Mugabe kung'olewa kijeshi.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,943
698
Kuna habari zilizovuja jana 28/06/2008 kuwa USA ina Military Option on the table kama Diplomacy na Pressure haitafanya kazi. Hata hivyo George Kichaka amewaagiza mawaziri wa Mambo ya Nje pamoja na fedha ku-table new sanctions on Zim. Kuvuja kwa habari hizo tokea White House zilipitia kwenye CNN katika kipindi cha Newsroom kilichokuwa kikirushwa hewani 04.00 pm EST badala ya kipindi cha Situation Room. Mpaka sasa White House haijathibitisha au kukanusha habari hizo.

Nguvu za kijeshi kutumika kumuondoa Mugabe zimeongezewa uzito na Mwanaharakati Askofu Desmond Tutu. Akinukuliwa na BBC leo, Askofu Tutu amedai kuwa kama Jongwe hatakubali ku-step down diplomatically basi nguvu itumike kumng'oa madarakani. Kwa habari zaidi kuhusu Tutu soma hapa chini:-
Archbishop Tutu: Good Argument For International Force In ZimbabweLONDON (AFP)--There is "a very good argument" for sending an international force into Zimbabwe if diplomatic pressure fails to sweep away President Robert Mugabe, Archbishop Desmond Tutu said Sunday.

The Nobel Peace Prize laureate said the African Union could take a lead role in any such action, as he urged the bloc not to recognize Mugabe as Zimbabwe's head of state at its summit in Egypt this week.

"That crisis has to be resolved sooner rather than later and yes, I think that a very good argument can be made for having an international force to restore peace" under U.N. auspices, he said, responding to a question on BBC television on whether there should be military intervention.

"If you were to have a unanimous voice saying quite clearly to Mr Mugabe ... you are illegitimate and we will not recognize your administration in any shape or form, I think that that would be a very, very powerful signal and would really be able to strengthen the hand of the international community," Tutu said, urging African leaders not to recognize Mugabe's re-election.

Mugabe is to be inaugurated at 1300 GMT Sunday after a run-off election in which he was the only candidate following the withdrawal of Morgan Tsvangirai of the Movement for Democratic Change because of violence against his supporters.

Also speaking on BBC television Sunday, the second most senior Anglican cleric in the U.K., Archbishop of York John Sentamu, called for the U.K. to close its embassy in Harare.

Military intervention shouldn't be ruled out, he added.
 
Pale Kuna Tatizo Moja Lingine Nalo Ni Majeshi Ya Uchina Nchini Zimbabwe Pamoja Na Yale Ya Angola Na Baadhi Ya Nchi Za Kiafrika Ambazo Zinamuunga Mkono Mugabe Kwa Kificho Naamini Kama Nguvu Zikitumika Basi Itakuwa Chakaza Sana Na Vita Hiyo Inaweza Kuvuka Mipaka Zaidi

Ni Tatizo Kama Sudan Ambao Wanalindwa Nauchina Sema Tatizo La Sudani Ni Tofauti Na Zimbabwe Sema Usawa Unakuja Kwamba Majeshi Yakeyakokatika Nchi Hizi
 
Hamna lolote ni udaku tuu
Marekani haina waziri wa fedha

Nashukuru kwa kunisahihisha, I meant Secretary of Treasury. Sasa kutafsiri sijui nilitakiwa niandike Waziri wa Hazina au.......labda ungenisaidia hapo maana Kiswahili shuleni nilijitahidi sana nikapata F+. Nitashukuru kama utanisaidia hilo (translate) kwa manufaa ya wasomaji.
 
Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe imemtangaza rasmi Mzee Robert Mugabe kuwa ameshinda uchaguzi,sasa tusubiri steps nyingine,kwani USA na UK wamedai kuwa wanajiandaa kutumia nguvu kumuondoa Madarakani Mzee Mugabe.Katika kipindi cha "GPS" cha Fareed Zakaria (CNN), Waziri Mkuu wa UK, Gordon Brown amesema wazi kuwa UK haiutambui Uchaguzi wa Zimbabwe,na Viongozi wa Afrika wanazungumza ili kujadili hatua za kuchukuliwa dhidi ya Mugabe na serikali yake,amekataa kuweka wazi kwamba kutatumika Nguvu kumuondoa Mugabe.Suala la kutumia nguvu litakuwa wazi baada ya mazungumzo ya African Leaders
 
Nashukuru kwa kunisahihisha, I meant Secretary of Treasury. Sasa kutafsiri sijui nilitakiwa niandike Waziri wa Hazina au.......labda ungenisaidia hapo maana Kiswahili shuleni nilijitahidi sana nikapata F+. Nitashukuru kama utanisaidia hilo (translate) kwa manufaa ya wasomaji.

..hamna haja ya kutafuta tafsiri.

..ulichosema ni sawa [kutokana na mazingira yetu huku]

..ingekuwa tafsiri ya maneno inakuwa moja kwa moja tungepata shida sana kuyasoma na kuyaelewa maandiko makuu ya kidini.
 
Bush yuko busy anaplan vita ya Iran sasa hivi...issue ya Zimbabwe itamalizwa na sisi Waafrika wenyewe.....!!!!
 
..kweli? ina nini?
Ina Rais ambaye ni waziri wa fedha
mtambue kuwa Amerika hapigani vita kwa political gain sasa ukiangalia zimbabwe hamna economic gain at all ni bora awaachie waafrica tuu washughulikie
Kama Zimbabwe kungekuwa na chochote cha economic gain angekuwa ameondoka kitambo sana
 
Nashukuru kwa kunisahihisha, I meant Secretary of Treasury. Sasa kutafsiri sijui nilitakiwa niandike Waziri wa Hazina au.......labda ungenisaidia hapo maana Kiswahili shuleni nilijitahidi sana nikapata F+. Nitashukuru kama utanisaidia hilo (translate) kwa manufaa ya wasomaji.

Kama wangekuwa na Oil or any precious mineral ungeuona moto pale
Yankee hapeleki jeshi pale labda ampiganishe na jirani yake labda malawi
 
Mmarekani anatafuta mwanya wa ku mobilize R2P. Kikwete kashaonyesha willingness.
 
Kikao kinachoanza leo Sham el sheikh hawataongelea Zimbabwe kwani ameshawapa warning kuwa kiongozi yeyote aliye msafi na ajaribu kusema chochote kuhusu zimbabwe akione cha moto na amesema ataudhuria ili aweze kuwakomesha wanaojipendekeza kwa nchi za magharibi.
 
Kikwete Kama Hata Mugabe Anamtoa Nishai Basi Ajiuzulu Tu!
Kwani Hii Bifu Wanaweza Hata Kutuvamia Wakidai Ni Uhuru Wa Afrika!
Nilishangaa Sana Kuona Yuko Na Kichaka!
Hawa Watu Ni Either Walitegwa Kama Theory Ilivyo.
Ama Kwa Makusudi Waliuza Nchi!
Wairudishe Mara Moja!
 
Hamna lolote ni udaku tuu
Marekani haina waziri wa fedha
Marekani ina Waziri wa Fedha wao wanamwita Secretary of Treasury, na kwa taarifa Marekani haiwaiti Mawaziri wake as "Ministers" wanaita Secretaries mfano Condolleza Rice anaitwa Secretary of State katika maana ya Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani. Waziri wa Ulinzi wao wanamwita Secretary of Defence, nk......!!!
 
Naomba kujua ..... kwani "umoja" wetu wa africa hauwezi kukaa na kukubaliana kumng'oa kijeshi
 
Sitaki kuamini kuwa uchaguzi wa Uganda unaotambulika ni halali zaidi kwenye macho ya jumuiya ya kimataifa kuliko wa Zimbabwe.

SITAKI kuamini kuwa uchaguzi wa Rwanda ambao ni mfano wa demokrasi una uhalali zaidi kuliko wa Zimbabwe.

SITAKI kuamini uchaguzi wa Zaanzibar una uhalali zaidi kuliko wa Zimbabwe.

SITAKI kuamini kuwa uchaguzi wa Kenya una uhalali zaidi kuliko wa Zimbabwe.

SITAKI kuamini uchaguzi wa Nigeria una uhalali kuushinda wa Zimbabwe.

SITAKI kuamini kuwa Hosni Mubarak ni rais halali wa Misri kuliko uhalali wa Mugabe.

SITAKI kuamini kura ya Wapalestine kwa HAMAS haina uzito kuliko kura ya Wazimbabwe kwa Tsivangilah.

Ukiangalia kwa makini hapo, tatizo sio MUGABE isipokuwa tatizo ni power politics, na Tsivangilah ni Charabi wa Zimbabwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom