Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) - Mlongazila, imesema huduma ya kupunguza uzito na upasuaji rekebishi zinazotarajiwa kufanyika hospitalini huko, zitahusisha pia wanaume wenye maumbile kama matiti.
Mkuu wa Idara ya Upasuaji MNH-Mloganzila, Dk. Eric Muhumba, alibainisha hayo na kueleza kuwa huduma hizo kama alivyoeleza awali, zitatolewa kwa siku mbili kuanzia Oktoba 27 mwaka huu.
"Huduma hii ya kupunguza uzito ni kwa jinsi zote mbili kwa kuwa kumekuwa na minong’ono kwamba, mbona mmependelea wanawake. Huduma itafanyika kwa watu wote wenye uzito mkubwa," alisema.
"Tumeona wanaume kwa bahati mbaya inatokea miili yao wanakuwa kama wana matiti badala ya kifua cha kiume, nao watafanyiwa upasuaji rekebishi katika siku hizi mbili," alisema.
Bingwa huyo aliwatoa hofu Watanzania kwa kuwaeleza kuwa, upasuaji huo ni salama na ni sawa na upasuaji mwingine unaofanywa hospitalini huko.