Muhimbili madaktari watimuliwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kwa taarifa nilizozipata muda huu uongozi wa hospital ya taifa ya muhimbili wamewatimua madaktari Interns wote katika hospital hiyo

Barua iko hivi;

Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi yatarehe 23 Juni 2012. Baada ya tathmini hiyo,

Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:

(i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;
(ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.
(iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa.
(iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;
(v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na
(vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo.

Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla.
Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.

Dkt. Gabriel Upunda
KAIMU MWENYEKITI BODI YA WADHAMINI
 
Solidarity forever,i appeal to you all intern doctors,Registrars and Specialist to go beyond the point of no return.
 
They need really to unite manake ni shida. Ila jamani hospitali zetu zinatia aibu. Sasa hivi 80% ya vipimo na dawa unaambiwa nenda hospitali binafsi. Wananchi wenzangu haya yanatugusa? Au ndo tunakuwa na ule upeo wa aah madaktari wanadai maslahi. Nenda hospitali sasa uandikiwe dawa uone. Ila kwa bahati mbaya sana mheshimiwa hakuthubutu kutaja hayo. Tumempoteza rafiki yetu wa bodaboda kisa kapata ajali kaumia kicwa kwa kuvila damu na nothing was done kwa vite scan ya kichwa haifanyiki. Wadau hali ni mbaya mno!
 
Serikali itakuwa imewapa nafasi zaidi ya kujipanga na kujadili future yao. Who is looser? JK anataka kuwapa kazi Wa Iran na wape sasa
 
Solidarity forever,i appeal to you all intern doctors,Registrars and Specialist to go beyond the point of no return.
Watu wanatofautiana kiuchumi nakwambia mwingine anaweza kuendelea kugoma kwa kua ana hospitali yake anapata chochote ila nakwambia kwa hii move ilipofika wote wanarudi kazini. Wameshashikwa pabaya na hawawezi tena kua na nguvu nakwambia
 
They need really to unite manake ni shida. Ila jamani hospitali zetu zinatia aibu. Sasa hivi 80% ya vipimo na dawa unaambiwa nenda hospitali binafsi. Wananchi wenzangu haya yanatugusa? Au ndo tunakuwa na ule upeo wa aah madaktari wanadai maslahi. Nenda hospitali sasa uandikiwe dawa uone. Ila kwa bahati mbaya sana mheshimiwa hakuthubutu kutaja hayo. Tumempoteza rafiki yetu wa bodaboda kisa kapata ajali kaumia kicwa kwa kuvila damu na nothing was done kwa vite scan ya kichwa haifanyiki. Wadau hali ni mbaya mno!
Kwa nini kwenye madai yao hii ya kuboresha mazingira hawakuipa kipaumbele?
 
Ni aibu kwa serikali Dhaifu kucheza na fani kama Udaktari ata USA na UK Madaktari awatoshi.inachukua miaka 5 mpaka 7 kumtrain Dokta mmoja.let see miracles
 
Tatizo la nchi kutokua na kiongozi mtoa maamuzi anachojua ni kusoma hotuba.Mbona wasifanye mjadala live pande zote mbili tusikie nani mkweli nani mwoga ?majibu tunayopata ni ONE sided ukisikiliza bunge haliruhusiwi kuzungumza MGOMO huu Madaktari hawana pa kusema zaidi ya vyombo vya habari vichache ambavyo vimeweza kupata hizo taarifa zao.

Timua timua ni nyepesi kwa viongozi wao wanatibiwa nje ,je sisi tutakaobaki kwenye WODI ZISIZO NA MADAKTARI NA WAHUDUMU WALA HUDUMA HILI JAMBO TUNAWAANGALIA WATU TULIOWAPA DHAMANA YA MAISHA YATU NA NCHI YETU WAKIKURUPUKA ?
 
Ni aibu kwa serikali Dhaifu kucheza na fani kama Udaktari ata USA na UK Madaktari awatoshi.inachukua miaka 5 mpaka 7 kumtrain Dokta mmoja.let see miracles
usijali kiongozi ma dr wote wanarudi kazini nakwambia
 
Back
Top Bottom