Muhimbili madaktari watimuliwa

Ni kweli kabisa Mkuu, inabidi kipindi hiki washikamane sana katika kudai haki zao na pia madai ya kuboresha sekta ya afya nchini.
Hivi sekta ya afya ni ma dr tu ndio waajiriwa?
 
They need really to unite manake ni shida. Ila jamani hospitali zetu zinatia aibu. Sasa hivi 80% ya vipimo na dawa unaambiwa nenda hospitali binafsi. Wananchi wenzangu haya yanatugusa? Au ndo tunakuwa na ule upeo wa aah madaktari wanadai maslahi. Nenda hospitali sasa uandikiwe dawa uone. Ila kwa bahati mbaya sana mheshimiwa hakuthubutu kutaja hayo. Tumempoteza rafiki yetu wa bodaboda kisa kapata ajali kaumia kicwa kwa kuvila damu na nothing was done kwa vite scan ya kichwa haifanyiki. Wadau hali ni mbaya mno!

Niambie ni kipimo gani ambacho serikali haikuwahi kukinunua? Madaktari hawa hawa ndio wahusika wakubwa wa wizi wa vifaa vya mahospitalini, wahusika wakubwa kwenye wizi wa madawa kwenye mahospitali ya serikali, hata kuharibika kwa CT scan ya Muhimbili ni hujuma ili kuzipa biashara hospitali za binafsi semeni jingine.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Hao wa iran hawajafika tu?

Sasa mr dhaifu atawatibu, simuoni muhimbili.

Dr. Slaa yeye si mwenyekiti wa taasisi ya CCRT? Mbona hajatoa tangazo la kuwatibu bure akina mama na watoto wasio na uwezo? Hivi mnataka kutufanya sisi machizi maarifa? Liwalo na liwe mambo mdundo!!!

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Mimi nafikiri warudi tu kazinin wakaokoe maisha ya walala hoi wenzao, kama ni mgomo wawafanyie hao wakubwa siku wakiuugua
 
Pole mkuu wewe nadhani ndo haupo TZ na kama upo basi huna unachokijua na kama unakitu unachokijua basi wewe ni sehemu ya matatizo ya watanzania wa kawaida na kama vile haitoshi wewe utakuwa ni mfuasi wa Nape na unyinyiemu wenu.kwanza kama hujui mimi ni mmoja wa watu nilekataa kujipendekeza,kunyanyaswa,kuwa mnafiki kwa serikali,na wala sikuwa na ujinga wa kuamini kuwa nje ya serikali hakuna maisha.lakini ktk yale niliyoyapigania leo yamesaidia watanzania japo bado kuna machache huko nilikokuwa hayajarekebishika.ila kwa hali iliyokuwepo siku moja hali ingechafuka kama wakubwa wasingesikiliza madai tuliyoya-table kwao kwa vinywa vyetu.
Na unadhani JK ni imara basi kwenye hotuba yake angetamka direct kuwa madaktari amewafukuza kazi,huyo ni dhaifu na ndio maana anafanya kwa kupima upepo huku akitumia wakuu wa idara kuweka mashinikizo ya kuwagawa madaktari.yeye angelikuwa anawaza kama wewe unavyowaza basi angetamka tu kuwa wote wamefutwa kazi sio kuwaambia wajiondoe,tamkeni mmewafukuza kazi single sentence inayojitosheleza.zaidi kinachotafutwa sasa ni kupandikiza utengano ili wavunje umoja wao washindwe kutetea maslahi yao na ya wananchi.
usidhani ni rahisi kihivo kufukuza madaktari,leo unaweza kufukuza waalimu wa shule ya msingi na sekondari wote na kesho hata wewe ukaenda kufundisha moja ya shule huko kijijini kwenu lakini to be honest kwa fani ya udaktari huwezi ukaokoteza na ukajaza.think twice we gamba
Anyway namshukuru Mungu mimi si sehemu ya Kikwete. Cause naamini ningewafundisha watu namna ya kutii na kuiheshimu serikali, hasa pale wanapogombania kitu kisichowezekana. Daktari mwenye degree moja anapotaka alipwe milioni 3.5 na marupurupu juu, professor atalipwa bei gani? Kwa mtindo huo si bajeti yote ya mwaka itaishia kulipa mishahara?

Lets be realistic, kitendo cha madaktari kugoma kurudi kazini kwa ajili ya mshahara na wakati marupurupu yao kibao yamepitishwa ni ukosefu wa uzalendo. And if I were JK, ningewafuta kazi waliogoma wote, nawanyangánya hati za kusafiria, halafu nawadai warudishe hela niliyowasomeshea within seven days. Sasa mmemuokota Kikwete dhaifu, basi mmeona mtumie udhaifu wake kumnyanyasa.

Mwanzoni nilikuwa naunga mkono mgomo wa madaktari, but from Kikwete's speech sina sababu ya kuwaunga mkono tena! Maana hata mkisingizia kwamba mnagomea sijui infrastructures, bado haziwezi kujengwa kwa siku moja. It will take sometimes. Hamna sababu ya msingi ya kuwaacha watanzania waendelee kufa kwa kukosa huduma eti kisa mshahara wa milioni 3.5, ambao mnajua kabisa hauwezekani. Acheni hizo bwana.
 
Kama serikali haiwezi ulipa mil 3.5 je inaweza kulipa shilingi ngapi?na je una sababu gani za msingi zinazokufanya uridhike ya kwa serikali haiwezi kurekebisha infrastructure na pia haiwezi kulipa mshahara mzuri?na if possible ule uliopendekezwa n madaktari?
Hebu tuelimishe ni kwa vipi serikali inaona haiwezekani?je unaweza pia kutuambia mbali na sekta ya afya serikali yako imeweza nini tu?Elimu au Kilimo?
Mshauri JK awanyang'anye paspoti za kusafiria na atende zaidi ya hayo na hata zaidi ya waliyomtendea Dr Ulimboka,then utakuja kunikumbuka kwa maneno yangu.
 
wahenga wanasema usifanya maamuzi ya hasira serikali ingekutana nao kwa ajili ya majadiliano kuwafukuza sio solution kabisaa ukuizingatia taaluma yenyewe ilivyo ngumu our pres.... somewho is st,,,,
 
watakwenda kwenye point of no return wakiwa nyumbani kwao? Ujue mgomo huwa unawezekana mkiwa tu mahali pamoja ambapo mnakutanika kwa pamoja. Sasa mkishakuwa kwenu, mtajiorganize vipi? Maana ujue mkishafukuzwa, hamruhusiwi tena kuonekana mazingira ya kazini kwenu kwa zamani, mtakutana wapi, na mtakuwa mnafanya nini mkikutana.

Chadema square ipo kwa ajili yao
 
hahaha...very funny, TZ ina
neurosurgeons 4,
Orthopeadics Surgeon less than 15,
Physician 30,
Otorhinolaryngolist 7,
Anaesthesiologist 25,
Ophthamologist(sio optician) 20,
Psychiatrist(not psychologist) 20,
Pediatrician 35,
Obstetrician and Gynaecologist 35,
Surgeons(Urologist,Thoracic,Pediatrics,Gastro, Plastic, Vascular and Oralmaxillofacial) 40,
Radiologist 12,

wote hawa wamegoma, hebu tuone kama serikali yetu ya kutufukuza na pamoja na wadogo wetu(residents, registrar, intern) tuone mtatupatia wapi?!
besides hata hao AMO wenyewe(madaktari wa fastafasta waliosoma miaka 3) inawahitaji tena kusoma 5years again!!
you dont know what someone can do until you push him to the edge, ..we have reached ours!

Statistics za mwaka 1992
 
Solidarity forever....kamwe msikubali hivi vitisho mkigawanyika tu mmekwisha
 
Kwa taarifa nilizozipata muda huu uongozi wa hospital ya taifa ya muhimbili wamewatimua madaktari Interns wote katika hospital hiyo

Barua iko hivi;

Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi yatarehe 23 Juni 2012. Baada ya tathmini hiyo,

Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:

(i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;
(ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.
(iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa.
(iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;
(v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na
(vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo.

Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla.
Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.

Dkt. Gabriel Upunda
KAIMU MWENYEKITI BODI YA WADHAMINI

Timua timua ina mwisho wake,kwani madaktari ni wachache na huduma ni kubwa,hivyo serikali inapaswa kufikiri jinsi ya kuwashawishi madaktari kurejea kazini.
 
Good move kwa serikali.

Tuone kama Intern nae atapata kazi Botswana...

Anaweza sana,in short intern anaweza kwenda nchi yyte na,akasema yy ana degree ya dr,na hajamaliza mafunzo...kwanza anapewa mtihani,then akifaulu anapewa kitengo km intern bt chini ya uangalizi,akimaliza na kufaulu anasajiliwa na anaajiriwa!coz tofauti ni kuwa anakuwa hajasajiliwa kweny bodi ya madaktari na ili usajiliwe lazima uwe umemaliza hayo mafunzo(intern)
 
Sidhani kama wana muda huo...
 
Kwenye stori zetu mahali flani jamaa akaja na mada kua eti kuna hati hati ya madaktari kama 78 Hv ambao hao walikua vinara wa mgomo kufukuzwa muda si mrefu..watu bwana hawaishi na stori zao..
 
sio tu kupata kazihopitali binafsi ila wana uwezo wa kufanya kazi popote pale duniani tofauti na sekta nyingine kama mahakama(inabidi kusomea sheria ya sehemu mahalia), Si rais, wabunge,mawaziri wala wahasibu ila madaktari na wachoraji wa ramani(architects) tu!
 
Naipongeza serikali kwa kufanya maamuzi magumu,watakaotaka kurudi warudi kwa masharti,kuna msemo wa kiswahili unasema "ukizira wenzio wala" na masharti yenyewe wakatuanzishie zile kambi za JKT,waende huko kwanza,wakakanyagwe sawasawa mbona wengine tulipigwa sana huko na tumejaa woga wa nchi na mungu.kwanini isiwe wao, au JK kutaka kuongeza idadi ya madaktari nchini imekuwa nongwa?.Safi sana liwalo na liwe.

chezea gwaride wewe? Mr.dhaifu mwenyewe aliingia mtini, hakuwahi maliza huo mziki. ile mambo ni mutu mugumu wala sio mutu soft kama dhaifu.
 
Niambie ni kipimo gani ambacho serikali haikuwahi kukinunua? Madaktari hawa hawa ndio wahusika wakubwa wa wizi wa vifaa vya mahospitalini, wahusika wakubwa kwenye wizi wa madawa kwenye mahospitali ya serikali, hata kuharibika kwa CT scan ya Muhimbili ni hujuma ili kuzipa biashara hospitali za binafsi semeni jingine.

Chama
Gongo la Mboto DSM

Ni udhaifu wa usimamizi kwa maana serikali ingeweka usimamizi mzuri wa vifaa hivyo vingeendelea kuwepo hadi sasa pamoja na uduni wake. In this life, no body cares if you are dead or alive. vipimo vingine ni vya mwaka 1947 huko haviendani na usasa alafu tunajitapa tuna vifaa, wapi ndugu, nenda mahospitalini ukajioneee mwenyewe wala usiniulize source, kajioneee mwenyeweee alafu uje utuambie umeona nini huko.
 
Back
Top Bottom