahi kuitika kumbe si yeye mwenye faili,ikabidi nurse aanze kupekua faili kuangalia Xrays. Hii ni simple scenario kwamba sisi hatujali risks zinazoweza kutokea kwenye medical systems. Dawa ni kuziba minya yote ya error kutokea. Ila kusema 100% kutakuwa error free hapana.
 
Nyani, exactly.. tatizo lililoonekana Muhimbili ni kukosa mechanism ya kusimamia mgonjwa toka anapoingia hadi anapofanyiwa upasuaji. Kwa mfano, badala ya kutumia majina namna hiyo, wangetumia namba na hizo namba siyo tu ziko kwenye kitanda bali pia mkononi kwa mgonjwa mwenyewe na kabla hajafanyiwa upasuaji daktari wake lazima ahakikishe ndiye mgonjwa mwenyewe. Haya ya kuingia wodini na nesi kuuliza tu "Immanuel ni nani".. inakuwa kasheshe. Ndio maana reaction yangu ya kwanza kabisa niliposikia habari hii nilisema; it is not as worse as we have seen in more developed countries. Ndiyo maana utaona hapa ni rahisi zaidi kuchanganya viungo kuliko mtu mwenyewe...

Mkuu Mzee Mwanakijiji,
Naungana na wewe moja kwa moja au 100% na ninaongezea kwamba kwakuwa wengine hawana mikono yako basi katika kadi zao wabandike picha zao kabisa ili faili la mgonjwa lijulikane pia kwa picha ya mgonjwa husika.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji,
Naungana na wewe moja kwa moja au 100% na ninaongezea kwamba kwakuwa wengine hawana mikono yako basi katika kadi zao wabandike picha zao kabisa ili faili la mgonjwa lijulikane pia kwa picha ya mgonjwa husika.

bubu na je wakifanana sura au bahati mbaya wote ni victims wa accident mbaya zinazohusisha sura? how will photo identification help?
 
bubu na je wakifanana sura au bahati mbaya wote ni victims wa accident mbaya zinazohusisha sura? how will photo identification help?

1. Wanaoweza kufanana sana ni mapacha nao ni rahisi sana kutambuliwa kwa picha zao.
2. Victims wa ajali mbaya zinazohusisha sura lazima kiwango cha kuumia kitatofautiana kwa kiasi fulani huwezi kuumia mkafanana kama mapacha wa vidonda mwingine ataumia paji la uso na mwingine akaumia kuanzia paji la uso hadi kidevuni wote huo ni uso.
SWALI KWAKO: Unataka kuniambia kwamba ndugu yako amepata ajali kaumia usoni huwezi kutambua kwa kuwa wengi wameumia nyuso zao? Au unataka malumbano kujaza thread?
 
Kwenda abroad kutibiwa kinachogomba ni mfwenge ndugu yangu. Cha muhimu kabla ya kupigwa nusu kaputi kama bado unajitambua inabidi uulize maswali kibao,,, je, ni operation gani nafanyiwa,,, etc. kuhakikisha hawajakuchanganya na mgonjwa mwingine.
 
bubu nop sitaki kujaza threads nataka tuwe realistic. Picha hata siku moja haiwezi kuwa source za identification. Ndugu yangu akiumia sura sitashindwa kumtambua kwa kuwa ni ndugu yangu.
Benki wenyewe huwa wanachemka kwa kutumia photo ID. Mi nishawahi kunchukulia ndugu yangu pesa kwa kitambulisho chenye picha and in reality hatufanani hata chembe.
Njia pekee ni kuwa na unique identification number ambayo kamwe haiwezi kujirudia hata aje mgonjwa ten years later. hiyo no iwe ktk file, mkononi na ktk kitanda.
pili kama alivyosema ndugu nesindiso kuwa huwa kuna general questions kati ya operating staff na mgonjwa like jina lako, umri, kazi halafu daktari anakueleza in brief kuwa tutafanya hihi na hiki na mwishoni ndio unapewa dawa ya usingizi. Vyote hivi vikiwa taken into account basi chances za error zitakuwa minimal.
 
Poleni Sana Ndugu zangu. jambo la kuhuzunisha kweli...

Pengine tungewasaidia hao Emanuels hapa kenya,

Tafadhali mlete Emmanuel Didas hapa....URGENTLY atibiwe..

http://www.karenhospital.org/
http://www.nairobihospital.org/default.asp
http://www.agakhanhospitals.org/nairobi/index.asp


Tanzanian surgery mix-up man dies




DAR ES SALAAM, Monday

A Tanzanian man who had a knee operation when he had a tumour in his brain, has died after finally having the operation he required.

Mr Emmanuel Mgaya, 19, died hours after the surgery, performed two weeks late.

Meanwhile, Mr Emmanuel Didas, 20, who had brain surgery although his complaint was in the knee, is slowly recovering but he remains partially paralysed.

The government has apologised for the mix-up, which has been blamed on both men having the same first name.

Mr Didas cannot move his right side following the unnecessary operation.

He said in hospital that he was able to eat his favourite food again – maize meal with fish and vegetables.

Health Minister David Mwakyusa said a commission has been set up to investigate the saga and pledged to send Mr Didas to India for specialised treatment.

He originally hurt his leg in a motorbike accident.



Mr Mgaya was also due to have treatment in India but died before this was possible.

He spent four days at the Muhimbili hospital’s intensive care unit in Dar es Salaam but his condition got worse on Thursday.

He was operated on but died several hours later. His family say they are not planning to sue the government – they always knew he only had a 50 per cent chance of survival, as the tumour had grown so large. He first sought medical treatment, complaining of migraines.

But they have urged the health ministry to employ qualified and compassionate medical staff.

Agencies

How low can Tanzanian wellknown ineptness sink?? I wonder...

Next they will be electing a Kenyan to their State House or something like that....si nilisikia wakisema eti Mkapa is a Kenyan...ehhh wacha tu
 
Hivi bado madakatari wauaji wanapeta mtaani? Maana sina taarifa za wao kukamatwa kwa mauaji au police wanafanya uchunguzi wa DNA ili kuestablish clinical evidence. TUME IUNDWE lakini mei nalia na waliohusika wapi sheria? waswekwe lupango kwanza then tujue mchawi alikuwa nani. mtu kafa still tume???? NO NO.
 
And it is this that makes the Muhimbili case disturbingly and foolishly unique! Mgonjwa wa kichwa anachanganywa na mgonjwa wa mguu! It is indefensible!

Hapo sijui kinachokushangaza ni mgonjwa wa kichwa na miguu kutibiwa kitengo kimoja? Mgawanyo katika taaluma za madaktari ndivyo ulivyo. Wale madaktari wa mifupa na kichwa wako kundi moja. Kwa hiyo yawezekana theatre iliyokuwa inatumika ni hiyohiyo, chumba kimoja au tofauti lakini ya idara hiyo. Na ninavyofahamu, madaktari wa kichwa wanafanya pia operesheni hizo za mifupa ikiwemo ya miguu.

Baada ya kupitia mengi yaliyosemwa na kuandikwa kuhusu tukio hili, nakubaliana na waliochangia kwenye threads nyingine kwamba kumbe tatizo hili liko kwenye mfumo wa hospitali na si kwa daktari mmoja. Wametaja kitu walichoita "standard operating procedures" au SOPs, ambazo kimsingi zinapaswa kuwa za taasisi, na kwamba ikitokea flaw katika hizi, mahali popote kwenye mlolongo (chain) wa mfumo huo, basi madhara makubwa kama hayo au zaidi hutokea. Nafasi ya mwisho ya kukwepa mistaken identity hizi ingekuwa ni kuzihakiki kabla mgonjwa hajapewa nusu kaputi, maana baada ya hapo hawezi kuzungumza tena, hana fahamu. Na anayehusika katika hatua hii si daktari mpasuaji, kwani mpasuaji wakati anajiandaa (kunawa na kuvaa mavazi maalum)ndipo na mgonjwa anapewa nusu kaputi. Mpasuaji akirudi anakuta mgonjwa amefunikwa (wenyewe wanaita "draping"), imeachwa wazi ile sehemu inayopaswa kupasuliwa tu. Hapa nadhani si sawa kumlaumu daktari mpasuaji.

Hata yule mtoaji wa nusu kaputi anapata taarifa kutoka kwa mwingine, ambaye pia anapata kutoka kwa mwingine etc, yaani it is a chain. What went wrong where? Hilo nadhani ndilo la kufanyia uchunguzi ili hali hiyo isitokee tena.
 
Mwanakijiji: Mimi ni mwalimu, hata kwenye kusahihisha mitihani tu ambalo sio jambo linalohatarisha maisha, hatufanya uzembe na ujinga kwa kiwango hicho. Siwezi ku-pick karatasi ya mwanafunzi na kujaza maksi kwenye black na red sheet bila kuangalia exam number, reg no., degree programme na mwaka anaosoma. Vinginevyo, watu wengi sana wangekuwa wanapata marks zisizo zao. Vivyo hivyo, siwezi kumsamehe daktari na nesi aliyesomea kazi yake miaka nenda rudi kufanya kosa kubwa kama hilo eti alichanganya majina. Patient and medical records is a whole course in medicine, na ninajua hawa wote wanajua sana mambo haya. hapa kilichofanyika ni gross negligence and they must take responsibility to send a strong message to others and especiially to the incoming generation of doctors and nurses. For sure, the mistake they did is only punishable rather inexcusable.

Kitila hapa umetudanganya bwana. Zipo kesi nyingi tu za watu waliopewa maksi zisizo zao tena university, kilichowasaidia tu ni kwamba wenyewe walikuwa wanatunza record zao za CA. Na kwa kuwa waliolalamika ni wale tu waliowekewa maksi ndogo kuliko zile halisi, basi inawezekana matukio haya ni mengi zaidi. Tukio moja ninalokumbuka ni mwanafunzi mmoja ambaye baada ya kuambiwa amefeli alifanya mbinu za "kimafia" akapata nakala ya waraka unaoonesha maksi walizopata wanafunzi wote wa kozi hiyo ikijumuisha CA na final grades. Akagundua maksi zilizojazwa kwenye ile column ya CA kwenye jina lake si sahihi, kwani alikuwa ameweka rekodi. Akakurupuka kuandika barua ya appeal, na kuambatanisha photocopy ya ule waraka ambao ulikuwa unadaiwa ni "confidential". Kesi ilikuwa kubwa sana,ingawa mwishoni alirudishiwa maksi zake, walimfungulia kesi mpya wakimtaka aseme alipataje waraka ule. Ukaanza mchezo mpya wa kutupiana mpira na kutafuta mchawi juu ya watu wanaotoa "siri" za idara kwa "wasiohusika".

Kwa hiyo ndugu Kitila, sitetei makosa, lakini tunapaswa kukubali kwamba makosa hutokea, na njia bora ya kushughulikia makosa hayo ni kuweka mazingira ya kuyazuia yasitokee, au kupunguza as much as possible uwezekano wa makosa kama hayo kutokea. Na nimekuthibitishia, na nina uhakika kuna wengine wenye mifano zaidi, kwamba Chuo Kikuu cha DSM makosa ya kuchanganya maksi za wanafunzi hufanywa sana, sana tu. Labda kama wewe unafundisha chuo kingine ambacho utendaji wake ni "error-free" (kama si kujipigia "debe").
 
Jamani kuna update kuhusu ripoti ya tume ambayo ilifanya uchunguzi wa tatizo la MOI? Maana tume ilishakabidhi ripoti kwa Wizara ya Afya kitambo.
 
Angalao hii tume ya pili naona imekuwa makini, majibu yake yako comprehensive. Hii ripoti hapa chini nimenakili kutoka gazeti la Majira la leo:

Ripoti ya upasuaji tata MOI yabaini:Uzembe ulitawala

*Aliyekagua mgonjwa usiku siye aliyempasua
*Mgaya ajieleza kuwa si Didas hakusikilizwa
*Jopo lilishaagiza arudi nyumbani lakini...
*Madaktari na wauguzi 12 sasa kushitakiwa

Na Reuben Kagaruki


TUME iliyoundwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kuchunguza upasuaji tata katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imebaini kuwapo usimamizi dhaifu katika baadhi ya vitengo vya taasisi hiyo.

Udhaifu huo ulidhihirika katika idara ya upasuaji mifupa, upasuaji mishipa ya fahamu, utoaji dawa za usingizi, vyumba vya upasuaji na uuguzi.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, wakati akisoma ripoti ya Tume iliyoundwa kuchunguza upasuaji tata wa Emmanuel Didas (20) aliyetakiwa kupasuliwa mguu, lakini akapasuliwa kichwa na marehemu Emmanuel Mgaya (19) aliyetakiwa kupasuliwa kichwa, lakini akafanyiwa upasuaji wa mguu.

Ripoti hiyo pia ilibainisha kutokuwapo kwa umakini wa kuwatambua wagonjwa wanapoingizwa chumba cha upasuaji.

Alisema matokeo ya taarifa ya Tume yaligawanywa katika maeneo matatu ya utawala, mfumo wa uendeshaji na utaalamu

Profesa Mwakyusa alisema wodini kabla ya upasuaji kumekuwapo kutofuatwa kwa makini taratibu za msingi katika kushughulikia wagonjwa, udhaifu ambao ulijitokeza wakati wa kuwaanda Bw. Didas na marehemu Mgaya.

Katika eneo la ukaguzi kabla ya kupata dawa za usingizi, Profesa Mwakyusa alisema mgonjwa anayetarajia kufanyiwa upasuaji, hufanyiwa ukaguzi na ofisa muuguzi mtaalamu wa dawa za usingizi usiku kabla ya upasuaji ili kuona kama atahimili au kuhitaji dawa gani ya usingizi, lakini haikufanyika hivyo kwa Bw. Mgaya.

Katika sakata la Mgaya, Profesa Mwakyusa alisema tume ilibaini kuwa ofisa aliyemkagua mgonjwa usiku si aliyetoa dawa ya usingizi wakati wa upasuaji.

"Hii ilichangia udhaifu unaolezwa hapa kwa upande wa idara ya dawa za usingizi, ofisa huyo angekuwapo katika chumba cha upasuaji, angesaidia kumtambua mgonjwa," alisema.

Alisema orodha ya wagonjwa waliotarajia kupasuliwa iliandaliwa na daktari wa ngazi ya chini wodini, bila kuthibitishwa na Daktari Mfawidhi wa Kitengo.

Alisema hali hiyo haikuzingatia utaratibu uliopo na kusababisha Bw. Didas kuingizwa kwenye orodha licha ya maagizo ya jopo la madaktari, kuruhusu aende nyumbani bila kufanyiwa upasuaji hadi baada ya wiki sita.

Aliongeza kuwa udhaifu wa wodi A pia ulijitokeza kwa kutofanya raundi kati ya Oktoba 26 hadi 30, mwaka huu.

"Kama wangelifanya raundi inavyotakiwa, wangegundua kuwa Bw. Didas hakupaswa kufanyiwa upasuaji na angeruhusiwa kwenda nyumbani kama jopo la madaktari lilivyokuwa limeamua hapo awali," alisema Profesa Mwakyusa.

Aliongeza kuwa kabla ya mgonjwa kupelekwa kwenye chumba cha upasuaji, ni lazima daktari ajadiliane naye na inapobidi hata ndugu wa mgonjwa hushirikishwa ili kutoa idhini.

"Lakini katika sakata la Didas utaratibu huo haukufuatwa na kuleta udhaifu unaotajwa kwa upande wa upasuaji na uuguzi," alisema na kuongeza kuwa Mkuu wa Idara hakuiona orodha ya upasuaji.

Profesa Mwakyusa alisema muuguzi wa wodi iliyohusika alipaswa kutomwandaa Didas kwa upasuaji, kwani jopo la madaktari lilishaamua aruhusiwe kwenda nyumbani na kurejea baada ya wiki sita.

Alisema licha ya maagizo hayo, muuguzi huyo aliruhusu maandalizi ya upasuaji yaendelee na hatimaye Didas aingizwe kwenye orodha ya upasuaji bila kuwapo agizo la Mkuu wa Idara.

Chumba cha upasuaji

Profesa Mwakyusa alisema Tume ilibaini kuwa katika chumba cha upasuaji hakuna umakini katika kuwatambua wagonjwa wanapoingizwa katika chumba hicho. Mbali na hilo alisema Ofisa Muuguzi Mfawidhi wa chumba cha upasuaji aliruhusu daktari kumpasua mgonjwa (Didas) ambaye hakuwa wake.

"Hakukuwa na ushahidi wa kuwapo na mabadiliko ya daktari, kinyume na taratibu," alisema Profesa Mwakyusa.

Alisema katika hali ya kawaida, muuguzi anapaswa kulinda usalama wa mgonjwa na utaratibu mzima na pale inapobidi kubadili daktari, mpasuaji hutakiwa kupata kibali maalumu kutoka kwa daktari bingwa na mkuu wa kitengo, lakini kwa sakata la Didas hilo halikufanyika.

Profesa Mwakyusa alisema katika chumba cha upasuaji waliokuwapo madaktari wa ngazi za chini na maofisa wanaotoa dawa za usingizi. Alisema wote hao walikuwapo wakati uamuzi wa kuahirisha upasuaji wa goti la Bw. Didas ukifanyika.

"Kwa kuwa walipaswa kumtambua mgonjwa huyu (Didas) hawakufanya hivyo na kuacha daktari kumpasua mgonjwa tofauti," alisema Profesa Mwakyusa.

Profesa Mwakyusa alisema sehemu ya dawa za usingizi ni eneo linalohitaji umakini katika kutambua wagonjwa kabla ya kuwapeleka katika vyumba vya upasuaji. Alisema taarifa zinaonesha kuwa wataalamu wa dawa za usingizi walikuwapo, lakini utambuzi ulikuwa dhaifu kwa kutumia jina moja la Emmanuel.

Mbali na hilo alisema muuguzi, mtoa dawa za usingizi na madaktari wa ngazi ya chini kwenye upasuaji walikuwa na jukumu la kutambua wagonjwa, lakini hawakufanya hivyo na kumwacha Daktari Bingwa kuendelea na upasuaji kwa mgonjwa tofauti.

Baada ya upasuaji

Alisema mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa mguu kwa makosa, Bw. Mgaya baada ya kurejeshwa wodini, alitoa taarifa kwa ofisa muuguzi wodini kuwa yeye si Didas bali ni Mgaya.

Profesa Mwakyusa alisema ingawa alirudia kusema hivyo zaidi ya mara mbili, muuguzi wa wodi hiyo hakumsikiliza, akidai mgonjwa amechanganyikiwa kwa sababu ya dawa za usingizi.

Alisema muuguzi wakati wote wajibu wake ni kumsikiliza mgonjwa hata kama akili zake si timamu au ana lalamiko dogo. Alisema muuguzi huyo kama angemsikiliza mgonjwa huyo, angeweza kuokoa upasuaji wa makosa wa kichwa uliofanyiwa Bw. Didas zaidi ya saa mbili baadaye.

Profesa Mwakyusa alisema Tume yake ilibaini kuwa wataalamu waliowashughulikia wagonjwa hao hawakufanya kazi zao kwa umakini, hali ambayo ilichangiwa na uhusiano duni kati ya mgonjwa na daktari/muuguzi.

Udhaifu huo ndio uliosababisha kuwachanganya wagonjwa hao, kwani ugonjwa haukuhusishwa na mgonjwa mwenyewe bali waliridhika kwa kuangalia majibu ya vipimo. Aliongeza kuwa kuna udhaifu katika kusimamia taratibu zilizopo zinazohusiana na upasuaji na huduma kwa wagonjwa kwa ujumla.

Alipoulizwa kama Serikali ipo tayari kutoa fidia kwa wagonjwa kwa wahusika, Profesa Mwakyusya alisema suala hilo lipo kwenye haki za mteja. Alisema mteja kama anaona hakutendewa haki, kuna njia za kufuatilia suala hilo na kuwa anayehusika na kulipa fidia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Alipoulizwa kama atajiuzulu kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakishauri, alisema Rais Jakaya Kikwete hakumchagua kushika wadhifa huo kwa shinikizo la watu, hivyo hawezi kujiuzulu kwa kushinikizwa.

Alisema hata pale alipoapishwa kushika wadhifa huo, hakuna alipoahidi kufuata nyayo za Ali Hassan Mwinyi wala Mzee Peter Kisumo. "Bosi wangu (Rais) akisema haridhiki, basi nitaondoka," alisema Profesa Mwakyusa.

Profesa Mwakyusa alipoulizwa kuhusu hali ya Bw. Didas anayetibiwa India inaendeleaje, alisema ameanza kuwa na kumbukumbu na anaeleza jinsi alivyopata ajali, anaweza kukaa na anazungumza. Aliongeza kuwa madaktari pia wameisharekebisha matatizo yaliyokuwa kwenye goti lake.

Hatua

Profesa Mwakyusa alisema tume zote mbili zilizofanya kazi zimeiagiza Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya MOI na menejimenti kuwachukulia hatua kali za kidhamu wafanyakazi wote 12 waliozembea katika kuwahudumia wagonjwa hao na iendelee kuchukua hatua kwa wengine watakaozembea baada ya tukio.

Pia Bodi imeagizwa isimamie menejimenti kulifikisha mara moja kwenye Baraza la Madaktari suala la madaktari wanne waliosimamishwa kazi kutokana na taarifa za Tume ya kwanza na wengine wanne ambao Tume aliyoundwa imewakuta wana masuala ya kujibu na hao ni wasaidizi wa madaktari bingwa na wa dawa za usingizi.

Pia menejimenti hiyo imeagizwa iwafikishe Baraza la Wauguzi na Wakunga, wauguzi wanne ambao hawakuwa makini katika kutekeleza majukumu yao kwenye kwa hatua hizo hizo.

Mabaraza hayo yana nguvu kisheria na pindi yakiwatia hatiani sehemu pekee ambayo wanaweza kukata rufaa ni Mahakama Kuu. Aliagiza Bodi kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa ndani ya wiki mbili na kumpatia taarifa.

Bw. Mgaya alilazwa MOI Oktoba 25 mwaka huu na baada ya kufanyiwa uchunguzi, jopo la madaktari liliona ana tatizo la uvimbe na kuamua afanyiwe upasuaji wa kichwa. Badala ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa Novemba mosi mwaka huu akafanyiwa upasuaji wa goti.

Bw. Didas alilazwa hospitalini hapo Oktoba 26 mwaka huu kutokana na ajali iliyomsababishia maumivu katika goti
Source: Majira
 
Habari zaidi kama ilivyo ripotiwa na Mwananchi...

Hatimaye Tume yagundua madudu MOI


*Yasema mfumo mzima wa taasisi hiyo ni mbovu
*Madaktari, wauguzi kufikishwa kwenye mabaraza

*Marehemu Mgaya alimweleza Muuguzi asipasuliwe mguu

*Muuguzi alimjibu kuwa amezidiwa na dawa ya usingizi

*Akafanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa


Waandishi Wetu


MADAKTARI bingwa wawili wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) watafikishwa katika ya Baraza la Madaktari kutokana na udhaifu katika usimamizi wa kazi zao na kusababisha upasuaji tata wa wagonjwa wawili uliofanyika katika taasisi hiyo Novemba mosi mwaka huu.


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, David Mwakyusa alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa madaktari wengine watatu wa ngazi ya chini na daktari mmoja wa dawa za usingizi pia watafikishwa katika baraza hilo kujibu tuhuma za uzembe huo uliogharimu maisha ya Emmanuel Mgaya.


Alisema pamoja na madaktari hao wauguzi wa dawa za usingizi wawili, wauguzi wa wawili wa upasuaji na wauguzi wa wodini wawili watafikishwa mbele ya Baraza la Wauguzi kwa udhaifu katika utendaji kazi uliochangia tukio hilo.


Mwakyusa alisema hayo alipokuwa akisoma ripoti ya tume iliyoundwa na Wizara yake kuchunguza tukio la upasuaji tata wa Emmanuel Didas na Mgaya ambapo alisisitiza kwamba kitaaluma hairuhusiwi kuwataja majina ya madaktari na wauuguzi hao mpaka mabaraza husika yatakapotoa hukumu.


Kwa mujibu wa sheria iliyounda mabaraza hayo, watuhumiwa hao wakibainika kuwa wana hatia, watahukumiwa kwa mujibu wa sheria hiyo na endapo hawataridhika na uamuzi wa mabaraza hayo, wana uhuru wa kukata rufaa mahakama kuu kupinga hukumu husika.


Profesa Mwakyusa alisema ripoti ya tume imegundua udhaifu wa usimamizi wa kazi katika utawala, mfumo wa utendaji na utaalamu katika MOI uliosababisha upasuaji tata waliofanyiwa wagonjwa hao wawili.


Mgaya alilazwa katika hospitali ya Muhimbili Oktoba 25 mwaka huu na baada ya kufanyiwa uchunguzi na jopo la madaktari alionekana kuwa na tatizo la uvimbe na kuamua afanyiwe upasuaji wa kichwa . Badala ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa tarehe Mosi Novemba mwaka huu alifanyiwa upasuaji wa goti.


Didas aliyelazwa hospitalini hapo Oktoba 26 mwaka huu kutokanana matatizo ya goti na baada ya uchunguzi kutakiwa kufanyiwa upasuaji wa goti Novemba Mosi mwaka huu alifanyiwa upasuaji wa kichwa.


Profesa Mwakyusa alisema ripoti imebaini kuwa kuna udhaifu wa usimamizi katika vitengo vya upasuaji mifupa, upasuaji mishipa ya fahamu na ubongo, utoaji wa dawa za usingizi, vyumba vya upasuaji na uuguzi katika taasisi hiyo.


"Tume imebaini kuwa afisa aliyemkagua mgonjwa usiku kabla ya siku ya upasuaji, siye aliyetoa dawa za usingizi wakati wa upasuaji, hii ilichangia udhaifu katika idara ya dawa za usingizi na kama angekuwepo katika chumba cha upasuaji angesaidia kumtambua mgonjwa," ilieleza ripoti hiyo.


Alisema kulikuwa na udhaifu wa utayarishaji wa orodha ya upasuaji na kuwa mzunguko haikufanyika tangu Oktoba 26 na kama ungefanyika Didas asingefanyiwa upasuaji tata.


"Utaratibu ni kwamba kabla mgonjwa hajaingizwa kwenye orodha ya upasuaji, lazima daktari ajadiliane naye kwa kina na mgonjwa atakayempasua na ikibidi ndugu wa mgonjwa wanahusishwa ili kutoa idhini, lakini hili halikufanyika," alisema Waziri.


Kwa mujibu wa Prof. Mwakyusa, upasuaji huo pia ulisababishwa na kitendo cha afisa muuguzi mmoja kupuuzia maelezo ya Mgaya aliyemweleza kabla ya kufanyiwa upasuaji wa mguu kwa makosa kuwa yeye sio Emmanuel Didas bali ni Emmenuel Mgaya, lakini muuguzi huyo akampuuza kwamba amelewa dawa za usingizi. Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu na kisha akafariki baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa.


Pia Prof. Mwakyusa alisema ameiagiza Bodi ya MOI isimamie uongozi kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na tume ya Prof. Mahalu na kumpatia taarifa ya utekelezaji ndani ya wiki mbili kuanzia jana.


Aidha, Mwakyusa ameiagiza Bodi imwagize Mkurugenzi Mkuu wa MOI, wakurugenzi wa Idara na vitengo kusimamia utendaji kazi ipasavyo na kuwasilisha taratibu mpya zitakazoimarisha usimamizi wa idara zote.


Pia Bodi imwagize Mkurugenzi Mkuu wa MOI kupitia upya mgawanyo wa kazi wa idara na vitengo kuongeza wigo wa madaktari bingwa wa upasuaji wa mifupa na ubongo.


Prof Mwakyusa ameitaka Bodi ichukue hatua kali za kinidhamu kwa wale wote waliozembea katika kuwahudumia wagonjwa na iendelee kuchukua hatua kwa wale ambao watafanya hivyo baadaye.


Pia MOI imetakiwa kuandaa vigezo vya utendaji vya madaktari, wauguzi na wataalam wa usingizi na chumba cha upasuaji, pia isimamie utekelezaji wake.


Prof. Mwakyusa alisema kwamba Katibu Mkuu wa Wizara atoe mwongozo wa utoaji wa huduma ya afya nchini kwa kuzingatia vigezo vilivyokubaliwa katika upasuaji.


Katika hatua, Waziri Mwakyusa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kudai fidia ni haki ya mteja na kwamba familia za Didas na Mgaya zinahaki ya kudai fidia.


Amefafanua kuwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ndiyo inayoshughulikia masuala yote ya madai ya serikali na kuongeza kuwa ni jukumu la watu walioathirika na upasuaji huo kuamua kupeleka madai yao au kuacha.


Kuhusu Didas aliyepelekwa India kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi Waziri Mwakyusa alieleza kuwa mgonjwa huyo anaendelea vizuri na ameanza kurudisha kumbukumbu.


"Kumbukumbu yake imekwisharudi na ameweza kuelezea jinsi alivyopata ajali na mwili wake umekuwa na nguvu," alisema.


Aidha, alielezea masikitiko ya serikali kuhusiana na tukio hilo na kusema kuwa, tukio hili limetokea na kunaonyesha kuwa usimamizi wa wagonjwa sio mzuri.


"Kulikuwa na kuaminiana kwingi kulikokiuka maelekezo ya utoaji ya huduma kwa wagonjwa,"alisema.

Source link: Mwananchi.

SteveD.
 
kinachozidi kuchefua ni kuwa hawa wanaoitwa wakubwa swala la kujiuzuru wanapojumuishwa katika uzembe huwa haliko akilini mwao kabisaa...sijui ni kukosa haya au?
 
Hivi hili sakata limeishia vipi au linaendleaje?.... any update pls...

Limeisha kama masakata mengine yanavyoisha. Kwa maneno mengine ni kwamba wengi wetu tumeshasahau, vyombo vya habari navyo vimeshasahau au kwa makusudi au kwa sababu wanazojua wenyewe, navyo vimeacha ufuatiliaji. Kwani sakata la Nimrod Mkono limeishia wapi? Mahalu je?
 
Back
Top Bottom