Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Kuhudhuria kwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati wa kuapishwa kwa rais Kikwete kunaelezwa na wanazuoni huenda ikawa sababu ya nchi nyingi hasa za magharibi kusita kumpongeza rais Kikwete aliyeapishwa leo.
Nchi hizo za magharibi zenye ushawishi mkubwa duniani zikiwemo Marekani na Uingereza, pamoja na kuwakilishwa na mabalozi wake inasemekana hadi sasa hazijatuma salamu za pongezi za kuchaguliwa kwa Kikwete kitu ambacho si kawaida yake.
Ikumbukwe kuwa wakati wa uchaguzi uliopita wa Zimbabwe ambao ulilalamikiwa sana na UK na USA kuwa haukuwa huru na wa haki umepelekea hadi leo Mugabe na familia yake kunyimwa hati ya kuingia katika nchi hizo isipokuwa kuhudhuria mikutano ya UN pekee.
Wachambuzi wa mambo wanahisi tukio la leo kwa Mugabe kuhudhuria linaweza kuwa limetia doa mahusiano ya Tanzania na nchi hizo ikizingatiwa kuwa kuna madai yanayotolewa na chama cha upinzani Tanzania kuwa kulikuwa na udanganyifu wa kura wakati wa kuhesabu.